Advertise here

Maumivu yasiyo kwisha (Endless Pain)

Kasomi

JT Founder
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!
.
Sehemu ya kwanza.
.
Mwaka 2016 ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuingia chuoni, ilikua katika chuo cha kimataifa cha Kampala.
Naikumbuka siku yangu ya kwanza nilikua naonekana mnyonge sana, hasa kutokana na ugeni wangu na kila mmoja ndani ya darasa alikua ameonekana kutokumzoea mwenzake.
.
Pindi lecture inaendelea, nilikua niko makini sana kusikiliza kile ambacho lecturer alikua akifundisha darasani, nikatupa macho yangu pembeni kuwatazama classmates wangu, kila mmoja alionekana yuko busy akimsikiliza.
Lakini pembeni yangu nilishangaa kumuona kijana mmoja akiwa ameduwaa, na wala hakuonyesha kufatilia kinachofundishwa. Nikapata shauku ya kutaka kujua kinachoendelea, anatazama nini hicho kiasi cha kumfanya aduwae kiasi kile, nikatupa macho kwa mbele zaidi kuelekea uelekeo wa macho yake.
.
Nilipigwa na bumbuwazi, nami niliduwaa zaidi ya yule kijana, macho yalinitoka huku nikiongeza umakini zaidi wa kutazama kile nilichokiona.
Macho hayana panzia, yalitua kwa msichana mmoja mrembo aliyefanya mimi na yule kijana tuduwae. Wala hakujua kama tunamtazama, alikua busy akifatilia lecture.
Nilitengeneza movie nyingi za mahaba kichwani mwangu juu ya yule msichana.
.
Ghafla nilishtushwa mawazoni mara baada ya lecturer kuuliza swali, na kuniomba mimi niliyeonekana sifatilii somo nilijibu swali hilo.
.
Lecturer: Differentiate between a manager and an entrepreneur???
.
Kwa mbwembwe zote, tena huku nikimtazama mtoto mkali, nikanyanyuka, nikamtazama lecturer na kujibu swali.
.
Siku ya kwanza ikapita kama hivyo, na ndiyo siku niliyoanza kumpenda.
.
Siku kadhaa zilipita, nikiwa tayari nimeshayazoea mazingira chuoni hapo, nikijulikana kama kijana mstaarabu na mcheshi ndani na nje ya darasa.
.
Siku moja nilipokuwa darasani nikifanya assignment kwenye laptop.
Ghafla ilisikika sauti nyororo yenye kumtoa nyoka pangoni, moyo ulinipiga Paaah, damu ikaanza kunichemka, nikapata shauku ya kutaka kujua ni nani huyu ananiongelesha.
.
Nikanyanyua uso ili nimtazame uso, macho yangu yalikutana na mavazi safi yenye kung'ara, zaidi ilikua ni harufu yake ya pafyumu iliyozidi kunivutia, nikapanda mpaka juu na kukutana uso kwa uso na msichana mrembo aliyekuwa akilini mwangu siku zote tangu nianze chuo.
.
Nilibaki nashangaa kwa sekunde kadhaa, ikabidi arudie salam yake.
Yeye: Hi.
Mimi: Hi, how umh how you doing?
Yeye: Doing great, sorry for disturbance, can you do me a favor?
.
Nikasikiliza jinsi anavyoteleza kwenye lugha ya kigeni, nikaona hapana, huku tunako endelea atanipoteza mwisho nipate aibu, mimi st.kayumba, English ilipanda ndege.
.
Nikamjibu: Bila samahani, wala hujanisumbua. Yes unaweza sema tu maybe naweza saidia.
Yeye: Onh asante kwa ukarimu wako, naomba unielekeze jinsi ya kuset hotspot kwenye iPhone, nataka niconnect na laptop yangu ".
.
Alizidi kunivutia kwa maneno yake matamu, nikajisemea kimoyo moyo "Haya ni maneno ambayo kina Mwajuma Ndalandefu uswazi hawawezi kuyasema, na leo ndo chance nzuri ya kujuana nae vizuri ".
Sikutaka kuchelewa nikachukua kiti, nikamsogeza karibu na kuanza kumpa maelekezo.
.
Nilipomaliza alishukuru sana, lakini alipotaka kuondoka tu akatupa jicho kwenye laptop na kugundua nilikua nafanya assignment.
Akasema na yeye alikua bado hajafanya, nikamuomba tujumuike ili tufanye wote.
.
Shida yangu haikuwa tufanye wote assignment, shida yangu ilikua tuzidi kuzoeana ili hata kesho yake nisipate tabu tena kuanza kujitambulisha.
Nilizidi kumnogesha kwa story ambazo zilimfanya azidi kucheka huku tukifanya assignment.
.
Tulipomaliza wala hakunyanyuka kama mwanzo, aliendelea kukaa na tukazidi kupiga story.
Nikaona nisichelewe kutaka kumjua.
.
Mimi: Hahah yale makoti hayafai kwa Dar es salaam hii, labda utembee huku na feni pembeni.
.
Akacheka, kisha akatazama saa yake, nikastuka nikajua huu utakua muda wa lunch au kuondoka tayari.
Nikamuwahi "Btw nimefurahia sana uwepo wako, na umefanya niione assignment nyepesi pia.".
.
Akanijibu "Asante sana, tangu nianze chuo leo ndo nimefurahi sana, ndomana nimetazama saa hapa nikashangaa leo nimebaki hadi saa 7".
.
Mimi: Onh nimefurahi kusikia hivyo, kwani haujapata marafiki bado?!
.
Yeye: You know what, mahali kama hapa pana watu tofauti, waliotokea kwenye malezi tofauti. Na usipokua makini kwenye uchaguzi wa marafiki, ukawa unaparamia tu, basi unaweza jikuta unapata marafiki wa hovyo hovyo.
Najiheshimu sana, na napenda niwe na marafiki wanao jiheshimu pia, hata wewe nimekufata mpaka kukuomba unisaidie, sababu nilijua wewe mstaarabu na ni tofauti na vijana wengine darasani."
.
Nikashusha pumzi nzito sana, maneno yaliniingia sana akilini. Mwanzo nilikua na wazo la kumuomba namba leo leo, lakin nikaona hapana huyu nikienda nae haraka nitampoteza, anajithamini na kujiheshimu sana tofauti na nilivyofikiria.
.
Nikamjibu: Uko sahihi kabisa, hata mimi ndio maana unaona nakaa peke yangu sana sababu hiyo hiyo, naogopa kujiingiza kwenye makundi ya watu wasio na maadili.
Hata hivyo, nimefurahi kujua kama uko tofauti na wasichana wengine, naitwa Chris. "
.
Yeye: Nice to meet you Chris, naitwa Careen".
.
Mimi: "Damn, nice name''
.
Akafurahi sana, tukaagana na kuondoka. Nakumbuka nilijilaumu sana kwanini sikumuomba namba yake ya simu, lakini nilijipa moyo kuwa huo ni mwanzo mzuri sana kwangu, na pia ni jambo zuri kutokumuomba namba mapema kiasi hicho kutamfanya asihisi chochote kuhusu hisia zangu kwake.
.
Siku iliyofata mambo yalizidi kuwa moto darasani, nakumbuka alibadili sehemu yake ya kukaa na kuja kukaa karibu nami, alikua akipenda kuniita kaka Chris, japo sikupenda kuitwa "Kaka" lakini nililivumilia tu sababu sikupenda ahisi kuwa nina hisia juu yake.
.
Watu walikua wakitutazama sana, na wengine kuulizana hawa Wamezoeana saa ngapi, sababu hakua na mazoea na mtu yeyote yule zaidi yangu, na wengine aliishia kuwapa salamu na story mbili tatu pale inapobidi.

Nilifurahishwa sana na mwenendo wake, hasa ukizingatia hakuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye Mcharuko, au anajifanya ana mazoea na kila mtu.
.
Nakumbuka siku ya tatu ya urafiki wetu, majira ya saa 6, nilimuomba twende tukapate lunch wote, hasa ukizingatia nilitaka niwe rafiki yake wa karibu zaidi ambaye ataweza kula nae, kuongea nae, kuniambia jambo lolote hata lile lisilo ambikika kiurahisi, ambaye atamkumbuka wakati wa huzuni na furaha.
Kwakifupi, nilitaka niwe kila kitu kwake, ili hata pale nitakapo muhitaji tuwe wapenzi basi asiweze kukataa, yani niwe nimemtengeneza kihisia zaidi.
.
Tulielekea wote mpaka maeneo pakulia, maarufu kwa jina la PEPSI, sote tulichukua chakula na kuelekea mezani, story zilikuwa nyingi na chakula kilinoga.
Alikua akiniambia jinsi anavyojisikiaga aibu kula mbele za watu hasa wanaume, ila anashangaa leo hii ameweza kukubali kukaa meza moja na mimi.
Nilimshika mkono, nikamtazama usoni, nikamwambia ''Mimi ni rafiki yako, usiniogope, usinioneee aibu, jisikie huru kufanya lolote unapokua nami, ili tuwe marafiki bora basi inabidi tusioneane aibu."
.
Alitabasamu na chakula kiliendelea kuliwa, tulipomaliza tukaelekea mahali pakulipia, kwavile mimi ndiye niliyemualika, na ndiyo mwanaume, basi nikataka kuvimba ili nilipe bill.
.
Nikaingiza mkono mfukoni ili kuchukua wallet, nikastuka, nikaanza kupagawa baada ya kuikosa wallet kwenye mfuko wa nyuma wa suruali ninako wekaga.
.
Nikasearch na mifuko mingine sikukuta kitu.
Mwanadada ambaye ndiye mpokea malipo akaniongelesha tena "Nakusubiria wewe kaka".
.
Careen aliyekuwa kwa pembeni akageuka na kunitazama usoni, ikabidi nivunge nisionyeshe wasiwasi wangu.
Nikarudisha mikono mfukoni kuhakikisha kwa mara ya pili, mapigo ya moyo yalizidi kunidunda baada ya kugundua kuwa mfukoni ni kweupe, na dada mpokea malipo alikua akinitupia jicho.
.
Mawazo yakawa huyu binti, atanionaje??? Je atanisaidia kulipa??? Au nae hana hela?? Sindo mwanzo wa kuaibika huu??!
.
_______________________________
Usikose sehemu ya pili
Itaendelea....

Soma Sehemu ya pili hapa Maumivu Yasiyo kwisha (Endless Pain)
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN).

Sehemu ya pili....

#Ilipoishia: Nilimuomba Careen tukapate wote chakula cha mchana, tulikula pamoja na kukifurahia, lakini tatizo lilikuja baada ya kufika wakati wa kulipa bill za chakula tulichokula.

Kama mwanaume nilijitutumua na kuingiza mkono mfukoni ili kulipa bill, bahati mbaya wallet haikuwepo mfukoni.
Nikachanganyikiwa sana, nikarudia mara mbili mbili kutafuta wallet mifukoni kote lakini sikuiona.
*****************
#Inaendelea:
Uso ulilowa jasho la ghafla, nilikuwa kama niliye changanyikiwa, sikujua la kufanya na zaidi kilichoniumiza ni kuwa leo hii na kwenda kuaibika mbele za msichana ninaye mpenda.

Nikapukuta mifuko yangu yote, bado kweupe, ikabidi nirudi mpaka kwenye viti tulivyokalia wakati wa kula ili kutazama endapo kama ipo wallet yangu.
Wala sikuikuta, nikawa narudi na mawazo mengi kichwani je atanielewa??? Nitaaibika kiasi gani???

Nilianzwa kulengwa na machozi, huku mwili ukiwa umetapakawa na jasho.
Nikapiga moyo konde na kusema liwalo na liwe.
Careen alinitazama kwa huruma pindi nilipokuwa narejea, sikumwambia nilichokua natafuta ila kwa zile purukushani basi nahisi alijua.

Nikamuona anaingiza mkono kwenye pochi yake, na kutoa noti ya wekundu wa msimbazi, kisha akarudishiwa chenji, akaipokea na kubaki akinisubiri ili tuondoke.

Nilikumbwa na aibu kubwa sana mbele ya msichana ninaye mpenda, lakini hata hivyo nilitamani nishangilie sababu niliona afadhali alivyolipa amenipunguzia kupata aibu kubwa zaidi.

Nikamsogerea, akanitazama na kuniambia "Umedondosha wallet??? "

Nilitamani kumjibu "Kwani ulikua huoni nilichokua natafuta au?", lakini nikawa mpole zaidi, nikainamisha kichwa changu chini kwa aibu, nikamjibu "Yeah, na sijui imedondokea wapi. I'm really sorry for what happened ".

Careen: Usijali, pole zaidi, kama hapa umeikosa basi ujue itakua umeidondosha darasani au umeisahau kwenye bag."

Mimi: Nadhani itakua hivyo.(nikazungumza huku tukiondoka, kidogo nilipata nguvu ya kujifuta jasho, lakini nilikosa kabisa nguvu ya hata kunyanyua uso wangu kumtazama usoni.)
.
Njiani nilitamani nitembee haraka niwahi darasani nilikoacha bag, nikatazame kama wallet ipo ili nimlipe pesa yake ... ila pia nafsi ikaniambia tembea nae taratibu tu, usijionyeshe dhaifu sana.)
.
Tulitembea kama mabubu, kuna muda alijaribu kuniongelesha lakini nilikua muitikiaji tu, nahisi hata angesema "Wewe mjinga" mimi ningeitikia tu "Ndio" bila kujijua.
Akanishika mkono, akaniambia "Sasa kaka Chris, tutaonana tomorrow, nahitaji kuwahi kwenda kwenye semina kanisani jioni "
.
Nilistuka, nikamjibu "Sawa, ila tungeenda hivi ili kama nitaikuta wallet basi nikurudishie hela yako".
.
Akanitazama, akatikisa kichwa akiashiria kukataa, akanijibu "Hapana usijali, wewe rafiki yangu, so sio mbaya leo nikalipa mimi, kesho utalipa wewe, tutakua tukishare kidogo tulichonacho.".
.
Maneno yaliniingia moyoni, nikahisi niko na mwanamke tofauti sana.
Najua hapa mwingine angenichamba au pale pale angeniacha niaibishwe mbele za watu.
.
Kwa aibu nikajibu "Dah, asante sana maana nilivurugwa ghafla, ubarikiwe sana ".
Akanijibu "Asante, what if ukikosa wallet huko? Chukua hii chenji itakusaidia hata kwa nauli ya kurudia nyumbani ".
.
Nikamtazama, nikamjibu "Anh no, no, asante sana, mi sikai mbali, nimepanga hostel ya hapo nje tu. Na nimeacha kiasi cha kutosha mwezi mzima hostel". (Nikazungumza kwa kujiaminisha ili nisionekane dhaifu).
.
Akaniamini, tukaagana na akaniachia mkono na kuondoka.
Sikutaka kumsindikiza kwa macho wala nini, nilitoka nduki mpaka kwa jamaa niliyemuachia bag langu, nikatafuta wallet na kuikuta imetulia bila wasiwasi kwenye kimfuko kidogo cha bag.

Nikasonya, nikaitia makofi matatu, "Shenzi kabisa, yani kuniaibisha kote kule kumbe umetulia tuli kwenye bag"- nilizungumza kwa hasira.

Hasheem: "Chris vipi? Mbona unaongea peke yako bro? "
Chris: "Dah acha tu bro, nimeitafuta wallet sana, kumbe iko kwenye bag ".
Hasheem: "Hahah hiyo kawaida sana, nilishawahi weka simu kwenye mfuko wa shati, halafu nikasahau, nilitafuta siku nzima, nikarudia sehemu zote nilizopitia siku hiyo. Baadae sana ndio nikaja kuiona mfukoni".

Chris: Hahaha (Nilicheka kinafki tu maana sikuwa hata kwenye mood ya kucheka kwa siku hiyo, nikaaga na kwenda hostel, mawazo yalikuwa mengi sana juu ya Careen na niliwaza sana je atanifikiriaje kwa huko alipo?? Si itakua nimejishusha vyeo vyangu, na thamani yangu imepungua zaidi, lakini jambo lililozidi kunivutia juu ya Careen ni jinsi alivyoweza kulimaliza swala kimya kimya, naamini angekuwa mwengine basi ningeaibika.).
.
Na hivyo ndivyo siku yangu ya tatu ilivyokua tangu niwe karibu nae.

Siku iliyofata kipindi kilikua saa sita, niliwahi mapema tu majira ya saa 4.
Macho yangu yalikuwa yakiangaza huku na huko ili kama naweza kumuona mtoto mzuri Careen.
Hamu yangu kubwa ilikua lazima nipate namba yake leo, na lazima nimchimbe kiundani mpaka nijue kama ana boyfriend au laanh.
.
Nilimuona kwa mbali akiwa ameketi peke yake maeneo ya garden, nikamuita muuza Ice cream, nikanunua mbili za kopo na kumfata mahali alipo.
Pindi naelekea nikapishana na waNigeria wawili wakinong'onezana kuhus uzuri wa Careen.
Nikaona hapa nikichelewa kumtongoza huyu msichana basi wengine wataniwahi.
.
Nikamfikia alipo na kutoa salamu.
Mimi: Hi, (Nilitoa salamu huku namkabidhi ice cream).
Careen: Hi, wow thank you. How are you???
.
Mimi: I'm good, yani niko poa mpaka najionea wivu...!!! Sijui wewe??.
Careen: Hahah una maneno wewe, niko poa sana na ashukuriwe Mungu kwahilo. Uumh asante sana kwa ice cream, hata hivyo nilikumiss sana.
.
Alinigusa sana, maana ni mara chache sana nimepokea neno "Asante", ex wangu alikua hana tabia hiyo... hata ukimpa laki moja ya kwenda kununua nguo basi lazima aulize "Na hela ya nauli je?".
.
Kwa Careen hili nililiona jambo la kipekee sana, nikatabasamu na kumjibu "Hata mimi nilikumiss sana mpaka nikapatwa na homa mpaka nikajihisi nitaambiwa R.I.P sasa hivi".
.
Akacheka sana, akajibu "Halafu nisingekuja kwenye msiba wako "
.
Mimi: "hahaha ningekununia".
.
Careen alicheka sana.
Nikaona huu ndo wakati wa kuomba namba.
.
Mimi: Halafu nimekumbuka, jana nilitumiwa soft copy ya notes, nikutumie kama unaitaka???
.
Careen: Ndo nilikua nataka nikamfate Cr anitumie, nitumie kwenye email basi.
.
Mimi: Anh email mzunguko wote huo, nitajie namba tu nikutumie WhatsApp chap tu. (Nikazungumza kwa msisitizo ili akubali, shida yangu ilikua namba tu, na nikajua hapa kivyovyote hawezi kuchomoka kwenye huu mtego).
.
Careen akanitazama usoni ikiwa kama mtu anayejaribu kusoma kitu kwenye uso wangu.
Kisha kwa utaratibu akanijibu ''Nitumie tu kwenye email sababu nitataka niifungue baadae kwenye laptop."
.
Nikashusha pumzi nzito baada ya kuona mtego wangu umefeli.
Nikajisemea kimoyoni "Dah huyu smart sana kichwani, hakamatiki kiurahisi, sasa hiyo email yake ina faida gani kwangu".
Nikachukua email yake kishingo upande na kumtumia notes.
.
Nikaona sio mbaya, anaonekana mwenye misimamo, ngoja nianze kumchimba nijue kama ana boyfriend ili nijue kama niko vitani, au ndio basi tena, au yuko single ili nislide moja kwa moja kabla wajanja hawajaniwahi.
.
Mimi: Leo nilikaa asubuhi nikawaza sana, hivi inakuaje mtu unampenda na yeye anaonyesha anakupenda pia, lakini mwisho anakusaliti?! Au anakuacha kabisa.
.
Akanitazama sana, akionekana mwenye kutafakari.
Akanijibu "Kaka Chris, moyo wa mtu kichaka na kamwe huwezi kujua lile alilolificha moyoni mwake juu yako."
.
Akanyamaza kidogo, akaendelea "Mwingine anakua anajifanya anakupenda sababu kuna kitu anakitaka, akishakipata tu basi anaanza kuonyesha makucha yake."
.
Akanyamaza tena, nilielewa sana points zake, ila shida yangu haikuwa kusikia maneno yake ya busara, shida yangu nikujua kama ana boyfriend au hana.
.
Nikaingiza neno "Kweli kabisa usemayo, moyo wa mtu kichaka. Ila rafiki yangu wewe unajitambua sana, natumaini boyfriend wako hana tabia mbovu mbovu, tena ulivyo mzuri hivyo, kwako kafika."
.
Careen akatabasamu sana, kisha akatoa jibu lililoniacha mdomo wazi, akajibu "Hata kama mimi mzuri, binadamu hawatabiriki, siwezi jiaminisha kwa asilimia zote kwa yeyote yule.".
.
Jibu lilikua zito sana kwangu, yani leo namba nikose, na ukweli kuwa ana boyfriend au hana nao nikose.
Nikamuona Careen ni mwanamke mwerevu sana, ana matumizi mazuri ya ubongo na kinywa chake.
.
Uvumilivu ukanishinda, ikabidi nitupe swali kavu kavu, nikauliza "Kwani una boyfriend au huna??! ".
.
Alinigeukia na kunitazama, nikapata shauku ya kutaka kusikia atakachojibu.
Akatabasamu, akanishika mkono na kuniambia "Usijali, bado mapema sana,kuwa na subira utanijua tu".
.
Nikachoka kabisa kwa jibu lake, nikajiuliza huyu ni mwanamke wa aina gani huyu?? Mbona ananishangaza kwenye kila jambo.
Ila nilibaki na kujilaumu kwanini nimeharakisha mambo mapema hivyo.
.
Nilihisi ameanza kunistukia kuwa nina hisia juu yake, nikajisikia vibaya sana. Ikanibidi niombe kwenda toilet mara moja, nikanyanyuka na kuelekea toilet, nikakaa kwa muda wa dakika 5, pindi narejea kutoka toilet ndipo nilipoona kwa mbali jambo lililonistua sana.
.
Nilimuona kijana mmojawapo kati ya wale waNigeria wawili niliopishana nao mwanzo.
Alikuwa ameketi pale pale nilipokuwa nimeketi, na alikuwa akionekana Akizungumza na Careen kwa hisia zaidi.
.
Nilisimama kwa mshangao, mapigo ya moyo yalizidi kunienda mbio, nikawaza je ndo ananiwahi mapema kiasi hiki?? Ndo naibiwa??
Roho iliniuma zaidi baada ya kuona mNigeria anachukua simu yake na kumnyooshea Careen achukue aandike namba.
.
Nilishika kichwa nikijua kuwa tayari mbuzi kashafia kwa muuza supu.
Nilizidi kushangaa zaidi baada ya kuona jambo ambalo Careen alilifanya
.

Je Careen alifanya jambo gani???!!
.
Usikose sehemu ya tatu*

Itaendelea....

Sehemu ya Tatu soma hapa

Maumivu yasiyo kwisha (Endless Pain)
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!!

Sehemu ya tatu...

#Ilipoishia: Baada ya kutoka na kwenda toilet kwa muda wa dakika 5, pindi narejea ndipo nilipomuona mmojawapo kati ya wale waNigeria wawili akiwa ameketi karibu na Careen, alionekana akizungumza kwa hisia sana, kisha akachukua simu yake na kumpa Careen aandike namba.

Moyo ulizidi kuniuma sana baada ya kumuona Careen akiipokea ile simu na kuandika kitu kama namba hivi.
************
#Inaendelea
Nafsi yangu ilijutia sana kwanini nilitoka na kwenda toilet, kwanini nisingebaki pale pale angalau mNigeria angeogopa kuja.

Nilibaki nimesimama kwa muda mrefu sana, nikiwa na mawazo mengi sana, nilijua ndo tayari tena Careen kasharubuniwa na mwanaume mwingine, nilijutia sana kuchelewa chelewa kwangu, nilijutia sana kupenda kutumia kwangu mzunguko mrefu hadi kwenye uombaji wa namba.

Kwambali nilimuona mNigeria akiaga na kuondoka, ndipo nami nikaanza kuchukua hatua kuelekea alipo Careen.
Kwavile nilikua kwenye huzuni kubwa, na wala sikutaka anigundue kuwa nimekasirika, basi ikabidi nifike tu na kumuomba niondoke nielekee darasani kwa kisingizio kuwa nataka nisome kwanza kabla kipindi hakijaanza.

Careen: Ndo unataka kuniacha nibaki peke yangu?! Nisubiri twende wote.(Aliongea kwa msisitizo huku akinyanyuka)

Mimi: Anh no, wee baki tu ule upepo.(Niliongea huku nikianza kukanyaga hatua kuelekea mbele).

Careen: Chris nisubiri bwana.(Akanyanyua vitu vyake na kuanza kunifata nyuma).

Ikanibidi niongozane nae tu hivyo hivyo kishingo upande.
Kiukweli sikupenda kutembea nae, wala kuwa nae karibu kwa siku hiyo.
Nilikua nimetingwa na mawazo mengi kichwani hasa nikiwaza je itakua ametoa namba kweli, au amempa namba ya uongo, na kilichoniumiza zaidi, kwanini ampe namba yule mNigeria ambaye hata hawajuani lakini mimi ninaye juana nae ameninyima.

Nikakumbuka maneno ya dada yangu Rachel, aliwahi niambia mwanamke anaweza kupa namba hata ya uongo ilimradi usiendelee kumsumbua.
Nikajipa moyo, nikatabasamu na kuendelea na safari mpaka darasani ambapo nilikaa nae karibu, nilionekana nasoma notes kwenye laptop, lakini kiukweli sikuwa nasoma chochote, nilikua mbali kimawazo.

Saa sita ilipofika tukaingia kwenye kipindi, kilipoisha nilinyanyua bag langu na kutoka nje, siku hiyo sikutaka kabisa kuzungumza mengi, nilisahau hadi kuagana na Careen.

Mara nikasikia Careen ananiita, "Chris, chris".
Nikaitikia "Yes, " na ikabidi nizuge ili asigundue kuwa nilikuwa naondoka bila kuaga.
Akaanza kuniwahi, mpaka aliponifikia.
.
Careen: Utakua free kwa kesho???
Mimi: Hapana, nitatoka asubuhi halafu nirudi jioni kwaajili ya kuparty, siunajua kesho kutakua na bhash.(nilimdanganya nitakua busy ili nipate nafasi ya kua nae mbali kwa kesho).
.
Careen: Onh basi, nilitaka twende wote sehemu kesho mchana.
.
Niliposikia neno "Twende wote sehemu " nilistuka sana, ikabidi nibadilishe mada "Anh usijali tunaweza kwenda tu, mahali kwenyewe nilipotaka kwenda sio muhimu sana ".
.
Careen: Afadhali, nilikua nawaza ningeenda kuwa mnyonge.
.
Mimi: Okay usijali nipo kwaajili yako, niambie sehemu gani sasa mamie?!

Careen: Kuna mNigeria nilikua naongea nae leo mchana, kanialika kwenye party yake ya birthday.

Sasa akili ikaanza kunijia vizuri kichwani, nikapata picha kuumbe Careen hakutoa namba kwa gia ya kutongozwa, kumbe alitumia gia ya party.
Nikapata amani ya moyo, nikaanza kujiona mjinga kwa kukasirika vitu vidogo sana, japo nilijua wazi kuwa mNigeria alikua na nia yake tofauti na party.
"Lakini na misimamo yake yote hii, anaweza kukubali party kwa mtu asiyemjua?" Nilijiuliza swali kimoyo moyo.

Mimi: Kwani unamjua yule mNigeria??
Careen: Yeah namjua japo sio sana, anaitwa Peter, nilikutana nae siku niliyokuja kufanya usajili, ndiye aliyekuwa akinipa maelekezo.
.
Mimi: Anhaa kumbe, maana nikashangaa unawezaje kukubali kwenda sehemu kwa mtu usiyemjua.
.
Careen: Hata hivyo nilitaka kukataa, ila kwavile alinionyesha ukarimu kwenye siku yangu ya kwanza, ndio maana imenibidi nikubali, hata hivyo ndomana nataka niende na wewe.
.
Mimi: Okay nimekubali, ila sasa tutawasiliana vipi?? Na maeneo gani? Muda gani?

Akanitazama na kuniomba simu, nikampa na akaandika namba yake.
Moyoni nilikua najisemea 'Leo umeshaingia kwenye 18 zangu".
Akanirudishia simu na kuniambia party itafanyika nyumbani kwa kina Peter, maeneo ya Kunduchi Beach, majira ya saa 8 mchana.

Tukaagana na niliondoka na furaha sana baada ya kuwa nimepata namba ya Careen, na siku yangu ya 4 tangu tujuane ikawa imeisha hivyo.
.
Siku iliyofata kama kawaida, nilivunja kabati, nikatupia kuliko siku zote, nikahakikisha nanukia safi.
Safari ikaanza kutoka Gongo La Mboto mpaka Simu 2000, ambapo ndipo tulipopanga kukutana na Careen.
Tulifurahi sana kukutana tena, alikua anang'ara sana, kapendeza, nikamsifia mpaka nikahisi sasa nitasifia mwisho nitukane.

Tukachukua tax mpaka nyumbani kwa kina Peter.
Tulikaribishwa vizuri sana, utambulisho ndio ulifata.
Careen alinitambulisha kwa Peter, na rafiki yake Peter ambaye anaitwa Abdulrahman Okechi.
Naye Peter alitutambulisha mimi na Careen kwa rafiki yake.

Tulipewa vinywaji, na party ikawa ikiendelea.
Lakini kuna nyakati nilihisi kuna kitu hakiko sawa, hawakuonyesha kuwa karibu nami, ilikuwa kama nimetengwa hivi.
Rafiki yake na Peter alikuwa karibu sana na Careen, kiasi cha kuanza kunitia wasiwasi.
Niliona aibu sana, party ilikua na watu wengi, lakini kila mmoja alikua karibu na anayefahamiana nae, ni mimi tu ndiye niliyekua mkiwa.
.
Nilitamani party iishe ili tuondoke tu maana nilihisi moyo kupasuka.
Party ilivyoisha tukajiandaa kuondoka, lakini Careen aliniambia subiri tutarudishwa na magari yao.
Nikashangaa sana.
.
Lakini lililo nishangaza zaidi ni pale Peter na Abdulrahman walipokuja na kuniambia mimi ninae enda Gongo La Mboto nipande gari la Abdulrahman.
Na Careen atapanda gari la Peter.
.
Nilistuka, nikaona mbona picha ninayochezewa ni ya kihindi...
Nikauliza "Kwani Careen nae si tunaelekea njia moja, si anakaa Tabata??"
.
Careen akajibu "Yeah ila siendi nyumbani sasa hivi, kuna mahali naelekea na Peter kakubali kunipa lift".
.
Niliumia sana, nilijua hapa nadanganywa, nikajiuliza au ndo vile vinywaji tulivyokunywa kwenye party ndo Careen anaenda kuvilipa.
Nilijilaumu sana kwanini najiita mwanaume wakati sina hata uwezo wa kununua baiskeli, niliamini ningekuwa na gari langu, haya yote yasingetokea.
.
Nikapanda gari la Abdulrahman japo sikupenda, na Careen aliondoka na Peter, nasi safari ikaanza.
.
Baada ya kimya cha muda mrefu, tulipokuwa tunakaribia maeneo ya Mwenge, Abdulrahman akaanza story.
.
Abdul: Is she your bestfriend?!(Yule ni rafiki yako mkubwa??)
.
Mimi: Yes (Nikamjibu kwa kifupi ili tusisumbuane).
.
Akaendelea, "She is so damn beautiful (Ni mrembo sana)".
Nikamjibu kwa kiswahili "Sifa na utukufu kwake muumbaji ".
.
Nilidhani hatonielewa, kumbe alielewa na akanijibu kwa kingereza maneno yaliyo maanisha "Ni mzuri sana, Peter anampenda sana Careen, na kwajinsi navyomjua Peter, najua hawezi muacha kizembe leo ".
.
Mimi: What?? (Nilistushwa sana na kauli hiyo) nikamtazama Abdulrahman kwa mshangao.
Nikauliza, "Kwani wameenda wapi?? "
.
Abdul: Bahari Beach.

Mawazo ya ghafla yakanijia kichwani, itakuwaje mzigo ukiliwa leo?? Sindo mwanzo mimi nitaonekana boya tu??, noo, nishuke niwahi Bahari Beach?? Au nivumilie tu??.

Ghafla nikasikia Abdul amezungumza tena kauli tata kwa kingereza, iliyokuwa ikimaanisha "Na jamaa yuko vizuri sana kwenye kushawishi wanawake, huwa hawamkatai".

Hapo ndipo nilipopatwa na hasira za ghafla, jasho lilianza kunitiririka, na kumwambia Abdul "Naomba unishushe hapo Mwenge".

Abdul: Why??(Kwanini)
Mimi: Just drop me there(We nishushe tu hapo) kuna mtu nataka kuonana nae.
.
Akanishangaa sana, ila akasimamisha gari na kuniacha kisha akakanyaga mafuta na kuondoka.

Sikujali Abdul atanionaje, nilikua na wazo moja tu kichwani.
Kupanda gari na kuelekea Bahari Beach.


Je Chris ataelekea Bahari Beach??? Au ataghairi?? Na kitatokea nini huko mbele ya Peter na Careen???

******-Usikose sehemu ya 4*****
#Itaendelea...

Sehemu ya nne soma hapa
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!!

Sehemu ya nne...

#Ilipoishia: Baada ya Abdulrahman kuniambia kuwa Careen na Peter wameelekea Bahari Beach, nilipatwa na hofu ya ghafla, hasa kwa kuzingatia nipo kwenye vita na Peter, ya kugombania kumpata Careen.

