Masudi kipanya na mohamed said katika historia ya miaka mia

Mohamed Said

New member
KUTOKA DHUHR HADI ALASIRI NA MASUDI ''MTU SPECIAL'' KIPANYA

Leo ilikuwa siku makhsusi yaani special sana kwangu kwa kuwa katika chumba kimoja na Masudi Kipanya na vijana wake ''sharp'' wa Clouds Plus.

Hiki kwa hakika si chumba kwa maana ya chumba kama tulivyozoea bali ni Maktaba ya Elite Bookstore Mbezi Samaki.

Masudi Kipanya alinikaribisha ndani ya Maktaba hii nadhifu sana si kwa kuangalia na kusoma vitabu bali kwa ajili ya kufanya kipindi cha televisheni.

Mvua kubwa iliyonyesha kipindi cha adhuhuri kwa kiasi cha saa moja hivi ilitosha kunionya kuwa ile ilikuwa tahadhari kwangu kwa mfano wa ''thunder and lightning,'' (radi na kimulimuli) katika mchezo wa Mcbeth kuwa mchana wangu hautakuwa wa kawaida.

Kwa muda wa saa mbili Masudi Kipanya akitembea katika mengi niliyopata kuandika katika historia ya Tanganyika alinirudisha nyuma miaka 100 hapa hapa Dar es Salaam ya 1920s akitaka kujua maisha ya wazee wangu waliosukuma gurudumu la historia ambayo si wengi wanaifahamu.

Masudi Kipanya kama ni mchezo wa masumbwi nitamwita, ''South Paw,'' kwa jinsi alivyonitaabisha na maswali ya kushtukiza na wakati mwingine kunibana nisema nisiyopenda kusema na wakati mwingine kunitoa kwa haraka katika niliyodhani yangefaa kusemwa.

Muda ulikwenda kwa haraka sana jua likazama nikiwa sina habari na hatujamaliza safari yetu ya miaka 100.
Screenshot_20220417-190846_Facebook.jpg

Pichani ni Masoud Kipanya (kulia) pamoja na Mohamed Said (kushoto)​
 
Hakika ni jambo jema kupata muda wa kubadilishana mawazo na vijana.

Maana bila shaka kukutana kwako na Masoud Kipanya kuna kitu cha kujifunza. Na huu ni mfano mzuri kwetu.
 
Hakika ni jambo jema kupata muda wa kubadilishana mawazo na vijana.

Maana bila shaka kukutana kwako na Masoud Kipanya kuna kitu cha kujifunza. Na huu ni mfano mzuri kwetu.
Alinihoji kwa saa mbili na tukafanya vipindi vinne vilivyorushwa na Clouds Plus.
Alitaka kumjua ni nani Abdul Sykes katika TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Iko video ya kwanza hapa, ''Siasa Kama Zilivyokuwa 1950s.''
 
Ni jambo jema sana,

Hata mimi binafsi nina shauku hiyo siku moja kukutana na Mzee Mohamed Said ili kubadilishana mawili matatu hivyo.

Natumaini muda ukifika nitafanikiwa kwa hilo.
 
Back
Top