Advertise here

Mahojiano: Lissu Ambana kwa Maswali Shahidi wa Serikali

Kasomi

JT Founder
Lissu Ambana kwa Maswali Shahidi wa Serikali
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

1758546306436.jpg

TUNDU Lissu ameendelea kumbana shahidi kwa maswali ya dodoso kulingana na ushahidi alioutoa tarehe 6 Aprili 2025 ambapo shahidi wa kwanza wa Jamhuri, Bagyemu, aliendelea kutoa maelezo katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Kwanza: Ushahidi Kuhusu Video Clip ya Jambo TV

Lissu: Wakati unaongoza hiyo timu, ulisema tarehe 6 Aprili ulimtafuta Mkurugenzi wa Jambo TV John Marwa?
Bagyemu: Siwezi kukutajia ila nilipata namba ya kiongozi wa Jambo TV, sikujua jina lake kama ndiye Marwa.

Lissu: Huyu kiongozi wa Jambo TV uliyemtafuta ulimuomba akupatie video clip halisi iliyochukuliwa kwenye mkutano?
Bagyemu: Ni kweli.

Lissu: Ni kweli huyo kiongozi alikwambia mfanyakazi yupo Dodoma?
Bagyemu: Ni kweli, alinipa namba ya simu pia ya huyo mfanyakazi wake.

Lissu: Ni kweli namba hiyo ulimpa DCP Ng’anzi?
Bagyemu: Ni kweli nilifanya hivyo.

Lissu: Ni kweli Ng’anzi alimpatia Andrew Churu yule polisi mwingine?
Bagyemu: Hilo sijui kwakweli.

Lissu: Ni kweli tarehe 7 Aprili DCP Ng’anzi alisema amempata huyo aliyerekodi?
Bagyemu: Ndio, ni sahihi kabisa.

Lissu: Na memory card nayo alikwambia imepatikana?
Bagyemu: Ni kweli aliniambia hivyo.

Lissu: Ni kweli DCP Ng’anzi alikwambia kwamba memory card na card reader yake vitaletwa siku hiyo hiyo na Andrew Churu ofisini kwako?
Bagyemu: Ni sahihi kabisa.

Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba siku ya tarehe 7 Aprili Andrew Churu alisafiri kutoka Dodoma hadi ofisini kwako na kufika usiku?
Bagyemu: Ni sahihi kabisa.

Lissu: Je alikuja na hizo card na vitu vingine?
Bagyemu: Ni sahihi alikuja navyo na pia alikuja na hati ya makabidhiano.

Lissu: Acha kiherehere, hiyo hati sijakuuliza. Je, ulisoma maelezo ya P hiyo tarehe 7 ulivyoletewa?
Bagyemu: Ni kweli nilisoma.

Lissu: Kwa vile ulisoma, kweli au si kweli huyo P alisema ni yeye ndiye alirekodi mkutano na akarusha kwenye akaunti ya Jambo TV?
Bagyemu: “Kuwa mimi nakumbuka mkutano...” (kabla hajamalizia, Wakili Katuga anasimama).

Wakili Katuga: Haya maelezo sio ya kwake shahidi, kwa hiyo asiulizwe.

Lissu: Anajibu shahidi mwenyewe kuwa alipelekewa maelezo ya huyo P na akasoma, na maelezo hayo ndio yanasema nani alichapisha?

Jaji: Msomee wewe tafadhali.

Lissu: P anasema ni wao Jambo TV ndio walikuwa wanarusha na wao ndio walirekodi.

Lissu: Je, mimi ndiye niliyesambaza na kuchapisha?
Bagyemu: Ndio, ni wewe uliyechapisha.

(Wakili wa Serikali Katuga) amesimama na kuiomba mahakama waende mapumziko:
“Tunaomba twende kwenye health break, tutaendelea.”

Lissu: Sawa twende maana huyu shahidi ili nimalizane naye nahitaji siku zingine kama mbili au tatu.

Majaji wakaahirisha shauri mpaka saa tisa mchana kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Sehemu ya Pili: Ufafanuzi Kuhusu Kosa la Uhaini

Lissu: Katika ushahidi wako ulisema kwa ufahamu wako maneno niliyosema ni uhaini?
Bagyemu: Kweli nilisema.

Lissu: Ulisema lengo waisikie Watanzania na wasio Watanzania?
Bagyemu: Ndio nilisema hivyo.

Lissu: Kuita waandishi wa habari ni kosa la uhaini?
Bagyemu: Itategemea.

