john achila mukumwa
Member
Daudi alitenda kosa gani hadi Waisraeli wengi wakafa
Hebu tuangalie maelekezo ya Mungu kuhusu kuhesabu Waisraeli.
Kitabu cha Hesabu 1:1-3:
1 BWANA akanena na Musa katika bara ya Sinai, hemani mwa kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri, akamwambia,
2 Fanyeni hesabu ya mkutano wote wa wana wa Israeli, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina ilivyo, kila mtu mume kichwa kwa kichwa;
3 tangu mwenye miaka ishirini umri wake, na zaidi, wote wawezao kutoka kwenenda vitani katika Israeli; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kuandama majeshi yao.
Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli 603,550. Idadi hiyo haijumuishi Walawi, wanawake, wala watoto chini ya miaka 20.
Lengo la Mungu kutaka sensa hiyo ifanyike ni kutaka Waisraeli wafahamu idadi yao wakati wa kuondoka Misri. Jumla ya takriban watu milioni 2 waliondoka Misri.
Kitabu cha Hesabu 26:1-2, 51, 64-65:
1 Ikawa baada ya hilo pigo, BWANA akanena na Musa na Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, na kuwaambia, 2 Fanya jumla ya mkutano wote wa wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani.
51 Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli 601,730. Idadi hiyo haijumuishi Walawi, wanawake, wala watoto chini ya miaka 20.
64 Lakini katika watu hao hapakuwa na mtu hata mmoja wa wale waliohesabiwa na Musa na Haruni kuhani; waliowahesabu wana wa Israeli katika bara ya Sinai.
65 Kwa kuwa BWANA alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.
Japokuwa ni watu 2 tu kati ya watu 601,730 ndio waliingia Kanaani, lengo la Mungu kutaka sensa hiyo ifanyike ni kutaka Waisraeli wafahamu idadi yao wakati walipokaribia kuingia nchi ya ahadi.
Sasa tuangalie mazingira ambayo Daudi alihesabu Waisraeli.
Mfalme Daudi alihesabu wana wa Yakobo, apate kujua idadi yao kamili (1Mambo ya Nyakati 21:7). Jambo hilo lililoonekana chukizo kwa Bwana, hadi kusababisha watu sabini elfu waangamie kwa tauni.
Je, ni uovu gani hapo Daudi aliufanya hadi ulete madhara hayo yote?
Na torati ilisemaje kuhusu watu kuhesabiwa?
Jibu ni kuwa hakukuwa na uovu mkubwa kivile katika kuhesabu watu, japo Daudi alifahamu hakupaswa kufanya vile kwa wakati ule. Lakini, yeye aliendelea kufanya hivyo, ndiyo maana baadaye alikuja kujutia makosa yake, na kumwomba Mungu msamaha.
Tuangalie kitabu cha 2Samweli 24:10-16, kisemavyo:
10 "Ndipo moyo wake Daudi ukamchoma baada ya kuwahesabu hao watu. Naye Daudi akamwambia BWANA, Nimekosa sana kwa haya niliyoyafanya; lakini sasa, Ee BWANA, nakusihi uuondolee mbali uovu wa mtumishi wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa.
11 Na Daudi alipoondoka asubuhi, neno la BWANA likamjia nabii Gadi, mwonaji wake Daudi, kusema,
12 Nenda, ukanene na Daudi, BWANA asema hivi, Nakuwekea mambo matatu; katika haya uchague moja, nikutendee hilo.
13 Basi Gadi akamwendea Daudi, akamweleza, akamwambia, Basi, miaka saba ya njaa ikujie katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie mbele ya adui zako, huku wakikufuatia? Au siku tatu iwe tauni katika nchi yako? Fanya shauri sasa, ufikiri, ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.
14 Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.
15 Basi BWANA akawaletea Israeli tauni tangu asubuhi hata wakati ulioamriwa; nao wakafa watu toka Dani mpaka Beer-sheba, sabini elfu.
16 Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili auharibu, BWANA akaghairi katika mabaya, akamwambia huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye yule malaika wa BWANA alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi".
Hata hivyo, swali linabaki pale pale: Ni kwa nini kwa kosa lake yeye mwenyewe lisababishe zaidi ya watu ya elfu 70 kuangamia kwa tauni?
Daudi mwenyewe alimlalamikia Mungu, na kumwambia kwa nini unawaadhibu watu wengine wasio na hatia kwa kosa langu mwenywewe?
