Øffïçïäl Dülly Tz
New member
Story.........PENZI LA MTEKAJI
Present.....Simulizi Za Dully
Mtunzi.....Official Dully Tz
WhatsApp...0628924768
Mkasa..wa..kusisimua
Sehemu..Ya..{03}
(Seaeon two)
ILIPOISHIA.....
Walimuona mtu akija kwa mwendo wa kuyumba huku mwili wake ukiwa na majeraha mengi yaliyokuwa yakivuja damu hivyo Mr Mbega alipomtazama vizuri yule mtu alimuona akiomba msaada ila bado hawakumtambua alikuwa ni nani na ni nini kimemfanya aumie kiasi hicho....ENDELEA....
Kila mmoja alibaki ameduwaa sio Mr Mbega wala kijana wake yaani wote kwa pamoja walikuwa wakimtazama mtu huyo aliekuwa akiwaomba msaada huku akisogea walipo wao, lakini kabla hajawafikia alianguka chini na kutulia,
Haikufahamika alikuwa amekufa au amepoteza fahamu lakini Mr Mbega alifungua mrango ili kushuka ila kijana wake Godwin alimshika mkono ishara ya kumtaka asishuke na kwenda kutoa msaada kwa mtu huyo ambae awamfahamu wala hawajui amepatwa na nini.
"Baba unataka kwenda wapi, unataka kwenda kumpa msaada unamjua mtu yule, je kama ni watu wabaya alafu wanakutega unafikiri si itakuwa rahisi kukushika.!?"
Godwin alizungumza kumwambia baba yake huku akionekana mwemye umakini wa hali ya juu kuhusu jambo hilo ambalo anataka kulifanya baba yake.
"Hapana sifikirii kama ni mtu mbaya ila naamini atakuwa ni mtu wa kawaida anahitaji msaada kwahiyo twende tukampatie msaada"
Mr Mbega baada ya kuzungumza hayo alifungua mrango na kuteremka lakini Godwin hakutaka kushuka kumfuata baba yake ila alikuwa akimsindikiza kwa macho mpaka alipofika kwa mtu yule.
"Yaani mzee anataka matatizo usiku huu, unaweza kumsaidia mtu ambae humjui, huwezi jua ni mtu mbaya anataka kukufanyia ubaya alafu kirahisi tu unasogea.!!"
Godwin alijikuta akijisemea mwenyewe lakini mwisho ilibidi nae afungue mrango na kushuka kisha alijongea taratibu mpaka alipo baba yake.
"Duuh inamaana ndio amejeruhiwa kiasi hiki.!?.
Godwin aliuliza kwa mshangao baada ya kufika alipo mtu huyo na kumuona jinsi alivyoumia sehemu mbali mbali za mwili wake.
"Hebu acha kushangaa sana na huu sio muda wa kupoteza tumchukue, tumpakie kwenye gari safari ianze kuelekea hospital huenda akasaidika"
"Mh baba sifikiri kama atapona maana kwa jinsi alivyoumia labda itokee miujiza ya Mungu lakini bila hivyo hawezi kupona, damu nyingi sana amepoteza.!!"
Godwin alikuwa kizungumza huku akisogea zaidi na kumgeuza mtu huyo maana wakati anaanguka sura yake ilikuwa imeelekea chini.
Hakuwa mwingine ila alikuwa ni Brey, na huyo ndiye alikuwa ni mtekaji ila hawakufahamu kama ndiye mtu aliemteka Karina.
Walimchukua na taratibu sana walimpakia kwenye gari yao kisha safari ilianza kuelekea hospita lakini wakiwa njiani Brey alirejewa na fahamu na kujikuta ndani ya gari ila hakufahamu alikuwa anapelekwa wapi.
"Mnanipeleka wapi naombeni mnishushe hapa.!?"
Brey alizungumza kwa sauti ya chini maana hali yake bado ilikuwa mbaya sana.
"Hebu subiri bro tunaelekea hospital, bado kama dakika kumi na tano tutakuwa tumefika kwahiyo ondoa shaka kila kitu kipo sawa"
Godwin alimtuliza huku akitazama saa yake na muda ulisomeka ni saa nane na nusu usiku kuelekea saa tisa.