Nikamuomba anishushe, akakubali na kunishusha haraka.
Nilivyoshushwa, wala sikuwa na wazo lingine tena zaidi ya wazo la kupanda gari na kuelekea Bahari Beach.
Niliwahi haraka na kupanda daladala, lakini akili ikanijia kuwa daladala zinasimama simama sana hivyo zitanichelewesha, nikashuka haraka kabla halijaondoka, ikanibidi nitafute tax haraka sana.

#Inaendelea:
Mimi: Kanyaga mafuta, tembea fasta bro.

Dereva: Unakwenda wapi??
Mimi: Huko huko mbele bwana aanh.
Dereva: Mbele kwenye zipu au??
Mimi: Acha utani, niwahishe Bahari Beach.

Akakanyaga mafuta kwa speed kali, lakin nilihisi kama anatembea taratibu.
Ghafla simu iliingia message, niliiwahi sana nilidhani ni Careen, kuitazama nikakuta missed call mbili na message moja, zote zimetoka kwa classmate wangu, Hasheem.
Alikua akiulizia niko wapi na party inakaribia kuanza chuo, nikaona ananipotezea muda, nikachukua simu nakuitia mfukoni.

Kichwa changu kilikuwa kizito sana, kilijawa na mawazo mengi sana juu ya Careen, kuna muda nilijiona mjinga sana, kwanini nafanya yote haya?? Hata huko nakoenda nitafaidika nini hasa?

Pindi gari lilinakaribia maeneo ya Mbezi Beach Tangi bovu, nilikatishwa kwenye mawazo baada ya simu yangu kuita.
Niliidharau sikuipokea, "Hasheem huyu anapiga piga kila mara hadi kero sasa ''- Nilijisemea kwa nguvu bila kuitazama simu kujua anapiga nani.

Simu iliita mpaka ikakata, lakini ikapigwa tena kwa mara ya pili, nikaona sasa Hasheem kazidisha fujo, nikaitoa simu mfukoni ili nifunge mtandao kwa kuweka "Airplane Mode".

Nilipoichukua na kuitazama, nilishangaa kukuta ni Careen ndiye ananipigia.
Sikuamini, nikaitazama simu mara mbili mbili mwisho nikaipokea.

Careen: Hallow.
Mimi: Hello, uko okay?

Careen: Niko poa ila umeniudhi, simu uliweka kwenye kibubu nini?? (Aliuliza huku akijichekesha).

Sikucheka wala nini, nikamjibu "Hapana, niliiweka mfukoni halafu ilikua na sauti ndogo. Bado uko na Peter?? " - (Ilibidi niulize kabisa adui yangu yupo au laanh.)

Careen: Hapana aliniacha tu mahali na kila mtu akaendelea na safari yake.

nikastuka kidogo, nilitamani kuuliza "Mbona Abdulrahman alisema mpo wote Bahari Beach ", ila ikabidi ninyamaze ili nipewe uhakika zaidi.
Nikauliza "Kwani uko wapi sasa hivi??".

Careen: Nipo Kinondoni sasa hivi, nitalala huku huku kwa dada yangu.
Hata hivyo nimekupigia nijue umefikia wapi??

"Kheee " nilitoa mshangao, nikajisemea kimoyoni "Sasa kwanini niliambiwa yuko Bahari Beach?"

Sikujibu swali la Careen, nikakata simu kwanza, na kumwambia dereva tax asimamishe gari "Oya broo, hebu simamisha mbele hapo kwenye zipu, tangi bovu " (Nikatumia utani wake).
Akaniuliza "Vipi mbona umekatisha safari? "

Nikamwambia "Anh nayemfata hayupo huko "
Akajibu "Basi niongeze mkwanja nikurudishe mpaka Simu 2000".
Nikamcheck, nikamjibu "Acha ujinga wewe, daladala nauli bei chee tu."

Akasimamisha gari, nikashuka na kumlipa hela yake.
Nikaelekea moja kwa moja mpaka kwenye kituo cha kusubiria daladala.

Nilijicheka sana, nikajiona boya, lakini nilijiuliza sana kwanini Abdulrahman alinidanganya, nikapata jibu kuwa huenda wanahisi kitu kati yangu na Careen, hivyo wanajaribu kunipima hisia, au kuniharibu kisaikolojia.

Kutokana na tabu ya usafiri, nilifika Gongo La Mboto majira ya saa 4 usiku, kwavile nilichoka sana, nilienda hostel tu kulala na wala sikuwa na hamu ya kwenda kwenye bhash chuoni.

Weekend niliitumia vizuri sana kuchat na Careen, na ilizidi kunoga zaidi na zaidi, huku nikionyesha umahiri wangu kwenye kujali, kuheshimu , kumthaminisha na kumchekesha pia.
Alifurahia sana kuchat na mimi, na kuna nyakati alinipigia tukazungumza sana kwa muda mrefu mazungumzo ya maisha na mambo mbalimbali.

Lakini mwisho tulijikuta tumedondokea kwenye mazungumzo ya mahusiano.
Careen: Unajua kaka Chris tangu nikujue, unanifurahisha jambo moja.

Mimi: Jambo gani hilo mamie??

Careen: Unanijali sana, unanipa sana kipaumbele, na hata kunithamini pia. Kiukweli najisikia furaha sana kuwa na rafiki kama wewe.

Mimi: Asante sana, ni jukumu langu kuhakikisha rafiki yangu anajisikia yupo na rafiki anayejali uwepo wake.

Careen: Nashukuru sana kwa hilo, Mungu akuweke miaka mingi. Huwa unanikumbusha mbali sana.

Mimi: Mbali wapi tena mamie?

Careen akakaa kimya kidogo, kisha akaendelea maongezi "Leo ngoja nikupe siri moja maana umeshakua rafiki yangu, na ni zaidi ya rafiki, umekuwa kama ndugu kwangu.
Kaka Chris unanikumbushaga mwanaume ambaye sikuwahi kumpenda hapo zamani, alikua anaitwa Khalfan."

Akanyamaza kidogo, nikazidi kupata shauku ya kutaka kujua zaidi, maana nilijua nikijua madhaifu ya Careen basi lazima nitafanikiwa kumpata kiurahisi.

Akaendelea "Huyo kaka tulianza uchumba kipindi hicho niko form two, alinipenda sana ila tatizo mimi sikumpenda, nilimkubali tu sababu enzi hizo kundi langu wote walikua na maboyfriend kasoro mimi, halafu Khalfan alikua na vijisent kidogo "

Nikaguna "mmmh ", akaendelea "Sasa kipindi hicho nilikua sijui mapenzi nini, kwahiyo zile kuonyesha kunijali, mara message, mara anipigie simu, halafu alikua na wivu.
Basi nikawa naona kero sana, mpaka kuna muda nilikua namkatia simu, au naizima tu kwa makusudi "- (akazungumza huku anajichekesha).
.
Nikamuuliza "Kwahiyo bado mpo pamoja??? "

Akajibu "Hapana, tuliachana form 4. Aliniheshimu sana, na wala hatukuwahi kusex."

Nikamjibu "Duh kweli huyo alikupenda "
Akaniambia "Kweli kabisa, na najutia kumpoteza.
Sababu akili ilikuja kunijia pindi nilipokuwa form six, ndipo nilimpata huyu boyfriend wangu wa sasa "
Nikastuka sana kusikia neno "boyfriend wake wa sasa "

Akaendelea "Nilikuja kugundua mapenzi ni nini baada ya kumpenda huyu boyfriend wangu wa sasa, yani wala hanijali wala kunithamini, yani yeye kila kitu ni ubabe na kuniforce tu, najitajidi sana kujitunza kwaajili yake lakini yeye hajali, na ananisaliti mara kwa mara.
Nayatamani sana maisha yangu ya zamani, natamani ningekua na Khalfan"- (Alizungumza kwa hisia sana na kuonyesha akimaanisha kile anachosema)

Niliyapokea maneno hayo kwa masikitiko makubwa sana, nikamtia moyo, pia nikajaribu kumpa ushauri wa kinafki ili aone kama namsapoti.
Akanishukuru sana kwa ushauri wangu, na kumtia moyo, na mwisho akanitakia usiku mwema.

Jumatatu iliyofata niliamka nikiwa mwenye furaha sana, huku nikiwa na matumaini mapya ya kumpata Careen hasa ukizingatia nimeshajua madhaifu yake yako wapi, nini anakosa kwa boyfriend wake.

Nilimtumia message, akaniambia yuko anapata kifungua kinywa kwenye mgahawa wa kifahari wa Legacy, uliopo ndani ya chuo.
Nikawahi mpaka mahali hapo, lakini sikufurahishwa na nilichokiona, nilimkuta Careen akiwa anapata breakfast pamoja na Peter na Abdulrahman.

Nikasonya kwa mbali.
Nikawasogerea, nikatoa salamu, kisha nikaagiza chakula na kujumuika nao.
Story zilinoga, tukamaliza kula, tukanyanyuka na sote tukaelekea mahali pakulipia bills.
Kimbembe kilianza wakati wakulipa bill.

Muhudumu: Jumla Tsh.9500.
Nikamtazama muhudumu, nikajisemea kimoyo moyo "Leo lazima niwavimbie hawa watu ".
nikaingiza mkono mfukoni na kutoa noti ya Tsh elfu 10 na kumpa muhudumu, nikamwambia "kata yote".
Peter kwa kutaka sifa nae, akasema "Bro, don't worry, i'll pay(Kaka usijali, nitalipa mimi)".

Nikamtazama Peter, nikamsisitizia muhudumu "Kata yote humo humo tu "
Abdulrahman akanitazama, aliniona pindi naichungulia pesa mfukoni, alijua wazi sina hela nyingine zaidi ya hiyo elfu 10 niliyotoa.

Akamtazama muhudumu, na kumwambia kwa kingereza maneno yaliyo maanisha "Utaniletea juice ya elfu 3 ya Azam Mango kwaajili ya Careen, na maji ya kilimanjaro lita moja kwaajili yangu, atalipa Chris."

Nikashangaa sana kauli alizotamka Abdulrahman, nilihisi huyu jamaa ana nia ya kuniua kwa presha.
Nilianza kuvurugwa akili, nikajihisi kama mwenye bahati mbaya siku zote, kila siku niaibike mimi tu.

Careen aliustukia mchezo na kutamka maneno yaliyonipa nguvu, akasema "No, sihitaji juice, nitachukua maji tu, na Peter utalipia bill yote."
Akageuka na kuelekea kwenye fridge la kuchukulia maji.

Peter akatoa hela na kulipa, kipindi Abdulrahman akinisogerea karibu, akanong'ona "Hey young man, did you really follow her that day?? (Hey kijana, ulimfata kweli siku ile???).

Nikajua sasa bifu la mafahari wawili, ndipo linapoanzia.
Nikamjibu, "Its none of your damn business bro"(Haikuhusu kaka).

Akacheka kinafki, akaongeza sauti na kusema kwa kingereza maneno yaliyo maanisha "Hahah kumbe unampenda sana eenh??!! Hujaona wasichana wengine? Wewe sio wa aina yake, anahitaji mwanaume, sio mvulana kama wewe."

Nilipandwa na hasira, nikasahau niko maeneo gani, sikutazama nyuma yangu kuna nani, nikaropoka " Kwa uzuri gani hasa aliokua nao, nimpende yeye nani?? Wewe kula kulala ndio unajiita "Mwanaume ", unachekesha sana, sina shida na huyo kinyago wenu, Careen Careen, kwanza sio type yangu. Kimwanamke kimechongoka kama spoku, mxieeeeew.
Nikasonya ".

Wote wakabaki wananitazama, sikuelewa kwanini hawakujibu walibaki wameduwaa, niligeuza macho pembeni nikaona jinsi wengine pia wanaokula kwenye meza wakinitazama.
Nilijistukia, lakini nilishangaa zaidi kuona Peter na Abdulrahman wakiwa wameduwaa kuelekea upande mmoja, ikanibidi nigeuze macho yangu kutazama wanachotazama.

Uso kwa uso, macho yangu yalikutana na ya Careen aliyekuwa amebaki ananishangaa huku akilengwa na machozi
.

Je nini kitafuata??! Careen atamchukuliaje Chris???.

******Usikose sehemu ya 5*****
#Itaendelea...

Sehemu ya 5 soma hapa
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)..!!!

Sehemu ya tano...

#Ilipoishia : Kutokana na hasira ilivyonipanda nilijikuta namtolea maneno makali Abdulrahman juu ya Careen.
Wote walibaki wakinitazama kwa mshangao mkubwa, hata watu waliopembeni pia.
Lakini Abdulrahman na Peter wao walionekana kuangalia kuelekea upande mmoja, nyuma yangu, ndipo nilipopata wazo la kugeuka kutazama wanachoshangaa.

Macho yangu yalikutana uso kwa uso na Careen aliyekuwa ananishangaa, huku akilengwa na machozi.

#Inaendelea:
Moyo ulistuka sana, nilihisi mwili kama umemwagiwa maji ya baridi, nikajiuliza kimoyomoyo "Nimefanya nini mimi leo ".

Careen alikuwa ameganda kama sanamu akinitazama, macho yake yalikuwa yakimlenga lenga machozi, alionekana kuguswa na kuumizwa juu ya yale maneno machafu niliyo yatoa hasa ukizingatia mbele za watu.

Akashindwa kuvumilia, akaanza kulia huku akianza kutembea kwa haraka sana kuelekea nje ya mgahawa.

Akili ya fasta ikanituma nimkimbilie nimuombe msamaha hapo hapo, nikamuwahi kwa mbele, alikua na hasira sana, akanisukumiza pembeni na kuongeza mwendo kama anakimbia vile.

Nikanyanyuka na kumkimbilia tena.
"Careen, Careen, pls nisamehe, nimeropoka hasira tu"- Nilizungumza huku nimemkamatia mkono wake wa kushoto, akautikisa kwa nguvu na kuongea kwa hasira "Niache, niache kabisa, "- Alizungumza kwa hasira huku analia.

Lakini sikumuachia mkono wake, ikabidi atumie nguvu kuniachisha mkono, bado nikawa nimeng'ang'ania huku naomba msamaha.
Ghafla akaja Peter na akaunyofoa mkono wangu mikononi mwa Careen na Careen akaendelea na safari yake anakokujua mwenyewe.

Nilibaki nimeduwaa nisijue nini cha kufanya, moyo uliniuma sana.
Kugeuka pembeni yangu alikua amesimama Peter na Abdulrahman, kwa mbali nyuma yangu kulikua na wanafunzi kadhaa waliokuwa wakishuhudia picha ya kihindi niliyokua naicheza.

Machozi yalinitoka, ndio mara yangu ya kwanza kuona mwanaume anamwaga machozi.
Nilihisi kama mtu amenigusa bega langu la kushoto, nikageuza shingo ili kumtazama ni nani, nikakutana na uso wa Abdulrahman.

Akazungumza kwa kejeli maneno ya kingereza yenye maana ya "Kijana, huu mchezo hauhitaji hasira".
Kisha akacheka kwa dharau, Peter nae alikuwa akinitazama kwa dharau huku akijichekesha.

Nilijiona mjinga sana, nilitamani kuwapiga hata ngumi za uso, ila tatizo sheria za chuo zingeniandama, nikavumilia hivyo hivyo japo nafsi iliuma sana.
Nilirudi mgahawani na kuchukua begi langu, kisha kuondoka huku watu wakinitazama, wengine wakinicheka sana, na kina Peter walionyesha kufurahi baada ya mpango wao kutimia wa kunitoa kwenye reli ya Careen.

Nilizunguka chuo kizima, kila kona, kila darasa, kila faculty, lakini sikumuona Careen.
Nikajipa moyo labda atakuja darasani kwenye kipindi, lakini nako hakuonekana.
Nilikaa darasani kwenye kipindi, akili yangu haikuwa kwenye kile kinachofundishwa, kipindi kikaisha na sikutaka kubaki chuo, nikarudi hostel kupumzika.
Nilimpigia simu, hakupokea, sms hakujibu, Whatsapp aliniblock.
Na siku yangu iliisha vibaya kama hivyo.

Siku tatu mfululizo mambo yalikuwa tofauti kati yangu na Careen, hata darasani hatukukaa pamoja tena.
Hatukuwa na story wala salamu, alikuwa akinipita kama hanijui.
Alikua akitoka kwenye kipindi, basi lazima utamkuta yuko na Peter na Abdulrahman.

Nilikua naumia sana, nilimtumia message nyingi sana za kumuelewesha, na hata za kumuomba msamaha.
Kuna nyakati nilikua najaribu kumuongelesha ana kwa ana tukikutana, lakin alikua kama hanisikii.

Siku ya nne tangu aninunie, niliamua kushinda hostel tu pamoja na classmates wangu, Hasheem na Ramadhan, tukawa tukipiga story mbili tatu.
Hasheem: Kwani Chris vipi siku hizi na yule manzi? Mbona naona mnakwepana sana, au ndio umemtongoza kakuchomolea?!

Mimi: Anh hamna, nilimkorofisha kidogo, basi kanuna kabisa hataki hata tuzungumze.

Ramadhan: Umemfanyaje kwani?? Maana mpaka kakununia, basi ujue umemkera sana.

Ikabidi niwaelezee vizuri toka mwanzo mpaka mwisho.
Wote walionekana wakinisikiliza kwa umakini zaidi, na pindi nilipomaliza, Hasheem alinipa pole sana lakini akaniambia "Wewe kidume bwana huna haja ya kumnyenyekea mwanamke, mpige chini bwana, kwanza hana faida kwako ".

Lakini Ramadhan alizungumza maneno yaliyo niingia.

Ramadhan: Bro hilo sio tatizo dogo, ni tatizo kubwa sana.
Wanawake wameumbwa na aibu sana, hawajiamini sana, kwahiyo anapopata maneno yenye kumsifu huwa anapata uwezo wa kujiamini, anaua ile aibu yake na hujikuta anampenda sana yule mwenye tabia ya kumsifu, sababu ndiye anayempa nguvu".

Nikakumbuka kweli Careen aliwahi niambia nifungukia kiasi gani ananikubali kwa kumjali na kumthaminisha kwangu, na vile ninavyomfanya amkumbuke boyfriend wake wa zamani.

Nikarudisha masikio yangu tena kumsikiliza Ramadhan, akaendelea kusema "Anapopitia mateso ya kihisia kwa kumpenda boyfriend ambaye hamjali, hamthamini, anamshusha hadhi, haonyeshi kumpenda, anatoa kauli za kejeli, basi hata kama yeye ni mzuri kiasi gani, hujikuta anaanza kujichukia, anajiona labda ana nuksi, labda mbaya, anakosa kujiamini, anakosa kujithamini.

Sasa anapokuja mwanaume mwingine hata kama ni rafiki, lakin anaonyesha kumjali, kumuheshimu, na kumthamini, basi hujikuta anapata mwanga mpya wa maisha yake.
Kosa baya ambalo humrudisha kwenye maumivu, ni pale huyu mwanaume anapokuja kutoa kauli za kejeli, basi hujikuta anarudia kuyakumbuka machungu yale yale ya mwanzo anayoyapata kwa boyfriend wake ".

Alinyamazia hapo, maneno yaliniingia kisawa sawa, mwanzo niliona kama Careen amenuna sababu ya kikosa kidogo sana, lakini sasa nikawa nimepata mwangaza wa ukubwa wa kosa langu.

Nikamuuliza "Dah man umenigusa sana, ila sasa unanishauri nifanyaje ili anielewe"

Akaguna kidogo, akakaa kimya kwa dakika kadhaa, kisha akazungumza "Kwasasa hapokei simu zako, hajibu sms zako, hataki kuongea na wewe ana kwa ana, anahisi aibu kuzungumza nae, anapata hasira kuonana na mtu kama wewe uliyeongeza donda lake lililosababishwa na boyfriend wake.".

Akatafakari tena kisha akaendelea "Kuna njia moja tu unayoweza mshawishi, nayo ni SMS. Sababu simu ukipiga hatojibu, ana kwa ana unaweza hata tukanwa au ukamzidisha hasira, lakini sms atake asitake kwa kiranga chake lazima atasoma tu.".

"Kaa chini tulia, andika sms moja nzito sana, weka hisia zako humo jinsi gani unauthamini uwepo wake, weka machungu yako humo jinsi gani unajutia kosa lako, na uweke ukweli halisi kwanini uliropoka yale maneno, sababu Careen haelewi bifu lililoko kati yako na kina Peter, muweke wazi vita inayoendelea, lakini chunga usionyeshe hisia zako kuwa unamtaka kimapenzi sababu kwasasa ana machungu ya boyfriend wake, lazima utamuongeza hasira."- Akaishia hapo.

Nilishusha pumzi nzito sana, nilijihisi kama niliyetua mzigo mzito kifuani kwangu, hakika sikujutia kutoa yaliyonisibu kwa hawa watu wawili, japo Hasheem alitoa ushauri mbaya, lakini nilipata Ramadhan aliyetoa ushauri wenye kunivua matatizo yangu.

Niliwashukuru sana, na kuamua kukaa chini kiutulivu na kuandika message iliyowakilisha machungu yangu na kumtumia Careen.
Ilikua ni message ndefu sana iliyojaa kila kitu alichonishauri Ramadhan.

Baada ya kama dakika 26 hivi nilistukia simu yangu inaita, kutazama mpigaji alikuwa ni Careen, niliruka ruka juu kwa furaha kama chizi nusura nivunje Laptop ya Hasheem.
Wote wakabaki wananishangaa, lakini ghafla nilipoa, nikaanza kujipa maswali ya kijinga kichwani kuwa itakuwaje endapo Careen ananipigia ili anichambe, lakini Ramadhan akanipa moyo na kusema "Pokea tu, jiandae kwa lolote utakaloambiwa, na kama amepanga kukutusi basi asingehangaika kukupigia"

Kipindi napokea ushauri huo, nikastuka simu tayari imeshakata, lakin baada ya sekunde kadhaa, akapiga tena na sasa nilikua tayari kumsikiliza.

Tulisalimiana, lakini alikuwa akizungumza kama mtu mwenye kulia, aliniomba msamaha kwa kuninunia bila kujua sababu, lakini alinilaumu sana kwanini sikumuweka wazi mapema kuhusu bifu kati yangu na kina Peter.

Akaniambia kuwa hawezi kuwa na marafiki ambao wao kwa wao hawaelewani, hivyo kesho majira ya saa 10 jioni tukutane Mbalamwezi Beach Resorts, mimi, yeye, Peter na Abdulrahman, ili tuweze kuweka upatano kati yetu.
Nikakubali alilosema, mwisho na kuahidi kufika maeneo hayo mapema.

Kesho yake kama kawaida nilivunja kabati na kuwahi Mbalamwezi Beach, nilipofika niliwasubiri kama nusu saa kisha nilianza kuona Careen akija, baadae Peter na Abdulrahman wakija pamoja.

Tulikaa mahali tulivu tukipata vinywaji huku tukiyazungumza, tukayajadili sana mwisho tukafikia maelewano, tukaanza urafiki hapo hapo na Careen aliamuru tupeane na namba za simu ili tuwe tunachat, na bifu likaisha japo niliamini moyoni mwa kina Peter na kwangu bifu lilikuwa bado lipo.

Wakati wa kuondoka, tulipewa lift kwenye gari walilokuja nalo kina Peter, mpaka buguruni, wao walikua wakielekea Mbagala kwa siku hiyo.
Tulishuka na kwenda kugombania magari ya kwenda Gongo La Mboto.
Lakini cha ajabu Careen alinipa simu yake na mkoba nimshikie sababu anaogopa kuibiwa pindi tukitaka kugombania gari.
Nikaupokea mkoba wake, nikaushika mkononi, na simu nikaiweka mfukoni.

Daladala ikaja japo imejaa kiasi lakini wote tukaigombea mpaka tukapanda, nilisimama mbali kidogo na Careen.
Bus lilipofika njia ya panda segerea, Careen aliomba kushuka, akashuka na kuniomba mkoba wake dirishani, nikampa.
Lakini kwa bahati mbaya nilisahau kumpa simu, na kwa haraka aliyokuwa nayo Careen kwa siku hiyo, wala hakutazama kama simu ilikuwa ndani ya mkoba wake au laanh, aliondoka na huku bus letu liliendelea na safari.

Pindi nimefika hostel majira ya saa 3 usiku, nilistukia simu inaita mlio tofauti na wangu, nikapapasa na kushangaa kukuta ni simu ya Careen, ndipo nilipostuka kuwa sikumpa simu Careen.
Kutazama anayepiga ilikuwa ni namba iliyoseviwa "Mom", nikajua ni mama yake Careen anapiga, nikaogopa kupokea.
Simu ikakata, baada ya sekunde mbili ikaingia message.

Nikajaribu kuikumbuka Pattern lock ya Careen, sababu kuna siku aliwahi chora pattern mbele yangu.
Nilivyoikumbuka nikaijaribu na ikakubali.

Kuisoma message ilikuwa ni kutoka kwa "Mom", ilisema "Hi Chris, nimeshindwa kukutafuta kwenye namba yako sababu sijaikariri na iko humo kwenye simu. Najua unaijua Pattern yangu na message hii itakua umeisoma. Please, naomba uizime simu, ni kheri boyfriend wangu aikute simu haipatikani kuliko ikiwa haipokelewi. Na pls usipokee simu ya mtu yeyote ".

Nilimuelewa sana alichomaanisha, nikamjibu "Sawa usijali "
Kisha nikashika kitufe na kutaka kuizima simu yake.
Lakini ghafla wazo likanijia kichwani, kwanini nisisome kwanza message wanazotumiana kati ya Careen na Peter??
Nikafunga minara kwa kuweka "Airplane Mode ", kisha nikazama inbox na kuanza kusoma message Careen na Peter.

Nilichokiona kiliniumiza sana, Peter alikua amefikia hatua nzuri sana ya kumpata Careen, huku akionekana mwenye kumjali zaidi yangu, hata kumtumia mara kwa mara pesa za matumizi.
Niliumia sana, niliona kama nilishazidiwa kete.

Lakini kilichoniumiza zaidi, ni baada ya kuona message za Peter akizungumza kuhusu mimi, kiukweli ziliniumiza sana, Peter alikua ananipondea sana, akaniharibia vya kutosha, na hata kumshauri Careen aue urafiki na mimi.
Ilinichukua masaa mawili na nusu kusoma messages zao na zilinipa hasira sana.

Nilishtushwa na muito wa simu yangu, kuitazama alikua ni Peter akinipigia, kwa hasira nilizonazo nikaikata.
Hakuridhika akapiga tena, sikuipokea, akarudia tena kama mara 4 na wala sikuipokea.
Mwisho akaamua kutuma message kwa kingereza, yenye maana ya "Hey Chris, Umezungumza na Careen kama amefika?? Nampigia simu yake hapatikani."

Nikajisemea kwa nguvu "Ina maana huyu mwehu hakuwa ana nia na mimi, ila ana nia ya kujua kama Careen kafika??! Anachowaza ni Careen tu? Ndiomaana ananikandia kwa manzi ili ampate yeye, sasa ngoja nimuonyeshe".

Kwa hasira nilizonazo baada ya kuchefukwa na message zake alizochat na Careen, na sasa ananiuliza kuhusu Careen.
Nikamjibu message yake kwa kingereza, nikimaanisha "Bro acha usumbufu, Careen niko nae kalala "

Inaonekana message ilimstua sana, akapiga tena mara mbili, nikakata, nikamuongeza message nyingine "Nishakwambia acha usumbufu, Careen kalala, kwangu, kifuani kwangu, kama huamini piga tena kwenye namba yake ".

Nilivyomtumia hiyo message, nikaifungua minara haraka ya simu ya Careen, baada ya sekunde kadhaa Peter alipiga simu kwenye simu ya Careen, nikaipokea na kumsikiliza Peter alivyokuwa akilalama, kwa dharau na hasira juu nikamfokea kwa nguvu "BRO acha usumbufu watu tumelala "- Nikazungumza na kukata simu hapo hapo kisha kuzima simu ya Careen na simu yangu.

Nikacheka sana, sikujali kitakuja kutokea nini, nilichojali ni kuwa leo nimemnyoosha adui yangu, na lazima afe kwa presha leo "Sambaaf mxieeew"...!!!


Je, kitatokea nini kwa Peter?? Careen atajisikiaje akija kugundua yaliyotokea??

Usikose sehemu ya 6
Itaendelea....

Sehemu ya sita soma hapa
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Sita

#Ilipoishia: Nilimfokea Peter kwa ukali sana na kumuambia kama haamini niko na Careen, basi ajaribu kupiga simu ya Careen ili nimthibitishie.

Peter hakuamini nilichosema na kuamua kupiga kwenye simu ya Careen ili kuthibitisha kama ni kweli nimelala nae au namzingua tu.
Alivyopiga nikapokea, nikamsikiliza kwa dakika kadhaa anavyolalama, kisha nikamjibu kwa ukali "Bro acha usumbufu watu tumelala "- Nilivyomaliza kuongea tu nikakata na kuzizima simu zote, yangu na ya Careen.

#Inaendelea:
Moyo wangu ulijawa na amani sana, nikufurahia kwa kiasi kikubwa sana nikijua kuwa leo nimefanikiwa kumlaza na presha adui yangu.
"Wamenitesa sana, na kuanzia sasa itakua zamu yao"- nilijisemea kwa nguvu huku nikitabasamu.
Na mwisho nikalala nikiwa natabasamu kubwa sana.
.
Asubuhi nilipoamka, jambo la kwanza lilikua ni kuwasha simu yangu.
Mara message ikaingia, nikaifungua nikakuta ni Hasheem amenitumia, ilikua inasema "Oya njoo chuo mara moja, nimekutana na Careen hapa anakuulizia, tumekupigia hupatikani, we jamaa chenga sana".
.
Nikajua tu wazi Careen alikuja chuo kwaajili ya kufata simu yake, nikaamka haraka na kujiandaa ili kumpelekea simu yake.
Njiani wakati naelekea nikakumbuka kitu, sikufuta kumbukumbu ya simu aliyopiga Peter, "Najua Careen atakuja kutazama watu waliompigia, halafu tatizo mimi niliipokea"- nilijisemea kimoyo moyo.
"Na itakuwaje kama atakuta messages za peter akizungumzia mimi kulala na Careen? Endapo kama ametuma pindi nilipoizima.
Ngoja niwashe na kuhakikisha kabisa."- Nilijiuliza kwa sauti ya chini.
.
Nikaichukua simu ya Careen na kuiwasha, nikaingia upande "Call logs", na kufuta kumbukumbu ya simu ya Peter kwenye "Received calls".
Nilipomaliza, nikataka kuizima lakini ghafla ikapigwa simu hapo hapo.
Ilikua ni namba iliyoseviwa "Honey ", nikajua wazi huyu atakua ndiye boyfriend wake Careen ambaye nilishawahi elezewa na Careen.
.
Sikuipokea simu yake, nikaicha iite mpaka ikate, kisha nikaenda kufuta kumbukumbu ya simu hiyo iliyoingia kwenye "Missed calls " kwa kuhofia kuwa Careen asije gundua kuwa niliwasha simu yake wakati aliniambia niizime.
Nilipomaliza kufuta nikaizima.

Nilipofika maeneo ya chuo, nikakutana na Careen ambaye alipendeza sana, nahisi aliaga kwao anaenda kanisani, tukasalimiana.

Careen: Vipi hakupiga mtu yeyote jana?? (Aliuliza huku akiiwasha simu yake).

"Hapana hajapiga mtu, niliizima tu pale pale uliponitumia message kuwa niizime" (Nilizungumza kwa kujiamini japo nilijua kuwa nilikua nadanganya).

Kupiga jicho kwa mbali nililiona gari la Peter likiwa linaingia ndani ya chuo.
Nikajua wazi ni Peter na Abdulrahman wamekuja kuhakikisha kama ni kweli nililala na Careen usiku wa jana, au labda walitaka kuja kuulizia kwa marafiki zangu kuhusu mahali napoishi ili waje kunifanyia varangati.

Nikapiga hesabu za haraka, nikagundua kuwa roho yao itawauma sana wakinikuta nimesimama na Careen, sababu itathibitisha kuwa ni kweli nililala nae jana.

Nikaona huu ndio wakati muafaka wa kuzidi kuwaumiza roho, nilitaka wasinikute nimesimama nae tu, bali wanikute hata nafanya nae jambo ambalo litawaumiza zaidi.

Nikaona wamepark gari lao, wakashuka na kuanza kupapasa macho huku na huko kutazama kama wanaweza niona mimi au hata rafiki yangu.
Wakamuona Hasheem, wakamfata na kuzungumza nae, nikamuona Hasheem akiwaelekeza mahali ambapo tulipo.

Wakaanza kuchukua hatua na kujongea maeneo ya garden ambapo niliposimama na Careen.
Nikaona huu ndo wakati muafaka wa kuanza kumsogeza Careen karibu ili watukute tunafanya kitu chochote cha kumuumiza roho.

Wazo likanijia kichwani haraka, nikaichukua simu yangu na kuweka wimbo wa Marc Anthony uitwao "I need you".

Careen alipousikia huo wimbo akaacha kuchezea simu na kuanza kuuimba.
Nikamwambia "Unaweza kuuimba, unajua na kuucheza au? "

Akanijibu "Anh mie noma sana kwenye hiyo miondoko, au nikuonyeshe?" (Akaongea huku anajichekesha).
.
Nikamuambia "Unaonaje ukicheza nikuone?? "- (Nikamtupia swali la kiuchokozi).

