Advertise here

Tunasoma, tunakariri, tunafundishwa na kuelekezwa lakini kuna kitu tunakisahau ambacho kwa sehemu kubwa ndicho kimebeba mafanikio makubwa kwenye vile

Kasomi

JT Founder
Anaandika Emmanuel Minga


Tunasoma, tunakariri, tunafundishwa na kuelekezwa lakini kuna kitu tunakisahau ambacho kwa sehemu kubwa ndicho kimebeba mafanikio makubwa kwenye vile tunavyoshughurika navyo.

Nilikuwa najifunza kwa habari ya ubunifu, hili eneo ni kama linapuuzwa sana na watu wengi wanaosema wanatamani kufanikiwa.

Wengi wanaiga tu njia na mifumo waliyotumia wengine na wamekosa kujiongeza zaidi ya hapo.

Kwenye mahusiano watu sio wabunifu, kuna hata watu wanajiita wajasiriamali lakini nao pia si wabunifu.

Ngoja nikwambie kitu cha kukusaidia hapa, ubunifu ndio unaoongeza thamani yako, ubunifu ndio utawapa wateja sababu ya kwanini wanapaswa kununua kwako au kukuhitaji wewe na sio kwengine au mtu mwingine.

Ubunifu ni ule uziada ambao mtu anapata kama nyongeza au zawadi kutoka kwako. Ubunifu ni ubora na mvuto wa ziada kutoka kwenye ukawaida uliozoeleka kila wakati.

Tatizo tulilo nalo leo tunataka kuiga kila kitu tutakachosikia kina faida( inshort hatutaki kufikiri) , bila kuchunguza mbinu zilizotumika na gharama zake zote.

Mtu anakwambia tu ukilima matikiti heka 2 kwa sh milion 4 , ukijakuuza unapata mara tatu ya mtaji wako. Mara waaaa watu wote ni wakulima wa matikiti. ( Sasa wakulima wa matikiti mmekuwa wengi thamani imepungua) na haujui ufanye nini tena.

Bidhaa inapokuwa nyingi sokoni thamani yake inashuka, unapaswa ufanye kitu cha ziada kuiongezea thamani ili wateja waone umaana wa kuja kununua kwako.

Hivyo hivyo hata kwenye mahusiano, leo sex ni very easy kupata na hivyo ni kama mahusiano hayanathamani kama ile ya mwanzo, so unapaswa uwe na kitu cha ziada chenye thamani kumpa mtu wako ili awe na wewe.

Kuna siku niliweka tangazo la kuuza kitabu changu kimoja jamaa yangu mmoja aliniuliza nikinunua kitabu chako nitapata nini? Nikagundua huyu jamaa anahitaji kujua uziada nilionao kutofautisha na waandishi wengine walioandika kwenye jambo hilo hilo, huyu jamaa nilimwelekeza akaelewa na yeye akaniletea na mteja mwingine.

So watu wanahitaji uziada watakao upata kwenye kazi, biashara au kutoka kwako wewe binafsi.

Ukikosa uziada utaonekana wa kawaida kama watu wengine tu. Kama kwenye mahusiano utaachika kirahisi, kama biashara utauza kawaida n.k.
 
Back
Top