Advertise here

Tutaweza kuongea na kuelewana na Aliens kupitia hesabu na Fizikia

Kasomi

JT Founder
012345.jpg

Kama itatokea siku tukakutana na viumbe wa angani (aliens), huenda tusiweze kuongea nao kwa sauti au maneno kama tunavyofanya binadamu, lakini hisabati na fizikia zitakuwa ndiyo lugha yetu ya kwanza.

Hizi ndizo sababu kwanini mawasiliano yatawezekana:

Sheria za Ulimwengu ni Moja.

Hata kama alien anaishi kwenye galaksi nyingine, anafuata sheria zilezile za asili tunazofuata sisi.
Mfano: Nguvu ya mvuto (gravity) inafanya kazi vilevile kote ulimwenguni.

Atomu: Atomu ya Hidrojeni hapa Duniani ni sawa na atomu ya Hidrojeni kwenye sayari yao. Kama wameweza kutengeneza chombo cha angani hadi kutukuta, basi lazima wawe wameelewa kanuni za kimahesabu ili kufanikiwa kusafiri angani.

Lugha" ya Picha (Geometry).

Hesabu si namba tu, bali ni maumbo, duara, pembe tatu, na mistari sambamba (parallel lines) ni dhana ambazo hazibadiliki.

Tukichora Theorem ya Pythagoras (a^2 + b^2 = c^2) kwenye mchanga, kiumbe chochote chenye akili kitatambua kuwa huyo aliyechora anaelewa uhusiano wa kijiometri.

Mantiki ya Binary (0 na 1)

Hii ndiyo ngazi ya chini kabisa ya mawasiliano. Ni mfumo wa "Ndiyo" au "Hapana." Kwa kutumia mfululizo wa ishara hizo, tunaweza kuanza kufundishana msamiati mdogo mdogo. Kwa mfano, ishara ya 1+1=2 kwa kutumia milio, kisha 2+2=4. Huu ni mwanzo wa kujenga uelewa wa pamoja.

Changamoto kubwa haitakuwa namba, bali itakuwa utamaduni na hisia. Tunaweza kuelewana kuhusu hesabu, lakini inaweza kuwa vigumu sana kuelezea dhana kama "upendo," "huzuni," au "utani" kwa sababu hizi ni sifa za kibailojia za binadamu.
 
Back
Top