Careen: Mmmh hapa?? Hadharani kama hivi?"
.
Nikamjibu "Yeah tena leo jumapili unajiachia tu, hakuna watu wengi, au unataka tucheze wote? "- (Nikaongeza uchokozi).
.
Akanitazama kwa sekunde kadhaa, kisha akajibu "Unaweza? "
Nikamjibu "Ndio, njoo tucheze "- (Nikaongea huku namsogerea kwa ukaribu zaidi).

Nikamshika kiuno kwa mkono mmoja na kukisogeza karibu yangu kabisa, mkono wangu mwingine ukiwa umeshikana na mkono wake wa kushoto.

Akanitazama usoni, nami nikamtazama usoni kwa jicho la mahaba, kisha nikamkonyeza, akatabasamu na tukaanza kucheza.

Careen alionekana mjuzi sana, lakini nami sikuwa nyuma kwenye kuonyesha umaridadi wangu.
Kutokana na miguso ya ukaribu, na jinsi nyimbo ilivyo ya hisia, na aina yetu ya uchezaji ilikua yenye uchokozi mwingi.
Tulijikuta tukiongeza ukaribu zaidi na zaidi.

Kutupia jicho kwa mbele, nikamuona Peter na Abdulrahman wakiwa hatua chache mbele yetu, walibaki wakiwa wameduwaa, na niliona machungu aliyonayo Peter moyoni mwake.

Macho yake yalionekana kuvimba kuashiria kuwa hakulala, na alilia usiku kucha.
Kwavile niliona wananitazama, na Careen hajagundua kama kuna watu, ndipo nilipozidisha utundu kwa kumsogeza karibu zaidi na kupeleka lips zangu kutaka kumbusu shavuni.

Ghafla nikakatishwa na sauti ya Peter akiita "Careen".
.
Careen akastuka, sote tukageuka na kuwatazama.
Wakatusogerea karibu, Careen alijihisi aibu, lakini mimi wala sikujali.
Nilikuwa mwenye furaha sana moyoni.

Wakatusalimia, kisha Peter akamvuta Careen kwa hatua kama kumi hivi pembeni yetu.
Nikawa nimebaki na Abdulrahman ambaye alionekana akinitazama kwa jicho la hasira, lililojaa uchu wa kunipiga hata ngumi ya uso.

Akanitazama kwa hasira, kwa sauti ya chini akauliza "Ulilala nae kweli?? ".
.
Nikaona sasa wakati wa kuanza kuwatambia umefika, nikamsogerea, kisha nikacheka kwa dharau na kumuambia "Ulitaka nirecord na video ili uamini?? Siwezi kufanya ujinga huo."

Akaanza kupandisha hasira, nikamwongeza neno lingine, "Nahisi sasa ushaanza kuelewa Careen anahitaji nini maishani mwake, haitaji mwanaume tu, anahitaji mwanaume kamili aliyekamilika kama mimi, na sio Peter".

Akapandisha hasira zake na kutaka kunipiga ngumi ya uso, lakini ghafla akasita baada ya kusikia akiitwa na Careen ili wakajadili kitu pamoja na Peter.
Ikabidi azuge kama alikua anataka kunitoa sisimizi kwenye shavu.
.
Nikacheka kwa dharau, alipotaka kuanza kuondoka kuelekea kwa kina Careen, nikamuita, akasimama.
Nikamuwahi kwa nyuma na kumshika bega lake kwa dharau, huku nikimtamkia maneno ambayo yeye aliwahi nitamkia.

Nikamuambia "Kijana, hii ni mechi ya wanaume wa shoka, kuwa makini, huu mchezo hauhitaji hasira".
.
Maneno yalimgusa sana, nilimuona akikunja ngumi yake lakini hakufanya lolote zaidi akapiga hatua kuelekea mahali walipo kina Peter kwaajili ya majadiliano.

Nilisimama huku nikiwa mwenye furaha baada ya kuwanyoosha kisawa sawa, nikajisemea "Malipo hapa hapa duniani".
.
Mazungumzo yao hayakuonekana yenye kunipa wasiwasi kuendana na nyuso zao, lakini sikutaka kujihakikishia kwa nyuso tu, nilitaka kusikia japo kidogo ili kuthibitisha.
Nikatafuta sababu ya kunyanyuka na kujisogeza hatua kadhaa huku nikijifanya natafuta kijiti, nikaanza kusikia mazungumzo.
Peter alikua akijaribu kumficha Careen kuhusu sababu za kuvimba kwa macho yake, na kwanini mekundu.
.
Akamficha sana, ndipo nilipogundua kuwa sio mimi tu ambaye huwa hapendi Careen ajue hisia zangu juu yake, kumbe hata Peter hapendi kujulikana hisia zake juu ya Careen.

Nikaokota kijiti, na kujifanya nafungulia simu kisha nikarudi kupumzika kwenye benchi lililopo karibu.
Walipomaliza kuzungumza wakaja kuniaga, kwa mara ya kwanza Careen alinikombatia wakati wa kuagana.

Hii ilizidi kuwaumiza zaidi kina Peter, wakanitazama kwa jicho la chuki.
Tukaagana na wao wakaondoka kuelekea walikopark gari, nami nikarejea hostel.

Mchana Nilichat sana na Careen, na alikuwa mwenye wasiwasi sana kuhusu boyfriend wake.
Aliniambia kuwa boyfriend wake hapokei simu, wala hajibu message na anahisi ni kwasababu simu yake ilizimwa usiku kucha, ila mimi nilijua wazi kwavile sikumpokelea simu mida ile asubuhi, ndiomaana ameongeza hasira zaidi.

Majira ya saa mbili usiku, simu yangu iliita.
kutazama alikuwa ni Careen, kuipokea tu nikasikia sauti ya Careen akiwa analia.

Nikauliza "Careen nini? Mbona unalia?? "- (Niliuliza kwa hofu kubwa nikitaka kujua kwanini alikuwa analia).

Careen: Chri...chri...chris, Boyfriend wangu, ameni...(Alishindwa kumalizia na kubaki akilia sana).
.
Nikajitahidi kumbembeleza ili angalau anyamaze anieleze vizuri, hofu yangu kubwa ilikuwa huenda jambo nililofanya asubuhi ndio limeleta tatizo.

Careen Akanyamaza kidogo na kuanza kunielezea japo huku sauti inakwama kwama "Boyfriend wangu aligoma kupokea simu zangu leo kutwa nzima, wala kujibu message, nimemtumia message nyingi sana nikijaribu kumuelewesha kwanini simu yangu haikuwa hewani ".

Akagoma kidogo na kulia kwanza, kisha akaendelea
"Amenitumia sms za matusi, na bado akaniambia mimi malaya, ndiomaana jana nilizima simu usiku ili nilale na mwanaume wangu.
Nimejitetea sana, lakini akaniambia mbona asubuhi nimekupigia na hukupokea na bado ukanizimia simu".- (Akagomea hapo na kuanza kulia zaidi).

Nilistuka sana kusikia maneno hayo ya mwisho, hasa ukizingatia mimi ndiye niliyeiwasha simu asubuhi halafu sikuipokea simu ya boyfriend wake.

Careen: " Kaka Chris kwani kweli uliiwasha simu leo na yeye akapiga simu??? Au ananitafutia sababu tu ya kuniacha? "- (Aliuliza swali kwa uchungu mno, huku akiendelea kulia).
.
Niliposikia hilo swali, nilibaki nimezubaa kama sanamu nisijue nini cha kujibu.

Nikajiuliza, itakuwaje nikijibu ndio, atanichukuliaje??? Na wakati yeye anampenda sana boyfriend wake.
Na nikikataa je itakuwaje???
Nilibaki nimenyamaza nisijue nini cha kujibu, nikaamini kweli "Mbio za sakafuni, huishia ukingoni.".
Mbwembwe zangu zote zimenipeleka kubaya.

Careen akauliza tena "Nijibu kaka Chris
"

"Je Chris atajibu nini???"

Usikose sehemu ya 7
#Itaendelea......
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Saba

#Ilipoishia: Careen aliniuliza swali tata huku akilia kwa uchungu, aliuliza kama ni kweli niliwasha simu yake, na kama ni kweli boyfriend wake alipiga.
Nilibaki najiuliza maswali mengi sana kichwani kuwa itakuaje endapo nitajibu NDIO, na itakuaje endapo nitakataa, hasa ukizingatia kuwa Careen anampenda sana boyfriend wake.

#Inaendelea :
Nikapiga hesabu za haraka haraka, nikakumbuka kuwa tumeambiwa tuishi na wanawake kiakili.
Nikaona njia bora ni kumdanganya, sababu nikimuambia ukweli basi atazidi kunichukia.
.
Nikamjibu "Hapana, sikuiwasha kabisa simu ".
.
Akanisisitiza kwa uchungu, "Kaka Chris niambie ukweli ".
Lakini bado nilisimama kwenye jibu langu lile lile.
.
Aliniamini nilichosema huku akisisitiza kuwa huenda boyfriend wake ametafuta tu sababu ya kumuacha.
Nilibaki nimenyong'onyea nisijue cha kuongea, akashindwa kuzungumza mwisho akakata simu.
.
Nilihangaika usiku kucha kutaka kujua anaendeleaje, niliogopa asije kuchukua maamuzi mabaya sababu ya kuachwa na ampendae.
Lakini sikufanikiwa kujua liendelealo, simu yake ilikua imezimwa muda wote.
Nilijihisi mwenye makosa sana, nilijilaumu kwa ujinga wangu wa kusahau kumkabidhi simu yake siku ile kwenye gari, lakini nilijilaumu zaidi kwa ujinga wangu wa kutaka kuwaoshea kina Peter, kumbe mwisho nimekuja kusababisha maumivu kwa mwanamke ninaempenda.
.
Kutokana na mawazo niliyo nayo, sikupata usingizi kabisa, na nilishindwa kabisa kusoma notes kujiandaa kwaajili ya mtihani wa kesho chuoni.
.
Mitihani ya kujipima maarufu kama C.A.T(Continuous Assessment Test) one, ilikuwa ndiyo inaanza kwa siku ya kesho yake Jumatatu, na mtihani wetu wa kwanza ulikua ni English And mmunications Skills, utakaofanyika majira ya saa mbili asubuhi.
Sikuwa na mawazo ya mtihani wa kesho, nilikua na mawazo juu ya Careen.
.
Nilipitiwa na usingizi majira ya saa 10 alfajiri, na kujikuta nimestuka usingizini majira ya saa 2 na dakika 6 asubuhi.
Nilistuka sana, niligundua kuwa nimeshachelewa dakika 6 tangu mtihani uanze.
Nikajiandaa tu haraka haraka, hostel mpaka chuo hapana umbali sana, lakini ilibidi nichukue bodaboda ili niwahi.
.
Nikafika chuo, nikashuka kwenye bodaboda na kulipa.
Pindi nataka niingie ndani mlinzi akauliza "Kitambulisho tafadhali? "
.
Nikaanza kukitafuta kitambulisho mifukoni, nikakikosa, nikatafuta kwenye begi na bado nikakikosa.
Ndipo nikakumbuka kuwa nilikiacha kwenye mfuko wa shati nililovaa siku iliyopita niliyokuja chuo.
.
Kutazama muda, nimechelewa kama dakika 12 tayari, na siwezi ingia ndani ya chuo, wala ndani ya chumba cha mtihani bila kitambulisho.
Nikaita boda boda haraka, nikarudi hostel na kukichukua.
Nilichanganyikiwa sana, lakini nilichelewa sana.
.
Nilihojiwa maswali kadhaa kwanini nimechelewa, nikajitetea kuwa naishi mbali sana na chuo.
Nikaruhusiwa kuingia ndani ya chumba cha mtihani.
Nikatupa jicho, wanafunzi wote walikua busy kasoro Careen ambaye alionekana kama ametulia tu akiwaza.
.
Nikakaa kiti kilicho kando yake, nikayatazama maswali na kugundua hayakua magumu sana, na Careen anayajua vizuri sababu tuliwahi jadili wote hizi topic.
.
Ndani ya nusu saa nzima ya mtihani, Careen alikua ameinama tu akiwa mwenye mawazo, hakuonekana kujibu lolote.
Nikagundua kuwa bado ana mawazo ya kuachwa na boyfriend wake.
Nilijua hakuna chochote ambacho angeweza fanya kwa wakati huo.
.
Nikatazama mbele, nikaona msimamizi anazungumza na mkaguzi wa ledgers, nikaona huu ndio mwanya wa kuweza kumsaidia Careen.
Nikamuita kwa sauti ya kunong'ona "Careen "
.
Akanitazama, nikamuonyeshea ishara "Vipi?? Mbona huandiki".
Akabaki amenitazama tu, nikajua hajanielewa, nikarudia ishara zile zile.
.
Ghafla nilishtushwa na sauti ya msimamizi, aliyezungumza kwa kingereza akimaanisha "Chris na Careen mnazungumza nini??".
.
Sote tukamtazama tukijua kuwa tayari tuko matatizoni, na kweli kilichofata alituletea fomu tujaze namba ya usajili, jina, na sahihi kwa kosa la kukutwa tunapiga chabo.
.
"Chabo ni kinyume na sheria na kanuni za chuo chetu, ndiomaana tunajitahidi kuhakikisha mnapata elimu bora, tumewawekea mazingira bora, vifaa vya kutosha vya kujifunzia, walimu kuingia kwa wakati kwenye vipindi na kuhakikisha kuwa wanakufundisha mpaka unaelewa.
Hebu tuambie Chris, wapi unahisi tulishindwa kukupatia elimu bora, ili tujirekebishe??? "
.
Nikamtazama msimamizi, nikashindwa kujibu sababu elimu tunayopatiwa ni ya kiwango kikubwa sana.
Lakini nilijua tatizo lilikuwa hajaelewa kwanini tulikua tunazungumza.
.
Nilizidi kuiona siku yangu mbaya, hasa ukizingatia nilizidi kumuweka Careen kwenye wakati mgumu.
Nimemkosesha boyfriend wake, na sasa nimemkosesha mtihani wake na bado anasubiri adhabu ya chuo juu ya kosa la kupiga chabo.
.
Tulitoka nje na kuelekea maeneo garden, alizidi kulia sana.
Alijumlisha machungu yote aliyonayo.
Nilijitahidi sana kumbembeleza lakini hakutulia mpaka akaja kunyamaza mwenyewe.
.
Baada ya kama masaa 3 mbele, Peter na Abdulrahman walikuja kwa pamoja na kumkuta Careen akiwa kwenye majonzi.
Peter akauliza kwa kingereza akimaanisha "Mbona unaonekana umenyongea??? Unaumwa mpendwa?? "
.
Careen: Hapana. (Akajibu huku anaanzwa kulengwa na machozi)
Ikanibidi niwaombe wasimsumbue, ili apate mapumziko.
.
Peter akanitazama kwa jicho la kunitamani japo aning'ate, lakini akanistahi tu.
Akamshika Careen na kuanza kumhoji taratibu, Careen alianza kuficha ficha mambo, lakini baadae alijikuta akianza kufunguka.
Hofu yangu ilizidi, nilikua nawaza litakalo fata hasa akianza kugusia juu ya story ya simu.
.
Careen: Boyfriend wangu ameniacha.
.
Peter akajibu "Sikuwahi kuwaza kama una boyfriend, na kwanini amekuacha.??."
.
Kila maneno waliyozidi kuzungumza, yalizidi kunipa hofu, nikaropoka tena nikimtaka Peter aache kumsumbua Careen kwa maswali.
.
Careen akaniambia nisijali, akaanza kuelezea jinsi boyfriend wake alivyomnyamazia siku nzima, na jinsi alivyoanza kumtusi na maneno aliyomuambia.
Mwisho akamaliza "Anasema mimi nimelala kwa mwanaume mwingine na simu sijampokelea".
.
Peter na Abdulrahman wakastuka, nami pia nikastuka sababu nilijua kuwa kinachofata ni majanga kwangu.
Nikawaambia kina Peter ''Inatosha, mwacheni apumzike "

Peter akamtazama Abdulrahman, Peter akaropoka "Kwani juzi jumamosi ulilala wapi??? Na kwanini ulizima simu?? "
.
Hapo ndipo presha ilipozidi kunipanda na kutamani ardhi ipasuke niingie.
Careen akajibu "Nililala nyumbani, na simu niliisahau kwa Chris pindi nilipokuwa kwenye gari "

Peter na Abdulrahman wakaguna kwa nguvu huku wakitazamana, lakini mimi nilikua nahisi nafsi inataka kupasuka nife hapo hapo.
.
Peter akachukua simu yake, na kumuonyesha Careen kumbukumbu za simu alizopiga na kupokelewa, Careen alikuta namba yake nayo ipo kwenye list.
Careen akanitazama kwa mshangao, akarudisha macho kwa Peter.
Abdulrahman akaongeza "Na Chris alisema tusiwasumbue, umelala nae, chumbani kwake, kifuani kwake "- (Alizungumza kwa msisitizo).
.
Peter akaongeza, "Na nadhani, Chris aliiwasha simu yako asubuhi, na hakuipokea simu ya boyfriend wako".
.
Careen aligeuka na kunitazama kwa hasira, nahisi alitamani hata kuninyonga, machozi yalimjaa machoni mwake.
Uso ulinijaa aibu, lakini hofu kubwa ilinizidi.

Nilijua leo ndio nampoteza Careen, nikageuka na kuwatazama, kwajinsi walivyokuwa wakiniangalia, nilitamani hata ningekimbia, au hata ningerudisha muda nyuma ili niyafute makosa yangu yote.

Careen alinitazama kwa hasira, kisha akazungumza maneno yaliyo nifanya nihisi moyo unataka kunitoka
.
.
Je Careen alizungumza maneno gani!!??? Chris atafanya nini???

Usikose sehemu ya 8
#Itaendelea
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Nane

#Ilipoishia: Careen alinitazama kwa hasira sana baada ya kupewa ukweli kuwa mimi ndiye niliyefanya boyfriend wake amuache, na bado nilijibu uongo kuwa sikuhusika.
Lakini pia nimempakazia kashfa kwa Peter kuwa nililala nae.

Alikasirika, alinitazama utadhani anataka kunivamia.
Nilibaki nimenyongea nisijue nini cha kujitetea.
Ndipo akanyanyua kinywa chake na kuzungumza kwa hasira.
**************
#Inaendelea:
Careen: Nilikuheshimu sana, nikakuthamini na kukufanya kama rafiki chaguo la kwanza kwangu, nikaona haitoshi, nikakufanya kama ndugu wangu wa damu."

Akalia kwa uchungu kisha kuendelea tena "Chris siamini kama ni wewe ndiye uliyenifanyia haya yote...!!! Rafiki yangu wa dhati, kumbe ndiye mbaya kwangu.
Nilikueleza zima simu kwasababu fulani, lakini ukaona njia pekee ya kuniharibia ni kwa kuiacha on.
Na ukaona haitoshi, ukaamua kunipakazia"

Nilibaki nimeinamisha kichwa chini, aibu ilinijaa, nilitamani hata kukimbia lakini miguu ilikosa nguvu kabisa.
.
Nikamjibu "Careen, ni bahati mbaya tu, wala sikunuia kufanya yote hayo ".

Akanitazama kwa hasira zaidi, akafuta machozi kwa mkono wa kushoto, na kupandisha mafua yatokanayo na kulia.
Akanijibu "Bahati mbaya?? Kunipakazia nayo bahati mbaya??? Kuiwasha simu bahati mbaya???
Ulinidharirisha pale mgahawani Legacy, nayo ni bahati mbaya!??? Nilidhani yale maneno yalikutoka kwaajili ya hasira, kumbe Chris una lako una lako unalolitaka, nakuchukia kuanzia sasa "
.
Peter akasogea karibu na kumshika bega, Abdulrahman akachukua bag lake, wakimsisitiza waondoke waniache.
Careen akaniangalia kwa mara ya mwisho, na kusema "Naomba kuanzia leo, usinijue, nami sikujui, tusijuane, sitaki wanafki kwenye maisha yangu"- (Akazungumza kisha akasonya na kuanza kuondoka huku akiwa ameshikwa bega na Peter) .
.
Maneno yalinigusa sana, nilijihisi mkosaji, nilivyosikia tu ameanza kupiga hatua kuondoka ndipo nikapata nguvu ya ghafla na kunyanyuka kumfata kwa nyuma japo nimuombe msamaha.
Lakini Abdulrahman aliniekea mwili.
Na kwajinsi nilivyo kimbao mbao, Abdulrahman mwili nyumba, basi nilijikuta kama nimesombwa na fuso.
.
Nikadondoka chini, nikabaki nawatazama wanavyopotea mbele ya mboni ya macho yangu.
Tangia hapo ndipo ukawa mwisho wa urafiki wangu na Careen, nilijilaumu kwa mengi sana, niliumia sana.
Njiani tulikua tukipishana kama magari, tambo za kina Peter zilizidi na zilizidi kuniumiza zaidi.
.
Nakumbuka mitihani yangu ya CAT one sikuweza kuifanya vizuri kutokana na mawazo niliyo nayo, niliitwa kuhojiwa kuhusu maendeleo yangu, lakini pia nilihojiwa juu ya kesi yangu ya kupiga chabo, nikajitetea vya kutosha.
Nikapewa adhabu ya kufutiwa matokeo ya mtihani niliopiga chabo.
.
Kuna nyakati nilijitahidi kumtumia messages za kumuomba msamaha Careen, lakini hakuzijibu, simu hakupokea, njiani wala hakuwa na muda wa kunisikiliza.
.
Mwezi mmoja ulipita nikiwa mbali na Careen, nilirudisha majeshi upande wa kina Hasheem na Ramadhan, na nikabahatika kupata rafiki wapya wawili, mmoja wa kiTanzania aitwae Nasra, na mwingine wa Zambia aitwae Ivan.
.
Angalau walijitahidi kurudisha furaha yangu, walinifanya niamini kuwa "Sio kila mtu huja kwenye maisha yako ili kuwa nawe milele, wengine huja kwa muda mfupi tu ili kukupa funzo fulani".
Nami niliaamini Careen alikuja kunipa funzo kubwa sana.
Nasra alijitahidi kunisahaulisha maumivu yangu juu ya Careen, lakini alishindwa jambo moja tu "Kunifanya niache kumpenda Careen".
.
Siku moja maeneo ya nje ya geti za chuo, palisimama vijana kadhaa waliokuwa wakitoa vipeperushi kuhusiana na semina ya mahusiano kwa vijana kuhusu "Njia za kuepuka mateso ya hisia", semina itakayo fanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, siku ya Jumamosi, mchana.
.
Kwavile Nasra alijua kuwa napitia mateso ya kihisia juu ya Careen, basi alinialika twende wote labda naweza jifunza kitu kipya.
.
Mapema siku hiyo, majira ya saa 4 nikawahi na kukutana na Nasra katika ukumbi huo.
Na semina ikaanza, lilikua ni somo kuhusiana na "Jinsi ya kupambana na maumivu ya kutendwa "
.
Mwalimu wa siku hiyo alikua ni Dkt Leonard, na alikuwa akiendelea kutoa mafunzo, mada zake ziliwagusa watu wengi ndani ya ukumbi huo.
Nilimtazama Nasra ambaye alionekana yuko makini zaidi.
Nikarusha macho yangu pande zote na kuona jinsi watu walivyo busy kusikiliza kinachozungumzwa.

Lakini ghafla macho yangu yalikumbana uso kwa uso na macho ya Careen ambaye nae alinitazama na kugeuzia shingo mbele.
Nikatupa jicho pembeni yake, nikamuona Peter akiwa makini pia akifatilia mafunzo.
.
Nikajiuliza "Hadi nyinyi mpo?"
Lakini nilijua kuwepo kwao kwenye ukumbi mmoja na mimi kusingeleta mabadiliko yoyote yale, sababu tayari hawana muda wa hata kuongea na mimi.
.
Mwalimu wa mahusiano akazungumza jambo "Wengi wetu tunachukulia kuachwa kama adhabu ya kifo, kwamba ukiachwa hautakuja kupendwa tena.
Ngoja nikwambie kitu, kuna nyakati unaachwa ili uwe imara, ili umpate aliye bora zaidi yake, ili umpate aliyeumbwa kwaajili yako.

Achana na tabia ya kujiona kama una nuksi, huna thamani, hutopata mwingine...hizo ni fikra potofu.
Acha kujichukia, acha kuyachukia mapenzi, unapoachwa basi lia unavyoweza lakini mwisho wake jifute machozi na useme sitorudi nyuma kamwe maana nishapata funzo jipya juu ya mapenzi, nishapata nafasi mpya ya kumpata aliyeumbwa kwaajili yangu.
Be positive ".
.
Akakwama hapo na kututazama wasikilizaji wake, akaendelea "Kuna mtu unaweza ukajitoa kwake kwa kila kitu, ukaonyesha kumpenda, ukawa umewekeza muda wako, nguvu zako, pesa zako, na kila kitu ulichonacho kwaajili yake, lakini kwavile yeye ni limbukeni wa kupendwa basi akaanza kuzitesa hisia zako, akihisi kuwa huwezi ishi bila yeye kwahiyo anakufanya vile atakavyo."

Nilihema kwa nguvu, mada inanipa funzo kubwa sana.
Akaendelea "Mwingine anaingia kwenye mahusiano na wewe labda sababu ya upweke wake, au kwa tamaa zake za kimwili, mali zako.. kwakifupi haingii kwenye mahusiano na wewe sababu ya upendo wake kwako, no.
Sababu ya kile anachotaka kwako, akikipata tu basi huwa haoni sababu ya kuwa na wewe tena. Huanza kuleta visa mbalimbali, atakutesa, atakusaliti, atakutafutia visababu mbalimbali vya kukuacha, lakini kwavile wewe unampenda kwa dhati, unajikuta huwezi kumuacha, unateseka kila kukicha kwaajili yake".
.
"Wewe ni wathamani sana, huna haja ya kung'ang'ania unapoumizwa kila kukicha, usipopendeka.
Akitafuta sababu ya kukuacha, shukuru Mungu kwa kukuondolea uozo maishani mwako"
.
"Kuna nyakati Mungu anaweza mleta mtu yeyote yule ili aharibu mahusiano yako, ukaanza kumchukia mtu aliyeharibu, kumbe sio kosa lake, ametumika kuondoa nuksi kwenye maisha yako, na kuleta baraka kwako.
Iwe ni mchepuko wake, au wazazi, ndugu, rafiki, iwe ni yeyote yule ambaye ameharibu mahusiano yako na mtu ambaye hakupendi, anakutesa, anakusaliti, anakupiga, anakutafutia visababu vya kukuacha, hana malengo na wewe" mshukuru sana huyo mtu aliyeyaharibu."- Niliposikia maneno hayo nilijikuta napiga makofi sana baada ya kuona mada imegusa mahala husika.

Mwalimu aliendelea na somo, na lilipoisha sote tulitoka nje ya ukumbi.
Nilimvuta Nasra ili tusogee kwa mbele kidogo, tutoke kwenye msongamano wa watu.
Lakin ghafla nilisikia sauti ya mtu ikiniita.

Nilistushwa na sauti hiyo, ilikua ni ya mtu ninaye mfahamu, nikasimama na wala sikugeuke nyuma, shida yangu ilikua nisikilize kama ni kweli naitwa au masikio yananiletea maigizo.

Sikusikia tena, nikajua nimejidanganya tu, nikaanza kutembea tena.
Nikasikia naitwa tena "Chrisss" "Chriss".
Hapo ndipo nikagundua ni kweli naitwa, nikapata hamu ya haraka ya kugeuka nyuma ili kuthibitisha kwa macho yangu mwenyewe.

Kugeuka na kutazama, sikuamini macho yangu, nilibaki nimepigwa na bumbuwazi huku nafsi ikijiuliza maswali mengi.

Ananiita mimi kweli au anatania??? Au anataka anidharilishe mbele za watu??? Anataka kunieleza nini
?! .

Je Chris anaitwa na nani?? Na kwanini??? Nini kitatokea.

Usikose sehemu ya 9
#Itaendelea.....
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Tisa

#Ilipoishia: Nilisikia kama naitwa, sauti ya mtu ninaemfahamu, lakini sikuamini masikio yangu nikahisi kama yananidanganya, nikaanza kuchukua hatua kuelekea mbele.
.
Mara nikaitwa tena, "Chris, chris " hapo ndipo nikagundua kuwa sikua najidanganya, ni kweli nilikua naitwa.
Kutokana na sauti ya muitaji, nilipata shauku kubwa kutaka kuthibitisha kama ni kweli mwenyewe.
Nikageuza shingo haraka, kutupa macho mbele yangu nilimuona Careen ambaye alionekana anatembea mwendo wa haraka kuniwahi mahala nilipo.
.
#Inaendelea:
Sikuamini kama ni kweli leo, baada ya mwezi, nakuja kuitwa na mrembo Careen.
Nilihisi kama naota, nikapata shauku ya kutaka kujua anataka kuniambia nini leo.
.
Lakini mawazo ya ajabu yakanijia akilini, kuwa huenda anataka kunifanyia jambo la udharilishaji mbele za watu.
Nikajiandaa kisaikolojia kwa lolote lile litakalo tokea.
.
Nasra akajisogeza kwa pembeni ili kuacha nafasi Careen akifika niweze kuongea nae.
Alipofika Careen, akanisalimia.
.
Careen: Hi - (Alitoa salam kama mtu asiyejiamini hivi, nahisi labda alidhani nisingeitikia).
.
Nikamjibu "Hi" na wala sikutaka kuongeza neno lolote ili kumwacha aingie moja kwa moja kwenye alichotaka kusema.
.
Akaanza "Najua unashangaa kwanini leo aliyekuambia sikujui na usinijue, ndiye anayekuita leo." - (Akazungumza kwa kujihami mapema).
.
Sikutaka kuonyesha udhaifu wangu, ikabidi nionyeshe uanaume wangu.
Nikamjibu "Bado najiuliza hata jina langu umelijuaje??? Tulishawahi onana mahali? ". (Nikazungumza kwa kujiamini, na kumkazia macho).
.
Kauli ilimgusa sana, akainamisha kichwa chini kwa aibu huku akitafakari cha kunijibu.
Ikabidi nimuongeze mzinga "Dada sema ulichoniitia, rafiki yangu ananisubiria".
.
Nilizungumza maneno ya kujiamini huku nikijua kuwa nafsi yangu inaumia, nilitamani hata kumkombatia nimshukuru hata kwa kuniita jina leo.
Lakini sikutaka kuonyesha udhaifu wangu kwake, nilitaka nimuonyeshe jinsi gani naweza ishi bila yeye.
Ikabidi nitikise kibiriti baada ya kumuona anajifikiria sana kujibu, nikageuza mwili na kujifanya nataka kuondoka.

Ghafla akanishika mkono, "Chris, kwanza naomba usilichukulie hasira, usinichukie, nimekuita leo kwa nia njema tu ili tuyamalize yote yanayo tufanya tuchukiane." - (Alizungumza kwa utaratibu, na hisia zaidi).
.
Wahenga walisema "Hakuna mkate mgumu mbele ya chai", ndipo niliamini wakati huo, maana sauti nyororo iliyobeba hisia na utaratibu, ya kwake Careen, ilinifanya niwe mpole ghafla na kuanza kumsikiliza kwa makini.
Hapa ndipo nilipogundua kuwa kinywa cha mwanamke kina nguvu kubwa ya ushawishi kwa mwanaume.

Akanitazama usoni, kisha akashusha macho yake kwa aibu na kuendelea kuongea huku akinitazama kwa kuibia ibia, akaendelea "Siku zote nilihisi wewe ni mkosaji sababu uliniharibia kwa mwanaume ambaye nilimpenda kwa dhati.
Lakini leo nimejifunza, nimegundua umuhimu wako."
.
Nikamjibu "Careen sioni umuhimu wangu kwako, mimi mnafki, mimi nimekuharibia, mimi nimekupakazia, umuhimu wangu uko wapi??" - (Nilimuuliza kwa upole zaidi).
.
Akajibu "Chris naamini yale yote yalikua kwa makusudi maalumu.
Somo limenifanya niligundue hilo leo.
Umeniondolea uozo ndani ya maisha yangu, yule mwanaume alinitesa sana, kanifanyia visa vya kila aina, kanisaliti vya kutosha, na kuna siku niliwahi kumhoji kwanini, Chris huwezi amini alinipiga yule kaka". - (Alizungumza kwa machungu sana huku machozi yakianza kumlenga).
.
Akaendelea "Sio mara ya kwanza kunitafutia sababu ya kuniacha, lakini nilikua king'ang'anizi sababu nilimpenda sana, sikutaka aniache.
Lakini aliniacha kwasababu ndogo sana, nimeishi kwa mateso mwezi mzima, nimelia sana, Chris unaona hadi nimepungua." - (Nikaanza kuyaona machozi yanaanza kumtoka).
.
Sikutaka kupoteza point 3 muhimu, nikafanya kama wanavyofanyaga wazungu kwenye tamthilia, nikamvuta na kumkombatia kwa nguvu.
Nikamwacha alie kifuani mwangu, huku nazipapasa nywele zake kwa mkono mmoja, mkono mwingine ukiwa umemlaza vizuri kifuani.
Nikamwambia "Lia mamie, lia unavyoweza, lakini kamwe moyo wako haustahili kumpa asiyejua thamani yako."
.
Nikaendelea "Unastahili kupendwa, kumpata anayekujali, atakaye kufanya ujihisi kama Malkia, kwanini ujutie kuachwa na anayeutesa moyo wako.".

