Kasomi
JT Founder
Matairi mengi ya kisasa yana namba ambazo hubeba taarifa muhimu na tofauti lakini watu wengi huwa hawana uelewa wa namna ya kuzisoma, kuzitafsiri na kuelewa maana ya namba hizo.
Leo tuanze na alama ya kiwango cha kasi (speed rating), inayoonyesha kasi ya juu ambayo tairi linaweza kuhimili bila kupoteza uimara wake.
Jinsi ya kutambua kiwango cha kasi, tazama ubavuni mwa tairi, utaona namba zikiwa kwenye mfumo huu: P205/60R16 82H.
Herufi ya mwisho, “H” ndiyo speed rating ambayo hubadilika kulingana na aina ya tairi na aina ya gari.
Kila herufi inaendana na kasi maalum:
T– hadi 190 km/h (magari ya familia)
H – hadi 210 km/h (magari ya kawaida ya kasi)
V – hadi 240 km/h
W – hadi 270 km/h
Z – zaidi ya 240 km/h (magari ya michezo ya kasi kubwa)
Viwango hivi hupimwa maabara chini ya hali maalum (tairi lililojaa hewa vizuri, gari likiwa salama, hali nzuri ya hewa).
Katika matumizi halisi, mambo kama uchakavu, shinikizo la hewa, hali ya barabara na mzigo vinaweza kupunguza uwezo huo.
- Tumia kiwango cha kasi kinachopendekezwa na mtengenezaji wa gari
- Hakikisha matairi yote manne yana kiwango sawa
- Epuka kuendesha zaidi ya mipaka ya kisheria licha ya uwezo wa tairi
Speed rating si tu kipimo cha kasi, bali ni kigezo muhimu cha usalama na utendaji wa gari. Kuchagua tairi sahihi kunaweza kuboresha uendeshaji na kupunguza hatari barabarani.
Hakikisha unafahamu speed rating ya matairi ya gari lako, ambayo mara nyingi huandikwa kwenye sehemu ya ndani ya mlango wa dereva au kwenye 'manual' ya gari.