Advertise here

MONKEY wa PAKISTAN aliyejifanya chizi Kumbe JASUSI hatari wa INDIA

Kasomi

JT Founder
MONKEY wa PAKISTAN aliyejifanya chizi Kumbe JASUSI hatari wa INDIA
1000707681.jpg

Katika vitu vinavyofurahisha saana kuvisoma ni stori za kijasusi yaani huwa zinavutia mno ni kama movie lakini unaiona kwa kuisoma tu

Basi moja ya kitu kilichonifurahisha ni story ya jasusi aliyeitwa Ajit Doval wengine humuita James Bond wa India
India na Pakistan ni majiran wanapakana na kuna viugomvi vya hapa na pale vinavyohusiana na nchi hizi mbili...Pakistan ina waislam wengi na India ina wahindi wengi kwahyo hata zile movie za kihindi zinaelezeaga viugomvi vyao vya kila siku

Kabla ya mwaka 1971 nchi ya Bangladesh ilikua sehem ya pakistan ikitambulika kama East Pakistan
Utenganisho wa umbalu kat na Eat pakistan na West pakistan haikuwa sabab kuu ya kutengana kwao isipokuwa East Pakistan walikuwa wanalalamika kuwa Rasilimal zao zinatumika kwa manufaa ya west pakistan ..hata lugha yao ya kibengali haithaminiki ...jeshi na serikali vilitawaliwa na West Pakistan ila mgogor ulikuwa mkubwa baada ya uchaguzi Sheikh Mujibur Rahman alishinda kutoka East Pakistan lakin hakupewa mamlaka kamili..hilo lilipelekea kuibuka kwa vita vya Indo-Pakistan

India ikawaunga mkono East Pakistan ikawasapoti kijeshi nakadhalika ...matokeo yake Pakistan ikapoteza na East Pakistan ikajipatia uhuru na kujiita Bangladesh

Baada ya vita hivyo kiongozi wa Pakistan wa wakati huo Zulifikar Ali Bhuto aliapa akisema Pakistani itakula hata nyasi lakini lazima wapate la Nyuklia..

Hiyo ikawatisha India na ndio ikazaliwa Operation ya Kahuta na Ajit Doval akaingia kazini
India waliona kwamba kama Pakistan wangekuwa na silaha za nyuklia ingekuwa hatar kwao..lakin pia siasa za Asia kusini zingebadilika kibaya zaidi inteligence ya kawaida isingejua hatua walizofikia Pakistan kwenye mrad wao wa nyuklia

Ajit Doval akawa muhusika mkuu kwa sababu ana uwezo wa kuongea lugha nying kiufasaha...hiyo ni moja ya sifa kubwa kwenye uwanda huu yaan kwa mfano mimi mkerewe napelekwa kwa ujasusi nchi ya wamakonde nahitajika niwe na uwezo wa kuongea kimakonde kisawasawa yaan kusiwe na utofaut wowote wa wewe na mmakonde kwenye kuongea ili mtu asikutilie shaka....

Ajit Doval pia alikuwa na uwezo mkubwa wa kuigiza..uvumilivu A+ na psychological manipulation
Akaingia kazini kama mtu wa kawaida

Ijayo tutaona ni kwa vipi aliwezaje na kwa namna gani na Je alikamatwa au alifanikiwa??

Credit: BWANA FACT
 
Back
Top