Nikaona Careen anaifunga mikono yake mgongoni mwangu kwa nguvu, nami nikaona nisichezee hii nafasi.
Nikahakikisha mwili wake unapata joto langu vizuri ili kuongeza misisimko kati yetu.
Nikamwambia "Naamini yale makosa yote, niliyafanya kwa kusudi maalumu, sababu hakuna hata moja nililowahi kulifanya kwa kukusudia. Nisamehe sana Careen, tusahau yote yaliyopita, tumshukuru Mungu kwakila jambo na tuanzishe maisha mapya".
.
Careen kwa sauti ya chini, akanijibu "Kaka Chris haina haja ya kuomba samahani, moyo wangu mweupe sasa, nimeijua thamani yangu na nimemjua rafiki bora aliye letwa na Mungu kwangu.
Nilikumiss, nilimiss vituko vyako". - (Akazungumza huku akitoa kicheko cha taratibu kilichochanganyika na hisia).
.
Ikabidi nimchekeshe "Twende mgahawani tukale leo, ila nitasahau wallet tena".
.
Careen akacheka, akanipiga kifuani na kuniambia "Nitaosheshwa vyombo leo, halafu wewe watakuacha na boxer tu"
Sote tukacheka kwa furaha, kisha kukombatiana kwa nguvu zaidi.
.
Kutupa jicho mbele, nilimuona Peter akiwa anatutazama kwa jicho la chuki, nilijua wazi kuwa hakufurahia kile alichokiona.
Kutazama upande wa Nasra, nako palionekana mabadiliko.
Niliona uso wa Nasra ukiwa hauna furaha, ameukunja, alionyesha kitu kama wivu ndani yake.
Nilihisi kuwa Nasra hakufurahishwa kuona mimi na Careen tunarudisha urafiki wetu, nilianza kuhisi kuwa labda Nasra alikuwa na hisia juu yangu.
.
Peter alisogea mahali tulipo, akakohoa kinafki "hnh hnh", Careen akastuka na kugeuka nyuma.
Peter akaongea kwa kingereza, akimaanisha "Nimeshangazwa kuona mpo pamoja".
.
Careen akajibu kwa lugha hiyo hiyo akimaanisha "Yeah nimeona ni vyema kumrudisha rafiki yangu aliyeletwa kwa kusudi maalumu, somo limenibadilisha leo". - (Akazungumza kwa tabasamu kubwa mno).
.
Peter akanitazama kwa jicho ambalo tafsiri yake ni kama alitaka kuniambia "Nakumaindi nikupige vichwa wewe".
.
Ikabidi nimuite Nasra, akasogea mahali tulipo na kumtambulisha kwa Peter na Careen.
Akampa mkono Peter kikawaida tu, lakini kwa upande wa Careen ni kama alitaka kumpa kisha akasita na kumpungia mkono kwa mbali kama anatoa "hi" vile, kisha akatoa tabasamu ambalo nilihisi halikua na ukweli ndani yake.
.
Careen akamwambia Peter, "Tumemrudisha Chris kwenye kundi, na chuki ziishe, mpeane mikono" - (Akazungumza huku amemshika bega Peter, ili kuonyesha msisitizo).
.
Peter akanyoosha mkono, nami nikamshika mkono wake, tukatupiana macho, kwavile Careen alikua akinitazama ilibidi nitoe tabasamu la kinafki.
Lakini Peter alizidi kuonyesha chuki yake kwenye macho yake, nami nikajisemea kimoyo moyo "Acha mechi ya wanaume iendelee".
.
Story mbili tatu zikaendelea, lakini Nasra na Peter walikua kama hawapo vile, lakin sikuwajali, nilichojali ni kuwa leo nimerudisha furaha yangu, na moyo wangu una amani sana.
Kwambali nilimuona Dkt Leonard, nikaona huu ni wakati muafaka wa kwenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kuirudisha furaha.
.
Niliwaomba nitoke mara moja, na kumfata Dkt.Leonard, nikazungumza nae mambo kadhaa na kumpa shukrani zangu, pamoja na kubadilisha nae namba za simu sababu nilihisi ana mengi zaidi ya kunisaidia.
Nilipomaliza tuakaagana na yeye akaendelea kusalimiana na watu waliokuja kwenye semina.
.
Nilipogeuka ili kurudi nilipowaacha kina Careen, nilishangaa kumuona Nasra na Careen tu ndio wamebaki, wala Peter hayupo.
.
Nikatafakari kidogo, kisha nikaanza kuchukua hatua kusogea mbele, nikasikia sauti nzito inaniita "Chris".
.
Nikageuka, kumtazama alikua ni Peter, nikagundua kuwa kumbe alikua akinifatilia kwa nyuma.
Akaniambia "Maamuzi uliyo yachagua leo, yana madhara makubwa sana kwako kwa hapo baadae. Acha kumfatilia Careen"
.
Nikamshangaa, nikajua wazi hilo ndilo lililokuwa linamkereketa.
Nikamuuliza "Maamuzi gani hayo niliyo yaamua mimi?? " - (Nilimuuliza swali huku nikijichekesha kwa dharau).
.
Peter: Maamuzi ya kumfata Careen na kumuomba msamaha.
.
Nikagundua kumbe Peter anahisi mimi ndiye niliyemfata Careen kumuomba msamaha.
"Aaanhaaa kumbe ndo unachowaza, habari mbaya kwako, Careen ndiye aliyenishobokea". - (Nikazungumza kwa kujiamini zaidi, huku nikimtazama kwa jicho la dharau).
.
Peter alistushwa na kauli hiyo, nikaona anatafakari na kunijibu "Sasa nakuamuru, vunja kabisa mazoea na Careen, yeye ni mchumba wangu mtarajiwa, kaa nae mbali" - (Alitoa kauli iliyojaa ukali na hasira).
.
Nikaona sasa muda wa kutambiana umeisha, huu ni muda wa kuonyeshana kwa vitendo, nikamjibu "Bro, siku zote hizo nilizokuwa mbali nae umeshindwa kumfanya awe wako??? Kweli wewe domo theeeeege hahaha" - (Nikazungumza kwa dharau na kuivuta "Theeege" huku nikicheka kwa dharau).
.
Akajisikia aibu sana, akakosa la kuongea.
Nikaona kama Peter ananipotezea muda, nilitaka niwahi mahali walipo Careen na Nasra.
Nikageuka chap na kuanza kuchukua hatua kadhaa.
.
Nikasikia tena "Chris" (Peter alikua akiniita).
"Shit" - (Nikajisemea kwa nguvu baada ya kuchukizwa na kupotezewa muda na Peter).
.
Sikugeuka, Peter akanifata na kunishika bega, kwa hasira nilizo nazo, nikageuza shingo na kumtazama kwa jicho la hasira.
.
Akaniambia "Wewe mwanaume, mimi mwanaume, sote tunataka kitu kimoja, ngoja tuone nani atakipata, na ambaye atakipata ndiye mwanaume. Atakaye kosa, atavalishwa dera na wigi" - (Akazungumza kwa kujiamini, na kwa hasira zaidi).
.
Niliposikia maneno hayo, nilijua wazi mchezo wa kuBet, Careen ndiye dau.
Nikakumbuka kauli moja "Mapenzi ni kama kamali, kuna kula au kuliwa".
Nilimtazama Peter kwa masaa, nikamtafakari muonekano wake, mali zake, nikagundua ana nguvu ya pesa tu, nikajitafakari nikasema nikikataa basi lazima nitaonekana boya.
.
Na je nikikubali, itakuwaje endapo nitashindwa?!
.
Akaniambia tena "Hizi ni mbio za wanaume, na ni mwanaume mmoja tu ndiye atakae ibuka mshindi"
.
Akaendelea "Chagua kupambana ili uibuke mshindi, au ushindwe na uvalishwe dera na wigi mbele za marafiki zetu??? "
.
Nikastuka sana, nikajua kuwa Peter hakuwa akitania, alimaanisha alichosema, na niliwaza kinachompa ujeuri ni pesa alizonazo.
Lakini amekaa na Careen mwezi mzima, lazima atakua anajua mengi kuhusu Careen, na amepata wakati mzuri wa kumjenga kihisia Careen.
.
Nikabaki na maswali mengi kichwani, "Nikubali mechi, au nikatae mechi
"

Je Chris atakubali???"
.
Usikose sehemu ya 10
#Itaendelea
....
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Kumi

#Ilipoishia: Peter alitangaza mechi kati yangu na yake, na atakaeshindwa basi atavalishwa dera na wigi.
Nikajifikiria kwa mengi sana hasa kwa kuzingatia muonekano wa Peter, nguvu yake ya pesa, pamoja na ukaribu wake na Careen kwa kipindi chote hicho nilichokua siongei nae.
Nikabaki najiuliza sana, nikubali au nikatae?! .
.
#[COLOR]Inaendelea[/COLOR]:
Nikafikria hii ni kamali, na naweza kushindwa, mwisho nitaaibika, najua hawatonivisha dera tu nakuniacha, lazima watanipiga picha na kuzisambaza.
.
Sura yangu nitaiweka wapi?? Wazazi, ndugu, na marafiki zangu watanifikiriaje??
Nilipofikiria hayo tu, ndipo nilipuuzia maneno aliyosema Peter na kupata nguvu ya kuanza kutembea kuelekea mbele.
.
Peter alibaki amesimama, akaanza kucheka kwa dharau.
Akaongea "Siku zote wanawake ndio huwa waoga, ila kumbe hata wanaume pia " - (Alizungumza huku akijichekesha kwa dharau).
.
Nikajikuta nimesimama ghafla, nikafikiria la kumjibu.
Akaongea tena "Kuna matokeo mawili tu, kushinda au kushindwa, na siku zote waoga ndio hujitabiria kushindwa hata kabla ya mechi".
.
Maneno yalinugusa sana na kunipandisha hasira, yakanichoma kisawasawa, nikageuka na kumtazama kisha nikamjibu "Wanaume huwa hawapambani kwa maneno kama waimba taarab, vitendo huwa ndo vinafata". - (Nilizungumza kwa msisitizo na kujiamini zaidi).
.
Akanitazama kama mtu anaetaka kunirukia, nikamwambia "Nimekubali mechi, nitashinda, na wewe njoo na make up kabisa, ili upendeze pindi umevaa dera na wigi". - (Nikamkejeli, na kugeuka nyuma na kuanza kuondoka).
.
Lakini nikapiga hatua mbili mbele, kisha nikasimama na kumtazama adui yangu, nikamwambia "Huu mchezo hauhitaji hasira" - (Nikazungumza na kuondoka huku nacheka).
.
Peter alinifata nyuma nyuma huku akiwa amenyongea, mpaka tulipofika mahala waliposimama Careen na Nasra.
Tuliwakuta wakizungumza mawili matatu, lakini Careen ndiye aliekuwa mzungumzaji zaidi, na Nasra msikilizaji huku akichangia moja moja.
.
Tulipofika wala hatukupoteza muda sana, tukaagana na Careena aliondoka na Peter.
Nami niliondoka na Nasra.
Njiani Nasra alionekana mwenye mawazo sana, nikajua kuna kitu Nasra anakiwazia kuhusu mimi na Careen.
.
Nikamuuliza "Mbona umenyongea hivyo?? "
.
Nasra: Mmh kwani naonekana nimenyongea!!!?! Mbona najiona niko sawa tu. - (Akajifanya kuruka ili nisijue kilicho mfanya anyongee).
.
Nikaona anaweza kunificha, nikaamua kumtupia mada za kiuchokozi.
"Leo nimefurahi sana kurudisha urafiki wangu na Careen". - (Nilizungumza huku natoa sauti iliyojawa na furaha sana).
.
Nasra akawa amegeukia upande mwingine huku akijifanya hajasikia nilichosema.
Nikaona bora ninyamaze, lakini nilijua wazi kuwa Nasra hajafurahishwa na uwepo wa Careen kwenye maisha yangu, na nilijua huenda akawa na hisia juu yangu.
.
Tulipofika Gongo La Mboto, tukaagana na kila mtu akaelekea kwenye hostel anayoishi.
Lakini kwajinsi tulivyoagana, nilizidi kupata wasiwasi juu ya hisia za Nasra juu yangu, nikahisi kuwa huenda zikaja kuniharibia mipango yangu ya kumpata Careen.
.
Jumatatu iliyofata kama kawaida ndani ya chuo, nikawa nimeketi maeneo ya Garden, pamoja na Hasheem na Ramadhan.
Tukawa tukipitia notes huku tukipiga story mbili tatu.
.
Ramadhan: Leo unaonekana hauko sawa??? - (Alinitupia swali mimi).
.
Nikamjibu "Yeah, kuna jambo linanisumbua kichwa na sijui nitalimaliza vipi".
.
Akaniambia "Jambo gani??? Kuhusu Careen tena au??? " - (Aliniuliza huku akinitazama kwa jicho la uchu wa kutaka kujua kiundani zaidi).
.
Nikatuliza nafsi kwanza, nikapoa, kisha nikaanza kumweleza kiundani zaidi kuhusu mechi niliyo ingia kati yangu na Peter.
.
Alinishangaa sana kwa maamuzi magumu niliyo chukua.
Akaniambia "Nadhani kwasasa una mambo mengi sana ya kufanya Chris, hukuwa na haja ya kuuthibitisha uanaume wako kwa Peter."- (Akazungumza huku akionekana mwenye kumaanisha anachosema).
.
Nikageuka na kumtazama usoni, akaendelea "Chris kumbuka umekuja chuo kwaajili ya kutengeneza maisha yako ya baadae, haya maswala ya kujiingiza kwenye mahusiano ni sehemu mojawapo ya kuharibu focus yako kwenye masomo".
.
Akahema kidogo kisha akaendelea, "Unakumbuka mitihani yako ya Cat one uliharibu??? Sababu ilikua ni mahusiano, Cat two umefanya vizuri, sababu ulikua mbali na yule unayempenda.
Hebu fikiria Chris, usikubali hisia ziendeshe maisha yako.
Leo hii umekua mtumwa, unafanya kila ambacho hisia zako zinasema, lakini laiti ungekua na control nzuri kwenye hisia zako, kwasasa usingeshindwa kuacha kusoma na kuwaza mahusiano".
.
Nikamsikiliza Ramadhan kwa umakini, lakin niliona kama ameanza kunioea wivu.
Ramadhan akatoa kauli za mwisho, akasema "Kwasasa chuo kinakufatilia kwa umakini na ukaribu zaidi tangu uharibu kwenye Cat one, wanajitahidi sana kukupa elimu bora wakidhani labda una uelewa mdogo darasani, kumbe tatizo tayari akili yako inaendeshwa kihisia.
Hebu zinduka Chris, huo mchezo ulio uingia haufai kwako.
Hebu fikiria siku ukija valishwa dera, nani atakaye aibika??? Ni wewe.
Kina nani wataaibika??? Wazazi wako.
Utawapotezea sifa kina nani!?! Chuo chako.
Hebu zinduka Chris". - (Akazungumza kwa msisitizo, kidogo maneno yaliniingia japo mwanzo nilihisi kama ana wivu na mimi).

Nikaanza kufikiria jinsi wazazi wangu walivyohangaika kunisomesha huko nyuma, nikawazia mkopo naopewa na serikali ili nisome, nikawazia chuo changu kinachojitahidi kunipa elimu bora, nikawazia rafiki zangu, nikajiwazia mimi mwenyewe na future yangu.
Nikajigundua nina mzigo mkubwa sana kwenye maisha yangu, kuna watu wengi wanategemea uwepo wangu, wanategemea matunda yangu ili waje kunufaika na kujivunia kupitia mimi.
.
Nikajisemea kimoyo moyo "Nahitajika kuwa balozi mzuri wa chuo changu, wazazi wangu, rafiki zangu, wote wananitegemea mimi".
.
Hasheem akanishika bega, akasema "Watu wengi wanapoingia vyuoni huwa wanasahau lile walilo lifata chuo, matokeo yake hujikuta wanajiingiza kwenye maswala ya mapenzi.
Wewe mtu mzima tayari, kwa umri ulionao hauwezi jizuia kupenda hasa katika mazingira kama haya yenye watu wengi wazuri.
Lakini ni vyema kabla ya kujifunza kupenda, ukajifunza kuzicontrol hisia zako ili usije changanya mapenzi na masomo, au mapenzi na maisha mengine.
Ukiishi kwa kuendeshwa hisia zako utakua mtumwa kwa unayempenda, utakuwa na wivu na kuzidi kuumia hata kwenye mambo madogo, na mbaya zaidi utajikuta unafanya maamuzi ya kijinga kama haya ambayo unayafanya."
.
Hasheem akanitazama na kuniambia "Fikiria kabla ya kutoa maamuzi yoyote maishani mwako, kuna wengi sana utawaumiza endapo ukitoa maamuzi kwa kufata hisia zako zinavyosema.
Cha kukushauri, ukimpenda mtu, usitake kushindana na mpinzani wako, wewe nenda wewe kama wewe na umweleze jinsi unavyompenda.
Najua hofu yako ni juu ya majibu yake, unahofu endapo atakukataa au laa, lakini huwezi jua saingine anakupenda pia, na kuchelewa kwako kukamfanya aone kama humpendi mwisho akamchagua mwingine.
Lakini itakuaje endapo utamwambia halafu akakukatalia??? Uzuri ni kuwa akikukataa, utaumia lakini tayari umeshapata ukweli ambao utakuweka huru.
Kuliko kusubiri miaka mingi na kuhofia atakukataa, mwisho unakuja kusikia anaolewa na mtu mwingine".
.
Maneno yaliniingia akilini, nikajihisi mjinga sana kwa kuchelewa chelewa kwangu, nimeumia vya kutosha, nimepoteza muda vya kutosha, na bado nimeteseka vya kutosha.
Nikasema "Nahitaji kuwa mwanaume, nahitaji kujitambua, nahitaji kujua kuzicontrol hisia zangu, na nahitaji kufaulu masomo yangu ili iwe furaha kwa chuo, rafiki, serikali, na wazazi wangu".

Hasheem akaniambia "Kuwa mwanaume, ishi kiume, kama kweli unampenda, jiandae kisaikolojia kwa jibu lolote utakalopewa, lakini nenda ukamweleze hisia zako leo.
Na mwambie Peter kuwa huna haja ya mechi yake, mapenzi sio mpira kusema mshindanie kombe". - (Akanisisitiza na kunitaka ninyanyuke niende).

Nilitamani kunyanyuka ili kumfata darasani, mahali ambapo Careen yupo, lakini miguu iliishiwa nguvu, nikaanza kutetemeka na miguu na mikono.
Mwili mzima ulikua kama kuna kitu kinanitembea, mapigo ya moyo yalizidi kunipiga.
.
Nikanyanyuka, nikaanza kutembea kama mtu ambaye haoni mbele vile.
Jasho lilikua likinimiminika utadhani nimetoka kumwagiwa maji, kwavile nilikua mwenye mawazo tani 1000, nilijikuta nimejikwaa ghafla.

Watu walio maeneo ya garden wakacheka, nikanyanyuka na kuanza kutembea tena.
Nilikua natembea kama kuna mtu ananisukuma, mapigo ya moyo yalikua yanadunda mpaka shati lilikua linadunda kama limebebea sabufa.

Nikaingia kwenye corridor ya kuelekea darasa alilo Careen, kila nilivyozidi sogea ndivyo nilivyozidi kupunguza mwendo, ghafla nilijistukia nimejigonga kwenye kiti kilicho kwenye corridor.
Nikainama na kutazama goti langu nililojigonga, nikawa naugulia lakini ndipo nilipogundua kuwa kumbe nilichafuka wakati nilipodondoka.

Nikachukua leso na kujifuta, lakini jasho nalo likawa linamwagika.
Nikaamka na kujifuta jasho pia.
nikajiweka sawa mavazi yangu na kuanza kupiga hatua kuelekea darasa alilo Careen.

Pindi nakaribia darasa mapigo ya moyo yalinizidi, lakini ghafla nilisikia sauti mbili zilizokuwa zikizungumza.
Sauti moja ilikua ni ya Careen, nyingine ya Nasra.
.
Nilistushwa na mazungumzo yao, nikahisi kama mipango yangu yote inataka kuharibiwa leo.
Careen alimuuliza Nasra, "inaonekana wewe na Chris mmekua marafiki wakubwa sana "
.
Lakini jibu la Nasra ndilo lililoniharibia siku yangu, alijibu "sio bestfriends tu, ni boyfriend wangu".
.
Careen aliye ndani alistuka, nami niliye nje nilistuka.
Nilitamani hata kumfata Nasra nimtie vichwa.
.
Pindi bado nafikiria jambo la kumfanya Nasra, ndipo Nasra alipo muongeza Careen maneno mengine yaliyo niacha mdomo wazi
.

Je Nasra Alizungumza nini!!??
.
Usikose sehemu ya 11
#Itaendelea
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Kumi Na moja
.
#Ilipoishia: Pindi nakaribia darasa alilo kuwepo Careen, ndipo nikasikia sauti mbili tofauti zikizungumza.
Moja ilikua ya Careen, na nyingine ilikua ya Nasra.
.
Mazungumzo yao yalizidi kunitisha hasa pale Careen alivyouliza kuhusu urafiki wangu na Nasra, kisha Nasra kujibu kuwa mimi sio bestfriend wake tu, bali ni boyfriend.
.
Nilistushwa sana na jibu hilo, nilihisi hasira zinanizidi kupanda, nilitamani niingie darasani nikamtie vichwa Nasra hasa baada ya kuona tayari keshaniharibia mipango yangu yote.

#[COLOR]Inaendelea[/COLOR]:
Pindi bado natafakari cha kumfanya Nasra, ndipo nikasikia Nasra akizidi kumlisha maneno ya uongo Careen.
.
Nasra: Chris ni aina ya mwanaume ambaye mwanamke yeyote mwenye kuihitaji furaha ya kweli, upendo wa dhati, basi kamwe hawezi kumuacha.
Anaujua udhaifu wa kila mwanamke duniani, ni kuwa na mwanaume mwenye kujali, kuthamini, kupenda na kuheshimu. Hayo ni mambo ninayo jivunia kwake, nampenda sana na ananipenda pia" - (Alizungumza kwa kujiamini sana, huku akitoa sauti yenye kumaanisha anachosema, ni ngumu kwa Careen kudhani kuwa amedanganywa.).
.
Careen; Hilo ni kweli, Chris ni mwanaume mwenye kujali sana. Hongera sana Nasra.
.
Nasra: Asante sana best.
.
Careen: Ila Chris ana tabia mbaya sana, hajaniambia. - (Alizungumza kwa kuonyesha kukwazika).
Na kwanini sasa siku ile alikutambulisha kama rafiki tu???!!!
.
Nasra akabaki kimya kwa dakika kadhaa.
Nikagundua hana jibu la kutoa, nikaona huu ndo wakati muafaka wa mimi kwenda kumuumbua mbele za Careen.
Nikaanza kuchukua hatua, pindi naweka mguu tu kwenye mlango wa darasa, ndipo nilipoona Nasra amestuka kuniona, huku Careen akionyesha furaha kama aliyekuwa ananisubiri kwa hamu.
.
Nikasogea mpaka mahali alipo Nasra, nikawatazama wote wawili.
Nilitamani nianze na Nasra kumuuliza maswali mbele za Careen kuwa mimi na yeye tumeanza lini uchumba.
.
Nasra akaniwahi "Chris umechafuka, ulikuwa unafanya nini?? " - (Alizungumza kwa kuonyesha kushangazwa na kuchafuka kwa nguo zangu).
.
Ndipo Careen nae aliponitazama nguo zangu kwa mshangao, nae akauliza swali hilo hilo.
Nikaona kama maswali yao yanataka kunipotezea muda na kunisahaulisha nilichotaka kumuuliza Nasra.
.
Nikamuita "Nasra".
Akanitazama usoni, nahisi alianza kupata wasiwasi kuwa huenda nilisikia maongezi yao.
.
Nikaona nisichelewe, nikafungua kinywa na kutaka kumuuliza.
Ile nataka tu kumuuliza, ghafla nilikatishwa na sauti ya mtu mlangoni, aliyemuita Careen kwa nguvu sana "Careen nakuomba mara moja".
.
Nikapiga jicho mlangoni na kugundua kuwa alikua ni Madam Irene akimuita Careen.
Nikaona kama kaharibu inshu yangu, nilitaka nimuumbue Nasra mbele ya Careen.
.
Nikamtazama Nasra kwa jicho la hasira na kumuuliza ''Nani kakwambia umwambie Careen kuwa mimi ni boyfriend wako??? "
.
Hakuwa na jibu, akabaki anaona aibu baada ya kugundua kuwa nimesikia yote aliyo kuwa akizungumza.
Nikamwongeza "Hukuona watu wengine??? Kwanini iwe mimi??? Unataka kuniharibia sio??? Sasa akija umwambie ukweli, mbele yangu"
.
Nasra akastuka baada ya kumwambia atoe ukweli kwa Careen.
Akapatwa na wasiwasi na kujikuta akijibu "Lakini Chris nafanya yote kwa faida yako ".
.
Akaendelea "Chris ulitengwa tu na ukawa kama chizi, kumbuka niliko kutoa mpaka hapa ulipo, unadhani nafurahia kuona aliyewahi kuipoteza furaha yako anarudi tena?"
.
Nikamsikiliza Nasra, nikaona kama ananitibua tu.
Na kwa hasira nilizo nazo wala sikutaka kuendelea kukaa nae karibu, lazima ningefanya kitu kibaya.
.
Nikamuambia "Niwe napata furaha, niwe nateseka, hayo ni maamuzi yangu, akirudi Careen umwambie ukweli. Kama huwezi nitamuambia mimi mwenyewe " - (Nilizungumza kwa hasira na msisitizo).
.
Baada ya kumuambia hayo nikageuka na kuondoka, huku nikimuacha akinitazama kwa huzuni nyingi.
.
Majira ya saa 2 usiku pindi nikiwa hostel, nikapokea simu kutoka kwa rafiki yangu wa kiZambia, Ivan.
Tulizungumza mengi sana, lakini mwisho ikabidi aweke wazi kilichofanya anipigie.
.
Ivan: Chris kuna mchezo mbaya sana unaendelea kati yako, Nasra, na Peter.
.
Nikastushwa na kauli yake, na kupata shauku ya kutaka kujua kiundani mchezo wenyewe ni upi.
.
Akaendelea "Leo asubuhi nilimuona Peter akizungumza na Nasra, japo sikuelewa walichokuwa wanazungumza." - (Alizungumza na kuonyesha kuwa kuna kitu anahisi kinaendelea nyuma ya pazia).
.
Maneno yale yalianza kunifumbua macho juu ya kile alichokifanya Nasra pindi alipokuwa na Careen, nikagundua kuwa huenda Nasra ameanza kutumiwa na Peter ili kumvuruga Careen asiwe na mawazo yoyote kuhusu mimi.
.
Ivan hakuishia hapo, akaniambia "Na kuna muda leo mchana nilienda nae kula, akapokea simu ambayo nahisi ilikua ni Peter kuendana na mazungumzo yao. Walivyomaliza kuongea, Nasra hakumaliza kula, aliniaga na kuondoka.
Nikapata wasiwasi sana, ilibidi nianze kumchunguza anako elekea, ndipo nilipomuona anapanda kwenye gari la Peter, na ndani yake alikuwepo Careen na Peter pia". - (Ivan alinieleza kwa utaratibu na kuonyesha wasiwasi wake juu ya mwenendo wa Nasra).
.
Hapo akili yangu iliaanza kuvurugika, nikahisi kuwa tayari Peter ameshaongeza nguvu ya mashambulizi kwangu.
Njia wanayoitumia ni kujaribu kuweka umbali wa hisia kati ya Careen na mimi, ili iwe rahisi Peter kumpata Careen bila kipingamizi.
Na Nasra alijua kuwa Careen akiwa na Peter, basi nami sitakua na chaguo lingine zaidi yake.
.
Ivan akaniambia "Chris, kama unataka kufanya lolote, jua kwamba niko nawe bega kwa bega kama rafiki, lakini tafadhali naomba usifanye lolote litakalo muumiza Nasra, shida yangu ukimpata Careen, nami nitampata Nasra." - (Alizungumza kwa hisia, na kufunguka ya rohoni).
.
Hapo ndipo nilipostushwa zaidi baada ya kuujua urefu wa mnyororo uliopo kati yetu, "Ivan anampenda Nasra, Nasra anampenda Chris, na Chris anampenda Careen, Careen ambaye anawindwa na Peter" - Nikajisemea kimoyo moyo.
Kisha kuagana na Ivan, na kukata simu.
.
Nikawaza kumbe ukionacho cha nini, mwenzako anawaza atakipata lini.
.
Nilifikiria mbinu nyingi sana juu ya kupambana na Nasra na Peter.
Wazo la ghafla likanijia kuwa niwatumie messages Nasra na Careen, wote nikawauliza "Uko wapi".
.
Nasra akajibu "Nilikua na Careen kwao Tabata, ndo narejea hostel".
.
Nikajua kweli alichosema Ivan kuwa Careen alikua na Nasra, na Peter, nikakithibitisha hapo.
Pindi najiandaa kumuuliza maswali mengine ili kumuhoji zaidi, ndipo simu yangu ikaita hapo hapo.
.
Kutazama kwenye screen, ilikua ni simu kutoka kwa Careen, nikaipokea.
"Hallow Chris" - (Alisalimia Careen).
.
Nikamjibu salamu yake, na hapo hapo Careen akaanza kunishushia lawama "Kwanini Chris umepata girlfriend na hukuniambia rafiki yako??? "
.
Nikaona njia pekee ya kunisaidia ni kukana mashtaka, nikasema "Sina girlfriend mimi, yeyote aliyekueleza utumbo huo ni muongo".
.
Careen akajibu "Yani Chris bado unamkana Nasra, sio girlfriend wako yule??? "
Bado nikamjibu "Sio girlfriend wangu, ananipakazia uongo".
.
Careen ikabidi atoboe siri, akasema "Hata mimi nilidhani nadanganywa, ila akanithibitishia hadi kwa messages zenu mnazoitana itana majina ya mapenzi, ndio nikaamini".
.
Hapo sikuwa na lakujibu, nakumbuka ni kweli Nasra alikua akipenda kuniita "Baby, Sweetheart, honey, darling ", majina ambayo nilidhani labda tunataniana tu, kumbe alikua anajua anachokifanya.
.
Nasra alinizoesha kuchat kwa sms za mapenzi kipindi nimetengwa na Careen, kwavile nilikua mpweke basi sikupinga chochote zaidi ya kufurahia messages zake.
Lakini sasa ndio zimetumika kumthibitishia ukweli Careen kuwa mimi na Nasra tuwapenzi.
.
Nilikosa cha kujibu, nikaamua kukata simu na kuizima kabisa ili ionekane imezima chaji.
.
Nikawaza mengi sana, nikaanza kupiga picha jinsi dera na wigi litakapo valishwa mwilini mwangu.
Nikabaki na maswali mengi sana, ni kweli nimekosa mbinu madhubuti za kuwanyoosha hawa watu?? Kweli nakubali kushindwa kirahisi?? .
Nilianza kuona dalili za kushindwa mapema, lakini nikajisemea kuwa "Mwanaume huwa hachoki kupambana"
.
Pindi bado nipo kwenye dimbwi la mawazo, ghafla nilisikia mlango wa chumba changu unagongwa.
Kufungua ilikua uso kwa uso na Abdulrahman akiwa ameongozana na Ramadhan na Hasheem.
.
Nikajiuliza leo Abdulrahman amefata nini kwangu, anataka kuniambia nini.
Lakin kwajinsi alivyokuja, na kwavile amekuja na marafiki zangu, nikajua wazi kuwa leo hajaja kunifanyia vurugu bali amekuja kwa jambo lingine tofauti.
.
Ramadhan akanyanyua mdomo na kuniambia "Chris kuna kitu Abdulrahman anataka kukuambia".
.
Abdulrahman akanitazama kama mtu aliye na kitu anatamani kuniambia haraka, akaniambia kwa kingereza, akimaanisha "Usiniogope, leo nimekuja kwa wema, na ni kwa faida yako."
.
Nikapata shauku ya kutaka kujua anachotaka kuniambia, nikamwambia "Niambie nakusikiliza".
Lakini Hasheem akanikatisha na kuniambia "Atakwambia huku umetusimamisha hapa nje?? "
.
Ndipo nikagundua kuwa muda wote huo nilikua sijawakaribisha ndani, nikajisikia aibu na kuwaribisha ndani.
Kwavile nilikua na shauku ya kutaka kujua anachosema nikamuuliza kabla hata hajakaa chini.
.
"Enhee Niambie ulichotaka kuniambia" - (Nikazungumza kwa kuonyesha hamu yangu ya kutaka kujua).
.
Akakaa kwanza kwenye kitanda karibu yangu, na kuniambia "Nimeamua kurudi upande wako "
.
Nikastuka, "What?? " - (Nikauliza kwa mshangao mkubwa).
.
Akaendelea "Ndani ya mechi yenu, nami kuna kitu ambacho nakitaka, na najua kwa upande wa Peter siwezi kukipata.", akakwamia hapo, akashusha pumzi nzito na kunitazama.
.
Nikaanza kujiuliza maswali mengi kichwani, ni kitu gani hiko Abdulrahman anakitaka, kiasi cha kutaka kumgeuka rafiki yake Peter.
.
Akaniambia "Kama utampata Careen, nami nitafanikiwa kukipata nachotaka, niambie kama uko tayari kuungana nami ili tumpindue Peter??" - (Akaniuliza swali huku akionyesha anamaanisha anachosema).
.
Nikamtazama, na kumuona jinsi alivyo serious, uso wake ukiwa umebeba hisia juu ya kile alichokuwa anakisema.
Nikazidi kupagawa zaidi na zaidi, hamu ya kutaka kujua anachokitaka ikanipata.
.
Nikamtazama usoni, na kumkazia macho kisha nikamuuliza "Ni kitu gani hicho unachokitaka.??"
.
Kwa kuonyesha kuwa yuko serious na anachotaka, akazungumza "Namtaka Nasra".
.
Ndipo nilipobaki namshangaa bila kujua nijibu nini, hasa kwa kuzingatia naye Ivan amejiunga nami ili kumpata mtu mmoja huyo huyo.
.
Abdulrahman akaongeza "Kumbuka kuwa tayari Nasra ameshajiunga na Peter, kama ulikua hujui hilo.
Niunge kwenye team, nitakupa pesa, pamoja na mipango yote ya kwake Peter.
Kama utashinda, basi nami nimeshinda.
Na endapo utanikatalia, basi jiandae kukosa vyote".
.
Nikabaki na maswali kichwani, nimkubalie au nimkatalie??? lakini je itakuwaje endapo Abdulrahman amekuja kama mpelelezi wa mbinu zangu???, na vipi kuhusu Ivan, nitakuwaje na watu wawili kwenye team wenye nia moja??
.
Na hapo ndipo nilipobaki nimevurugwa akili, nisijue nini cha kujibu.
Abdulrahman akauliza tena "Umekubali au bado
?? ".
.
Je Chris atakubali???"
.
Usikose sehemu ya 12
#Itaendelea
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Kumi na Mbili

