ACHA KUMUANGALIA VIBAYA NA KUWA NA WIVU JUU YA MTU ANAYEKUSAIDIA KWA SABABU ANAMSAIDIA MWINGINE VITU VIKUBWA KULIKO WEWE

Minga

New member
ACHA KUMUANGALIA VIBAYA NA KUWA NA WIVU JUU YA MTU ANAYEKUSAIDIA KWA SABABU ANAMSAIDIA MWINGINE VITU VIKUBWA KULIKO WEWE.

Wivu una chanzo.
Hauji kwa bahati mbaya.

Mara nyingi hutokea pale mtu anapojihisi kwamba thamani yake haitambuliwi vya kutosha, au jitihada zake haziangaliwi kwa jicho la kipekee.

Lakini wivu huu unakuwa wa ajabu pale unapouelekeza kwa mtu anayekusaidia & kujitoa kwako kwa njia yoyote ile.

Labda nikwambie kwanini unateswa na wivu huu angali ni wewe ndiwe unayesaidiwa, huna moyo wa kuridhika unataka wewe tu ndio uwe kipaumbele chake.

1::Unajilinganisha kupita kiasi

Tatizo unapima msaada uliopokea kwa kutumia vipimo vya mtu mwingine...

Hapa huwezi kukwepa kutojiona huthaminiwi hata kama unayesaidiwa ni wewe, hii kitu huwasahaulisha wengi kwamba wanasaidiwa na hujikuta ni kama kile kitu walistahili wao. Acha hii kitu.

2::Kutokuwa na shukrani

Shukrani ni kinga ya ndani inayopunguza makali ya wivu.Ukikosa moyo wa kushukuru, utaona kila jambo kama haujatendewa haki.

Hata kama umepewa kitu bure utaanza kuona mapungufu yake, utaanza kujilinganisha na wengine, kwasababu moyo wako haujui kuthamini kile unachopewa.

3:: Unaangalia sana ulivyopungukiwa.

Tatizo lako unaangalia sana vile ulivyokosa na kupungukiwa huku unasahau ulivyonavyo, hii hali inakufanya ushindwe ku appriciate hata ule msaada uliopewa.

Unapofokasi sana na ulivyopungukiwa huwezi kufurahia hata vile ulivyo navyo au unavyopewa.

Ikabili hii hali na kisiwepo chochote cha kukufanya ukose furaha

Soma kitabu cha furaha yako haitapotea tena.Leo nitakupatia kwa offer sh.7000.

E.M✍️
 
Back
Top