Kasomi
JT Founder
Abdulaziz Abubakar Chende Maarufu kama Dogo Janja mgombea Udiwani kata ya Ngarenaro kupitia Ccm Jijini Arusha anatuhumiwa kumpiga Risasi tatu mwanafunzi wa Kidato Cha nne shule ya Sekondari sombetini Bakari Khalifa kwa madai ya kuwa kijana Huyo ni kibaka.
Wakizungumza katika eneo la Tukio ambalo kijana huyo amepigwa Risasi mdogo wake Bakari pamoja na wananchi wa mtaa wa Simanjiro wamesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa tano walisikia milio ya risasi tatu walivyotoka wakamuona Dogo janja akiwa na bastola mkononi na vijana wengine wanne wakiwa na mapanga mkononi wakingia kwenye gari aina ya Alphard Nyeusi na kuondoka kwa kasi.
Mmoja wa majirani hao ambaye ni kanali Khamisi alitoa gari yake na kumkimbiza kijana aliyejeruhiwa kwa risasi hospital kwa ajili ya matibabu kabla ya kuondoka alieleza kuwa amepigwa. RISASI na dogo janja akimtuhumu kwamba yeye ni kibaka wakati akiwa na mdogo wake Baada ya tukio hilo kijana aliyepigwa risasi alipewa pf 3 kwa ajili ya matibabu lakini baada ya muda aliporudi polisi alishikiliwa akiwa na mama yake mdogo mpaka sasa.
Dada wa kijana huyo amesema licha ya kumpelekea mdogo wake chakula walifukuzwa polisi na hawaruhusiwi kumuona ndugu yao licha ya kuwa na majeraha ya Risasi.
Hata hivyo mpaka sasa jeshi la polisi halijatoa taarifa yeyote juu ya tukio na simu zao zilita bila kupokelewa.
Hata hivyo familia hiyo ambayo mtoto wao amepigwa Risasi amekamatwa Mama yake mdogo na mdogo wa kijana huyo aliyepigwa Risasi.