#Ilipoishia: Baada ya Abdulrahman kutoa ombi lake la kutaka kujiunga nami, huku akiwa na mawazo kuwa mimi nikimpata Careen, basi naye atapata urahisi wa kumpata Nasra.
.
#Inaendelea:
Nilibaki na maswali mengi kichwani nisijue nini cha kumjibu Abdulrahman, nilikumbuka maneno aliyo niambia Ivan juu ya Nasra, nikaona kuwa wote wana nia moja hivyo inaweza leta ugomvi kwa hapo baadae.
.
Lakini nikimtazama Abdulrahman, naona kabisa ana msaada mkubwa sana kwangu endapo nitaamua kumtumia.
Nikaona nisitumie akili yangu peke yangu, nikawaomba Ramadhan na Hasheem tutoke nje kidogo tujadili.
.
Ramadhan: Wewe mkubalie, kuna kitu kimoja kinaitwa "Divide and rule", ukitaka kumshinda adui yako, lazima kwanza utumie akili kwanza kuitawanya nguvu yake, ili iwe rahisi kupambana nae.
.
Hasheem: Hapo naona mambo mawili, ukimkubalia itakusaidia kupata mipango yote ya Peter, utapata nguvu ya pesa, lakini pia utapata support kubwa itakayo fanya iwe rahisi kumshinda Peter".
.
Nikawasikiliza wote wawili, nikaona hoja zao zina mashiko ila tatizo zimeangalia upande mmoja.
Nikawauliza "Na vipi kuhusu Ivan??? Maana nae ana nia sawa na Abdulrahman ".
.
Wote wakanitazama kwa mshangao, "na Ivan pia??? ''- (Aliuliza Hasheem).
.
"Yeah" - Nikamjibu huku natikisa kichwa.
.
"Kheee...!!!!" Ramadhan alitoa mshangao na kubaki mdomo wazi.
.
Hasheem akafikiria kwa muda kidogo kisha akajibu "Naziona mechi mbili za wanaume, na wewe unatumika kama daraja kwenye mechi moja".
.
Akashusha pumzi kidogo, na kuendelea "Kama utakua makini kucheza na akili zao wote, badala ya wewe kutumiwa kama daraja, wewe ndio utawatumia'".
.
Nikageuza shingo kumsikiliza Hasheem kwa umakini, kisha macho yangu nikayatupa kwa Ramadhan ambaye nae alinyanyua kinywa chake.
Ramadhan: "Umesema kweli Hasheem, wakubaliwe wote, lakini akili itumike zaidi ili kuepusha migongano kwa hapo baadae".
.
Akatulia kidogo na kuendelea "Mwisho wa yote, Ivan na Abdulrahman watabaki na mechi yao ya kuwania kumpata Nasra, kipindi hicho wewe ushampata Careen".
.
Mawazo yao yaliniingia akilini vizuri, nikaona yana mashiko.
Tukamaliza mazungumzo na kurudi chumbani ambapo tulimwacha Abdulrahman peke yake.
.
Jibu kubwa nililotoa kwake, ilikua "Ndio, nimekubali".
Alifurahi sana na kuniambia sasa jiandae kurusha makombora kwa Peter.
.
Akanyanyuka, ili kuanza safari ya kurudi nyumbani kwake.
Tukamsindikiza mpaka nje ya nyumba ambapo alipo park gari lake.
Pindi tuna agana akaniambia "Unajua kama kesho kutwa ni birthday ya Careen??? Na umepanga kufanya nini siku hiyo".
.
Nilishangaa, maana siku zote tangu Careen awe rafiki yangu, sikuwahi kujua siku yake ya kuzaliwa.
.
Nikamwambia "Ulijuaje??? "
Akaniambia "Uko nyuma sana Chris, na hii mechi usinge iweza endapo vitu vidogo kama hivi na vyenye umuhimu kwenye maisha ya mwanamke, huvijui, sijui ulikua unashindana nini na Peter".
.
Nilibaki na tafakari maneno yake, nikajiona mjinga sana, nimekaa na Careen miezi mitatu mpaka sasa.
Tangu tuanze chuo mwezi wa 11, mwaka jana, mpaka leo hii mwezi wa kwanza, na sijajua vitu muhimu kama hivi.
Nikajiona niko nyuma sana kwenye kuwasoma wanawake.
.
Nikamuuliza "Kweli hata mimi nimejishangaa, utakua free kesho tuelekee mahali??? " - (Nilimuuliza kama atakua huru ili tuweze kuelekea kwa dkt Leonard ili kupata msaada wa kifikra juu ya wanawake).
.
Akanijibu "Niko huru, unataka twende wapi?? " - (Akaniuliza kwa mshangao).
.
"Posta, kwa Dr.Leonard " - (Nikampa jibu.).
.
Akanikubalia, na kuniaga na kuondoka na Hasheem na Ramadhan.
Nikachukua simu na kuweka appointment ya kuonana na Dr. Leonard majira ya saa 6 mchana, kwa siku ya kesho yake.
.
Kesho yake, Abdulrahman alinipitia mapema tu maeneo ya Gongo la mboto, nakuelekea wote hadi ofisini kwa Dr. Leonard.
.
Nilimwelezea mengi sana Dr. Leonard na akanipa majibu.
Akasema "Kumjua mwanamke inahitaji utulivu mkubwa sana, lasivyo unaweza kutoka kapa".
.
Akaendelea "Kuendana na jinsi ulivyo nieleza, unahitajika kuelewa mambo matatu makubwa.
1: Unahitajika kujijua wewe mwenyewe kwanza, unamtaka Careen kwa muda mfupi tu, au kwa kuwa nae milele?? Kama ni muda mfupi tu, basi huitaji mzunguko, acha kumfatilia, sababu siwezi kukushauri uende kumchezea mwanamke. "
.
Nilimtazama, nikagundua Dr. Leonard ni mwanaume mwenye kujali sana thamani za wanawake.
Akanywa maji kidogo, na kuendelea "Lakini kama unamuhitaji kwa kuwa nae milele, hapo nakushauri uwe mtulivu, utumie akili nyingi kuliko nguvu. Jijenge kihisia na ujue kujicontrol, ili kuepuka kuwa na maamuzi mabovu, unahitaji hekima na busara za hali ya juu".
.
Akaniangalia na kusema "Namba 2: Unahitajika kuwa na maarifa juu ya wanawake, nini wanapenda na nini hawapendi.
Vitu vidogo sana kama kujaliwa, kuthaminiwa, kuheshimiwa, kupewa kipaumbele, kufurahishwa, na kupenda kusikilizwa, humfanya mwanamke ajione mwenye bahati sana chini ya jua.
Lakin kuna mengine pia unahitajika kuyajua, kama mambo ambayo wanawake huvutiwa kwa wanaume. ''
.
"Mh" - Nikaguna, akaeleza mengi sana kwenye namba mbili.
Kisha akarukia namba 3.
.
Akaendelea "Namba 3: Unahitajika kumjua kiundani mwanamke unaye mtaka.
- Kama ana mtu, kuna vitu vya kufanya, ila hapa sitakushauri chochote, sitaki laana ya kuachanisha watu."
.
Akaendelea "Kuna wale wapweke, hawa huitaji nguvu sana wala kupoteza muda sana. Kuna wale waliotoka kuumizwa, hawa ndio kazi ilipo, ukimfata kichwa kichwa basi unaweza ambulia kukataliwa, au kama atakubali basi jiandae kuumizwa.
Unahitajika hekima, uvumilivu, busara ya hali ya juu sana kuubadilisha moyo wake ili kuja kupenda tena.
Na kufanya mwanamke akufungukie haya, basi uwe na akili ya kumfanya akuamini na kumjengea uwezo wa kukuambia lolote lile.
Na hii huletwa na urafiki mzuri, akikuamini, na ukiwa unaonekana una hekima ya kumshauri mambo mazuri".
.
Alizungumza mengi sana kuhusu wanawake ambayo yalinifumbua macho, na kujiona wapi nilipokuwa nakosea siku zote.
Nakumbuka aligusia umuhimu wa kukumbuka birthday ya mwanamke, na kuifanya siku nzuri sana kwake kwa kumtengenezea kumbukumbu nzuri kichwani kwake.
Hapo ndipo nilipoona umuhimu wa kuifanya tarehe 12, siku ya kuzaliwa Careen, kuwa siku bora ndani ya maisha ya Careen.
.
Nilitoka nje ya ofisi na kukutana na Abdulrahman ambae alikua akinisubiri kwa hamu, nilimueleza yote nae alipata mwangaza wa jambo la kufanya kwenye siku ya kuzaliwa ya Careen.
.
Akaniambia "Peter amepanga kumfanyia Surprise Careen, na amealika marafiki zake wengi tu. Na party itafanyika kesho mida ya saa 2 usiku, maeneo ya Kiota Jungle. "
.
Nikamsikiliza Abdulrahman kwa umakini zaidi na kumuambia, "Unadhani sisi tutafanyaje ili kumuharibia mipango Peter, na kuweza kumfanyia jambo kubwa Careen".
.
Abdulrahman akafikiria kwa muda kidogo, kisha akanipa majibu "Jiandae kwaajili ya kumfanyia surprise Careen kesho, usijali kuhusu pesa, ukumbi, keki, vinywaji, na zawadi."
.
Akazungumza kwa kujiamini huku akiingiza mkono mfukoni na kunipa $1000(dollar 1000).
Nikapokea huku nikiwa siamini nachokiona, akaniambia "Nenda kafanye maandalizi".
.
Tukaondoka maeneo ya ofisini mpaka kwenye gari, huku tukijadili mambo kadhaa.
Tukiwa ndani ya gari, tuliweka mipango yote sawa ya jinsi tutakavyo uendesha mchezo ili kumzidi kete Peter.
Kwavile Peter aliandaa Party saa 2, sisi tukaandaa party saa 12 jioni, maeneo ya hostel yetu, ili iwe rahisi kumtoa Careen kutoka chuo mpaka hostel kabla Peter hajamtuma Nasra na Abdulrahman kumfata Careen chuo.
.
Mipango ilikua hivi, Abdulrahman atakua na Nasra kwenye gari ili kumfata Careen chuo, Abdulrahman atafanya kila jambo ili kuchelewa kufika kumchukua Careen.
Atakitumia kipindi hiko kujenga ukaribu na Nasra.
Wakati Ramadhan akitumia kipindi hiko kumchukua Careen kumleta hostel.
Na zitatumika kila mbinu ili kumfanya Careen akose kuenda kwenye party aliyo andaa Peter.
.
Niliona mchezo utakua mwepesi sana, na nilijihisi kushinda mechi kabla ya yeyote yule.
Pindi bado tunajadili kabla gari haijaanza kuondoka, ndipo Peter alipopiga simu na kumuuliza Abdulrahman yuko wapi, na nani?!
.
Abdulrahman: Niko Posta Peter, peke yangu. - (Ikabidi adanganye).
.
Peter: " Niko maeneo hayo hayo, nimekuja kwa Dr. Leonard, nipo kwa nje hapa nimeona gari kama yako imepark."
.
Tukastuka wote, tukanong'onezana Abdulrahman adanganye sio gari lake, itakua amefananisha.
.
Pindi anajiandaa kumjibu, ndipo Peter alivyozungumza "Ndo lenyewe, nimeona plate number".
.
Sote tukabaki tunashangaa tusijue nini cha kufanya, kutazama huku na huko ndipo tulimuona Peter akiwa umbali wa hatua 10 kukaribia upande niliokaa mimi.
.
Tulichanganyikiwa ghafla, Abdulrahman akashika kichwa.
.
Mwisho nilibaki nimeduwaa nisijue cha kufanya.
.
*Je nini kitatokea?? Peter atajisikiaje kuwakuta Abdulrahman na Chris pamoja
???
.
Usikose sehemu ya 13
#Itaendelea

=====

MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Kumi na Tatu

#Ilipoishia: Baada ya Peter kuliona gari la Abdulrahman, ndipo alipoaanza kupiga hatua kuelekea mahali gari lilipo.
Tulipagawa sana huku nikiwa natafuta mahali pakujifichia ndani ya gari.
Lakin sehemu zote nikaona kama Peter akiingia ndani ya gari itakua rahisi kuniona.
.
Nikabaki nimeduwaa, sikujua nini cha kufanya, wala Abdulrahman hakujua nini cha kufanya huku akiwa ameshika kichwa.

#Inaendelea:
Pindi Peter anakaribia kama hatua 6 hivi kufika kwenye mlango nilipo mimi, ndipo simu yake ilipoita.
Nikaona amechukua simu na kuanza kuongea, nami ndipo nilipopata wazo la haraka kuwa Abdulrahman ashuke na kumfata huko huko alipo.

Abdulrahman alinielewa, na kwavile gari ilikua na tinted, tuliamini kuwa hakuweza kutambua Abdulrahman yuko na nani ndani.
Tukashauriana kuwa endapo wataondoka wote kuelekea kwa Dr Leonard, basi nami nitatumia hiyo nafasi kutoka ndani ya gari na kuelekea kwenye kituo cha daladala.

Abdulrahman akanielewa na kushuka ndani ya gari kumuwahi Peter.
Peter alipomaliza kuongea na simu, akawa akionekana akimuuliza maswali mengi Abdulrahman huku akiwa na wasiwasi na gari la Abdulrahman.
Lakini mwisho walielewana na kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye ofisi ya Dr Leonard.

Nilipoona tu wameshaingia ndani ya mjengo, ndipo nami nikashuka na kuelekea kwenye kituo cha mabasi kurejea chuo.

Nilipofika chuo niliwakuta Careen na Nasra wanapiga story, nikajua leo ndo siku ya kumthibitishia Careen kuwa Nasra sio girlfriend wangu.
Nikawasalimia "Habari zenu wadada".
Careen: Mh hadi mama watoto nae unamwita dada - (Akimaanisha Nasra).
.
Nikamjibu "Sijapata bado, nikimpata nitamsalimia hivyo".

Careen akabaki ananishangaa sana, nikaona nisipoteze muda, nikaondoka hapo hapo kuelekea hostel.
Nilimuacha Careen akiwa na maswali mengi sana kichwani.

Niliporudi hostel nilikutana na Ivan, Ramadhan na Hasheem na kuwapa mipango ya kumfanyia surprise Careen kwa siku ya kesho.
Lakini nilificha kuhusu mpango wa Abdulrahman na Nasra, ili Ivan asijue kinachoendelea kwa upande mwingine.

Majira ya saa 6 usiku, ya usiku wa kuamkia tarehe 12.
Niliandika ujumbe mzuri sana, na wenye kubeba hisia.
Nakumbuka Dr Leonard aliniambia jitahidi sana uwe miongoni mwa watu wa tatu wa kwanza kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa, na ujumbe wako usiwe mfupi tu, jaza pilipili, chumvi na ndimu humo humo.
Ulipomfikia Careen, akausoma na kunipigia simu muda huo huo.

Alikuwa mwenye furaha sana, na kwajinsi nilivyompa sifa na maneno yaliyojaa hisia, alijiona mwenye thamani sana.

Akaniambia "Chris, wewe ndo mtu wa kwanza kunitakia kheri ya siku yangu ya kuzaliwa, na nashangaa umejuaje"

Nikapigwa swali, nikaona bora nijibu kiujanja ujanja "Anh ukiijua thamani ya mtu maishani mwako, kamwe huwezi shindwa kuijua siku yake muhimu kama hii".

Careen alifurahi sana, lakini akakumbuka kuniambia "Chris nimepata uthibitisho kuhusu wewe na Nasra kutoka kwa Abdulrahman, ameniambia ukweli kuwa yule sio girlfriend wako".
Nikajua kuwa tayari Abdulrahman ameshasawazisha mambo.

Nikamweleza kwa undani, kisha tukatakiana usiku mwema na kila mtu kulala.

Kesho yake, siku ya tarehe 12, tulianza maandalizi mapema asubuhi.
Na kumaliza mida ya mchana.

Sikwenda chuo kabisa, na ni Ramadhan pekee ndiye aliyekuwa chuoni akipeleleza kila hatua ya Careen.

Careen aliuliza kuhusu mimi, alipewa majibu kuwa najisikia homa ndomana sikuja chuo.
Alinijulia hali kwa simu, na kuniambia kuwa kabla ya kuondoka, atakuja kuniona hostel.

Nami nikaona mpango wetu wa kwanza wa kumpata Careen ushatimia.
Ilipofika majira ya saa 11, Abdulrahman akanitumia message kuwa Kiota Jungle mambo yako tayari, na Peter amemtuma yeye pamoja na Nasra kuenda chuo kumfata Careen.
Kwahiyo itumike mbinu ya haraka ya kumtoa Careen chuo ili wao wakienda wasimkute.
Na tutumie kila njia ili simu ya Careen aidha isipatikane au iite tu bila kupokelewa.

Tulipoona watu kadhaa tulio waalika kisiri tayari wameshafika kwenye party.
Papo hapo, tukamtumia message Ramadhan ajiandae kuigiza kuwa kapokea taarifa mbaya kunihusu mimi.
Kisha Hasheem akampigia simu Careen na kumuambia kuwa "Chris ana hali mbaya, wahi hostel tumsaidie".

Careen: "Mungu wangu, nakuja hapo haraka, ngoja nimfate Ramadhan anilete".
.
Akazungumza haraka na kukata simu, kisha kumuwahi Ramadhan ambaye nae alijifanya kachanganyikiwa.

Haraka haraka wakatoka nje ya geti, na kupanda bodaboda.
Kwavile walikua na haraka na purukushani za kuwahi hostel, Careen alipokea simu ya Abdulrahman kwa haraka na kumjibu "Nitakupigia, nitakupigia".

Abdulrahman hakutaka kuhoji maswali mengi sababu alijua kinachoendelea.
.
Ikabidi ajifanye anapiga piga kila mara, lakini Careen hakuweza kupokea.
Abdulrahman akanitumia message "Kazi nzuri, mipango inaenda vizuri, nami ndio nakaribia kwenye geti la chuo''.
.
Abdulrahman na Nasra wakaingia ndani ya chuo na kujifanya wakimtafuta Careen kila pande baada ya kuona simu yao haipokelewi.

Kipindi mimi na Hasheem tuliwaambia wageni waliokuja kwenye party wote waingie ndani, tukaondoa viatu vyao nje, tukafunga mlango, taa zikazimwa, na kuwaomba wote wanyamaze kimya ndani ili isijulikane.

Ghafla tulisikia mlango unagongwa, tukajua wazi itakua ni Careen na Ramadhan.
Hasheem alienda kuwafungulia mlango, akawakaribisha.
.
Ile kipindi Careen anaingiza uso tu, ndipo taa zikawashwa, kelele za watu waliomo ndani zikapigwa "Surpriseeeeeeee".

Careen alistuka sana, akawa amebaki ameshika mdomo wake, hakuamini alichokiona, alijikuta akianzwa kulengwa na machozi.
.
Watu wote ndani wakaanza kuimba "Happy birthday to you".

Nilimsogerea Careen, na kumkombatia, hakuwa akiamini alichokiona, nilibaki nimemlaza kifuani mwangu nikimwacha akiwa analia kwa furaha.
.
Kwavile tulijua kuwa Peter na Abdulrahman watapiga simu ya Careen mara kwa mara, ndipo mpango wa kuifanya simu ya Careen iwe busy ukafata.
Ivan alimuomba simu Careen ili aitumie kumpiga picha za ukumbusho, Careen alikubali na kuitoa.
.
Hasheem akamnong'oneza, yeyote atakaye piga, basi atakatiwa simu.

Sherehe ikaendelea, vinywaji vikagaiwa, picha za ukumbusho zikapigwa na wakati wa kukata keki ulipofika, kama kawaida mwenye siku yake akakata keki na kuwalisha wote.

Lakini kwangu siku hiyo ilikua tofauti, nililishwa na kupewa busu zito la shavu.
Na Ivan hakufanya makosa, alikumbuka kupiga picha pindi ananibusu.

Peter alihangaika sana kumtafuta Careen kwenye simu, lakini simu yake haikupokelewa, Ivan alikua anakata kila muda.
Abdulrahman nae alipiga simu za kinafki ili aonekane anamtafuta Careen, mwisho akajifanya amechoka na kwenda kupumzika kwenye gari na Nasra.
Akatumia muda huo kuyajenga na Nasra na baadae wakaondoka na kurudi Kiota.

Peter alivurugwa vya kutosha, alikua akituma messages kila sekunde kwa Careen na Abdulrahman.
Abdulrahman akanitumia message "Peter atakufa kwa presha, huko kwenye party yake ni aibu tupu".
.
Nikamjibu "Mwache ale keki yake mwenyewe".

Tulicheka sana na marafiki zangu.
Nakumbuka ile dollar 1000 niliyopewa na Abdulrahman niliitumia vizuri kwa bajeti, na mwisho kupata zawadi nyingi kwaajili ya Careen.
Na kiasi kingine niliwapa marafiki zangu ili nao wapate zawadi ya kumpa Careen ili sote kwa pamoja tuonekane tulijipanga.

Hii ilikua ni mbinu aliyotoa Dr Leonard, alisema itamfanya Careen ahisi kuwa hii party ilipangwa siku nyingi, hivyo itamfanya ajione mwenye thamani na kupendwa sana.

Wakati wa zawadi ulipofika, sote tulimtunza, Careen hakuamini yote yalikuwa yakitendeka, aliona kama ndoto.

Sherehe iliisha mida ya saa 3 usiku, na mwisho wageni wakaondoka, na kupata wasaa wa kuzungumza na Careen machache.
Tulijikuta tukizungumza mengi sana, Careen aliniambia kuwa katika maisha yake hakuwahi kulia machozi ya furaha kama siku hiyo.

"Ndio mara yangu ya kwanza kufanyiwa surprise kubwa kama hii, hakika umeifanya siku yangu kuwa yenye kumbukumbu kubwa sana maishani mwangu.
Nimejiona mwenye thamani maishani mwako, asante kwa kunijali na kunipa kipaumbele "- (Alizungumza kwa hisia, huku akiwa mwenye furaha mno).

Akafungua saa mkononi mwake, kisha akachukua mkono wangu wa kushoto na kunivalisha.
Akanitazama usoni na kunipa tabasamu mwanana, kisha kuniambia "Tunaishi ndani ya dunia kwa muda maalumu, naomba saa hii iwe ukumbusho kwako juu ya ahadi nitakayo iweka kwako ".

Nikaitazama saa, kisha kunyanyua macho kumtazama Careen, akasema "Nakuahidi nitakuthamini siku zote za maisha yangu. Na endapo nitasahau ahadi yangu, saa hii itumike kunikumbusha."
.
Moyo wangu ulizidi kupata amani sana, kwa upendo nilionao juu yake, nilijikuta namkombatia na kumwambia "Hakika wewe ni wathamani sana kwangu, saa hii pia itumike kunikumbusha umuhimu wako maishani mwangu".

Ivan alipiga picha ya ukumbusho tena tukiwa tumekombatiana.
Careen akaomba simu yake, na akawa anatazama picha.

Lakini ghafla simu ya Peter ikaingia, Careen akapokea.
Peter akawa anaongea kama mtu ambaye tayari ameshapanic, akamwambia Careen aende Kiota Jungle.
Careen akauliza "Saa 3 hii??"
Nikaona anatafakari lakini mwisho akakubali, na kukata simu.
.
Nikaona sasa Peter nae anaweza akapata nafasi kama niliyopata mimi, nikahisi kama mchezo wetu unataka kuharibika.
shida yetu ilikua Careen alale na mawazo ya surprise yangu tu.
Pindi bado atafakari.
.
Lakini ghafla simu ya Careen ikaita, kutazama kwenye screen ni baba yake.
Alipopokea tu akakumbana na sauti ya baba yake iliyojaa ukali, alifokewa vibaya sana kwanini amechelewa kurudi nyumbani mpaka sasa saa 3 na dakika 46 hajarudi.
.
Careen kwa uwoga wa ukali wa baba yake, akamtumia message Peter hapo hapo kuwa hawezi kwenda.
.
Na kuniaga kwa kunikombatia, na sasa sikutaka kufanya makosa, nikampiga busu la kwenye paji la uso.
.
Na kumtafutia usafiri wa kurudi wa kurudi kwao Tabata.
.
Wakati huo huo nikakumbuka kuchukua simu na kumtext Abdulrahman, "Kaka Tumefanikisha. Pongezi nyingi sana kwako".
.
Akanijibu "Nami nimefanikiwa kupata namba ya Nasra, na kujenga nae ukaribu zaidi".
.
Akaniongeza "Niko na Peter hapa, kama kaloweshwa maji tank zima, kwa jinsi alivyolowa jasho. Waliokuja kwenye party wamemcheka sana".
.
Nikacheka sana, na kuwachekesha kina Hasheem.
Ivan akatoa wazo, kwanini tusiharibu usiku wa Peter kwa kumtumia picha ya party.
.
Nikachukua simu, na kumtumia picha ya Careen akinilisha keki, na kumtumia maneno "I wish ungekuwepo".
.
Muda huo huo Abdulrahman akapiga simu, "Chris umefanya nini??? Mungu wangu" - (Akauliza kama aliye changanyikiwa)
.
Nikamuuliza "Vipi kwani??? ".
Akaniambia jambo ambalo lilinifanya nibaki mdomo wazi.

Je alielezwa jambo gani??? Nini kimetokea???

Usikose sehemu ya 14
#Itaendelea
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya kumi na Nne

#Ilipoishia: Ivan alitoa wazo la kuufanya usiku wa Peter kuwa mbaya zaidi.
Kwavile aliandaa party kwaajili ya Careen, na hakufanikiwa kumpata Careen, hivyo kumtumia picha tukiwa na Careen kwenye party ingemfanya aumie zaidi.

Nikaona ni wazo zuri sana, nikachukua simu na kufungua WhatsApp, na kumtumia picha Peter nikiwa nalishwa keki na Careen.
Pamoja na ujumbe "I wish ungekuepo".

#Inaendelea:
Baada ya dakika kadhaa, Abdulrahman akapiga simu na kuniuliza kama mtu aliyejawa na wasiwasi sana.
"Chris umefanya nini!?? Mungu wangu" - (Aliuliza Abdulrahman).

Nilishangazwa na swali la Abdulrahman, ikabidi niulize "Kwani vipi??? "

Akanijibu "Peter amezimia na...na..." - (Alishindwa kuendelea kuongea na kukata simu).

Nikabaki nimeduwaa, na marafiki zangu nao walibaki wakinishangaa.
Ramadhan: Vipi??? - (Aliuliza baada ya kuona hali yangu tofauti).

"Peter kazimia" - Nikamjibu Ramadhan.
"Aaanh...!!!" - (Wote waliitikia kwa mshangao mkubwa).

Tukatazamana na tusijue nini cha kufanya, tukabaki tukiulizana itakuaje endapo jambo hili litakuwa kubwa zaidi ya tujuavyo.

Ivan ambaye ndiye aliyetoa wazo, akaanza kuonyesha ameingiwa na uoga mkubwa, lakini Ramadhan akasema "Kuna njia za kupambana na tatizo".
Sote kwa pamoja tukamtazama kwa makini zaidi kutaka kujua yale atakayo yasema.

Akafikiri kidogo kisha kusema "1: Kulishinda au kushindwa na tatizo huanzia ndani mwako mwenyewe, ukilichukulia tatizo kama ni kubwa sana kwako basi lazima utashindwa, na ukilichukulia kama ni dogo sana, pia utashindwa sababu utadharau kufikiri sana jinsi ya kulitatua.
Kinachotakiwa tulichukulie tatizo kawaida tu, na tuwe na imani kuwa tunaweza kulitatua, na kwa imani tuliyo nayo juu ya kulishinda tatizo ukimjulisha na imani tuliyo nayo juu ya Mungu ambaye kamwe hashindwi kitu, basi hakuna tutakacho shindwa kwenye tatizo hili".

Tukawa tumebaki kimya tukitafakari maneno yake, na mwishowe akaendelea "2: Kuwa na utayari wa kulikabili tatizo, na kuanza kulitambua tatizo, tafuta njia za kulitatua tatizo, na pia chukua hatua za kulitatua tatizo, na uwe na njia za kuliepuka tatizo ili siku nyingine lisije jirudia".

Akanyamaza kidogo, ndipo sote kwa pamoja tukaanza kuondoa wasiwasi wetu na kuanza kujijenga kiimani kuwa haliwezi kuwa tatizo kubwa sana.

Ivan akazungumza "Njia pekee ya kulitatua tatizo, sio kwa kulikimbia, ni kwa kuwa tayari kulikabili haijalishi litakua kubwa kiasi gani, tufate vile Ramadhan amesema.".

Nikaona njia ya kwanza ni kumtafuta Abdulrahman atueleze vizuri kilichotokea, ili tuwe na utayari wa lolote litakalo tokea.
Nikampigia simu, lakini alikata.

Tukabaki tunawaza la kufanya, lakini ghafla ikaingia message kutoka kwa Abdulrahman akielezea tukio lililo tokea.

Alisema " Peter alikuwa kachanganyikiwa baada ya kumtafuta Careen bila mafanikio.
Akazidi kuvurugwa baada ya kuona watu waliokuja kwenye party wakianza kuondoka mmoja baada ya mwingine.
Kuna rafiki yake mmoja ambaye ni mtani wake sana, anayeitwa Hans, ambaye alilewa sana, akawa anamtania Peter kwa sauti ya juu "Wamekuibia wajanja, ona hajaja sasa."

Peter kwa hasira aliyonayo alijikuta anamtukana rafiki yake, na Hans kuamua kuondoka na marafiki wengine.
Baada ya muda kidogo Peter alirejesha furaha yake pindi Careen alipopokea simu yake na kujibu anakuja.
Aliruka ruka sana kwa furaha, wakati huo tulikua tumebaki watu wanne tu(Abdulrahman, Nasra, Magdalena(dada yake Peter), na Peter mwenyewe).
Tukarudi kuweka vitu vizuri, lakini ghafla furaha ilipotea tena baada ya Peter kutumiwa message na Careen kuwa hatofika kwenye party."

Message ya kwanza aliyotuma Abdulrahman iliishia hapo, tukawa bado tunatafakari.
Nilianza kuyahisi machungu ambayo Peter aliyapitia.
Pindi bado tunawaza na kuwazua, ikaingia message nyingine.

Ikisema "Peter alivurugwa kabisa, akawa kama aliyechanganyikiwa, akili yake haikumkaa sawa kabisa.
Alikua akizunguka zunguka, ghafla simu yake ikaita muito wa message.
Akachukua simu haraka akidhani labda ni Careen katuma, mwisho tulimuona kama amechanganywa na alichokiona, hali yake ilibadilika ghafla na kudondoka chini.
Sote tukamuwahi kumtazama, na kuanza kumpa huduma ya kwanza.
Niliiwahi simu na kutazama alichokuwa akisoma Peter, nikakuta ni wewe umetuma picha, lakini kabla sijaifuta dada yake alinipokonya simu na kutazama kilichomfanya kaka yake azimie".

Message iliishia hapo, tulianza kupatwa na wasiwasi zaidi, niliwaza sana itakuaje endapo Magdalena(dada yake Peter) atalifanya tukio liwe kubwa zaidi.
Ivan akazungumza "Mh majanga haya "

Tulinyanyua macho yetu na kumtazama, Hasheem alishindwa kuvumilia na kuropoka "Unasema majanga wakati wewe ndo uliyesababisha, ona sasa ulilosema tufanye lishaleta madhara". - (Alizungumza kwa kulalamika na ukali zaidi).

"Eeeenheee hebu acheni kuanza kutupiana lawama, tunahitajika kuwa tayari kwa lolote lile. Kama Ivan alitoa wazo bovu, mbona wewe hukukataza lisitekelezwe, tena ukashabikia kabisa". - (Alizungumza huku akimtazama Hasheem).

Nikaona sasa kama wanaanza kutupiana lawama wote, nikawaambia "Tulieni tujue tunalimaliza vipi".
Mabishano yakaendelea kati yao, Hasheem alizidi kumshtumu Ivan kwa kutoa wazo bovu lililosababisha madhara makubwa.

Pindi bado mabishano yanaendelea.
Abdulrahman akatuma message nyingine "Peter ameshapatiwa huduma ya kwanza, amezinduka japo ameumia kiasi kwenye mkono wa kulia kutokana na kujigonga sehemu aliyodondokea.
Tunamuwaisha nyumbani, atakuwa chini ya uangalizi wa daktari wa familia.
Ila na wasiwasi na dada yake ambaye ndiye mwenye simu, nitakujuza zaidi".

