Patrice Lumumba: Shujaa asiye na kaburi, Uovu waliyoufanya kwenye ardhi ya kongo bado inatesa akili za Waafrika

Kasomi

JT Founder
Patrice Lumumba: Shujaa asiye na kaburi, Uovu waliyoufanya kwenye ardhi ya kongo bado inatesa akili za Waafrika
1768163476733.jpg

Baada ya Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 hadi 1885 nchi ya DR' Kongo yenye ardhi tajiri zaidi Duniani ilitolewa kama mali ya kibinafsi kupitia Taji ya Kifalme la Ubelgiji na kupewa Mfalme Leopold II. Haki hii ya kipekee ya umiliki haikuhusu tu ardhi na rasilimali zilizo chini yake, bali pia binadamu na kazi zao.

Wakati wa udhibiti kamili wa taji la Ubelgiji juu ya Kongo, nusu ya watu wa DR Congo uaani Milioni 15 waliuawa kwa amri ya Wafalme Leopold II kama njia ya kudhibiti idadi ya watu ili apate faida kubwa kutoka kwenye rasilimali nyingi za nchi bila kutumia sehemu kubwa ya watu ambao walikuwa mali yake binafsi!

Wakati wa uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1960, watu 11 tu kati ya watu milioni 15 kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walikuwa na shahada ya Chuo Kikuu au wahitimu wa chuo kikuu. NDIYO, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuwa na wahitimu 11 pekee wakati wa uhuru, utawala wa zaidi ya miaka mia moja wa Ubelgiji, ulihakikisha kwamba wakazi wa DRC wanazuiwa kabisa kupata elimu au ujuzi wowote. Kwa sababu kutoa elimu au ujuzi kwa watu kutawafanya watu wasistahili kuwa watumwa au kunyonywa.

Hii ina maana kwamba, Kongo mpya iliyopata uhuru na Waziri Mkuu wa kwanza, Patrice Lumumba walipaswa kutegemea mfumo huo huo kandamizi wa kusimamia kila kitu. Serikali iliyokuwa huru ililazimika kutegemea wafanyakazi na vikosi vya Ubelgiji katika maeneo muhimu kama vile mawasiliano na ulinzi wa kijeshi yaani hakuwa na siri nia yake njema kwa nchi yake na hakukuwa na utetezi wa kumlinda patrice.

Patrice Lumumba alikuwa chini ya huruma ya Wakoloni wa Ubelgiji. Halikuwa jambo la kushangaza kwamba waliweza kumuua na kuuingiza mwili wake kwenye tindikali katika nchi ile ile aliyokuwa akiitumikia akiwa Waziri Mkuu. Hadi leo, hakuna eneo la kaburi kwa shujaa huyu mashuhuri wa Afrika isipokuwa jino moja ambalo lilirudishwa kutoka Ubelgiji hadi Kongo mnamo 2020.
 
Back
Top