"Hapana sihitaji kwenda hospital naomba simamisheni gari tafadhali nataka kushika hapa hapa"
Brey kwa mara ya pili aliomba tena kushuka ili aondoke zake maana alijua yeye ni mtu anae tafutwa kama pesa kwahiyo kama atapelekwa hospital basi itakuwa rahisi sana kushikwa.
"Ok sawa hakuna shida"
Mr Mbega hakuwa na namna kukubali ombi la Brey na kusimamisha gari kisha Brey aliteremka japo kwa taabu na kutokomea kwenye kiza.
Godwin na baba yake hawakuwa na namna hivyo waliwasha gari yao na kuondoka zao huku mioyoni mwao wakiwa na furaha baada ya Karina kupatikana akiwa mzima.
Huku upande wa pili Karina alifikishwa kwao na polisi kisha alikabidhishwa kwa mama yake ambae alikuwa na furaha sana baada ya kumpata binti yake kipenzi akiwa mzima wa afya kabisa.
"Mwanangu jamani nafurahi sana nimekupata yaani nilikuwa na wasiwasi sana kuhusu wewe, kama nisingekupata sijui hata ingekuwaje usiku wa leo"
Mama Karina alizungunza kwa hisia huku machozi ya furaha yakimtoka lakini polisi baada ya kumkabidhisha Karina kwa mama yake waliaga na kuondoka zao.
"Usijali mama nimerudi sasa nikiwa mzima kabisa, lakini baba na kaka Godwin wako wapi?"
"Naamini wapo njiani wanarudi maana niliwapiga simu na kuwaambia umepatikana kwahiyo nafikiri muda si punde...."
Mama Karina hakumaliza kuongea walisikia honi ya gari hivyo walijua lazima atakuwa baba na Godwin wamewasili.
Ni kweli walikuwa wao, baada ya geti kufunguliwa na gari kuingia ndani walishuka na kumfanya Karina afurahi na kuwakimbilia kisha aliwakumbatia kwa furaha maana alikuwa na shauku sana kuwaona.
"Oh jamani nashukuru Mungu binti yangu upo mzima, lakini una hata kovu jamani.!?"
"Hapana baba nipo kama nilivyoondoka wala usijali"
Basi furaha ilirudi upya katika familia hiyo lakini upande wa Brey alikuwa akitembea kwa kujivuta na mwisho alifika katika nyumba moja na kuanza kugonga geti.
Hazikupita dakika nyingi geti lilifunguliwa na alitoka mwanaume mmoja lakini mwanaume huyo alipomuona Brey alimshangaa sana.
Si kwamba alimshangaa kwakuwa hamfamu, lahasha alikuwa akimfahamu kwa undani zaidi ila alikuwa akimshangaa kwa jinsi ambavyo aliumia.
"Brey nini kimekukuta mtu wangu.!?"
Mwanaume huyo alimuuliza Brey huku akitazama huku na kule kisha alimtaka Brey aingie ndani ikiwezekana ampatie huduma na kumuondoa kwenye hali ya hatari aliyokuwa nayo kwa wakati huo.
Alimfikisha mpaka ndani na kumketisha sebuleni, alipiga simu mahali na baada ya dakika kama kumi alifika nesi ambae alipomuoma Brey alishamgaa.
"Brey nini kimekukuta jamani.!?"
Nesi huyo baada ya kumuona Brey alimuuliza kwa mshangao juu ya hali yake na ilionesha alikuwa akimfahamu sana maana alimtaja mpaka kwa jina.
Brey hakuwa na neno la kujibu zaidi ya kuwa kimya maana hata hayo maswali aliona yanamzingua kwa jinsi alivyokuwa na hali mbaya.
Basi huduma kwa upande wake ilianza kisha alichomwa sindano ya usingizi na kutundikiwa dripu ya maji ambayo ingeweza kumsaidia hali yake kutengemaa na kurudi kama zamani.