Nikashusha pumzi nzito, nikasema afadhali Peter ameamka.
Nasi tukarejea hostel kupumzika, usiku niliwaza mengi sana, niliwaza jinsi papara zangu na hasira zangu zinavyoharibu mambo yangu kila siku.
Nikajiona kama mtu mwenye matumizi madogo ya ubongo, sababu kila siku navurunda mimi tu.

Kesho yake majira ya saa 2 asubuhi, nilipokea simu kutoka kwa Careen ambaye alikua ananiambia kuhusu afya ya Peter kuwa anasumbuliwa na tatizo la Hypertension(Presha ya kupanda), pamoja na maumivu ya mkono aliojipigiza wakati amedondoka.

Lakini ghafla akili yangu ilivurugika baada ya Careen kuniambia anataka twende wote Kunduchi Beach, nyumbani kwa kina Peter, tukamjulie hali.
Nikaona kama Careen anataka kunipeleka kwenye tanuri la moto.

Nikajitahidi kukataa lakini akanilazimisha na kuniambia "Urafiki gani huo Chris ambao mwenzako akipatwa na matatizo huendi??? "

Nilitamani kumweleza Careen kwanini nakataa kwenda, lakini nikaona itamfanya anichukie.
Nikakubali na akaniambia tukutane Simu 2000, kama tulivyo kutana siku ya birthday ya Peter.

Akakata simu, nami nikaona bora niwatumie message marafiki zangu kuwajulisha kuwa Careen amelazimisha niende nae kwakina Peter, na nimemkubalia.

Abdulrahman akajibu "Onh My God, You're dead".
Ramadhan nae akajibu "Mmmmh ulishindwa kukataa???!".
Ivan "Chris unajipeleka mwenyewe"
Hasheem "Mungu wangu"

Message zao wote zilizidi kunichanganya, nikajiona kama nimefanya kosa kubwa sana kukubali kwenda na Careen.
Lakini nikajipa moyo na kufanya kama Careen alivyosema.

Tulifika Kunduchi Beach majira ya saa 6 mchana, Abdulrahman alikuja kutupokea getini.
Akamuacha Careen ametangulia mbele na kunisimamisha kwanza tutete jambo.

Akazungumza kwa kingereza akimaanisha "Maamuzi uliyofanya leo ya kujileta mwenyewe kwenye mdomo wa mamba, ni mabaya sana.
Wamemwacha mpaka sasa apumzike, party ilikua ya siri na wazazi wake wameshagundua kilichotokea na wanajaribu kuchunguza kwanini mtoto wao alizimia, na party iliandaliwa kwaajili ya nani "

Maneno yake yalinitia uoga zaidi, nilizidi kujutia maamuzi niliyochukua ya kuja kwa kina Peter.
Abdulrahman akaniambia "Twende ndani, ila hakikisha unakaa mbali na Magdalena maana anajua wewe ndiye chanzo cha matatizo yote ya kaka yake.
Aliona picha yako uliyomtumia Peter na jina lako. "

Nikazidi kupata wasiwasi, Careen alisimama kwa mbele kidogo akitusubiri.
Abdulrahman akaniambia "Twende", lakini nilibaki nimesimama nisijue nini cha kufanya.
Mawazo yakawa mengi kichwani, niendelee kuwafata, au nikimbie hapo hapo.
.
Careen akanitazama na kuniambia "Chris tunakusubiri wewe", ndipo nilipostuka na kuanza kupiga hatua kuwafata nyuma.

Tulipofika ndani tuliwakuta wazazi wa Peter wakiwa sebuleni, tukatambulishwa na wazazi wao walifurahi sana kuona wanafunzi wenzake na mtoto wao, wamekuja kumjulia hali mtoto wao.

Mfanyakazi alikuja na kuuliza aina ya vinywaji tunavyotumia, tukaletewa.
Tukaombwa kusubiri kidogo tutaenda kumuona Peter pindi daktari akimaliza kumkagua ndani.

Ghafla daktari alitoka, na wazazi wa Peter wakatoka nae nje ili kuzungumza nae.
Pindi bado tumezubaa zubaa, kutupa jicho mbele ndipo macho yangu yalivyokumbana uso kwa uso na Magdalena.

Moyo ukanipiga "Paaah", nilianza kuliona joto la jiwe, sofa nililiona kubwa sana nikaanza kujisogeza karibu na alikokaa Careen.
Magdalena alinipiga jicho lililojaa chuki, kama mtu aliyekuwa akimaanisha "Nakutamani wewe nikung'ate ng'ate".

Abdulrahman akatuambia "Tayari twendeni mkamsalimie".
Nilizidi kuona nyumba ya moto, ndani aliko Peter nilijua hapafai kuonekana hata sura yangu.
Na hapa sebuleni tayari kashakuja Magdalena ambaye anaonekana ana chuki moyoni mwake juu yangu.

Nikawa bado nafikiria, nikatolewa kwenye dimbwi la mawazo na sauti ya Careen aliyeita "Chris, Chris, nyanyuka".

Ndipo nilipostuka kuwa wenzangu tayari walishanyanyuka.
Nami nikanyanyuka na kuanza kuwafata nyuma, lakini presha ilinizidi baada ya kugundua kuwa njia tunayopita kwenda chumbani kwa Peter, ndio njia hiyo hiyo aliyosimama Magdalena.

Nikaanza kuongeza speed ili kuwawahi kina Abdulrahman.
Nikawa nao sambamba, lakini tulipomkaribia Magdalena ndipo niliposhangaa sote kuona wenzangu wote wamesimama.

Abdulrahman akafanya utambulisho, akaanza na Careen.
na pindi alipohamia upande wangu, hali ilikua tofauti.

Abdulrahman: "Na huyu anaitwa..." - Kabla hata hajamalizia, Magdalena akamalizia "Chris".

Nikatetemeka, akanipiga jicho, akakunja uso wake.
Baada ya utambulisho safari ikaanza kuelekea chumbani.
Lakini nilipopiga kama hatua mbili mbele, ndipo niliposikia sauti iliyonitetemesha.

"Chris" - Aliita kwa nguvu magdalena.
Nikastuka, sote kwa pamoja tukageuka kama vile tuliitwa wote.
Tulivyomtazama, akatoa ishara ya vidole kuwa Careen na Abdulrahman waendelee na safari, ananitaka mimi peke yangu.

Nikazidi kupata presha, nilihisi kama mwili umeanza kutoka jasho jembamba.
Mikono na miguu ilikua ikinitetemeka mpaka nikahisi naweza jikuta nimejikojolea hivi hivi.
Damu ikanichemka, mapigo ya moyo yalizid kunienda mbio.

Abdulrahman alizidi kupata wasiwasi, sababu alijua kilichokua kinaendelea.
Lakini nae aliondoka akijua kuwa labda ninaweza kuumaliza huu msala mwenyewe.

Magdalena akanisogerea, na kuchukua simu ya kaka yake, na kunionyesha message na picha niliyomtumia Peter kwenye WhatsApp.

Akaninyooshea simu, nikaitazama, na kuzidi kupata wasiwasi.
Akaniambia "Nafurahi umejileta mwenyewe, na maswali zaidi ya elfu moja. Na yote unahitajika kunijibu vizuri ".

Akazungumza kwa sauti ya chini iliyojaa hasira.
Huku akinitolea macho na kunikazia.

Nikaona nimuepuke, nikamjibu "Na haraka nataka kumjulia hali mgonjwa".
Nikazungumza kwa haraka na kugeuka nikitaka kuondoka.

Akanivuta shati na kunigeuza, kisha kunishika kwa nguvu shati langu sehemu za vifungo, na kunibana ukutani.
Akanikazia macho na kuniambia "Utanijibu maswali yote kabla sijakufanya chochote kibaya".

Sikutaka kuwa dhaifu kwa mwanamke, nikaanza kuhangaika kuinyofoa mikono yake na mwili wake kwenye mwili wangu.
Nikahangaika navyoweza lakini Magdalena alikua na mwili mnene, na mwenye nguvu, ukichanganya na ukimbao mbao wangu, ikawa inanipa shida.
Nikafanikiwa kuinyofoa mikono yake kwenye shati langu, lakini nilistukia vifungo vyote vimeachia na kudondoka chini.

Nikabaki na singlendi ikionekana.
magdalena hakukubali, akanikamata kwenye mbavu na kunibinya, nami nikaona nimsukume kifua niweze kumtoa vizuri.
.
Ghafla ilisikika sauti iliyojaa hasira, iliyotamka maneno ya kingereza yakimaanisha "Mke wangu unafanya nini?? "

Ndipo nilipostuka, nikakumbuka kuwa mikono yangu ilikua kifuani kwa Magdalena, huku Magdalena akiwa ameshika mbavu zangu.

Tukastuka na kuachiana, niliona tayari msala mwingine ushatokea.
Magdalena alichanganyikiwa ghafla asijue cha kufanya.
Na kwajinsi mumewe Magdalena alivyoona shati langu lilivyokuwa wazi kutokana na kukatika kwa vifungo, mikono yangu kaikuta iko kifuani mwa mkewe.
Huku mkewe akiwa amenishika mbavu zangu.
.
Alijikuta anafoka kwa ukali kwa kingereza, akimaanisha "Yani unafanya mapenzi na mgeni??? Tena hadharani???"
.
Hapo ndipo nilipotamani ardhi ipasuke, nidumbukie niepukane na aibu hiyo.
Kupiga jicho pembeni, niliwaona Abdulrahman na Careen waliotoka chumbani haraka kuja kushuhudia.
.
Ghafla ikasikika sauti nyuma yangu, "What??? ".
Kugeuka nyuma alikuwa ni baba na mama yake Peter wakija kwa hasira.
.
Hapo nilisimama kama mstimu, nisijue nini cha kufanya
.
.
Je Chris atafanya nini??? Nini kitatokea???

Usikose sehemu ya 15
#Itaendelea
 
MAUMIVU YASIYO
KWISHA(ENDLESS PAIN)
...!!

Sehemu ya Kumi na Tano...
.
#Ilipoishia: Baada ya purukushani za hapa na pale kati yangu na Magdalena ndipo mumewe alipotukuta na mawazo yake yakamfanya ahisi kuwa tulikua katika dimbwi zito la mapenzi kuendana na jinsi alivyotukuta.
.
Alifoka kwa nguvu kwa kingereza akimaanisha "Unafanya mapenzi na mgeni??? Tena hadharani???" - (Aliuliza kwa hasira sana huku akitutazama).
.
Nilistuka sana nikijua tayari msala mwingine umeshanikuta, kutazama pembeni ndipo nilipowaona Careen na Abdulrahman wakiwa nao wametoka chumbani kwa Peter baada ya kusikia kelele.
Nyuma yangu nako ilisikika sauti nzito iliyojawa hasira, "What?? "
.
Kutazama nyuma sauti inakotoka, ilikua ni baba yake Peter akija na mama yake Peter.
Hapo ndipo nilipotamani dunia ipasuke nidumbukie labda ningeweza kuuepuka msala huu.
Nilizidi kujilaumu kwa maamuzi yangu mabovu kila wakati, nilizidi kuziona athari za kuendeshwa kihisia, sababu nimekua mtumwa kwa Careen na sasa matatizo yote haya yananikumba kwasababu yake.
Nashindwa kuwa na maamuzi binafsi na matumizi mazuri ya ubongo, yote kwasababu yake.

#Inaendelea:
Mumewe Magdalena alipandwa na hasira sana, hakutaka kunilazia damu, akanirukia na kunitwanga ngumi ya shavu.
Akaniongeza makonde lakini ilibidi niweke gadi ya mikono ili yasinipate usoni.
Wakati huo huo Abdulrahman na Magdalena walimuwahi na kujaribu kumzuia.
Tukawa ndani ya vuta nikuvute, Careen nae akaja kuongeza nguvu.
.
Baba Peter alikua na hasira, wala hakuja kutoa msaada, alikuja haraka na kuanza kunipiga mateke huku akifoka kwa kingereza, alimaanisha
"Umekuja kuharibu amani ya nyumba yangu".
.
Ikabidi mama Peter na Magdalena wapambane kumzuia baba Peter, na Careen na Abdulrahman wapambane kumnyofoa mumewe Magdalena.
.
Baada ya purukushani wote walifanikiwa kushikwa vizuri, Careen akamuachia mumewe Magdalena na kuja upande wangu.
.
Nilitamani upenyo nilioupata niutumie kukimbia, lakini nikahisi kuwa nikikimbia watahisi kuwa ni kweli.
Nikabaki naomba Mungu tu.
.
Mabishano yakawa yanaendelea kwa lugha ya kingereza yakiwa na maana ifuatayo:
Magdalena akaongea kwa nguvu akijaribu kumuelewesha mumewe "Unachohisi sicho, wala sikuwa nafanya nae ulichokuwa ukidhani".
.
Mumewe kwa hasira akajibu "Nachohisi sicho?!! Mikono yake ilikua inakushika nini??! Na wewe ulimshika nini? Na mlikua mnakombatiana kombatiana, unadhani mimi ni mjinga?? " - (Alizungumza kwa hasira kama mtu aliyetamani kumrukia mkewe).
.
"Haukuelewa kilicho kuwa kinaendelea, nilikua nimembana anieleze ukweli kuhusu Peter, hakutaka kuniambia, ndomana tukawa tunakunjana, hukuona shati yake nimekata vifungo??" - Alizungumza Magdalena kwa ukali huku kama anataka kulia.
.
Baba yake Peter akadakia "Hivyo vifungo vimekatika sasa hivi hapa" - (Akazungumza kwa kukanusha kauli ya Magdalena).
.
Sikutaka kuchelewa nami nikatetea "Vilikatwa na Magdalena "
Ghafla nikazimwa "Nyamaza mwana haramu mkubwa" - (Alikua ni mama yake Peter aliyetoa sauti ya ukali).
.
"Ni kweli mama, vilikatwa tangu mwanzo" - (Abdulrahman nae akatetea upande wa Magdalena).
.
"Havikukatwa kwa ugomvi, wamevikata kwenye mahaba, nimeshuhudia kwa macho yangu mawili" - (Alizungumza mumewe Magdalena).
.
Akataka kuruka ili amfate mkewe amshindilie japo makofi ya uso, lakini Abdulrahman alisimama vizuri kumzuia.
.
"Kama ni kweli mlikua mnagombana. Ulikua unamuuliza kuhusu Peter ili iweje? " - (Aliuliza Mama Peter).
.
Magdalena akamtazama mama yake, na kuamua kutoboa siri kuwa Peter alizimia baada ya kupokea message na picha kutoka kwa Chris.
.
''Kuna uwezekano Chris anajua kila kitu kuhusu Peter, na kuna siri kubwa kati ya Chris na Peter.
Na nilimbana ili anieleze, lakini hakuniambia chochote ndiomaana tukabaki tukigombana" - (Alimaliza kama hivyo Magdalena, kisha kuchukua simu ya Peter, na kufungua message niliyomtumia Peter na kumuonyesha mama yake, na mama yake akamuonyesha baba yake.
.
Kipindi hicho chote nilikua nimebaki kama msukule, sikujua nini cha kufanya, kila sekunde zilivyozidi kwenda nilizidi kutamani hata ningekua na mabawa nipeperuke, au hata ningekua mchawi niyeyuke.
Lakini haikuwezekana, kutazama mlango wa kutokea ulipo, ulikua umerudishiwa, nikapiga hesabu za haraka haraka kutoka niliposimama mpaka mlango wa kutokea, na kutoka mlangoni mpaka geti la fensi, nikaona hii ndio chance ya kutokea.
.
Nikapata akili ya haraka kuwa nikimbie, sababu hata nikibaki bado nitapata shida ya kuingizwa kwenye kesi ya kumsababishia Peter matatizo.
Nikahesabu kimoyo moyo, 1, 2, 3, lakini nikasita baada ya kukumbuka kuwa nisingeweza kupita getini wala nisingeweza kuruka ukuta kwajinsi ulivyo mrefu.
Nikabaki nimesimama pale pale huku nikisubiri kama mfungwa anaye ngojea msamaha wa Rais.
.
Wakahoji mengi sana kuhusu message zangu kwenye simu ya Peter, lakini niligoma kueleza chochote na kusema kuwa "Peter ni rafiki yangu, na Careen ni rafiki yangu, ndio maana nilimtumia Peter picha ya birthday ya Careen na ndio maana nikamwambia "I wish ungekuepo" sababu hakuwepo."
.
Careen alistuka baada ya kusikia nimemtumia picha Peter.
Lakini Magdalena akawa tayari ameshapata jambo.
.
Akasema "Kama nyinyi ni marafiki, kwanini wewe uliandaa party kwaajili ya Careen, na Peter aliandaa kwaajili ya Careen???!!! Kwanini hamkuandaa wote kwa pamoja.
Na iweje Peter azimie baada ya kuona picha uliyo mtumia.??"
.
Nilishindwa kujibu lolote, nilihisi kuna kitu Magdalena anajaribu kuchimba.
.
Hapo ndipo Careen alipo gundua kuwa kumbe Peter alimuambia aende Kiota kwaajili ya kumfanyia surprise.
.
Baba yake Peter akamtazama Abdulrahman na kumuuliza swali, "Chris na Peter ni marafiki??? "
.
Abdulrahman akajibu "Ndio".
.
Mama yake Peter akasema "Nadhani majibu ya maswali yetu kichwani, yako kinywani mwa Peter
Na hatuwezi kumuuliza chochote Peter kwasasa mpaka presha yake itakapo kaa sawa".
.
Sote tukatazamana, nikaanza kupata mwanga mwa matumaini, nikajua wazi kuwa sasa naweza kutoka salama.
.
Baba yake akanitazama na kunikazia macho, akasema "Uko huru leo, ila tambua lolote tutakalojibiwa na Peter, ndilo litakalofanya uwe huru zaidi au laanh".
.
Nilinywea sana ila nikaona afadhali, nilishukuru Mungu sana.
Abdulrahman akaniambia tuondoke, Careen akawa tayari na tukaanza kuondoka.
Ghafla mumewe Magdalena akaniita, nilipomgeukia akanisogerea na kuniambia "Usidhani umeponyeka, ukweli ukijulikana ndio nitajua cha kukufanya. Hizi sababu bado hazijanifanya niamini kuwa hauna mahusiano na mke wangu".
.
Nilibaki nikimuangalia tu, Abdulrahman akamfokea "Michael inatosha".
.
Nikageuka na kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye gari la Abdulrahman.
Tulipanda na kuondoka, njia nzima tulikua mabubu na wala hakuna aliyemsemesha mwenzie.
Tulimshusha Careen Tabata, nami nikaletwa mpaka Hostel.
.
Pindi nataka kushuka kwenye gari, Abdulrahman akaniambia "Subiri Chris".
.
Akazungumza huku akichukua simu yake na kufungua Gallery, na kunionyesha picha ya msichana na kiNigeria.
.
Niliitazama ile picha na kumuona msichana mzuri tu.
Nikamtazama Abdulrahman, kiukweli sikuwa kwenye mood ya kuzungumza chochote.
Abdulrahman akaniambia ''Chris usijutie ulichotenda jana na rafiki zako, na hata kilichotendeka leo nyumbani kwa kina Peter".
.
Nikamtazama usoni kwa makini, nilihisi labda anataka kunipa moyo tu kwa maneno matamu, lakini nilitamani kumuuliza swali kuhusu picha ya msichana wa kiNigeria niliyeonyeshwa.
.
Akaniambia "Japo umepitia magumu, ila naona dalili zako za ushindi zinakaribia.
Sababu wazazi wa Peter wakishajua kuhusu jambo linalo endelea kati ya Peter na Careen. Basi jua kuwa mchezo umeshaushinda.".
.
.
Maneno yake yaliniachia maswali kichwani, nikawa bado natafakari, akaniambia "Na usidhani Magdalena anakuchukia, wala hakuchukii, Anataka kuujua ukweli kama Careen na Peter wana mahusiano au vipi.
Na hata alivyo alikwa kwenye party, alikuwa akihoji maswali mengi kuhusu Careen na Peter, na kuna sababu kwanini anahoji''.
.
Nilianza kupata shauku ya kutaka kujua kwanini Abdulrahman anayasema yote hayo, ikabidi nimwambie "Sijakuelewa bado, hebu nieleze vizuri"
.
Akaniambia "Peter anampenda Careen, lakini....wazazi wake Peter wa...wa...." - (Akakwamia hapo).
.
Nikapata shauku ya kutaka kujua wazazi wake Peter "Wa" wamefanyaje.?!
Nikarudia alikomwamia "Wa..???"
.
Akanipa jibu ambalo lilinifanya nisiamini masikio yangu, nilipata furaha ya ghafla, na kutamani hata niruke ruke ndani ya gari
.

Je Chris amepewa jibu gani!??! Na hiyo picha ni ya nani!?? Na Magdalena ana sababu zipi za udadisi wake???

Usikose sehemu ya 16
#Itaendelea
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Kumi na sita...

#Ilipoishia:
Abdulrahman alinipa picha ya msichana wa kiNigeria, na kunipa maneno kadhaa yenye kunitia moyo, lakini sikumuelewa hata kidogo nini alichokuwa akimaanisha.
.
Ndipo Abdulrahman akanitobolea siri kuwa Peter anampenda Careen, lakini wazazi wake wameshamchagulia mchumba kutoka katika familia ya kitajiri, nchini Nigeria.
Na kivyovyote vile, Peter hana uwezo wa kupingana na chaguo la wazazi wake.
*************
#Inaendelea:
Nilipatwa na furaha ya ghafla, moyoni nikaingiwa na amani nikijua kuwa kumbe shida zote nilizopitia zilikuwa na matunda mbele yake.

Lakini nikakumbuka jambo na kumuuliza Abdulrahman, "Kwani Peter hajui kama ameandaliwa mchumba??? Na wewe rafiki yake kwanini hukumwambia?? Na kwanini Magdalena anachunguza sana??? ".

Nilimtupia maswali mfululizo huku nikiwa nimemtupia jicho kavu, huku nikisubiri nipewe majibu yenye mashiko.

Abdulrahman akatafakari kwa sekunde kadhaa na kuniambia "Mchumba ametafutiwa hivi karibuni kipindi tayari ameshampenda Careen, na bado wameliweka siri.
Na siwezi kumwambia hii siri."

Akanyamaza kimya kidogo na kulamba lips, akafungua kinywa tena na kusema "Kuhusu Magdalena, anajaribu kuchunguza kama Careen na Peter wana mahusiano ili ayavunje, sababu nae anataka kaka yake amuoe binti wa kitajiri, chaguo la wazazi wake.''

Maneno yaliniingia vilivyo na kuanza kupata picha kwanini Magdalena alikua akinikazia nimweleze ukweli.
"Shit, ningejua ningetoboa siri pale pale. Shenzi "- Nilijisemea kimoyo moyo.
.
Nilianza kupata amani na kuendelea kuamini kuwa kweli kila jambo ndani ya maisha yetu, hufanyika kwa kusudi maalumu.
Nikaagana na Abdulrahman, na kwenda kupumzika hostel.

Kesho yake marafiki zangu walikuja kuniona na kunipa pole kwa yote yaliyotokea, Ivan alijisikia vibaya sana na kujilaumu mbele zangu kuwa yote hayo amesababisha yeye sababu ya wazo baya alilotoa afanyiwe Peter.
Nikamwambia usihofu, mimi ndiye mwenye makosa sababu nilikua na uwezo wa kukataa kutuma picha, na hata kukataa kwenda na Careen.

Ramadhan akaleta utani "Duh sema umechezea vitasa mpaka uso umeiva" - (Alizungumza kauli iliyojaa rejesta za mtaani, akimaanisha "umepigwa ngumi mpaka umekua mwekundu").

Wote wakacheka, Hasheem akaongeza "Ningekua mimi asingeweza kunipiga kizembe kama hivyo ".

"Mmmh mxieeew" - (Nikaguna na kusonya)

"We mbwembwe tu, ungefanyaje unadhani? "- (Ramadhan akauliza)
.
"Haaa, wehu nyie, nikubali kupigika kirahisi!??! ningetoka nduki kama Lamborghini hahahah "- (Hasheem akajibu huku akicheka)

Sote kwa pamoja tuliangua kicheko, na hili ni jambo kubwa ambalo najivunia kuhusu marafiki.
Haijalishi mna huzuni kiasi gani, bado utapata nafasi ya kucheka.
Tangu hapo nikaamini ile kauli ya wanasaikolojia kuwa kuwa na watu wanaoweza kukufurahisha, ni dawa mojawapo ya kuondoa upweke na huzuni.

Tulipika chakula cha mchana, tukala pamoja na mwisho wakaaga na kila mmoja kuondoka.
Nikarudi chumbani na kujaribu kuutafuta usingizi japo ilikua jioni, majira ya saa 10.

Pindi bado nautafuta usingizi kitandani, ndipo niliposikia mlango unagongwa.
Nikaamka na kwenda kufungua, kutazama alikua ni mwanafunzi mwenzangu anaekaa chumba kinachofata.
.
"Chris una mgeni nje " - Alizungumza Erick huku akigeuza na kuondoka.

Ikabidi nirudi ndani na kuvaa shati, kisha kutoka nje kutazama ni nani huyo.
Nikatoka nje na macho yangu yakakutana na Nasra aliyekuwa amesimama akinisubiri.
Ni mara yake ya kwanza kufika mahali napoishi tangu nijuane nae.

Nikamkaribisha ndani, na kumletea kinywaji.
Akanieleza jinsi alivyoelekezwa na Hasheem mpaka kufika.
Naye alikuja kunipa pole, pamoja na kuniletea dawa za maumivu za kujichua, pamoja na matunda.

Tukapiga story mbili tatu kama nusu saa, ghafla nikasikia mlango wangu unagongwa.
"Chris "- ilikua ni sauti ya Careen akiita.

Nikastuka, nikamtupia jicho Nasra na kumuona nae kakunja sura ghafla.
Nikajibu "Pita mlango uko wazi huo".

Careen akafungua mlango na kuingia, lakini alisimama ghafla, na kubaki ameduwaa kumkuta Nasra ndani.

Nilipata wasiwasi nikidhani labda Careen amestuka kumuona Nasra yuko ndani, lakini nilimuona akirudi hatua mbili nyuma na kuchungulia nje.
Nikapata wazo jipya kuwa huenda amekuja na mtu.

"Unamchungulia nani?! " - Nikamuuliza Careen.
"Anh ni Abdulrahman, nilimwacha anaongea na simu nje".

Akaingia ndani na kutusalimia, dakika mbele zilizofata, Abdulrahman akabisha hodi na kuingia ndani.
Nae alishangaa kumkuta Nasra ndani.

Nikawaletea vinywaji, na story ziliendelea.
Jambo lililomkera Nasra zaidi ni baada ya kuona Careen ananikabidhi dawa za maumivu tofauti na zake.

Akaropoka "Sidhani kama zinaweza kuwa nzuri kuzidi nilizoleta".
.
Wote tukamgeukia, Careen akajibu "Labda, sijajua".

Nikagundua kuwa Careen hakutaka kuleta mabishano, akamzima kijanja ili asiendelee na mada yake.
Story zingine zikaendelea na baada ya muda wote waliaga na kuondoka.

Wiki moja baadae, ikiwa ni siku ya Jumapili, nilipokea message kutoka kwa Abdulrahman aliniambia "Good News, Peter amehojiwa na familia, na ameeleza kuwa anampenda Careen".

Nikamjibu "Imekuwaje?? "
Akanijibu "Wazazi wamemkanya na kumuonyesha picha ya chaguo lao".

Niliruka na kufurahia sana nikijua tayari nimeshapunguza vizuizi vinavyo nikwamisha.
Abdulrahman akatuma message nyingine akisema "Careen amepigiwa simu na wamemuonya avunje mazoea na Peter kabisa".

Dakika mbili hizo hizo, simu yangu ikaita na nilipotazama kwenye screen nilikutana na namba ngeni.
Nilipopokea nikasikia sauti ya Magdalena.
Tukasalimiana na mwisho akaomba msamaha kwa kunishuku vibaya, pamoja na kuniletea kash kash nyumbani kwao.

Ghafla sauti ya Magdalena ikakata, na sauti ya kiume ikasikika ikikoroma kwa lugha ya kingereza, ikimaanisha "Na leo nimekukamata tena unazungumza na mke wangu".

Nilistuka baada ya kugundua ni Michael(mume wake Magdalena) ndiye aliyekuwa akinikoromea.
Nikabaki kimya, mapigo ya moyo yakizidi kunienda mbio.

Pindi nataka nikate simu tu, ndipo niliposikia anacheka na mkewe kwa nguvu, akasema "Chris muoga sana".
Ndipo nilipogundua kuwa nilikua nataniwa.
Nikajichekesha kinafki japo alinikera.

Michael aliniomba radhi kwa vurugu alizonifanyia, na aibu aliyoniletea siku niliyokuwa kwao.
Nikajisemea kimoyo moyo "Yani wewe ungekua karibu leo, ningekurudishia ngumi za uso".

Lakini nilishukuru Mungu baada ya ukweli kugundulika, nami kuwa huru.
Mazungumzo yakaisha, tukaagana na kukata simu.

Hazikupita hata dakika mbili, simu yangu ikaita tena, kutazama kwenye screen ilikua ni "PETER".
Sikutaka kuchelewa, nikaipokea, na kuisikia sauti ya mtu iliyojaa huzuni.

"Hey, asante kwa kuharibu furaha yangu.
Asante kwa kukatisha ndoto zangu.
Ila jambo moja tu, usidhani umeshinda.
Mechi bado inaendelea." - Peter akanyamazia hapo.

"Haaanh"- Nikaguna kwa dharau, kisha kucheka kwa nguvu sana.
Nikamjibu kwa dharau "Nilidhani umenipigia simu ili uniambie ni wapi, saa ngapi, tukutane ili nikuletee wigi na dera la kuvaa.".

Sikutaka kumkawiza, nikamuongeza "Bro, umeshashindwa mechi, usiniletee mikwara.
Subiri kesho nakuja na make up ili upendeze".
.
Nilipomaliza kusema kauli hizo, na simu nikakata hapo hapo.
Akapiga tena, nikakata.

Baada ya sekunde kadhaa, akanitumia message "Usilete dharau wakati bado hujampata, mechi bado inaendelea mpaka ajulikane mshindi nani".

Baada ya kuisoma ile message, kumbukumbu zikanijia kichwani kuwa kumbe hata mimi bado sijafanya lolote.

Pindi bado natafakari, nikaongezwa message nyingine "Nitahakikisha hakuna atakaye shinda mchezo huu, subiri na uone kitakachojiri".

Nilirudia kuisoma message mara mbili mbili, nikiwaza kile ambacho Peter anawaza kunifanyia.
Nikajisemea "Nilidhani mchezo umeisha, kumbe ndo kwanza unaanza".

Usikose sehemu ya 17
#Itaendelea
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Kumi na saba
.
#Ilipoishia:
Nilimtamkia Peter kauli zilizojaa dharau na kumkatia simu.
Haikuchukua dakika, alinitumia message za kunitisha kuwa nisidhani mchezo umeisha, bado mechi kati yetu inaendelea na atafanya kila analoweza kuhakikisha kuwa simpati Careen.

