KUMRUDIA X

Minga

New member
Kuna hili kosa wengi hulifanya na wengi wao huishia kujuta tu.

Mtu aliyekuumiza na kukuacha anapojaribu kurudi tena kwenye himaya yako haupaswi kuwa mwepesi wa kumruhusu tu kama kwamba hakijatokea kitu.

Unamruhusu et kwa sababu ;

::Mwanzo ulimpenda sana.
::Amejieleza sana kiasi cha wewe kumuonea huruma.
::Amekuahidi kubadilika au amekuoa ahadi zingine tamu.

Ukimsamehe mbwa mwitu kwa kukuibia kuku usishangae kesho akirejea na kukuibia mbuzi.

Wengi wameumizwa mara ya pili kwa sababu tu walipenda sana au kwa sababu ya huruma.

Usimwamini mtu kuwa atabadilika et kwa sababu ameomba msamaha...

Msamaha haubadili tabia ya mtu, wala yeye kukupa ahadi tamu haimaanishi ndio amekuwa mwaminifu.

Mara nyingi ukiona mtu aliyeondoka anarudi tena kwako ujue hajarudi kwa sababu yako ila amerudi kwa sababu yake.

Sasa huu sio upendo ila ni ubinafsi , unampokeaje mtu mwenye moyo wa ubinafsi?

Msamehe kwa ajili ya amani ya moyo wako ila mtu huyu asiwe sehemu ya mzunguko wako wa karibu tena.

Watu hawabadiliki kwa ajili yako, watu hubadilika kwa ajili yao.

Kama alikokuwa yamemshinda basi wewe usiwe jalala la kupokea walioachwa.

Mrudishe alikokuwa kapambane na hali yake.

Moyo unatakiwa kuwa na upendo lakini pia usipungukiwe hekima, kwa sababu hata mlango mzuri ukikosa kufuri kila mtu ataingia na kutoka anavyotaka.

Matapishi hayarudishwi kinywani hata yakiwa ni ya chakula kitamu kiasi gani.

Tumia uwezo wako mzuri wa maamuzi kuchagua upande bora wa maisha yako

E.M✍️

E.M✍️
 
Back
Top