Advertise here

Wanandoa wameweka rekodi ya dunia kwakuwa wanandoa walio jitoboatoboa na kuikarabati zaidi miili yao.

Kasomi

JT Founder
Screenshot_20221123-130701_1.jpg

Wawili hao pichani wameweka rekodi ya dunia kwakuwa wanandoa walio jitoboatoboa na kuikarabati zaidi miili yao.

Gabriela Peralta(50) anayetokea Argentina na Victor Hugo Peralta(51) ambaye kiasili anatokea nchini Uruguay walikutana miaka 24 iliyopita katika tukio la mambo ya pikipiki baada ya kufahamiana Kila mmoja akagundua wote wawili wanapenda kuikarabati miili yao. Baadaye walifunga ndoa ambayo ina miaka 14 sasa

Wameingia katika rekodi ya dunia ya Guinness kwa kuwa wapenzi waliooana au wanandoa ambao wamejitoboatoboa zaidi miili yao, ikiwemo tattoo, sajari etc ambavyo vyote jumla ni 98 kwa miili ya wote wawili

Mwanaume amesema ni furaha ya wao kushikilia rekodi hiyo kwani imesaidia pia atembelee nchi 20 ikiwemo kujifunza tamaduni mbalimbali na kukutana na watu wapya.
 
Back
Top