Kwa nini Mungu awaadhibu na watu wengine wasio na hatia kwa kosa la mtu mwingine?
Daudi hakufahamu sababu ya Mungu kufanya vile.
Ukisoma vizuri biblia, habari hiyo, katika kitabu cha Samweli utaona jambo fulani la kuzingatia:
2Samweli 24:1 “TENA HASIRA YA BWANA IKAWAKA JUU YA ISRAELI, AKAMTIA DAUDI NIA JUU YAO, akisema, Nenda, ukawahesabu Israeli na Yuda".
2 "Basi mfalme akamwambia Yoabu, jemadari wa jeshi la askari, waliokuwa pamoja naye, Zunguka sasa katikati ya kabila zote za Israeli, tangu Dani mpaka Beer-sheba, mkawahesabu watu, nipate kujua jumla ya hao watu”.
3 Naye Yoabu akamwambia mfalme, BWANA, Mungu wako, na awaongeze watu, hesabu yao ikiwa yo yote, mara mia, tena macho ya bwana wangu mfalme na yawaone; ila kwa nini neno hili limempendeza bwana wangu mfalme?
4 Lakini neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu, na juu ya majemadari wa jeshi. Basi Yoabu akatoka na majemadari wa jeshi machoni pa mfalme, kwenda kuwahesabu watu wa Israeli.
Ukisoma mstari wa 1, utaona, kuna jambo wana wa Israeli walilifanya huko nyuma, na kupelekea hasira ya Mungu kuwaka juu yao.
Kama ukisoma huko nyuma, utagundua kuwa Mungu alikuwa hapendezwi na njia zao tangu siku nyingi, na ndiyo maana wakati mwingine alikuwa anawatia katika mikono ya Wafilisti.
Na hapa pia ni vivyo hivyo. Kuna mambo maovu walikuwa wanayafanya pengine kwa siri au hadharani, japo biblia haijaeleza ni mambo gani. Lakini ni dhahiri kuwa matendo yao yalimuudhi Mungu sana. Mambo kama kuabudu miungu migeni, rushwa, kudhulumu watu, mauaji yasiyo na hatia, kuhalifu sabato, kubanika wana wao motoni, na kuwaonea wajane na mayatima. Hayo ni miongoni mwa mambo waliyokuwa wanayafanya wana wa Israeli kwa wakati ule.
Hivyo Mungu akaamua kumtumia Daudi nia, kama sababu ya kuwaadhibu makosa yao. Na ndiyo hapo tunakuja kuona Daudi anaingiliwa na shetani kufanya vile, kama tu vile Mungu alivyotaka kumwangamiza mfalme Ahabu, akaruhusu pepo la uongo likawavae wale manabii wake 400.
Vivyo hivyo, Daudi naye, aliingiwa na shetani kufanya mambo ambayo Mungu hakumuagiza. Baadaye tunaona tauni inakuja kuachiliwa juu ya Israeli, ili Mungu kujilipizia kisasi juu yao wote waliomuudhi.
Mfano mwingine unaweza kuona Mfalme Nebkadneza alikuwa ni diktekta. Aliteka mataifa yote ulimwenguni kwa nguvu na akayatawala kwa mabavu. Hata Taifa la Mungu Israeli liliwekwa chini wa utawala wa Nebkadneza.
Lakini katika biblia, utaona kuwa Mungu ndiye aliyemtia Nebkadneza nia ya kwenda kuteka mataifa yote ulimwenguni pasipo hata yeye Nebukadneza kufahamu chochote. Na Mungu alifanya vile ili kujilipizia kisasi kwa mataifa yote yaliyomwacha ikiwemo na Taifa la Israeli la watu wake.
Tunaona kuwa kosa ambalo Daudi alifanya ni kukosa imani na nguvu za Mungu, ambaye ndiye alikuwa anampigania siku zote. Akaanza kuwa na imani juu ya ukubwa wa majeshi yake; hivyo akaagiza ifanyike hesabu ya kujua idadi ya wapiganaji wake, badala ya kuendelea kumtegemea Mungu.
Matokeo yake, Daudi aliadhibiwa na Mungu kwa ugonjwa wa tauni kwa Waisraeli.
Katika hatua ya kutekeleza adhabu hiyo, watu elfu 70 wakawa wamekwishakufa, kabla ya Mungu kusitisha adhabu hiyo.
Hivyo tunapaswa tuwe makini na njia zetu, tumwombe Mungu kila siku, ili wengine wasifanyike kuwa fimbo ya Mungu kuadhibu wasiohusika.