Advertise here

PENZI LA KULAZIMISHA 01

omaryjr15

New member
PENZI LA KULAZIMISHA 01
????
????
????

321128687_850382499496864_5030839512561082868_n-jpg.399

Kama umeipenda stori ya HUSNA, basi hii ni kali kuliko hiyo!!!
Ni katika familia moja ambayo ni maskini sana yenye bibi na mjukuu wake wa kike aitwae Rashma.
Rashma ni mschana aliyelelewa na bibi yake kwasababu wazazi wake walifariki kipindi yupo mdogo sana ivyo bibi ake alichukua jukumu la kumlea na elimu yake iliishia kidato cha nne alipasi vizuri lakini pesa ya kumsomesha ilikosekana kutokana na bibi kutokua na uwezo wa kumsomesha.
Baada ya kukaa nyumbani kwa kipindi ilimradhimu kuhangaika kutafuta ajira viwandani ili kumsaidia bibi ake majukumu.
Siku hiyo alienda kwenye kiwanda kimoja maarufu kwa ajiri ya kutafuta ajira alionana na baadhi ya wafanyakazi wa kiwandani.
Kwa kuwa walikuwa wengi hivyo walipangiwa siku ya kwenda kufanya interview.
*****
Upande mwingine anaonekana kijana mmoja wa kimarekani kwenye asili ya Afrika Shedrak akiwa anarejea nyumban kutoka chuoni.
Baada ya kuingia ndani uso kwa uso alikutana na mama yake(Madam Asia) ambaye alikaa sebren alionekana ni mtu mwenye mawazo kiasi baada ya salamu mama akavunja ukimya
Mama: afadhali ulivyorudi maana nilikua nakungoja wewe tu.
Shedrack: Enhe kuna nini mama angu?
Madam Asia: Kesho nina safari ya kwenda Tanzania kuangalia biashara zangu
Shedrack: Yani mama umerudi juzi tu unataka kuondoka tena!.
Madam Asia: Nitakaa mwezi mmoja tu mwanangu.
Shedrack: Sawa mama mimi nakuombea usafiri salama.
Madam Asia: Nashukuru mwanangu nawapenda na ubaki salama na wadogo zako uwasisitizie kuhusu masomo (shedrack ana wadogo zake wa kiume wawili mmoja anaitwa sheby mwingine ambaye ndio mdogo wa mwisho anaitwa sulleyman)
Shedrack: Kuhusu hilo ondoa shaka mama angu
Basi siku ilipita na mama yao aliondoka walibaki wanaume watupu na dada wa kazi aitwaye Zai baada ya kubaki peke hao walikua na uhuru wa kufanya chochote.
Shedrack ambaye ndio mkubwa alipanga kuandaa bonge ya part nyumbani kwao kwa ajiri ya kumvesha mchumba yake pete alianza kuarika baadhi ya marafiki zake.
******
Siku ya pili yake asubuh Rashma alijiandaa kwenda kwenye Interview alikutana na wenzake wengi baada ya kufika zamu yake iliwadia aliingia akiwa na wasiwasi mno baada ya kuingia
Kwenye chumba cha interview alionana na (Supervisor)Msimamizi akaulizwa baadhi ya maswali mda Rashma anaendelea na interview aliingia mmama ambaye alionekana mtu mwenye pesa zake baada ya yule mama kuingia msimamizi alimtoa Rashma nje ili azungumze na yule mgeni lakini yule mama alimuangalia sana Rashma.
Msimamiz: karibu bosi.
Madam Asia: Asante
Msimamiz: za safari naona umekuja kimya kimya .
Madam Asia: Nzury tu vipi biashara inasemaje? kampuni inaendeleaje?
Msimamiz: Mauzo yapo vizuri tu ila kuna baadhi ya mikataba tumeivunja kutokana na mambo yaliyotokea nyuma kwahiyo tunatafuta wafanyakazi wengine watakaokaa nafasi zilizo wazi.
Madam Asia: Sawa tutaongea baadae kuhusu hilo.... yule mschana aliyetoka apa ana shida gani?