***********
Asubuhi kunapambazuka ilikuwa ni asubuhi tulivu sana, asubuhi ya kuvutia kwa kila mmoja pia ilikuwa ni asubuhi iliyojaa furaha katika familia ya Mr Mbega, walikusanyika mezani kupata kifungua kinywa kama kwaida yao kabla ya kila mmoja kuelekea kwenye majukumu yake.
Wakati wanapata kifungua kinywa television ilikuwa on hivyo ilikuwa ikirusha habari live lakini kwenye habari hizo kuna jambo Mr Mbega na kijana wake Godwin waliliona na liliwaacha mdomo wazi kabisa
Ilikuwa ni taarifa ikimuhusu Brey ambae alitoroka mikononi mwa polisi hivyo baada ya picha yake kuoneshwa kwenye television iliwafanya washangae maana alikuwa ni mtu ambae walimpa msaada.
"Baba yule mwanaune tuliempa msaada ndio huyu tunaemuona hapa kwenye television au watakuwa wanafanana tu.!?"
Godwin alikuwa haamini anachokiona na hata Mr Mbega alikuwa haamini maana mtu wanauona hapo ndiye mtu ambae walimpatia msaada.
"Ndiye huyu yaani aisee daaah kwahiyo tulimsaidia mbaya wetu bila kufahamu yaani kama ningefahamu mapema basi moja kwa moja ningempeleka polisi.!!"
"Lakini baba yote ulitaka wewe, mimi nilikwambia tusimpatie msaada lakini ukakaidi na kumsaidia ila kumbe alikuwa ni adui yetu mkubwa sana.!!"
Mr Mbega na kijana wake walikuwa hawaamini macho yao lakini kuto kuamini kwao hakukubadilisha kitu maana jambo lilikuwa tayari limetokea na walimpatia msaada mtu ambae alimteka Karina bila wao kufahamu wakidhani huenda ni mtu wa kawaida ambae hakuwa na tatizo.
"Jamani mimi naona sasa niwaache muendee kuzozana na kushangaa, natakiwa niwahi duscussion kwahiyo tutaonana baadae Mungu akipenda"
Karina baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa aliaga ili kuondoka lakini baba yake alimtaka asbiri.
"Hapana huwezi kwenda mwenyewe maana linaweza kukukuta jambo jingine kwahiyo nitakupeleka mimi"
"Lakini baba jamani usiwe na wasiwasi rafiki zangu wapo hapo nnje wananisubiri kwahiyo hakuna baya lolote ambalo litaweza kunikuta usijali kabisa"
Karina hakutaka kuendelea kusimama alipiga hatua mpaka mrangoni kisha aliigeukia familia yake na kuiaga mwisho aliondoka zake.
Alitoka mpaka nnje na kukuta rafiki zake wawili wakimsubiri hivyo alichukua gari yake na kuwapakiza kisha safari ilianza kuelekea chuo huku story za hapa na pale zikiendelea hasa kuhusu tukio la kutekwa kwa karina.
"Yaani Zebeda mimi nione hivi hivi tu Karina kama Karina ila ni mjanja sana mimi maana jana kabla polisi hawajafika kunipatia msaada nilikuwa tayari nimetumia ujanja kumlalisha yule jambazi na hata kama polisi wasingefika basi ningeondoka kiulaini kabisa"
"Mh kwahiyo unajiona kama shujaa lakini najua ulikuwa unalia hahahaa maana wewe kwa uwoga unaongoza"
Basi story zilikuwa zikisindikiza safari na mwisho walifika katika chuo ambacho ndicho walikuwa wanasoma, walipaki gari na kushuka lakini kila mwanafunzi alikuwa kimtazama Karina maana taarifa za jana kutekwa kwake haikuwa siri.
"Karina shoga yangu umekuwa maarufu ghafla yaani watu wote wanakutazama wewe.!!"
Ilikuwa ni kauli ya rafiki wa karina ambae alifahamika kwa jina la Rahma lakini Zubeda nae aliunga mkono na kujikuta wakicheka.
Lakini hawakutaka kufuatilia macho ya watu yaliyokuwa yakiwatazama ila waliongozana mpaka class ambapo walikuta bado mwalimu wa kipindi hajaingia hivyo ilibidi waketi sehemu zao na story zilianza kama unavyojua wanawake wakiwa sehemu moja asilimia kubwa lazima watapiga story.