#Inaendelea:
Nilibaki na mawazo juu ya Peter, anawaza kunifanyia nini.
Niliitazama safari yangu ya kumpata Careen kama safari iliyojaa shida, na misukosuko isiyo isha.
Nikajisemea kimoyomoyo "Siku nikimpata, lazima nifanye sherehe dadeck ".
Siku iliyofata, niliwahi chuo mapema na kukaa na Careen ndani ya darasa.
Alionekana mwenye huzuni sana na nilijua tu kauli za wazazi wake Peter zitakua zimemsononesha.
.
Nikamwambia "Magdalena alinipigia jana, wameniomba radhi".
.
Akanitazama kwa unyonge, na kuniambia "I wish nami ningepigiwa simu na kuambiwa maneno mazuri kama wewe.
Wamenisononesha sana, wamenitamkia kauli za ajabu sana.
Na mwisho wamenipa vitisho kuwa nivunje urafiki na mtoto wao".
.
Nilimtazama Careen kwa huruma sana.
Akaendelea "Potelea mbali, siwezi lazimisha urafiki.
Nilikua na rafiki kabla yake, na ninaye mpaka sasa.
Nafurahia bado upo nami Chris". - (Alizungumza kwa hisia sana huku akiwa amejawa na huzuni kubwa mno.).
.
Nikampa pole pamoja na kumpa moyo kuwa ndivyo binadamu walivyo, avumilie tu.
.
Kutupa jicho kwa mbele nilimuona Peter anachungulia ndani ya darasa kama anatafuta mtu hivi.
Akatazama huku na huko, mwisho akatuona na kutufata.
Akasalimia, na kuomba azungumze pembeni na Careen.
.
Careen akanyanyuka na kutoka nae nje ya darasa.
Nami nikaona nisipitwe na linalo endelea, nikanyanyuka na kunyata taratibu karibia na mlangoni.
.
Peter alikua akiomba msamaha juu ya kauli walizo zungumza ndugu zake, na kumuomba azipuuzie tu na urafiki wao uendelee.
.
Careen alimjibu " Hapana siwezi.
Nilikuheshimu kama kaka yangu, ila kwasasa sitaki ukaka wala urafiki na wewe.
Ndugu zako wamenitupia lawama kibao, na naomba nisiendelee kuongea na wewe, nilishaambiwa nikae na wewe mbali ". - (Careen akatoa kauli iliyojaa huzuni iliyochanganyika na hasira, akageuka na kutaka kuondoka)…
.
Peter akamuwahi na kumshika mkono, na kumuambia "Nisamehe mimi, nisamehe sana.
Halikua kosa lako japo wamekushutumu.
Ni kosa langu, kosa la moyo wangu kukupenda.
Ni kosa langu nilitaka kukusogeza karibu, ili uje kuwa wangu peke yangu, wa maisha yangu.
Najiona mjinga kukukosa, nailaumu familia yangu kwa kunikatiza ndoto yangu ". - (Alizungumza huku akilengwa na machozi).
.
Careen akamtazama usoni na kumjibu "Peter tusipotezeane muda.
Isije na ndugu zako wakanikuta hapa nimesimama na wewe mwisho ikawa nongwa.
Na nikukumbushe tu kuwa sijawahi, siwezi, na wala sitowahi kutamani kuwa nawe kimapenzi.
Ulikua kama kaka yangu, ila kwasasa hata ukaka hauna tena. Nitakuheshimu kama watu wengine ambao sijawahi kufahamiana nao.
Naheshimu mawazo ya wazazi wako, na natii onyo lao kwangu."
.
Akazungumza na kumwacha Peter amesimama.
Niliposikia anakuja ilibidi nibadilishe pozi na kujifanya kama nilikua najipiga selfie.
.
Careen akarudi darasani na kuchukua bag lake na kuelekea garden.
Peter alibaki amesimama pale pale nje.
Na mimi nikabeba bag langu na kutoka darasani pia huku nikiimba kiuchokozi.
"Kuachwa kuachwa aanh, kuachwa ni shughuli pevu.
Mbaya zaidi kwa unaye mpenda, wewe umesimama, yeye ameondokaaa hahahah "
.
Kisha nikacheka sana.
Peter akanitazama kwa hasira, nikaona huu msala, nikaongeza mwendo zaidi kuelekea garden pia.
.
Hatua kadhaa kabla sijafika kwenye benchi aliloenda kukaa Careen, simu yangu iliita.
Kutazama kwenye screen, ilikua ni simu kutoka kwa Abdulrahman.
.
Nikaipokea na kusalimiana nae, alionekana mwenye sauti iliyojaa huzuni na wasiwasi mwingi.
.
Akaniambia "Chris mambo yameharibika."
Nikamuuliza "Kivipi bro? "
.
Akanipa jibu ambalo liliniacha mdomo wazi, alijibu "Peter ameshagundua yanayo endelea kati yangu na wewe Chris. Na walikua wanafanya uchunguzi kisiri siri yeye na Nasra".
.
Nilistuka sana, nikajiuliza mengi sana kichwani, lakini Abdulrahman akanipa majibu.
.
Akasema "Peter alinifata nyumbani kwetu, jana majira ya saa 4 usiku.
Alinikuta chumbani kwangu nikiwa nimepumzika.
Kwajinsi alivyokuja tu nilijua tu hayuko sawa na kuna kitu anataka kuniambia".
.
Abdulrahman alinieleza mengi sana kwenye simu ambayo yalinichanganya sana.
Na alinieleza yafuatayo:
*********
Peter: Ulienda kwa Chris week iliyopita??.
.
Abdulrahman alishindwa kukataa kwavile alikutana na Nasra mahali napoishi.
Akajibu " Yeah, Careen aliniomba nimsindikize akamuone Chris."
.
Peter akamtazama Abdulrahman kama anamtafakari, kisha kumuuliza tena "Vizuri. Na kwanini ulikua unamtetea Chris siku ya ugomvi nyumbani!??? "
.
Abdulrahman akaanza kuhisi Peter ameanza kumhisi kitu, akaanza kupata wasiwasi.
Akamjibu "Sikumtetea Chris, nilitetea nilichokiona ".
.
Peter akaguna "Mh" na kuanza kupiga hatua kumsogerea karibu zaidi Abdulrahman, akamuuliza "Abdulrahman, unadhani ni nani huyo ambaye amemwambia Chris kila jambo lililotokea nyumbani???"
.
Alimtupia swali huku anamtazama kwa umakini zaidi, na kumshika bega.
.
Abdulrahman akageuza shingo na kumtazama Peter, lakini alishindwa kutoa majibu.
.
Peter akaongeza swali lingine "Amejuaje kama nimeshashindwa?".
.
Abdulrahman akafikiria kwa dakika kadhaa na kumjibu "Na wasiwasi itakua ni Magdalena ".
.
Peter akajibu "Nilimsikia kipindi Magdalena anazungumza na Chris, hakugusia chochote zaidi ya kuomba msamaha tu".
.
Abdulrahman akazidi kupata wasiwasi, alianza kuona kuwa mambo yanaharibika.
Akamjibu "Peter inaonekana huniamini, inaonekana unahisi labda nimekua mnafki kwako.
Kama kuhusu Chris kujua mambo yaliyojiri, huenda hata Careen amemwelezea.
Au unataka kusema na Careen nae hawasiliani na Chris??
Kama huniamini sema bwana". - (Abdulrahman akazungumza kwa ukali sana, ili kujaribu kujiaminisha mbele ya Peter.).
.
Peter alimtazama kwa mshangao mkubwa, na kumjibu kwa hasira "Abdulrahman, niliacha kukuamini tangu siku uliyompeleka Chris Posta, kwa dokta Leonard.
Na bado ukamficha ndani ya gari huku ukinidanganya umekuja peke yako" - (Peter alijibu kwa hasira na ukali sana).
.
Abdulrahman akastuka baada ya kusikia maneno hayo.
Peter akaendelea kuzungumza kwa ukali "Sikuwa na kufatilia, na wala sikuja kukufuma ukiwa na Chris.
Nilikuja kwa mambo yangu, Thank God nikasema nipumzike ndani ya gari kwanza mpaka muda wa appointment utakapofika.
Ndipo nilipowaona wewe na Chris mnatoka kwa Dr Leonard."
.
Peter akakwamia hapo, akawa tayari ameshapandisha hasira.
Abdulrahman alinywea, akawa mdogo kama Piriton.
.
Peter hakutaka kuendelea tena kubishana na Abdulrahman, akaamua kutoa kauli za mwisho zenye kuuvunja urafiki wao wa miaka mingi.
Kwa sauti ndogo na ya upole, akazungumza "Sikutaka kuamini, nikakupa nafasi nyingine, lakini nilimuomba Nasra akufatilie kwa ukaribu zaidi.
Na ukweli wa yote nimeshaujua."
.
Abdulrahman akashusha uso wake chini kwa aibu, lakini Peter alizungumza kauli zilizomstua Abdulrahman zaidi.
Peter alisema "Wewe ndiye uliyepanga kuharibu party yangu, na ukampa Chris pesa ya maandalizi ya party.
Wewe ndiye unayetoa siri na mipango yangu yote.
Wewe ndiye mnafki namba moja kwangu.
Usijiulize nimejuaje hayo yote, dunia haina siri hasa ukiwa unatumia akili na pesa.
Kuanzia leo naomba tusijuane".
.
Peter alimaliza kuongea na kuondoka.
Abdulrahman akabaki na maswali mengi sana kichwani kuwa ni nani ndani ya kundi letu, anatoa siri kwa Nasra au Peter.
********
.
Abdulrahman alinieleza yote yaliyomtokea, na kuniomba tufanye uchunguzi.
Tukaagana na kukata simu, lakini nami nilibaki na swali kichwani kuwa kati ya Hasheem, Ivan, na Ramadhan, ni nani anayetoa siri kwa Nasra na Peter?! .
.
Nikarudisha kumbukumbu nyuma, na kukumbuka siku ambayo Nasra alikuja mahala napoishi kwa mara ya kwanza, alisema Hasheem ndiye aliye muelekeza.
Nikajiuliza "Walianzia wapi story zao mpaka kufikia kuelekezana?".
.
Lakini pindi bado nimesimama natafakari, kwa mbali nikamuona Ivan akiwa anatoka na Nasra darasani.
Nikajiuliza "Au ni Ivan, kwa vile ana mazoea na Nasra?"
.
Pindi bado nipo ndani ya dimbwi la mawazo, nikastushwa na sauti ya Careen akiniita.
Nikasogea mpaka kwenye benchi alipokaa, na kumsikiliza.
.
Kwa upole, na sauti iliyojaa huzuni, akaniambia "Chris, unajua tangu jana nigundue kuwa Peter alikua ananipenda siku zote hizo, na kupewa kauli za ajabu na wazazi wake.
Nimejikuta nawaza mengi sana".
.
Careen alizungumza kwa hisia sana, akameza mate kidogo na kuendelea kuzungumza "Kuna muda nimewaza ni kheri nisingejuana nae, kheri nisingempa hata nafasi ya urafiki, labda asingenipenda na leo hii asingepitia maumivu sababu yangu".
.
Careen alianza kulengwa na machozi, alionyesha kiasi gani ameumia na jambo lililotokea kati yake na Peter.
Akaniuliza "Nitamkumbuka kwa mengi sana, amenifanyia mengi sana.
Nakumbuka kipindi nilichogombana na wewe, kipindi nilichoachwa na boyfriend wangu, Peter alikua kila kitu kwangu.
Alipambana kuirudisha furaha yangu.
Na hata ile semina tuliyo ombana msamaha siku ile, alinilazimisha yeye twende kwenye semina.
Siwezi kumsahau".
.
Nilibaki nimetulia tu nikisikiliza, nilianza kuuona umuhimu wa Peter ndani ya maisha ya Careen.
Na hakika haijalishi Careen atazungumza kwa ujasiri kiasi gani mbele ya Peter ili kukaa nae mbali kama alivyo onywa, lakini kamwe moyoni mwake hawezi kuisahau thamani ya Peter.
.
Nilikua nawaza mengi sana juu ya Careen na Peter, lakini ghafla nilistushwa na mkono wa Careen uliotua begani mwangu.
.
Aliyatamka maneno ambayo yalianza kuivuruga akili yangu, mapigo ya moyo yalizidi.
Nikaanza kukosa amani kabisa.
.
Careen alisema "Wakati wote huo niliokuwa nae sikujua kama ananipenda, nilidhani ananichukulia kama dada yake, kama nilivyokua namchukulia.
Hivi Chris, wanaume hamuwezi kumjali mwanamke bila kumtaka kimapenzi???".
.
Swali lilikua gumu sana kwangu kujibu, nikabaki nimenyamaza.
.
Hakuniacha nipumue, akaniongeza swali lingine "Mwanaume akionyesha kukujali, kukuheshimu, kukuthamini, kujitoa kwako kwa kila kitu. Ndio anamaanisha anakupenda??? "
.
Nikamtazama Careen usoni nikiwa naona kinywa kizito kujibu maswali yake.
.
Akaendelea "Kwajinsi nilivyopitia maumivu kwa boyfriend wangu aliyeniacha, sitamani tena kuwa na mwanaume wa aina yeyote yule".
.
"Chris, matendo yako yanafanana na ya Peter.
Naogopa usije pitia maumivu kama anayopitia Peter.
Naomba niambie ukweli leo, unanipenda??? ".
.
Kuendana na maneno aliyozungumza, na swali alilonipa.
Nilijikuta nimekaa kimya nisijue cha kujibu.
.
Anaogopa kupenda tena, itakuwaje nikisema nampenda.
Anasema hataki nipitie maumivu kama ya Peter, itakuwaje nikijibu nampenda.?
Nilibakisha maswali mengi kichwani, lakini Careen akaniambia "Chris, niweke wazi leo hii."

Je Chris atajibu nini??? Na ni nani mnafki anayetoa siri za kina Chris
.
Usikose sehemu ya 18
#Itaendelea...
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Kumi na Nane
.
#Ilipoishia:
Careen aliniuliza maswali mengi mfululizo ambayo yalinifanya niuone mdomo mzito.
Sikujua nini cha kumjibu wakati aliponiuliza kama nampenda.
.
Kauli yake ya "Matendo yako yanafanana na Peter" ilizidi kunipunguza nguvu ya kunyanyua mdomo kumjibu.
.
Nilibaki kimya huku nikiwa nimeinamia chini, nilikua na maswali mengi sana kichwani.
Careen atanichukuliaje nikimuambia "Ndio nakupenda ", je atanitenga kama Peter?
Itakuwaje nikimuambia ukweli halafu anikatae?.
Nilijikuta mdomo mzito kama nimefungwa mzigo wa tani 1000.
.
#Inaendelea:
Careen akanishika bega, na kuniambia "Chris, niweke wazi leo hii".
.
Moyo ukanipiga paaah, nikainua kichwa juu na kuzidi kupata wasiwasi.
Mikono yangu ilikosa nguvu na kuanza kutetemeka, nikajitahidi kujizuia ili Careen asigundue wasiwasi wangu.
Kuna sauti ndani yangu ikawa inaniambia "Kuwa mwanaume, funguka ya rohoni ".
Na sauti nyingine ilikua na nguvu zaidi, ilikua ikiniambia "Chris usiseme lolote, acha kabisa, atakukataa na kukutenga kama Peter".
.
Nilikaa kimya kwa muda zaidi, lakini mwisho nikajisemea kimoyo moyo "Liwalo na liwe, leo namuambia".
Nikataka kufungua kinywa, lakini bado nikasita.
.
Nikajisemea kimoyo moyo "Chris sema".
Nikanyanyua kinywa, na kumjibu "Yeah, ndio nakupenda. Tena zaidi ya sana".
Careen alistuka, akanitazama.
.
Inasemekana kuwa mwanzo huwa mgumu, nililiamini hilo.
Japo nilipata ugumu kutamka kauli ya kwanza, lakini baada ya kutamka hiyo kauli, ndipo nilipoanza kupata nguvu ya kunena zaidi.
.
"Careen nakumbuka nilikupenda tangu siku ya kwanza nakuona darasani, siku yetu ya kwanza kuja chuo.
Niliwaza mengi sana kukuhusu, na nilitamani kufanya mengi sana na wewe." - (Nilinyanyua kinywa na kumtamkia Careen).
.
Careen alikosa ujasiri wa kunitazama usoni kama mwanzo, akashusha uso wake na kutazama chini.
Nikampigilia misumali zaidi.
"Najua unajiuliza kwanini sikukwambia siku zote hizo.
Mwanzoni sikutaka kuzungumza sababu nilijua tayari una boyfriend, sikutaka kuharibu mahusiano yako.
Na hata mlipoachana sikutaka kukugusia hili jambo, nilitaka nikupe muda wa kuyasahau mapito yako kwanza". - (Nikanyamaza kidogo, na kumeza mate).
.
Niliiona mikono ya Careen ikitetemeka kwa mbali, sikutaka kupoteza nafasi hiyo.
Nikajisogeza karibu na kumshika mikono yake.
Careen alizidi kutazama chini.
.
Nikaendelea kuzungumza kwa hisia zaidi ili maneno yapenye moyoni mwake.
Nikamwambia "Careen, najua unapitia maumivu ya kutendwa. Najua umekosa kabisa imani juu ya mapenzi, na wala huwaamini tena wanaume.
Lakini kusema ukweli wanaume wenye upendo wa kweli wapo, wanaojua thamani yako wapo, wanaokupenda wapo, wanaotamani wangekua wako milele wapo.
Usiyachukie mapenzi, Usinichukie hata mimi ninayekueleza hisia zangu leo.
Nipe nafasi nikuonyeshe maana halisi ya upendo, nikuonyeshe thamani yako halisi.
Siwezi kukupa ahadi za uongo, nipe nafasi nikuonyeshe kwa vitendo.
Na kama bado haupo tayari kuingia kwenye mahusiano, niko tayari kukusubiri kipenzi hata ukichukua miaka ".
.
Nikanyamazia hapo, Careen akanigeuzia macho na kunitazama.
Akaniambia "Chris wanaume mmebarikiwa maneno mazuri mwanzoni, lakini matendo sifuri.
Leo unazungumza maneno mazuri, unalia, unanyenyekea, lakin ukishapewa nafasi tu unabadilika.
Chris, mimi si mtoto, nawajua wanaume vilivyo".
.
Alianza kuniletea vikwazo, lakini sikukata tamaa.
Nikamjibu "Kipenzi, hii ni Africa.
Wanaume wengi hawajui thamani ya wanawake, wala jinsi ya kuishi nae.
Ila wachache tu ndo wanaojua.
Tatizo ni moja tu Careen wangu, unapopewa kiroba kilichojaa mawe, ni ngumu sana kutambua kama kuna kipande kimoja cha dhahabu ndani.
Careen wewe mrembo sana, umebarikiwa kwa mengi, lazima utasumbuliwa na wengi walaghai ambao watakutumia na kukuacha.
Lakini hiyo isiwe sababu ya wewe kushindwa kutafuta dhahabu ndani ya kiroba kilichojaa mawe.
Niamini na unipe nafasi, hutojutia. Nakupenda sana.". - (Niliishia hapo, na kuamua kumsikiliza).
.
Careen alikaa kimya kwa muda mrefu sana akiwa kama anatafakari.
Lakini mwisho nilimuona anashika mkoba wake.
Na kuniuliza "Naweza kuondoka??? ".
.
Nikatingisha kichwa kuashiria ndio.
.
Akanijibu "Itakua vizuri kama hatutozungumzia hizi mada tena. Siko tayari kuwa na mahusiano na yeyote yule".
.
Jibu lake lilinistua sana, likaniumiza na kunifanya nianze kujilaumu kwanini nimemwambia ukweli kama nampenda.
.
Pindi anataka kuondoka, nikamuita "Careen".
Akageuka na kunitazama.
Nikamwambia "Baada ya yote tuliyozungumza, naomba usinitenge.
Tuendelee kuwa kama kaka na dada, usinichukie".
.
Careen akaniangalia sana, mwisho akanijibu "Siwezi kukutenga, kuwa na amani ".
Kisha akageuka na kuanza kuondoka.
.
Nilibaki nimekaa kwenye benchi, hata nguvu ya kunyanyuka sikuwa nayo tena.
Maswali mengi kichwani, ina maana leo ndio namkosa Careen??
Inamaana na mimi nimeshindwa kama Peter??
Inamaana na mimi nitavaa dera??
Niliumia sana.
.
Sikupata hamu ya kufanya lolote lile, nilinyanyuka na kuanza kutembea kama mtu aliyetembea umbali mrefu.
Sikuwaza kupanda boda boda, wala kufanya nini, njiani nilikua kama sioni watu.
Kichwa kilikua kizito, nilihisi maumivu ambayo sikuwahi kuhisi.
.
Nilijilaumu kwa mengi, na hapo niliamini kuwa mapenzi sio mchezo wa kubashiri.
Nilijiona mjinga sana kuwekeana mechi na Peter, nikajiona mjinga kumcheka Peter.
Nikakumbuka mateso na misukosuko niliyopitia juu ya Careen, sikuamini, baada ya mateso yote nakuja kutoka mikono mitupu.
Uvumilivu wote ule, leo nimekosa mbivu na kupata maganda.
.
Nilipofika hostel, nilikuwa naona kama chumba kikubwa.
Kitandani hapalaliki, kwenye kiti hapakaliki.
Nilizunguka chumba kama chizi.
Usiku wangu ulikua mrefu sana, nilianza kuelewa kwanini baadhi ya watu huamua kujinyonga baada ya kuachwa, maumivu hayavumiliki.
.
Kesho yake asubuhi nilikumbuka kumtafuta kwenye simu Dr Leonard, angalau anipe tulizo la moyo kwa maneno yake yenye kufariji.
.
Alipokea simu, na kuniomba nimuelezee vizuri.
Nilipomaliza kueleza akanipa pole kwa yote yaliyojiri lakini alikuja kuzungumza mambo yaliyonipa nguvu mpya na kujikuta nikianza kupata amani.
.
Dr Leonard: Kwanza nikupe pole kwa maumivu ambayo unapitia. Lakini pili nikupe hongera kwa kuchukua hatua kubwa sana ya kumpa ukweli wa moyo wako.
Usijutie kwa jambo ulilofanya, unatakiwa kufurahia mambo mawili.
1: Umemweleza hisia zako, sababu mwanzo kila jambo ulilokua unafanya alikua akidhani ni kama kaka yake. Lakini kuanzia sasa ataanza kurudisha mawazo nyuma na kukumbuka mambo yote uliyowahi kumfanyia, ndipo hapo ataanza kutengeneza picha mbalimbali kichwani mwake kukuhusu wewe.
Na jambo lolote utakalokuwa unamfanyia kuanzia sasa litakua linamfanya ahisi kuwa unafanya sababu unampenda.".
.
Alinyamaza kidogo, nikaanza kupata hamu ya kumsikiliza zaidi.
Akakohoa kidogo na kuendelea kuongea "Namba mbili: Furahi sababu amekuhakikishia nafasi ya urafiki, hiyo itakupa wepesi wewe wa kuendelea kumfanyia vitu vitakavyo mfanya akupende zaidi. Kwahiyo itumie vizuri hiyo nafasi, usikate tamaa mapema, mwanaume huwa hachoki kupambana.
Hiki ndo kipindi unachotakiwa kumfanya aamini upendo ulionao kwake kwa vitendo.
Ametoka kutendwa, hebu usikate tamaa, muonyeshe utofauti kati yako na boyfriend wake aliyemtenda, hakika atakupenda bila kutegemea".- (Alizungumza kwa kujiamini na kumaanisha alichokuwa anasema).
.
Hapo nikaanza kupata mwanga juu ya kitu nachotakiwa kufanya, lakini bado nikawa na hofu kuwa tayari nilishakataliwa, itabadilikaje zile kauli alizosema.
.
Dr Leonard: Chris unahofia kukataliwa, tena umekataliwa kwenye jaribio la kwanza tu.
Kama ulikua hujui, mwanamke yeyote mwenye misimamo na kuhitaji mahusiano serious, kamwe hawezi kukukubalia kiurahisi rahisi.
Anahitaji muda wa kukuwazia, kukutafakari na kutoa maamuzi.
Sasa kama umekata tamaa mapema, jua kwamba utamkosa.
Lakin kama hautokata tamaa mapema, na uko tayari kumfanya awe wako, basi jione kuwa kuanzia sasa uko ndani ya nusu fainali, bado fainali yenyewe.
Pambana Chris, mi naona ushindi kabisa hapo.
Angekua hakupendi, hata hiyo nafasi ya urafiki usingepewa".
.
Alimaliza kwa kusema hivyo, nilipata amani sana na nguvu mpya.
Nikasema sasa, Careen atakua wangu tu, sikati tamaa kamwe.
.
Nikaagana na Dr Leonard, akanipa maneno ya mwisho tu "Unakumbuka niliwahi kukwambia mwanamke anapenda nini? Basi usifanye makosa wakati huu" kisha akakata simu.
.
Wakati huo huo, nikaanza kwa kumtumia sms Careen, lakini hakujibu.
Sikukata tamaa, nikatuma tena jioni, lakini sikujibiwa.
.
Majira ya saa 2 usiku, ikabidi nimpigie simu, akapokea.
Alikua kapoa mwanzoni, lakini kila muda ulivyozidi kwenda nilizidi kunogesha maongezi na kujikuta tukizungumza kwa muda mrefu zaidi.
.
Siku kadhaa zilipita huku nikiwa nazidi kumsogeza Careen karibu.
Sikuleta papara nyingi, ilibidi nitumie akili zaidi kuliko kukurupuka.
Nilianza kuona mabadiliko kwa Careen, alianza kunizoea zaidi ya mwanzo na kuniweka karibu zaidi.
Nilijenga nae ukaribu kiasi cha kula nae, kufurahi nae, kumshauri, kusoma nae.
.
Nakumbuka niliwahi mwomba anisindikize hostel, akakubali.
Tulipofika sikutaka kufanya nae lolote zaidi ya kuweka movie, na kumuandalia kinywaji na biscuits.
Nikamuuliza angependa kula nini, akasema "Hapana nitaenda kula nyumbani".
.
Sikutaka aondoke hivi hivi bila kula, nikamlazimisha sana mwisho akakubali na kuniambia angependa kula wali na samaki.
.
Kwavile nilifunzwa vyema kwetu, suala la kupika wala halikunipa tabu.
Nilimuacha ndani na kwenda kununua vinavyohitajika, kisha kumuandalia chakula.
.
Tulikaa kwa pamoja na kula, hakula sana, akajifanya ameshiba.
.
Sikutaka kuipoteza nafasi hiyo, nikamwambia "mmh umekula kidogo tu,"
.
Careen: Kweli nimeshiba.
.
"Hujashiba bwana, kula hata kidogo, au nikulishe" - (Nikazungumza kimasikhara huku nimechota chakula kwenye kijiko na kumpelekea mdomoni.).
.
Akawa kama anaona aibu, lakini mwisho akanyanyua kinywa na kula huku anatoa tabasamu.
Nilifurahi sana na kumuongeza vijiko kadha wa kadha mpaka aliposhiba na kunipa shukrani kwa chakula kitamu.
.
Mazoea yalizidi, kuna siku nilimwomba Careen nitoke nae out usiku angalau tupate wasaa wa kuzungumza pamoja, na nilitaka nitumie nafasi hiyo kumkumbusha Careen jinsi gani nampenda sana.
.
Alikataa sana, na kusema kuwa hawezi kutoka usiku na wala si mazoea yake na wazazi wake hawataruhusu.
Nilizidi kuvutiwa zaidi na misimamo yake, na kuona kuwa Careen ni wife material.
.
Nikabadilisha maamuzi na kumuomba tutoke mchana, iwe mahala tulivu ambapo tunaweza zungumza na kufurahi pia.
Akakubali na kuniambia "Twende South Beach, jumamosi hii".
Nilifurahi sana baada ya kusikia maneno hayo.
.
Ni wiki 2 sasa tangu Abdulrahman na Peter watengane.
Na bado mnafki hajajulikana, ambaye anatoa siri zetu kwa Peter na Nasra.
.
Siku ya Alhamisi ya juma hilo, nilikua maeneo ya KBG nikipata kinywaji na mishikaki pamoja na Abdulrahman huku tukiwasubiria marafiki zetu wengine nao waje.
.
Tukawa tukipiga story mbalimbali, lakini ghafla ikaingia simu kutoka kwa Careen.
Tukazungumza kwa dakika kadhaa, na kuagana na kukata simu.
.
Abdulrahman akazungumza kwa kingereza akimaanisha "Naona siku hizi unazidi kumnogesha".
.
Nikacheka na kumjibu "Dah acha yani, mambo yanazidi kunoga".
.
Abdulrahman akanisisitiza nisijicheleweshe sana, nikajikuta namweleza "Usijali bro, na jumamosi naenda nae South Beach, nitamfungukia tena''.
.
Akafurahi sana kusikia hivyo, na kunipa $100(dollar 100) kama kilinda wallet kwa siku hiyo.
Walipokuja marafiki zetu(Ivan, Ramadhan, Hasheem) tukaendelea kufurahia kwa vinywaji na mishikaki.
.
Majira ya saa 3 usiku tukaagana na kutaka kuondoka, lakini jambo la kushangaza Ivan akaomba lift kwenye gari la Abdulrahman.
.
Nilipatwa na maswali mengi kichwani nikiwaza itakuwaje wawili hawa wakienda pamoja, nikahofia siri isifichuke kuwa wote wanamtaka msichana mmoja.
.
Nikajipa moyo kuwa haitowezekana, na tukaagana na kuondoka.
.
Siku ya Jumamosi ya miadi ilifika, na kukutana na Careen maeneo ya South Beach.
Nililipa kiingilio na sote tulienda kutafuta mahala pazuri pa kupumzika ili tuweze kuyazungumza vizuri.
Nikamchukua Careen mpaka maeneo ya ufukweni na kupumzika nae.
Tukapiga story mbalimbali, za vituko na matani, mwisho nikaanza kuleta story za hisia.
Nilimuona akianza kuonyesha utofauti, nikamshika mkono wake na kuanza kuubusu busu huku nikimweleza jinsi gani ananivutia.
Jinsi gani nampenda na natamani angekuwa wangu siku zote za maisha yangu.
Alinitazama na kuonyesha utofauti wake na siku ile ya kwanza, leo alinitazama na kuonyesha tabasamu lake, akaniambia "Chris nakupenda sana, na umenifanya nikuone utofauti kati yako na wanaume wengine ".
Akazungumza mengi sana, na hasa kunisifia.
Nilimkamata na kumpiga denda kwa dakika 5.
Na nilipomaliza nilimkombatia kwa nguvu sana.
.
Baada ya yote hayo tulianza kuchekeshana mambo mbalimbali yaliyopita kati yetu, lakini ghafla akaniambia "Tusimame".
.
Nikashangaa, "Tusimame tena?".
Nilipatwa na mshangao, lakini hakunijibu, akanyanyuka na kunishika mikono na kuninyanyua.
.
Nikanyanyuka, akanitazama usoni.
Akawa kama mtu anayenivizia hivi, kisha kunibusu shavuni na kukimbia huku akicheka.
.
Nikacheka sana, lakini niliamini kuwa lile busu lilikuwa na maana kubwa sana.
Nikamtazama na kumuuliza "Unaenda wapi sasa?? "
.
Akanijibu "Narudi sasa hivi, naenda kuchukua vinywaji".
.
Nikabaki namtazama huku nacheka, akaenda kuchukua vinywaji na wakati anarejea, akiwa kama hatua 15 kabla ya kunifikia.
.
Ghafla nilistukia kuna mtu kanikombatia kwa nyuma huku akisema kwa nguvu "Wow baby wangu".
.
Careen alistuka na kusimama baada ya kuona tukio lile.
Nami nilistuka na kutazama ni nani aliyenikombatia.
Nikatupa macho nyuma yangu, sikuamini macho yangu niliyemuona.
.
Akaongea tena kwa sauti "Chris baby wangu, nilikumiss sana ".
.
Hapo nilihisi kuwa pilau tayari limeingia mafuta ya taa baada ya kumuona Careen akiwa ameviachia vinywaji vilivyokuwa mikononi mwake na kuvidondosha chini huku akionekana akiwa haamini kile alichokiona.
.
Nilirudia tena kuitazama sura ya aliyenikombatia, sikuwa nikimjua hata kidogo, wala sijawahi kuonana nae hata mara moja.
Nikamsukumiza, akadondoka chini.
.
Kutazama mbele, nilimuona Careen akianza kuondoka kwa hasira.
Nikaanza kumkimbilia ili nimueleweshe kuwa huyo dada aliyenikombatia simjui.
.
Je ni nani aliyemkombatia Chris?? Na kwanini au katumwa na nani??? Careen atamuelewa tena Chris??? Na nini kitajiri hapo baadae???
.
Usikose sehemu ya 19
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Kumi na Tisa
.
#Ilipoishia:
Wakati Careen anarejea mahala nilipo, huku akiwa amebeba vinywaji.
Ghafla nilistukia nimekombatiwa kwa nyuma, nikageuza uso na kumtazama aliyenikombatia.
Sikuamini macho yangu, nilikombatiwa na mtu ambaye simjui na wala sijawahi kuonana nae mahala popote.
Pindi bado natafakari, ndipo alipoongea tena kwanguvu "Chris baby wangu, nilikumiss sana".
.
Sikutaka kumchelewesha, nikamsukumiza, akadondoka chini.
Kutazama mbele aliko Careen nilimuona akiwa anaondoka kwa hasira.
.
#Inaendelea:
Nikaanza kumkimbilia huku namuita "Careen, Careen "
Lakini kabla hata sijafika mbali nilistukia nimevutwa tena shati na mtu aliyekuwa akiongea kwa hasira "Nipe simu yangu, nataka simu yangu "
.
Sikuelewa huu mchezo uliotokea, nilishangaa haya yote anayo yafanya huyu msichana.
Nikamtoa mikono yake, na kumchapa kibao.
Wakati huo huo watu wakajaa na kutuzunguka.
.
"Dada vipi kwani? Kakuibia au?? Sema tumchezeshe kichapo"- Aliuliza mmoja wa watu waliozunguka.
Yule msichana akazungumza kwa sauti ya juu "Huyu bwana wangu, leo nimemfumania na demu mwingine.
Sasa kama anampenda huyo demu mwingine, basi anirudishie vitu vyangu nilivyo wahi kumuhonga" - (Alizungumza huku kanikunja kora).
.
"Mrudishie vitu vyake" - Mtu mwingine aliropoka.
"Mzee baba kumbe unalishwa!??? Hahahaha wenzako wanachepuka kiakili, we boya kweli yani.''- Mwingine akaongea.
Watu walizidi kutoa maneno ya kashfa, na wengine kuanza kutoa kelele "Mrudishie vitu vyake alivyokuhonga".
.
"Niachie'"- Nilizungumza kwa hasira na kuanza kukukuruka nae.
Sikutaka kumlazia damu, nikamtia vibao mfululizo.
.
Watu wakaniwahi na kunishika.
"Sister sema, huyu boya ulimuhonga nini na nini?? Tuvichukue sasa hivi'' - Aliuliza jamaa mmoja ambaye naye nahisi alikua ndani ya mpango mmoja na yule binti.
.
Nilizidi kupata aibu kwa kile kilichokuwa kinaendelea, lakini nilivyosikia hilo swali nikajua wazi nimeponyeka sababu yule msichana hajui vitu nilivyo navyo.
.
Akaropoka "Simu ", wengine wakaitika "Haya mpe simu yake".
Kwavile nilijiamini, nikajikuta nauliza "We umenipa simu??? Haya itaje ni simu ya aina gani?? "
.
Lakini nilijikuta nazidi kuuaminisha umati wa watu kuwa kweli nimehongwa, baada ya yule msichana kuitaja aina ya simu ninayo itumia.
Aliongea kwa kujiamini "Nimemuhonga Samsung J1 Ace, rangi ya Gold, ina cover jeusi".
.
Hakukosea hata kitu kimoja, hapo nilijikuta nazidi kushangaa haya yote yanayo nitokea.
"Haya itoe sasa umpe, usipende vya bure mtoto wa kiume utaolewa".
.
Sikukubali na nilisema hata wanipige sitoi kitu changu chochote.
Muda huo huo umati ukatawanyishwa na security guard.
Moyo ulisema "Afadhali nimeponyeka".
Walinikamata pamoja na huyo msichana na kwenda kutuhoji.
.
Kwa maelezo ya yake, iliwafanya security waamini kuwa ni kweli ni mpenzi wangu, sababu alizungumza utadhani ananijua.
Na kutaja vitu ambazo kweli ninavyo na hata walivyoomba wathibitishe, niliwapa na kujikuta naumbuka mimi.
.
Walitushauri twende nyumbani tukamalizane kimya kimya na kutuachia.
Nilitoka nje haraka na kumsubiri yule msichana ili nimuhoji vizuri.
Alionekana ni wa uswazi kutokana na dera alilovaa, wigi la bei rahisi, rangi yake aliyojichubua, na sauti yake kama radio mbovu.
Alionekana ni mtu anayependa shari muda wote na wala hana aibu, na inaonekana hii ndo kazi yake.
.
Alivyotoka tu akanisogerea na kuzungumza kwa sauti y chini "Mdogo wangu hapa mjini, tuliza ball. Usipende kushindana shindana na wenye mkwanja, utachezea chuma cha moto" - Alizungumza kwa dharau.
.
Nikamvuta mkono na kumuuliza "Nani kakutuma??? "
.
Akanitolea macho kama chura, na kunifokea "Wee weee wee babu tafa, tena unikome.. ooonh ushindwe babu kushika shika usivyo vijua.
Ndo unataka kunifanyia fujo?? Enh??? Nyoooo mxieeew.
Sasa kama hunijui mimi ndo Ashanti babu eenh.
Nipige nikuonyeshe " - (Alizungumza kwa haraka kama cherehani.)
.
"Sasa kama unataka kuchezeshewa kichapo na wanaume wa shoka, nipige uone.
Umewaona wale?? "- (Akazungumza huku akinionyesha kwa macho).
.
Nikageuza macho kuwatazama alionionyesha, nikaona kundi la wahuni watano.
Mmoja wao akaita "Oya Ashanti tusepe".
.
Nikamuachia mkono wake, akasonya na kuondoka huku akijitingisha japokuwa nyuma alikua kama kapigwa pasi.
.
Nilipatwa na wazo la kwenda kumtazama Careen maeneo yanapo egeshwa magari.
Nikidhani labda atakua bado hajaondoka, lakini sikumkuta.
Alikua tayari ameshaondoka, wazo likanijia na mimi niondoke.
.
Lakini ghafla nilistushwa na sauti ya mtu ikiniita kwa nyuma yangu.
"Chris"- Nikageuka haraka na kumtazama aliyeniita.
Sikuamini macho yangu, nilibaki nimeduwaa.
.
Nilikutana uso kwa uso na Peter akiwa na Ivan.
Niligundua kuwa kumbe mchezo wote huu ulisukwa na Peter na Ivan.
Nilipata ufumbuzi kuwa itakua Abdulrahman aliropoka kwa Ivan kuhusu safari yangu na Careen.
.
Peter akanitazama na kuongea "Najua unamtafuta Careen.
Usijali, yuko ndani ya mikono salama, Abdulrahman amemchukua na kumrudisha kwao.
Na kwajinsi navyomjua Abdulrahman, najua atamlisha maneno mengi Careen ili azidi kukuchukia.
Haha pole kwa kupokonywa tonge mdomoni". - Aliongea kwa dharau.
.
Nilitafakari kauli yake, nikajikuta najiuliza kimoyo moyo "Ina maana Abdulrahman naye yupo kwenye huu mchezo??''.
.
Ivan akaongea "Haya ni malipo ya kutuchezea akili mimi na Abdulrahman "
Peter naye akaongeza "Na ni mwendelezo wa ahadi yangu kwako kuwa hutashinda kamwe.
Na najua kuanzia sasa Careen hatokupenda tena, tukishamtumia picha na videos".
.
Nilistuka sana baada ya kusikia picha na videos, nikajua kuwa kuna mashambulizi zaidi yanakuja kwa hapo mbele.
Walipomaliza kuongea, wakaniacha na kuingia kwenye gari lao na kuondoka.
.
Nilibaki nimesimama na mawazo, sikujua la kufanya tena.
Niliwaza kumuomba Careen msamaha lakin bado nikawa nawaza "Je atanielewa kweli?? ".
.
Nilimuita dereva tax aliyenileta mwanzo, na kwavile sikuwa na pesa nyingi, akanirudisha mpaka Mbagala ambapo nilipanda daladala ya Gongo La Mboto kurejea Hostel.
.
Usiku kucha nilimtafuta. Careen kwenye simu bila mafanikio, simu yake ilikua imezimwa kabisa.
Na hata kesho yake ilikua inapatikana ila hakunipokelea kabisa.
.
Juma lililoanza, lilikua ni Juma ambalo tulikua tunaanza mitihani ya mwisho wa semester maarufu kama U.F.E(University Final Exam).
Sikuwa na furaha kabisa siku hiyo, na hata sikuwa nimejiandaa kwaajili ya mitihani.
Kichwa kilikuwa kimezidiwa na mzigo wa jina la Careen.
Pindi nafika maeneo ya chumba cha mtihani, nilishangaa kuona watu mbalimbali wakiwa wananitazama na kucheka.
Sikuelewa, nikajitazama juu mpaka chini labda nimevaa vibaya, lakini hapana nilikua nimevaa vizuri tu.
.
"Chris" - Nilisikia sauti ya Ramadhan akiniita.
Tukasalimiana, na kunipa pole.
.
Nilishangazwa na pole yake, nikamuuliza "Pole ya nini??? "
.
Akaniambia "Pole kwa yaliyo kutokea juzi".
.
Nikastuka, nikaanza kujiuliza amejuaje, lakini kichwani nikapata jibu kuwa huenda Ivan ndiye aliyemwambia.
.
"Kakuambia Ivan?? " - Nimamtupia swali.
Hapo hapo akachukua simu yake na kunionyesha videos na picha mbalimbali nilizopigwa wakati wa varangati kule South Beach.
Kilichonishangaza ni vile vipande vya video viliwekwa vile vipande muhimu tu ambavyo mtu yeyote akitazama lazima atasema kuwa ni kweli yule Ashanti ni mpenzi wangu.
.
"Darasa zima wameona hizo picha na videos, na hata Careen ametumiwa pia" - Ramadhan alizidi kunieleza.
.
Hapo ndipo mwili wangu ulipozidi kukosa nguvu, nikapepesa macho kila kona na kuona watu wanavyonitazama na kucheka.
.
Niliumia sana, nikakosa amani.
Niliingia kwenye mtihani lakini sikuufanya kwa akili yangu, nilikua hata sijui nilichokuwa naandika.
Hata nilivyotoka nje ya chumba cha mtihani, Careen alinipita kama hanijui.
.
Hata nilipomuita ili nimuombe msamaha na kumuelewesha, wala hakutaka kunipa nafasi ya kunisikiliza.
Usiku nilijitahidi kupiga sana simu, na kutuma message za kuomba msamaha na kueleza hali halisi.
Wala hakujibu, wala hakupokea simu.
.
Siku ya Jumatano, ya juma tuliloanza mtihani.
Nilituma message nyingi kwa Careen.
Wala hakunijibu, nikakata tamaa kabisa kuwa sasa sitompata tena Careen
.
Baada ya masaa 8 kupita, simu yangu iliita mlio wa message.
Nikajua tu itakua ni message ya Tigo wakitangaza promotion zao.
Nikaidharau, lakini baadae akili ikanijia hebu itazame hiyo message.
Huenda ni ya mtu muhimu.
.
Nikaichukua simu, kutazama kwenye screen ilikua ni message moja kutoka kwa Careen.
Nikapata shauku ya kutaka kujua alichonitumia, nikaifungua.
Pindi tu nataka kuanza kuisoma, hapo hapo mama akapiga simu.
Ikabidi nipokee simu yake, tukaongea muda mrefu lakini nilikua natamani nimuambie mama subiri kidogo nitakupigia nikimaliza kusoma message, lakini nilisita kusema hivyo sababu mama ni wa muhimu kuliko hiyo message.
.
Nilipomaliza kuongea naye, nikakata simu na tayari kuanza kuisoma message.
Nilipoanza tu maneno ya kwanza "Hizi video" hapo hapo simu ikazima chaji.
.
Nikapiga kelele kwa hasira "Anhaa" na kuirusha simu kitandani kwa hasira.
Nilidhani itatua kitandani na kutulia, lakini ilidunda mara mbili na kwenda kudondoka upande wa pili wa kitanda.
Nikashika kichwa nikijua tayari nishavunja kioo ca simu.
Kwenda kuitazama ilikua tayari ishaweka ufa kwenye kioo.