Msimamizi: Ni mmoja wao kati ya wanaohitaji kazi hapa.
"Anaonekana ni mdogo kiumri sidhani kama ataweza..... Ok kesho nitamuhitaji ofisini kwangu.
Yule msimamizi alimuita Rashma akamwambia kuwa kesho anatakiwa aonane na bosi wao.
*******
Siku iliyofuata Rashma alijiandaa kwenda kuonana na bosi alivyofika akaelekezwa ofisi ilipo akaingia na kukaribishwa kwenye kiti.
"karibu binti mrembo... Alisema Madam baada ya Rashma kuingia ndani.
"Asante shikamoo". Alisalimia Rashma
”Marihaba... Nadhani umeitikia wito."
"Ndio bosi.
"Usiniite bosi mimi nimekuita apa kama mwanangu hivyo sitapenda uniite bosi."
Alisema hivyo kwa sauti ya ukalimu.
"Sawa mama nisamehe kwa hilo.
"Usijali ningeomba unipe background ya maisha yako kwa ufupi binti yangu maana umri wako ni mdogo sana kipi kimekusibu kuja kutafuta kazi humu.
Rashma alianza kujielezea bila kuacha kitu "mimi naitwa Rashma umri wangu miaka 20 naishi na bibi wazazi wangu walifariki kipind nipo mdogo sana hivyo bibi yangu ndio mlezi pekee aliyobaki.
Elimu yangu ni kidato cha nne matokeo yangu yalikua mazuri lakini nilishindwa kuendelea kutokana bibi kutokua na uwezo wa kunisomesha.
"Historia yako inanisikitisha sana mwanangu lakini naahidi kukusaidia kwani nilikupenda tangia nilivyokuona". Alisema hivyo yule mmama huku akifuta futa machozi ambayo yalianza kumlenga
"Asante sana mama.
"Utakua teyar kuolewa na kijana wangu si kwamba nataka kukusaidia kwasababu uolewe na kijana wangu ila nimevutiwa sana na wewe na hata yeye akikuona nadhani atakupenda tuu.
Rashma: (Alikaa kimya hakujibu kitu)
"Okay nakupa mda ukiwa umepata jibu utanijulisha nimekupendaa mno usiniangushe
Baada ya hapo alimkabidhi Rashma Business card yenye namba yake huku akimisisitiza kuwa asikatae basi alirudi
kwao alimuhadithia kila kitu bibi yake.
Akamsihi binti ake akubali kwani ni bahati kubwa sana kwake ukizingatia bibi yake uzee nao ulikuwa unamsumbua kuumwa kila siku na pesa ya matibabu ndio hakuna.
******
Sherehe ya Shedrak iliwadia bas siku ya sherehe vinywaji vya kila aina vilikuepo watu walienjoy na Shedrack akamvesha pete mchumba wake Cath.
Cath ni binti mrembo sana ila ni mwenye dharau sana yote ni kwasababu kwao wana uwezo kifedha.
Baada ya tafrija kuisha shedrack na Cath walikua chumbani wanaongea
"Yaani sikuamini kama utanifanyia kitu kama hiki mpenzi wangu.
"Yote kwasababu nakupenda kweli mpenzi wangu.... Alisema shedrak huku akichezea nywele za mwanamke huyo.
Majibu ya Shedrak yalimfanya Cath afurahi alimkumbatia mpenzi wake wakaanza kuchokozana apa na pale mwisho wa siku wakaangukia kwenye ulimwengu mwengine )
Asubuh Shedrack akiwa amekaa na wadogo zake sheby na sulle wakaanza story
"vipi broo Cath alifurahia suprise yako?
Aliuliza Sheby.
"Yeah hakuamini ilikuwa ni bonge la suprise.
"Ila mimi na yule Cath sijui kama tutaelewana ana mashauzi mengi.... Alisema hivyo sulle.
"Heshima iwepo ni shemeji yako yule... Alisema Shedrack kumjibu Sulle.
"Sawa bhana tutaona ndio umuoe tena...
Shedrack: Aah mimi pale kuoa lazima.