Wakiwa hawana hili wala lile aliingia mvulana mmoja akiwa na kundi lake la wenzake sita na wote walikuwa wanafunzi lakini walikuwa ni wanafunzi wanaoogopeka sana chuoni hapo hasa huyo kiongozi wao ambae alikuwa na skendo za ukatili sana.
Mwanaume huyo baada ya kuingia alisimama mbele ya wanafunzi wote na kuanza kuangaza macho yake huku na kule lakini mwisho alijikuta akitabasamu baada ya macho yake kutua sehemu aliyokaa Karina na rafiki zake.
Ilionesha dhahiri alikuwa akimtafuta Karina hivyo baada ya kumuona alisogea mpaka pale na kuwataka Zubeda na Rahma kuondoka ili apate nafasi ya kuzungumza na Karina.
"Habari yako mrembo?"
Kijana huyo alianza kwa salamu lakini Karina aliitika akiwa na hofu kubwa sana.
"Ah mrembo mbona unaitika kwa wasiwasi jamani alafu wewe ni mgeni hapa chuo maana katika wanafunzi wote wa mwaka wa mwisho hasa mabinti wewe sura yako ni ngeni kwangu"
"Ndio mimi ni mgeni nimekuja hapa hata week bado kwahiyo ndi..ndio ni mgeni hapa.!!"
Karina alijibu huku akiwa na hofu maana alikuwa akisikia story za mwanaume huyo.
"Ok mimi naitwa Hanson sijui nani mwenzangu?"
"Mi...mimi naitwa Karina.!"
"Oh wow jina zuri sana kama wewe ulivyo mzuri lakini naweza kupata namba yako ya simu nahitaji uwe partner wangu au unasemaje?"
Hanson alimpatia Karina simu yake ili aandike namba yake, na Karina alipokea bila ubishi kisha aliandika namba yake na kurudisha simu kwa Hanson ambae aliisave ile namba na kurudisha simu mfukoni.
"Ok Karina acha niende class kwangu ila usiku mida ya saa mbili nitakupigia kwahiyo uwe hewani"
Hanson alikuwa akifanya mambo kibabe sana hivyo kwakuwa alikua akiogopeka chuo kizima basi Karina nae ilibidi amuogope kwa usalama wake.
*************
Taratibu sana siku ziliyoyoma na hatimae mwezi ulikata, hali ya Brey ilikuwa njema sasa na alikuwa akiishi hapo kwa rafiki yake mpaka alipokuwa salama na hali yake kitengemaa kabisa.
Usiku mmoja ilikuwa ni jumaapili kuamkia jumaatatu Brey alikuwa akipata chakula na rafiki yake lakini hawakuacha kuongea mambo mengi kuhusu masomo maana Brey licha ya kuwa mtu hatari na aliekuwa anajishughulisha na uhalifu ila alikuwa ni mwanafunzi wa chuo ambae alikuwa akisomea mambo ya biashara.
"Sasa Brey kama ambavyo ulisema utaachana na mambo ya uhalifu utawekeza nguvu kwenye kusoma basi fanya kweli maana siku hizi ukisoma basi elimu hiyo hiyo ndio itakuwa hazina yako sasa kesho unatakiwa kuamke asubuhi uripoti chuo"
"Sawa bro Stan lakini si tayari umefanya uhamisho na kila kitu.!?"
"Ya kila kitu tayari ni wewe tu kuripoti lakini acha nikwambie kitu kimoja mdogo wangu, hebu achana na ile sura maana imekuwa inatafutwa sasa"
"Yah hata mimi nimeona niachane nayo maana sura ile nilikuwa nikiivaa wakati naenda kufanya uhalifu kwahiyo sasa acha nitumie sura yangu halisi"
"Yah achana nayo kabisa kwa sasa nataka usome naamini kila kitu kitakuwa sawa mdogo wangu"
Waliongea mengi Brey na kaka yake lakini mwisho kabisa waliagana na kila mmoja aliingia chumbani kwake kujipumzisha maana muda ulikuwa umekwenda sana yapata kama saa tano usiku kuelekea sita kamili.
