Tundu Lissu kufikishwa mahakamani leo jumatatu

Kasomi

JT Founder
1024

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maeneleo (CHADEMA), Tundu Lissu, anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo, Jumatatu Mei 19, 2025, wakati kesi inayomkabili ikiendelea.

Lissu anakabiliwa na kesi mbili ambazo ni kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa YouTube na uhaini.

Awali, kesi hizo zilikuwa zinasikilizwa kwa njia ya mtandao, lakini Mei 6, 2025, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geofrey Mhini, alitoa uamuzi wa kumtaka Lissu kufika mahakamani kwenye kosa la kuchapisha taarifa za uongo badala ya kuendelea kwa njia ya mtandao huku kesi ya tuhuma za uhaini ikiendelea kwenye mtandao.
 
Back
Top