Advertise here

Somo Ukiambiwa zamani...

Emmanuel

New member
Ukiambiwa Dr Salim Ahmed Salim aliteuliwa balozi nchini Misri akiwa na miaka 22 halafu ukalinganisha na vijana wa leo wenye elimu na umri huo utaona kama vile tunarudi nyuma badala kwenda mbele...

Na ukiambiwa miaka ya 1970 hadi 1990 nchi yetu ilikuwa na vyama vya ushirika kila mkoa vyenye nguvu kabisa vya kuweza kununua mazao ya wakulima bila matatizo halafu ukalinganisha na Sacco's za sasa hivi za wasomi wetu utaona tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele...

Ukiambiwa zamani nchi yetu bila wasomi ilikuwa na viwanda vikubwa kama: Tanganyika Packers,Mutex Mwatex, Kiltex, Urafiki,Ufi,n.k na mashirika ya umma yenye mafanikio makubwa sana lakini baada wasomi kuyaongoza ndo yamefilisika kabisa,isipokuwa viwanda vya Pombe na vileo ndio vinashamiri; lazima utakuwa na mashaka na elimu za vijana wetu ...

Ukiambiwa zamani kwamba mzazi yeyote alikuwa anaweza kumchapa mtoto mkosefu ambaye siyo wake na mtoto akienda kulalamika kwao anaongezewa kipigo utajua maadili yanazidi kuporomoka kuliko zamani ...

Ukiambiwa zamani vijana walikuwa wanachaguliwa wachumba na wazazi wao na wanakubaliana kuoana na ndoa zinadumu tofauti na sasa vijana wanachunguzana miaka mitano lakini wakioana ndoa hazidumu utagundua watu wa zamani hawakuwa na elimu lakini walikuwa na busara kuzidi wa sasa hivi...

Ukiambiwa kuwa mama wa zamani alikuwa anaenda shambani na mtoto mgongoni anapitia maji kichwani na kuni kwapani, lakini wa siku hizi hata kupika ugali hawawezi utaelewa kuwa Siku hizi wamebaki wanawake majina tu wanatamani kutumia computer kupika wali ...

Ukiambiwa zamani wazee wa kimila walikuwa na maadili sana tofauti na viongozi wa dini wa siku hizi..utagundua dini zimekuja kwa nia nzuri lakini zinatumiwa vibaya....

*Au wewe unaonaje?* Kwamba baada ya miaka kadhaa ijayo tutakuwa na wasomi wengi wa mitandaoni lakini watendaji wa mikono hawatakuwapo.
 
Back
Top