Usiku ulikuwa mrefu sana lakini urefu wake haukufanya kushidwe kupambazuka, asubuhi kulipambazuka salama na Brey alijiandaa kisha alimuaga rafiki yake ambae anamchukulia kama kaka yake kisha alipatiwa funguo ya gari na safari ilianza kuelekea chuo akiwa na muonekano mpya usoni mwake na sio ule muonekano wa kihalifu ambao alikuwa akijivisha sura bandia.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kuripoti chuoni hapo na mazingira ya chuo yalimvutia sana hivyo alipeleka gari mpaka kwenye parking na kushuka kisha aliripoti mpaka ofisini kwa mkuu wa chuo ambae alimpatia taratibu zote na kumtaka aende kwenye darasani ambalo alimpatia maelekezo.
Alifika na kukuta masomo yanaendelea hivyo aliingia na kuripoti kwa mwalimu kisha alijitambulisha na kuoneshewa sehemu ya kukaa lakini wanafunzi wengi walikuwa wakimtazama hasa wa kike maana alikuwa akivutia sana.
"Ok jamani hebu acheni kumshangaa tuendeleeni na kipindi.!!"
Mwalimu ilibidi azungumze na wote kwa pamoja walitii lakini Brey sehemu aliyokaa alikuwa sambamba na Hanson maana Hanson nae alikuwa akisomea biashara.
"Oya dogo hapo utakaa alafu utatoka maana kuna mtu atakuja kwahiyo ukiona teacher ametoka basi na wewe utainuka hapo"
Hanson alizungumza kibabe na Brey ilibidi akubali hakutaka kuleta utata.
Huku upande wa Karina ambae alikuwa akisomea udaktari alikuwa akiwaaga wenzake maana hakutaka kuendelea kusomea udaktari ila ilibidi aende kwenye masomo ya bishara na alifanya hivyo kwa kulazimishwa na aliemlazimisha alikuwa ni Hanson.
"Jamani kwahiyo una uhakika na maamuzi yako au kuna mtu kakulazimisha huenda labda ni baba au mama.!?"
"Hapana Rahma ni maamuzi yangu mwenyewe kwasababu baba yangu ni mfanyabiashara mkubwa na ana makampuni mengi kwahiyo kama unavyoona baba yangu umri umeenda na anahitaji msaidizi japo kaka Godwin yupo lakini hawezi kuendesha makampuni mwenyewe kwahiyo acha nikasomee tu biashara ili nikihitimu huu mwaka uliobaki najua nitakuwa na ujuzi kwa kiasi fulani"
"Ok sawa aina shida lakini uwe unakuja kututembelea darasan kwetu.!?"
"Ok sawa msijali"
Karina aliwaaga rafiki zake kwa majonzi na kuelekea kwenye kozi mpya ambapo humo ndipo alipokuwa Hanson.
Brey akiwa hana ili wala lile, akiwa busy kukusanya baadhi ya notes ghafla alishangaa akipigwa kofi na alipomtazama aliempiga alikuwa ni Hanson, ilibidi amuulize alimpiga kwa kosa gani.
"Kwani si nilikwambia hii sehemu ya mtu na mwenyewe akija utampisha, basi ndio huyo ameingia kwahiyo tafuta sehemu ya kukaa kabla sijakuharibu"
Hanson aliongea kwa utemi na kumfanya Brey abaki akimtazama tu, ilibidi achukue kila kilicho chake na kusimama lakini alipotupa macho mbele kumtazama huyo mtu ambae aliwekewa nafasi na Hanson alistaajabu kumuona Karina na alimkumbuka ndiye binti aliesababisha kuingia mikononi mwa polisi....ITAENDELEA.....
- Je unafikiri nini kitafuata hapo maana mambo sasa yameanza kupamba moto, unafikiri Brey atafanya nini na je Karina atamtambua Brey ndiye mtu aliemteka ilhali yupo na muonekano mwingine..!!?
Hakuna mtu anaefahamu ila majibu utayapata ndani ya sehemu ya 04 na tufahamu ni nani ambae ametokea kumpenda mtekaji...yaani mambo ni moto kabisaa..????