Lissu: Soma kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code, kama kinasema kuita waandishi ni kosa la uhaini?
Bagyemu: (Anasoma kimya kimya) — Hayo maneno hayapo, hayajasemwa kwenye sheria.

Lissu: Je, kwenye maelezo yako kuna mahali ulisema kuwa mimi kuita waandishi wa habari ni uhaini?
Bagyemu: Hakuna, sijaandika hivyo.

Lissu: Katika kuonesha maneno yangu yalikuwa ya kihaini ni kutoa na kuchapisha taarifa hizo mtandaoni?
Bagyemu: Ni kweli nilisema.

Lissu: Hizi video kwa vile ziko mtandaoni, je litakuwa ni kosa la cyber?
Bagyemu: Ndio, litakuwa hata kosa lingine.

Lissu: Kosa langu ni kutoa na kuchapisha, hii kutoa ni uttering?
Bagyemu: Ndio.

Lissu: Soma kifungu cha 3 cha Cybercrime Act — maana ya “uttering”?
Bagyemu: Nimeona ipo, inasema “communication.”

Lissu: Sasa communication sijashitakiwa nayo.
Bagyemu: Uttering haipo sawa.

Lissu: Kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code — kuna neno uttering?
Bagyemu: Hakuna kabisa.

Lissu: Neno publish maana yake nini kwa mujibu wa Cybercrime Act?
Bagyemu: Publishing means distributing, transmitting, disseminating, printing or offering for sale.

Lissu: Kwa maelezo yako, aliyepeleka kwenye mtandao wa Jambo TV ni nani?
Bagyemu: Mfanyakazi wa Jambo TV.

Lissu: Kwa mujibu wa ushahidi wako, aliyerusha maneno hayo ni nani?
Bagyemu: Ni wewe Lissu na P.

Lissu: Kama nilichapisha mimi na P, kwanini P hajashitakiwa?
(Lissu akisema kwa msisitizo): “Tutafika tu, mmezoea kuwasingizia watu kwa kesi za uongo.”

Sehemu ya Tatu: Hoja Kuhusu Jambo TV na Uhalali wa Taarifa

Lissu: Umesema mimi ndiye niliyewaalika waandishi wa habari tarehe 3 Aprili?
Bagyemu: Ndio, ni wewe.

Lissu: Je, niliwaita kwa njia ya simu?
Bagyemu: Sijui.

Lissu: Barua?
Bagyemu: Sijui.

Lissu: Je, nilitangaza magazetini?
Bagyemu: Sijui.

Lissu: Ulimhoji Katibu Mkuu wa Chadema kuhusu utaratibu wa kualika waandishi?
Bagyemu: Sikumuhoji.

Lissu: Je, Amani Gorugwa ulimhoji?
Bagyemu: Sikumohoji.

Lissu: Brenda Rupia ulimuita lakini hakuja?
Bagyemu: Ndio.

Lissu: Basi hujui walialikwaje, hujui nani aliwaalika, ila unadai ni mimi?
Bagyemu: Mimi sijui kwa kweli.

Lissu: Waeleze majaji kama mimi ni mmoja wa wakurugenzi wa Jambo TV.
Bagyemu: Sina uhakika.

Lissu: Je, mimi ni mwandishi wa habari wa Jambo TV?
Bagyemu: Sina uhakika.

Lissu: Ni kweli video zilipatikana kwenye mtandao wa Jambo TV?
Bagyemu: Ni kweli.

Lissu: Je, nina password za Jambo TV?
Bagyemu: Sijui kama unazo.

Lissu: Kitaalamu, mtu asiye na password anaweza kuweka video?
Bagyemu: Sijui uliwekaje.

Sehemu ya Nne: Ushahidi Mwingine na Masuala ya Sheria

Lissu: Hizi video clip zilifanyiwa uchunguzi wa kitaalamu wa cyber forensic?
Bagyemu: Ni kweli.

Lissu: Kahaya ndiye alifanya kazi hiyo?
Bagyemu: Ndio.

Lissu: Maelezo yake umeyasoma?
Bagyemu: Sikuyasoma.

Lissu: Maelezo ya Andrew Churu umeyasoma?
Bagyemu: Sijasoma.

Lissu: Maelezo yako uliandikiwa na nani?
Bagyemu: Niliandika mwenyewe.

Lissu: Je, kabla ya kuandika uliomba ushauri wa kisheria?
Bagyemu: Sikuomba.