Mda wanaendelea na story zao Mama yao alipiga simu akawasalimia lakini akamwambia Shedrack.
"Kuna jambo nataka kuongea na wewe baadae nadhani naweza nikakupigia sitotaka pingamizi lolote kutoka kwako....
Alijibu shedrack "Hamna shida mama yangu siwezi kukupinga kwa chochote.
Jioni yake Mama Shedrack alimpigia simu mwanae na kuanza kuzungumza.
Mama: Nilikuambia kuna jambo nataka kuzungumza na wewe nadhani huu ndio muda muafaka wa kulizungumzia hilo jambo
"Nakusikiliza mama". Alisema Shedrack akiwa na shauku ya kutaka kujua.
"Si unajua umri unaenda mwanangu....
Shedrack alijibu "Nalijua hilo.
Aliendelea kusema "Hivyo basi nataka uoe ndani ya mwezi mmoja tu.
Shedrack Alifurahi sana baada ya kusikia hivyo kwa kuwa alikuwa anajua vyema angemuoa Cath wake akauliza "Lakini mbona ghafla hivyo mama!?.
"Wasiwasi wako uko wapi kila kitu nitashughulikia mwenyewe na mschana nishakutafutia
Shedrack Alishtuka sana baada ya kusikia taarifa hizo "Whaat jambo kama hilo haliwezekani mama yangu hapana siwezi kuoa mtu nisiyemjua.
Mama yake alisema bila wasiwasi "Utamjua tu akija mimi mzazi wako siwezi kukuchagulia kitu ambacho si sahihi kwako Una wiki moja tu ya kujifikiria.
Basi mama shedrack akakata simu. Shedrack alivulugwa sana.
Hakuwaficha wadogo zake aliwaadithia kinachomsibu.
"ujui mama amewaza nini ivyo mimi nakushauri ukubali bro.. Alisema Sheby
"Una kichaa nini na yule mschana wa watu nilomvesha pete!?.
Alidakia Sulle kana kwamba yanamuhusu "Kwani pete ndio ndoa kaka wewe oa tu au kama unamuona huyo Cath wako ndio bora kuliko mama usituombe ushauri.
Wote wakanyanyuka na kumuacha peke yake ana mawazo mengi sana kuhusu ndoa aliyoambiwa ikiwa ana mwanamke wake.
******
Basi ilipita wiki Rashma alimwambia Mama shedraki kuwa amekubali kuolewa.
Mama Shedy alifurahi sana kwani alimpenda sana Rashma hakujua kwanini ametokea kumpenda.
"Usijali kijana wangu ana miaka 28 na kuhusu shughuli ntaghalamikia mimi na shughuli itafanyika Amerika cha kufanya nataka nikaongee na mlezi wako
Mama Shedrack alionana na bibi waliongea sana wakafahamiana kiundani.
"Mjukuu wangu una bahati sana yani yule Mama tajiri ameahidi kunitibia... Alisema bibi kumwambia Rashma baada ya yule mama kuondoka.
Rashma alionekana kuwa na hofu sana. "Bibi mwenzako naogopa mwanaume mwenyewe simjui.
"Ondoa shaka mtaenda kujuana huko huko mimi furaha yangu kukuona mzima mjukuu wangu.
****
"Vipi Broo umeamua nini!?.
Aliuliza Sheby huku akimtazama Shedrack aliyekuwa busy na simu yake.
"Sielewi Nimechanganyikiwa tu.
"Huna chaguo jengine si unajua mama anavyotujali na kutupenda sidhani kama anaweza kukuchagulia mtu ambaye sio sahihi kwako.
"Unataka kusema mama yuko sahihi kwa anachonifanyia?.
"Yeah hujui ameona nini ni mtu mzima anaelewa anachokifanya.
"Hata kama nitakubali huyo Mschana atajuta kuingia kwenye maisha yang.................
ITAENDELEA,

full story inapatikana whatsapp 0629980412
 

Attachments

  • 321128687_850382499496864_5030839512561082868_n.jpg
    321128687_850382499496864_5030839512561082868_n.jpg
    40.6 KB · Views: 396
Last edited by a moderator:
Back
Top