john achila mukumwa
Member
Ushujaa wa rohoni haujalishi uzoefu wako
Roho au moyo wa ushujaa
Ili ipatikane lugha rahisi ya kuwakilisha roho ya mwanadamu ambayo haionekani kwa macho, neno moyo hutumika kama mbadala kwenye ushujaa wa roho.
Mungu aliyekuwa na wana wa Israel jangwani, yuko pamoja nasi hata ukamilifu wa uhodari. Yuko pamoja nasi, na zaidi ya yote amemuachilia Roho wake Mtakatifu mno akae ndani yetu, na kutuongoza na kutufariji na kutupa nguvu wakati wa mahitaji. Kwa msingi huo, hatupaswi kusitasita wala kuhofia au kuogopa jambo lolote zaidi ya kuwa na moyo wa ushujaa.
1Wakoritho 16:13 inasema “Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe Hodari”.
Hatuwezi kuwa na mafanikio yoyote yale katika mwili na katika roho kama hatutakuwa na moyo wa ushujaa. Maneno ya Mungu kupitia Musa mtumishi wake kwa wana wa Israel yalikuwa “iweni na moyo wa ushujaa, simameni kiume” (Kumb la Torati 31:6).
Sina shaka kama jinsi ambavyo watu wote hawana shaka kuwa Mungu akisema yuko pamoja nasi basi yuko pamoja nasi kweli kweli. Yeye siyo kama rafiki zetu ambao wanaweza kukuambia tuko pamoja mzee, lakini zinapotokea changamoto katika maisha yetu wanayeyuka.
Roho au moyo wa ushujaa ni nini
Kuwa na moyo wa ushujaa katika lugha ya Kiibrania ilikuwa na maana ya kusimama kiume, au kuonyesha uanaume kweli kweli. Yaani kuwa na uwezo wa kufanya jambo lenye kutisha kwa werevu. Au kwa weledi, au nguvu ya kukabiliana na jambo lenye kutisha au kuogopesha au hatarishi, kwa ushujaa mkubwa. Ni uwezo wa kuamua kupambana na maumivu, tishio, mateso, hatari, au jambo lenye kutisha bila woga wowote, wala hofu yoyote. Ni uwezo wa kuthubutu kufanya au kukabiliana na jambo ambalo kwa akili za kibinadamu linaonekana kuwa gumu, lakini kwa imani unaona kuwa utalifanikisha iwe mvua ama jua.
Kibiblia, ushujaa huu unaambatana na kumuamini Mungu. Ndiyo maana Mungu ameambatanisha na kuwa pamoja nasi, na ili kuifikia ile ndoto, au lile tumaini au ile ahadi, Waebrania 10:35-36 inasema, “Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi”.
Kwa hiyo, tunapokuwa na moyo wa ushujaa ndipo tunapoweza kupokea thawabu kuu na kutimiza mapenzi ya Mungu na kuifikia ile ahadi au ile ndoto au lile lengo tulilo nalo, ambalo ni mapenzi ya Mungu. Katika ulimwengu huu vilevile, ili tuweze kufikia malengo yetu ya kawaida, hatuna budi kuhakikisha kuwa tunavaa moyo huu wa kijasiri.
SIFA ZA MTU MWENYE MOYO WA USHUJAA
1. Hapaswi kujihurumia
Moyo wa ushujaa na mafanikio yake hauwezi kuwepo kwa mtu anayejihurumia.
Wengi tumeweza kuangamiza nafsi zetu kwa sababu ya kujihurumia. Tumeshindwa wakati mwingine kufikia ndoto kadhaa kwa sababu tuna tabia ya kujihurumia.
2. Hapaswi kuchoka
Ili tufanikiwe katika maisha yetu lazima tuwe na mioyo migumu, hatupaswi kuchoka.
3. Hapaswi kuogopa kubaki peke yake
Moja ya mambo ambayo yanaweza kumvunja mtu moyo ni pamoja na kuachwa peke yake. Watu wengi hukata tamaa wanapobaki wenyewe. Mtu mwenye moyo wa ushujaa wakati wote anakuwa tayari kupambana hata anapobaki peke yake.
4. Hapaswi kupoteza nguvu zake
Kumbuka kuwa tunazungumzia moyo wa ushujaa; hivyo hapa hatuzungumzii kamwe nguvu za kimwili. Shetani anajua kuwa ili aweze kutukwamisha anajua wazi kuwa anapaswa kuujeruhi moyo. Moyo wako ukishakubali kujeruhiwa, basi umepoteza nguvu zako, hata kama una miguvu kiasi gani. Ushindi wa mtu hautokani na muonekano wake wa kimwili bali mtazamo wake wa moyoni. Yako mambo ambayo ibilisi anaweza kuyatumia kujeruhi mioyo yetu ili tupoteze nguvu zetu. Watu wenye moyo wa ushujaa hawapaswi kupoteza nguvu zao.