Lissu: Nani aliyekukanya au kuthibitisha?
Bagyemu: Ni mimi mwenyewe.

Sehemu ya Tano: JKT na Utambulisho wa Kijeshi

Lissu: Ulisema mimi nina kiapo cha JKT na nilitoa kinyume cha kiapo changu?
Bagyemu: Ni kweli.

Lissu: Je, wewe umewahi kwenda JKT?
Bagyemu: Hapana.

Lissu: Nilikwenda JKT kambi gani?
Bagyemu: Mafinga na Itende.

Lissu: Ulikuwepo?
Bagyemu: Hapana.

Lissu: Kama nilienda miaka 39 iliyopita, mimi ni mwanajeshi?
Bagyemu: Wewe ni askari wa akiba.

Lissu: Je, Katiba inataja askari wa akiba?
Bagyemu: Hapana.

Lissu: Je, umeleta hati ya kiapo changu cha utii?
Bagyemu: Hapana.

Sehemu ya Mwisho: Uratibu wa Upelelezi

Lissu: Ni kweli National Prosecution Act inasema DPP anapaswa kujulishwa kama kosa lina adhabu ya kifo?
Bagyemu: Ndio.

Lissu: Je, ulitoa taarifa kwa DPP kati ya tarehe 4 hadi 8 wakati nakamatwa?
Bagyemu: Hapana.

Lissu: Je, DPP aliratibu upelelezi huu?
Bagyemu: Hapana

(Wakili wa Serikali Renatus Mkude): Mheshimiwa Jaji, muda umeenda, tunaomba kuahirisha hadi kesho kutokana na barabara kuwa mbovu.

Lissu: Waheshimiwa Majaji basi tuwakubalie, nami niende nikale. Huyu bado nahitaji kuendelea naye.

Majaji wamekubaliana na kuahirisha shauri hilo hadi kesho, tarehe 8 Oktoba saa tatu asubuhi, ambapo Tundu Lissu ataendelea kumuuliza shahidi huyo maswali ya dodoso.
 
Kesi ya lisu haitofautiani na ile ya Mbowe zote zina idhalilisha jamuhuri kwamba Haina watu competent na hawatoshi kwenye nafasi zao!!

Walau ku balance na ku spin kupotea kwa Humphrey pole pole ambayo ni blunder nyingine na uvivu wa kufikiri ni Bora wamwachie Lisu kupoza upepo Kwa sasa!!

Ishu ya pole pole ilihitaji spinning TU hasa kitengo Cha propaganda kingetumika vizuri sana kusaidia ku neutralize hoja zake!!

Lakini kitendo Cha sintofaham kinachoendelea kumhisu pole pole kinaamsha Ari ya chuki Kwa wapiga kura ndani na nje ya chama!hasta wastaafu wanajua Sasa kwamba wanaweza tekwa kama kuku na kuchinjwa bila polis Wala vyombo kujua na watapoteza Imani na mtia Nia kuhusu usalama wao!!

Naendelea ku support kauli mbiu ya Chama "KAZI na utu tunasongambele" lakini Cha kujiuliza mbona tumeshindwa kuonyesha utu Kwa wanachama wenzetu kama kina Humphrey pole pole nyakati hizi!!

"Oktoba tuta tick tukipata fursa ya kuiona ballot paper na tuta tickambaye tunahisi anaweza leta usalama wa raia na kukomesha unyakuo wa kutekwa ghafla"
 
Nazani kumtoa Lissu wanaogopa sababu akitoka atakuja na upepo wake hivyo mgombea wa sisiemu anaweza nyang'ang'wa point Tatu.

Maana jamaa anaupepo na nazani Madam Prez anatembea na kauli ya mzalau mwimba... Ndo maana hataki asogelewe hii ndo hata akina Mpina wamekosa hivyo
 
Kutick hakupo kama wewe mwenyewe utu hatuoni kauli mbiu umekosa uhalisia
 
Nazani kumtoa Lissu wanaogopa sababu akitoka atakuja na upepo wake hivyo mgombea wa sisiemu anaweza nyang'ang'wa point Tatu.

Maana jamaa anaupepo na nazani Madam Prez anatembea na kauli ya mzalau mwimba... Ndo maana hataki asogelewe hii ndo hata akina Mpina wamekosa hivyo
Madam anajua fika watz wamemchoka ila anafosi mambo tuuu, hata akiingia kiti kitakuwa cha moto sana na ataua wengi ili abaki salama
 
Back
Top