Advertise here

Njia panda: Nimeolewa na Wanaume wawili wote hawajuani

Kasomi

JT Founder
1742145603268.jpg

Mwaka 2019 nilifunga ndoa nyumbani kwetu Iringa na mwanaume ambaye nilikubali niolewe naye kwa sababu ya pesa. Kipindi hicho nilikuwa sina kazi, maisha yalikuwa magumu, nikakubali anioe lakini si mtu wa hadhi yangu. Yaani ni yule mtu hata kimuonekano huwezi kutoka naye.

Nilikaa kwenye ndoa kwa mwaka mmoja, nikagundua maisha hayawezekani. Pesa anapata, nina kila kitu, lakini sina furaha. Nilimuambia kuwa nimepata kazi Dar, hivyo nikaenda kufanya kazi. Lakini ukweli ni kwamba nilikutana na mwanaume mwingine hapa Dar, akanioa. Huyu mwingine maisha yake ni ya kawaida, hana pesa nyingi, lakini nampenda kwa sababu ana muonekano mzuri.

Nilifunga tena ndoa na huyu mwanaume wa pili bila kumuambia mtu yeyote zaidi ya mama yangu. Hivyo, nikawa na waume wawili—mmoja yuko Iringa, na kwa mwaka mzima nilikuwa naenda kumuona mara moja tu kwa mwaka. Nilimuambia kuwa niko kazini. Kama akija Dar, nilikuwa nimepangisha chumba, hivyo akija namdanganya mume wangu wa Dar kuwa ninaenda nyumbani kusalimia, kumbe niko na mume wangu wa Iringa mpaka aondoke, ndipo narudi.

Nilikuja kubeba mimba, mwanzoni sikujua baba halisi ni nani, lakini mtoto alipozaliwa, alifanana sana na yule wa Iringa, jambo ambalo lilizidi kunichanganya. Nimehangaika sana, na sasa hivi nina watoto watatu, lakini hawa wawili nilihakikisha wanajulikana kuwa ni wa huyu mwanaume wa Dar. Pamoja na kwamba hana pesa, lakini ana muonekano mzuri.

Sababu ya kuja kwako ni hii: Kila mwanaume anajua watoto wote ni wake, na kwa kiasi kikubwa wanahudumiwa na mume wa Iringa, kwani huyu mwingine hata hela ya chakula kutoa ni ngumu. Anajua nafanya kazi na nina duka, lakini ni dogo. Hata hivyo, haulizi chochote kuhusu kama maisha tunayoyaishi yanalingana na kipato changu. Yeye anaishi tu, yaani hakuna kitu. Nampenda sana, lakini shida ni kwamba hana kipato.

Sasa mwanaume wa Iringa anataka kuhamia Dar. Keshanunua kiwanja na amejenga na anataka kuhamishia biashara zake huku. Mimi kila siku nilikuwa namkatisha tamaa, lakini naona si rahisi. Najua akija huku atataka tuishi pamoja. Nifanye nini hapo? Kwa kweli nahisi kuchanganyikiwa. Maana akijua watoto wengine si wake, sijui kama ataendelea kuwa na mimi. Naomba ushauri, nifanye nini hapa?

Credit: Iddi Makengo
 
Back
Top