Ludmilla na mkewe Brunna Gonçalves wote wawili wakiwa ni Wanawake wamefanikiwa kupata mtoto

Kasomi

JT Founder
Screenshot_20250517-120038~2.png

Mwanamuziki maarufu wa Brazil, Ludmilla, na mkewe Brunna Gonçalves wote wawili wakiwa ni Wanawake wamefanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kike, aliyezaliwa tarehe 14 Mei 2025 huko Miami, Marekani. Mtoto huyo amepewa jina la Zuri.

Wenzi hao walitangaza habari hiyo kwa furaha kupitia mitandao ya kijamii, wakielezea kuwa ujio wa Zuri umeongeza upendo wao na kuwafanya wajisikie kama wako "peponi"

Ludmilla na Brunna walitangaza ujauzito wao kwa mara ya kwanza mwezi Novemba 2024, na baadaye walifanya sherehe kubwa ya kutangaza jinsia ya mtoto mwezi Desemba, ambapo walifichua kuwa wanatarajia kupata mtoto wa kike .

Jinsi Walivyopata Mtoto: Wenzi hao walitumia mbinu ya kisasa ya uzazi iitwayo ROPA (Recepção de Óvulos da Parceira), ambayo ni maarufu miongoni mwa wanandoa wa jinsia moja wa kike.

Katika mbinu hii Ludmilla alitoa yai lake (ovum).Yai hilo lilifanyiwa fertilization in vitro (IVF) kwa kutumia mbegu za kiume kutoka kwa mtoaji (donor).Embryo iliyopatikana ilihamishiwa kwenye mfuko wa uzazi wa Brunna, ambaye ndiye aliyebeba mimba hadi kujifungua.

Mbinu hii iliwapa nafasi zote mbili kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata mtoto: Ludmilla kama mama wa kibaolojia na Brunna kama Mama aliyebeba mimba, Brunna alielezea kuwa ilikuwa ndoto yake kubwa kuwa mjamzito, na Ludmilla alikubali kwa furaha kuwa sehemu ya safari hiyo.

Kwa kuwa Mtoto wao Zuri amezaliwa nchini Marekani, atakuwa na uraia wa Marekani kwa kuzaliwa. Pia, anaweza kupata uraia wa Brazil kupitia wazazi wake, hivyo kuwa na uraia pacha.
 
Back
Top