5. Hapaswi kuwaogopa wanadamu
Inasemekana kuwa mwanadamu ndiye mnyama anayetisha zaidi kuliko wanyama wote. Ili uwe na moyo wa ushujaa ni lazima ujifunze kutowaogopa wanadamu. Wao ndio viumbe tunaoshindana nao katika mambo yote; ndio wanaoweza kutumiwa na Mungu kwa mafanikio yako. Lakini vilevile, ndio wanaoweza kutumiwa na ibilisi wakasimama kama vikwazo ili usiweze kutoboa katika maisha yako.
Usiwaogope wanadamu: Kumbukumbu la Torati 3:21-22 “Nikamwamuru Yoshua wakati huo, nikamwambia, Macho yako yameona yote aliyowatenda Bwana, Mungu wenu, wale wafalme wawili, navyo ndivyo atakavyoutenda Bwana kila ufalme huko uvukiako. Msiwache, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, ndiye awapiganiaye”. Ili uwe shujaa Mungu anataka kuona ukimuogopa yeye tu peke yake, wale tunaoshindana nao ni wanadamu tu kama sisi.
6. Hapaswi kuogopa kushindwa
Kushindwa ni sehemu ya maisha. Tunajifunza mengi mazuri kwa watu walioshindwa kuliko hata walioshinda.
1Wakoritho 1:26-31: “Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi
wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana".
7. Haogopi kukataliwa
Watu wengi wanajiepusha na mambo fulani kwa sababu wanaogopa kukataliwa. Mtu anaweza kuona binti mzuri na akampenda, lakini akashindwa kusema chochote kwa sababu anaogopa kukataliwa.
Tuangalie asili ya ushujaa wa rohoni, ambao wakati mwingine tunadhani mpaka tuwe na uzoefu ndiyo tuweze kufanya makuu kwa Mungu.
Mfano wa Waisraeli na Washami
Wakati fulani Taifa la Israeli liliingia katika hali mbaya ya njaa isiyokuwa ya kawaida, hadi kufikia hatua ya baadhi ya watu kuchinja watoto wao na kuwala (2Wafalme 6:28-29). Hiyo ilikuwa ni kwa sababu ya kuzungukwa na maadui zao wenye nguvu kwa muda mrefu, walioitwa Washami. Washami walikuwa ni watu walioishi katika nchi ijulikanayo kama Syria kwa sasa. Hivyo Waisraeli wakashindwa kuingiza au kutoa chochote ndani ya mji kwa muda mrefu.
Hivyo hali ikawa mbaya sana. Mfalme akafunga mji, hawajui cha kufanya, watu wamepaniki, wanakula vitu visivyopaswa kuliwa, kiasi kwamba hata ‘mavi ya njiwa’ tu yalikuwa yanauzwa kama chakula.
Hebu piga picha, taifa kubwa kama hilo, linakumbwa na janga la njaa kali namna hiyo, hadi askari wake wazoefu wa vita, wanatetemeka na kujificha ndani ya mji, kwa sababu walijua wakitoka tu ni kifo. Na hiyo hali ndiyo maadui zao walikuwa wanakiisubiri: aidha watoke nje wawaue, au wafe na njaa humo ndani. Hivyo hali ilikuwa ni ya kutisha sana.
Siku moja, Nabii Elisha, alipewa unabii na Mungu, na kuambiwa kuwa siku ya kesho yake, chakula kitapatikana na kuuzwa kwa bei ya chini kiasi ambacho haijawahi kutokea hapo kabla. Yaani ni sawa na kuambiwa kuwa siku ya kesho, gunia la mahindi, litauzwa kwa shilingi 1, wakati unatambua kuwa, leo, bei ya soko haipungui shilingi 70,000 kwa gunia.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Israeli, Mungu alipompa Elisha unabii huo akaambiwa siku ya kesho yake, chakula kitauzwa kwa bei ya chini kabisa.
Kilichotokea ni nini
Kulikuwa na wakoma wanne, waliokuwa nje ya mji. Wakoma hawa walitengwa na taifa, kwa sababu ilikuwa ni kuwa watu walioathirika na ugonjwa huu watengwe mbali na makazi ya watu, ili wasije kuleta maafa hayo ndani ya jamii. Ni sawa na ugonjwa wa kipindupindu ukilipuka, tunavyouona siku hizi, hadi karantini zinawekwa ili ugonjwa usisambae. Ndivyo ilivyokuwa kwa ukoma pia, kwa wakati ule.
