Kasomi
JT Founder
Leo Oktoba 17, dunia inaadhimisha siku ya kumsamehe mpenzi wako wa zamani yaani Ex. Hii ni siku maalum ya kuhamasisha watu kuachilia maumivu na chuki za zamani kutoka kwa mahusiano yaliyovunjika.
Siku hii haikusudii wewe kurudiana na mpenzi wako wa zamani wala kutuma ujumbe, bali ni fursa ya kusamehe na kupata amani ya moyo. Waanzilishi wa siku hii wanasema kuwa kusamehe ni zawadi ya kihisia unayojipa mwenyewe, si kwa ajili ya mtu mwingine.
Tafiti kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins University huko nchini Marekani, zinaonyesha kuwa watu wanaosamehe kwa dhati hupata faida nyingi za kiafya, ikiwemo kupungua kwa msongo wa mawazo, shinikizo la damu la chini, usingizi bora, na hali ya furaha ya kudumu.
Haya tuweke maoni hapa kwa wapenzi wetu wa zamani, umemsamehe?