Advertise here

Tetesi: Wos born

Emido

New member
2e5ab19b-b01b-4b20-9954-e3630a447e01_0_watermark.jpeg
*MAADA: "Kupenda au kutumiwa? Jinsi ya kujua tofauti"*

Nimekaa nikawaza jana usiku...
Tuna watu wengi kwenye maisha yetu ambao wanakula wakati wetu, pesa yetu, na nguvu zetu. Lakini tunawaita "wapenzi".

*Ishara 3 za mtu anakutumia:*
1. Anakumbuka wewe tu anapohitaji kitu - pesa, ushauri, au faraja
2. Anakupigia tu usiku wa manane. Mchana yupo busy
3. Hajakuwahi kukutambulisha kwa marafiki zake au familia

*Ishara 3 za mtu anakupenda kweli:*
1. Anakupigia hata hana kitu cha kukuomba
2. Anajivunia wewe hadharani
3. Anakupigania hata mnapogombana, sio kukutupa

*Swali kwenu:*
Wewe upo kwenye #1 au #2?
Au umewahi kutumiwa halafu ukajifunza? Tuambiane hapa tusaidiane 👇
 
Back
Top