JESHI la Polisi Tanzania limesema linaendelea kumtafuta Augustino Polepole ambaye alijitambulisha kuwa ni Ndugu wa Humphrey Polepole ili aweze kulipa Jeshi hilo ushirikiano na kutoa maelezo yake na uthibitisho wa shutuma alizotoa kwamba Afisa wa Jeshi la Polisi alihusika kumteka Polepole...