Piga picha, watu hawa wakoma, walikuwa ni wagonjwa, hawana wa kuwatazama, na zaidi sana wamekuwa dhaifu kwa njaa kali. Lakini tunaona walishauriana jambo kisha wakafanya uamuzi, ambao ndio ulikuwa ukombozi wa taifa la Israeli.
Tuone maandikio yanavyosema:
2Wafalme 7:1 Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria. 2 Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula,
3 Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? 4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. 5 Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu.
6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.
7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao.
8 Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha.
9 Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme.
10 Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha. 11 Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme.
Ni nini kimejificha hapa?
Siri tunayoona, ambayo imejificha nyuma ya hawa wakoma wanne, ni kwamba, PINDI TU WALIPOAMUA KUFANYA UAMUZI WA KUJITOA MUHANGA KWA AJILI YA MAISHA YAO, NA KUANZA MWENDO, KUELEKEA KAMBI YA MAADUI, KUMBE KULE KWENYE KAMBI YA WASHAMI, WANASIKIA KAMA JESHI KUBWA SANA LA MAASKARI LINAWAFUATA. Hivyo wakakimbia kwa kasi sana, na kuacha kila kitu nyuma. Lakini wale maaskari wa Kiisraeli waliokuwa wazoefu wakati huo wamejifungia ndani ya mji hawadhubutu kuchukua hatua.
Yaani, watu waliokuwa dhaifu na wagonjwa, ndio waliowafukuza Washami na kuleta ukombozi Israeli. Watu wanne tu, waligeuka kuwa jeshi la maaskari elfu, rohoni.
Mfano wa Yonathani na Wafilisti
Katika kitabu cha 1Samweli 14:6, tunaona kuwa Yonathani alifanya ujasiri wa kwenda kupigana na Wafilisi, wakiwa wawili tu: yeye na yule kijana aliyekuwa akimbebea silaha. Aliseama: “Basi, Yonathani akamwambia yule kijana aliyemchukulia silaha zake, Haya! Na twende tukawavukie ngomeni hao wasiotahiriwa; yamkini BWANA atatutendea kazi; kwa maana hakuna la kumzuia BWANA asiokoe, kwamba ni kwa wengi au kwamba ni kwa wachache”. Wakapanda mlimani Kwenda kupambana na Wafilisti, wakawaua Wafilisti 20, wao wakiwa wawili peke yao.
Hiyo inatufundisha nini?
Sisi pia, pale tunapoamua kufanya jambo kwa ajili ya Mungu, bila kujali hali zetu au udhaifu wetu, tufahamu kuwa jeshi la shetani linaogopa na kutetemeka kuliko sisi tunavyoweza kudhani.
Daudi alijijua kuwa yeye si mtu wa vita, hana uzoefu wa vita, hawezi kutumia upanga wala mkuki, lakini yeye ndiye aliyesimama, kinyume na Goliathi, na kulifukuza jeshi lake lote. Daudi alikuwa shujaa wa kiroho.
Hupaswi kujidharau
Ikiwa umeokoka leo, au jana, usiseme mimi sina uzoefu, au sijui biblia vizuri. Kama kushuhudia watu wenye dhambi ambao wengine wameshindwa, wewe nenda, usisubiri mpaka mchungaji wako afanye hivyo. Hujui kuwa wakati huo ndio Mungu amekuchagua kuwa sababu ya ukombozi kwa wengine. Hivyo, popote unapojiona hukidhi vigezo, fahamu kuwa, rohoni ndiyo unakidhi. Unajiona hustahili, jua tu kwa Mungu unastahili. KUWA NA IMANI, chukua hatua, usingoje-ngoje.
Ushujaa wa kiroho hauhitaji uzoefu
Na hakika, rohoni, shetani atatoweka kama jeshi la Washami lilivyotoweka kupitia NGUVU ZA KIROHO ZA WAKOMA WANNE TU. Wakoma wale hawakuwa na uzoefu wo wote, bali walikuwa na nguvu za kiroho za kufanya uamuzi wa kiroho.
NGUVU HIZO ZA KIROHO NDIZO ZILIGEUZWA NA MUNGU, KUWA SAUTI KAMA JESHI KUBWA SANA LA MAASKARI LINAWAFUATA WASHAMI. Hivyo wakakimbia kwa kasi sana, na kuacha kila kitu nyuma. Kilichowakimbiza Washami siyo uzoefu wa upanga na vita, bali ni ushujaa wa kiroho.
Hivyo, tumia karama uliyopewa ndani yako kuujenga ufalme wa Mungu. Popote pale unapojiona unafaa, basi tumia nafasi hiyo kumtangaza Kristo kwa wengine. Mungu anakuona. ATAGEUZA USHUJAA WAKO WA KIROHO KUWA MAFANIKIO YAKO BARAKA ZAKO.