Nikaichomeka chaji na kuisubiria japo kwa dakika tano ili niiwashe.
Nilipoiwasha nikakutana na message mpya kutoka kwa mama akiuliza "Mitihani inaendeleaje??"
.
Nikamjibu message yake na kuendelea ya Careen.
.
Nikafungua message ya Careen, nikaanza kuisoma " Hizi video ni ushahidi tosha. Huyu dada hakuwa anaongopa. Vyote alivyosema ni vya ukweli.
Ishi maisha yako Chris, niache.
Nayajua machungu ya kusalitiwa, na kamwe siwezi vumilia kuwa na mwanaume msaliti.
Nilikupenda na kukuheshimu, lakini umejishusha CV. Achana na mimi".
.
Nilibaki nikiyatafakari maneno ya Careen, niliona machungu yake kupitia message yake.
Niliona jinsi gani bado ana kidonda cha kusalitiwa kwenye mahusiano yaliyopita, na sasa hataki rudia maumivu tena.
Moyo uliniuma sana, machozi yalinitoka hasa nilipowazia juu ya kumkosa Careen kwa kosa la kusingiziwa.
.
Nikaona nisipoteze nafasi hii, niombe msamaha navyoweza.
Akili yangu ilizidi kunivuruga.
.
Nikamtumia message mfululizo za kumuelewesha Careen kuwa hiyo ni mipango ya kina Peter.
Wala hakunielewa, tukawa tunabishana kwenye message, kipindi hicho nacho mama alikuwa akituma message na namjibu, huku akili ikiwa umevurugwa na Careen.
.
Baada ya muda nikastukia napigiwa simu tena na mama, kupokea nikasikia "Careen ndo nani!?? "
Nikashangaa Careen kamjuaje, akaniambia "Unanitumia message za mapenzi, unalia na kumuomba msamaha Careen.
Chris ukimaliza mitihani urudi nyumbani, dawa yako iko jikoni mpumbavu wewe ".
.
Alizungumza kwa hasira na kukata simu, nilibaki mdomo wazi.
Ikabidi nitazame messages, nikakuta nimechanganya za hovyo hovyo na nyingine zimeenda kwa mama.
.
Siku kadhaa zilipita bila kuzungumza na Careen, na marafiki zangu walibaki Ramadhan na Hasheem ambao pia sikuwaamini.
Siku ya mwisho ya mtihani, siku ya Ijumaa, kulikuwa kuna safari ya party baada ya mtihani.
Na party ilikuwa inafanyika Element Club.
Nilijua watu wengi wataenda, lakini sikutaka kwenda sababu nilijua kina Ivan pia watakuwepo.
Nilirudi zangu hostel kupanga vitu vyangu kwaajili ya safari kesho yake, nilitaka nirejee nyumbani kwa wazazi Arusha, nikajibu kesi yangu kwa mama.
.
Hakuna aliyejua kama naondoka kesho yake, zaidi ya Hasheem, Ramadhan, na Erick, mwanafunzi mwenzangu anayeishi chumba kinachofata hostel.
Ilikua ni siku ya huzuni kwangu, sikuwa na matumaini tena ya kuwa na Careen tena, nilijua nishampoteza.
.
Nikampigia simu Dr Leonard, na kumweleza jinsi marafiki zangu wanavyonizunguka.
Akaniambia "Chris una kasoro mbili.
Moja, hujiamini. Na pili, huna kifua. Na hivi ni vitu muhimu sana unavyotakiwa kuwa navyo.
Hujiamini ndomana unahitaji kuwa na backup, unahitaji watu wengi sana ili kumpata unayempenda, na hii ni hasara sababu penye watu wengi hapakosi unafki.
lakini kama ungejiamini na kubeba mahusiano yako kivyako vyako, wala usingekuwa na tabu ya kuwazia fulani kanigeuka.
Lakini pia kama ungekua na kifua, basi suala lolote kuhusu moyo wako, au mahusiano yako, basi lingebaki kuwa siri yako.
Marafiki zako hawahitajiki kujua linaloendelea kati yako na girlfriend wako. Unapowaambia siri za mahusiano yenu, basi inaweza leta madhara kama haya, aidha muachanishwe, au uibiwe mpenzi wako.
Awe ana madhaifu, muwe mnatoana out, au kufanyiana mambo mazuri, mipango yenu, kamwe usiyaseme kwa rafiki zako."
.
Maneno yaliniingia na kuona wapi nilipokuwa nakosea, nakujipa moyo mwenyewe kuwa sitarudia kwenye mahusiano yatakayofata.
Nilipokata simu, ikaingia message WhatsApp.
Kufungua ilikua ni picha imetumwa na Peter, akiwa na Careen, Abdulrahman, Nasra, na Ivan.
Na aliandika ujumbe "Natamani ungekuwepo".
.
Niliitazama sana, lakini sikuweza fanya lolote sababu tayari nilikua nishakata tamaa kuwa Careen hawezi kuwa na mimi tena.
.
Masaa mawili baadae, nikapokea message nyingine Whatsapp.
Kufungua ilikua ni Ivan aliyenitumia picha akiwa anampiga busu zito Nasra, na kunitumia maneno ya kingereza akimaanisha "Baada ya fitna zote ulizonifanyia... bado nimempata niliyemtaka.
Sina kinyongo na wewe tena, moyo wangu una amani".
.
Wakati huo huo Nasra akatuma nae picha na ujumbe "Siku zote kwenye maisha ni ngumu sana kukipata unachokitaka, utakipata kile unachostahili.
Asante kwa yote, siwezi kukuchukia, umenifunza kuwa maana halisi ya upendo ni kuthamini pale unapopendwa, sababu mara nyingi unapopenda huwa hupendwi."
.
Nilizidi kujiona mjinga sana, lakini tayari nilishakubali matokeo, nilishakubali kushindwa.
Nikaitazama saa ya ukumbusho aliyowahi kunipa Careen siku ya birthday yake, nilijikuta nalia sana.
Nilitamani usiku ungeisha haraka ili angalau niondoke ndani ya jiji hili la Dar es salaam, labda kumbukumbu za Careen zingefutika.
.
Kesho yake asubuhi nilifatwa na Hasheem na Ramadhan ambao walikuwa wamejiandaa kunisindikiza mpaka Gongo La Mboto.
Nikaagana na marafiki wengine pia niliokuwa nikiishi nao Hostel.
.
Tulipofika kituo cha ma-Bus cha Gongo La Mboto, nikaagana na Ramadhan na Hasheem kisha
Nikapanda bus linalo elekea Ubungo, na kwenda kutulia kwenye seat, na bus likaanza kuondoka taratibu.
.
Nikaitazama saa ya Careen, nikaona kuwa huu ndio mwisho wa kila kitu kati yangu na Careen.
Nikaivua saa, nikawa bado najishauri kuitupa dirishani.
Lakini ghafla kutupia jicho upande wa dirisha nililokaa, ndipo nilipowaona Hasheem, Ramadhan wakirudi kwa mbio kuliwahi bus nililopanda.
.
Moyo ulistuka, nikajua kuna kitu.
Kutupia jicho kwa mbele ndipo nilipoona Ivan na Nasra nao wanakuja kwa haraka.
.
Wote wakawa wanaita "Chris shuka, Chris"
Nikajiuliza kwanini wananiita.
Wakawa wanaita huku wanakimbia kuliwahi bus.
.
Nasra akawa anaita huku akionyesha ishara ya vidole, nikavifata vidole na kumuona Careen naye akija huku anakimbia.
.
Je Chris atashuka!?? Na je, anaitiwa nini??

Usikose sehemu ya 20
#Itaendelea
...
 
MAUMIVU YASIYO KWISHA(ENDLESS PAIN)...!!

Sehemu ya Ishirini
.
#Ilipoisha:
Niliagana na Hasheem na Ramadhan na kupanda bus la kuelekea Ubungo.
Bus lilipoanza kuondoka, nilikua nikiitazama saa ambayo nilipewa na Careen kama ukumbusho.
.
Sikuona tena umuhimu wa saa hiyo kubaki mkononi mwangu wakati tayari mimi na Careen hatuna chochote kinachoendelea kati yetu.
.
Nilikumbuka sana siku ambayo alinivalisha saa hiyo siku ambayo nilimfurahisha sana, ilikuwa ni siku niliyomfanyia surprise ya birthday yake.
.
Nakumbuka alikuwa akimwaga machozi ya furaha mbele yangu, huku akiniambia kuwa saa hii iwe ukumbusho wa thamani yangu kwake.
Nilizidi kuumia moyoni na kuzidi kuitazama saa ya Careen.
.
Kwa huzuni kubwa nikaifungua mkononi mwangu, na kujiandaa kuirusha nje ya dirisha.
Lakini nikasita, nikataka kuirusha tena, lakini bado nikasita baada ya kuona mahala napotaka kurusha pana watu.
.
Ndipo nikajishauri niirushe barabarani ili gari liipitie na kuivunja.
Nikatupa jicho kwa nyuma na kumuona Ramadhan na Hasheem wakilikimbilia gari nililopanda.
.
Niliwatazama kwa mshangao, wakaanza kuita "Chris shuka Chris ".
Nikajiuliza kwanini wananiita, na wakati tayari tumeshaagana.
Kupiga jicho kwa mbele, ndipo nilipowaona Nasra akiwa na Ivan nao wanakimbilia.
.
Nilizidi kujiuliza wana nini hawa, wanahitaji nini kutoka kwangu.
Lakini Nasra alikua anaita huku akionyesha alama ya vidole.
Nikafata vidole vya Nasra vinakoelekea na kumuona Careen nae akikimbilia.
.
#Inaendelea:
Nilipatwa na nguvu ya ghafla, nilianza kuhisi kuwa huenda ukweli umejulikana na wanataka kunipatanisha na Careen.
Lakini wakati huu sikutaka kuwa dhaifu, nilitaka kuwavimbia.
Nikaingiza kichwa ndani ya gari na kujisemea "Shit, zamu yenu kuteseka.
Na kama kweli ananipenda na ana nia na mimi, basi atanifata hata nikienda China.
Na yeye ataabike kwanza."
.
Nilijikuta natabasamu baada ya huzuni yote niliyokuwa nayo mwanzo.
Gari lilienda na kusimama Kituo Kipya.
.
Nikaona Nasra na Careen wamechoka kukimbia, wakaanza kutembea.
Lakini wanaume wao hawakuchoka.
.
Pindi wanakaribia Kituo Kipya, ndipo gari nalo lilipomaliza kupandisha abiria na kuanza kuondoka tena.
Walilikosa kwa mara nyingine, nikaona Ivan ameshika kiuno kwa kuchoka.
Huku Ramadhan akiwa amesimama na kushangaa, nahisi alikua anajiuliza kwanini sikushuka.
Hasheem alikuwa akirusha rusha mikono kama mtu aliyechukizwa na nilichofanya.
Ramadhan akachukua simu na kuwa kama anampigia mtu, nikajua wazi itakua ananitafuta kwenye simu wakati simu yangu ilikuwa imeshazimwa.
.
Mdomoni nikawa nacheka kuona leo wanavyotaabika kunipata, lakini moyoni nilikua na wasiwasi itakuaje endapo wataghair kuja.
.
Walipotea kwenye macho yangu, nikahisi kuwa labda wameghairi tena kuja.
Sikumuona yeyote yule hadi gari lilipofika Mzambarauni.
Nikaanza kuwa na wasiwasi kuwa mchezo wangu utanifanya nimkose mwanamke ninaye mpenda kwa dhati.
Na nilijua tu wazi kuwa huu wasiwasi ninao pata ni kwasababu nampenda sana.
Lakini nikajipa moyo kuwa kama yeye ndiye aliyeumbwa kwaajili yangu, basi atajitoa kivyovyote vile ili kunifata mpaka nilipo.
.
Nikatulia huku najipa moyo "Atatokea tu".
Kipindi tunashusha kilima cha kuingia stand ya Mombasa, ndipo niliona bodaboda tatu zinakuja nyuma kwa kasi.
Kuzitazama vizuri, walikuwa wamepakizwa Ivan, Hasheem na Ramadhan.
.
"Daaaamn"- Nikasema huku natoa tabasamu kubwa nikijua kuwa mpango wangu umetimia.
Lakini bado kiu yangu ilikua ni kumuona Careen akinifata.
.
Bus lilipofika Mombasa, likasimama na kupakiza abiria.
Ndipo walipowahi haraka mpaka dirishani.
.
"Chris shuka man, manzi wako ana ana anakufata wewe" - Alizungumza Ramadhan huku anakwama kwama sauti.
.
"Achana nae, simtaki." - Niliwavimbia ili nisionekane dhaifu lakini moyoni nilikua natamani hata dereva asinzie ili niwavimbie halafu ndo nishuke kabla halijaondoka.
.
"Chris acha ujinga, hii ni nafasi uliyokuwa ukiota kuipata "- Hasheem akaongea huku akinitazama kama baba anavyozungumza na mwanae.
.
"Ndoto muda wake usiku, sahivi asubuhi nishaamka kiakili na kihisia.
Nishawaambia simtaki tena Careen, na kwanza nawahi usafiri nisije nikachelewa bus".- Nikazidi kuwavimbia.
.
Watu ndani ya bus wakabaki wananishangaa kuendana na aina ya maongezi tuliyokuwa tunazungumza.
.
Jicho langu likawa bado halikauki upande ambao magari ya Gongo la mboto yanatokea huku nikitamani nione japo sura ya Careen ikinifata.
.
Kwambali nilianza kuona bodaboda mbili zikija, na abiria walikua Careen na Nasra.
Nikaanza kupata moyo na kuanza kuijua thamani yangu kwenye moyo wa Careen.
.
Haraka nikaivaa saa aliyonipa ili akija nimtambie jinsi gani nampenda mpaka nashindwa tupa vitu vyake.
Ghafla nikasikia konda anagonga akiashiria dereva aondoshe gari.
Nikajikuta naita "Konda subiri nishuke".
.
Abiria waliokuwa wakinishuhudia nilivyokuwa najibu majibu ya kujiamini mwanzo wakacheka.
"Nyooo siulikua unajishaua hapa" - Aliropoka dada mmoja aliyekuwa seat ya nyuma yangu.
Nikamuona Ramadhan anacheka, alijua zote zile mbwembwe.
.
Niliposhuka tu, na Careen na Nasra nao walikua washafika.
Nasra akanifata na kunitia kikofi.
"Mjinga, hicho cha usumbufu "- Aliongea baada ya kunichapa kikofi.
.
Nikamuona Careen kama alikuwa anajiandaa kuja kunikombatia, nikaona nizidi kumvimbia.
"Haya semeni mlichoniitia maana mnazidi kunichelewesha, nisije ninakosa bus "- (Nikazungumza kwa kujiamini).
.
Careen akashusha uso chini.
Ivan akafikicha pua, na kunisogerea karibu.
Na kuanza kuelezea kuanzia mwanzo, siku ambayo alikunywa sana Whiskey na Hasheem.
Hali iliyomfanya Hasheem alewe na kujikuta akitoboa siri zote.
Ivan aliumia sana baada ya kugundua kuwa nimemtumia yeye na Abdulrahman kwa manufaa yangu binafsi, na tangia hapo ndipo alipoamua kuwa anatoa siri kwa Nasra ili mipango yangu juu ya Careen ivurugike.
.
Ivan alivyoelezea mpaka hapo, nikagundua kuwa kumbe aliyefanya Abdulrahman agombane na Peter alikua ni Ivan.
.
Ivan akaendelea kusimulia jinsi alitumia mwanya wa kupanda gari moja na Abdulrahman ili ampe siri ya mchezo ambao nilikua nawafanyia kati yao.
Abdulrahman nae alikasirika na wote kurudi kwa Peter.
Hawakutaka kunistua mapema kinachoendelea, walitaka kunipa surprise ya maumivu kwa kuniharibia kwa Careen, ndiyo maana wakaamua kuuharibu mtoko wangu na Careen kwa kumkodisha mwanamke maarufu Manzese kwa kufanya vurugu, Ashanti.
.
Mpaka hapo nilimtazama Ivan kwa hasira, hasa nikikumbuka vurugu na aibu niliyoletewa na Ashanti.
Lakini akili yangu iliniambia "Chris tulia, haya yote uliyasababisha wewe mwenyewe ".
.
Ivan aliendelea kusimulia jinsi alivyompata Nasra na vile Abdulrahman alivyokubali matokeo ya kumkosa Nasra.
Na tangu hapo hakuona tena sababu ya kuendelea kupambana na mimi.
.
Ivan alinyamaza na kusimulia ""Leo nilipoamka nilimuambia Nasra azma yangu ya kuwarudisha Careen na Chris pamoja.
Nasra aligoma lakini baadae akaelewa, ndio tukaamua kumtafuta Careen asubuhi na kumweleza kila kitu.
Careen allilia sana na kujutia aliyokufanyia, na tukashauriana tuwahi asubuhi hii hii kuja kwako sababu tulisikia tetesi unataka kuondoka."
.
Ivan akahema kidogo, na kuendelea "Mimi na Nasra tuliwahi hostel, na Erick akatuambia umeshaondoka dakika tano zilizopita.
Tukawahi kituoni, bahati nzuri Careen nae alikuwa ndio ameshuka kwenye gari.
Na ghafla tulionana na Hasheem na Ramadhan.
Ona kiasi gani unapendwa Chris ".
.
Nikamtazama Ivan huku nikitafakari swali la kumpa, nikamuuliza "Nashukuru kwa yote uliyonitendea, lakini kwanini umegeuka msaliti kwa marafiki zako!?? "
.
Nasra akataka kujibu, lakin Ivan akamuwahi.
.
Ivan: "Chris sijatenda hili kwaajili yako, bali kwaajili ya Careen. "
.
Nikastuka, na kuuliza "Kwaajili ya Careen? "
.
Careen aliinamisha kichwa chini, na Ivan akaendelea kuongea "Chris ulikuwa unapendwa, unapendwa, na utazidi kupendwa zaidi ya ujuavyo ".
.
Nikaona kama anaongea taratibu, nilitamani azungumze haraka zaidi.
Ivan akazungumza "Siku ya birthday ya Careen nilichukua simu yake ili niwe napiga picha, huku nafanya kazi ya kukata simu za Peter kama tulivyo ahidiana."
.
Akanyamaza kidogo, na kuendelea "Ndiyo siku niliyogundua kuwa Careen anakupenda zaidi. Nilipekua sana simu yake na kukuta ameandika ujumbe mbalimbali za hisia zake juu yako, na alisave kwenye Notebook ya simu yake.
Nilitamani kukueleza siku hiyo hiyo lakini nilihisi ningekupagawisha akili mwisho uanze kumringia, nilitaka uhangaike mwisho useme wewe mwanaume kwa mdomo wako, ili iwe rahisi nyie kuwa pamoja.
Najua Careen asingeweza kukueleza hisia zake".
.
Hapo nilinywea, nikashusha pumzi nzito na kushusha uso wangu chini.
Ramadhan akazungumza "Siku ya birthday sote tulipanga tumdanganye unaumwa ili aje hostel, njiani Careen alikua kama chizi akizungumza peke yake "Chris nisubiri, pepo la homa lishindwe ".
Alikua akizungumza mengi, na nilijua kabisa kuwa Careen anaficha hisia zake juu yako".
.
Nasra akasema "Pindi nilipojenga nae ukaribu, alikua hachoki kukuzungumzia. Na siku niliyo mwambia wewe ni boyfriend wangu, ni kwasababu nilikua nakupenda na alikua ananikera na maswali yake kila mara kukuhusu... na nilijua ni kwasababu anakupenda ".
.
Nikawatazama wote, nilijikuta machozi yananitoka.
Nilikumbuka jinsi nilivyo hangaika kumpata Careen halafu leo naambiwa nilikua napendwa.
Nimepitia misukosuko yote ile, sikuwaamini.
Nikawaambia "Nyie wote mnasema mnachohisi, ila siri iko moyoni mwake. Acheni kunidanganya".
.
Careen akanitazama huku akidondosha chozi.
Watu walio pembeni walikua wakitutazama huku wakiwa hawaelewi kinachoendelea.
Careen akanisogerea na kunishika mkono ambao nilivaa saa yake.
.
Akaniambia "Nilikupa hii saa kama ukumbusho wa thamani yako kwangu.
Nilidhani ipo siku itaharibika na utaifungua na kukuta ujumbe niliouweka."
.
Maneno yake yalinifanya nifikirie kwa sekunde kadhaa, ndipo nilipo ichukua saa na kuifungua mfuniko kwa nyuma na kukuta kipande kidogo sana cha karatasi kilicho viringitwa na kuwa kidogo sana mpaka kutosha.
Nikakifungua na kukuta vimaneno vidogo sana kutokana na udogo kipande cha karatasi, vimaneno hivyo viliandikwa "I <3 u Chris".
.
Nilijikuta nalia sana, nikajisemea kimoyoni "Ndio maana nilishindwa kuitupa hii saa leo".
.
Akaichukua simu yake na kunipa mkononi na kuniambia nichore Pattern yake kwa vile naijua.
Nikachora, akaniambia pattern ni alama ya "C" inaamana ya jina lako.
Lakini sikuwahi kumpa mtu yeyote pattern yangu zaidi yako, na Ivan siku aliyotaka kupiga picha.
Kuna sababu moja tu kwanini nilikutajia pattern yangu, nilitaka uwe nayo huru simu yangu ili siku upekue na kukuta siri ya moyo wangu."
.
Akafungua App ya notebook na kunipa ujumbe mmoja aliowahi kusave, ulisomeka hivi "Chris amenifanya nimkumbuke Khalfan, mwanaume aliwahi kunijali.
Lakini Chris amezidi, ananijali zaidi na nazidi kuvutiwa nae kila siku".
Nilikwambia kusoma hapo, na kukumbuka Careen aliwahi niambia jinsi gani namkumbusha Khalfan, na akanipa sifa za Khalfan.
.
Nikafungua nyingine ambayo iliniliza zaidi, aliandika "Nampenda sana, ila siwezi kumwambia na wala sina nguvu ya kuzieleza hisia zangu wala kuzionyesha.
Anaonekana ananipenda pia, lakini naye ni mwoga wa kuniambia."
.
Ujumbe Mwingine "Leo amenitamkia jinsi gani ananipenda, lakini siwezi kumuambia kama nampenda pia.
Nilishindwa kumkubalia kwa kuhofia ataniona malaya, nilitamani kumjibu pale pale."
.
Kila ujumbe ambao Careen aliuandika ulinifanya nizidi kulia machozi ya furaha baada ya kujua jinsi gani alivyokuwa akinithamini siku zote hizo.
Nakumbuka kilichowahi kunifanya nimpende zaidi ilikua ni misimamo yake, kujitambua kwake na kujithamini kwake.
Nilikumbana na mmoja "Ameniudhi jana, amekombatiwa na mpenzi wake mwingine mbele yangu.
Tena aliniacha niondoke wala hakunifata fata sana kunibembeleza.
Natamani nimpigie, natamani nipokee simu zake, ila acha tu ninyamaze, sitakiwi kuwa dhaifu kwake.
Nitamnunia na hata salamu yake nitajifanya sitaki. "
.
Mpaka hapo niliishiwa nguvu ya kusoma zaidi na kujikuta nikimkombatia kwa nguvu na kummiminia mabusu.
.
Pindi bado tumekombatiana, niliona wote wakitabasamu huku Nasra akitoa machozi ya furaha.
Lakini kwa mbele niliona Peter na Abdulrahman wakiwa wamesimama wakitutazama kwa mshangao.
.
Nikauliza "Nani kawaita wale?? "
.
Ivan akajibu "Usiogope, mechi tuliyoianzisha hatuwezi iacha hivi hivi.
Peter leo alikua airport anamsubiria mchumba wake wa kiNigeria.
Nikaona bora niwataarifu kuwa namaliza mechi yenu leo, na mimi ndo refa".
.
Niliwatazama Peter na Abdulrahman, nao wakatutazama kwa mshangao mkubwa.
Peter akasogea huku anakunja ngumi.
.
Nikawa nimejiandaa kuwa leo akizingua namchezesha kichapo.
Akaikunja ngumi yake na kutishia kama anataka kunipiga lakini akaipoza na kunipa ishara nipige tano.
Nikacheka na kupiga tano.
.
Peter akazungumza "Leo nimegundua kuwa mapenzi hayahitaji ushindani.
Kama unampenda mtu, usihitaji kutaka kupambana na mpinzani wako wala kuwekeana nae mchezo wa kubashiri."
.
Akahema na kusema "Umeshinda, sioni haja ya kuendelea kushindana na wewe wakati tayari mbingu na ardhi zinathibitisha kuwa Careen ni ubavu wako".
.
Nilimtazama Peter, nikamuuliza "Vipi umekuja na dera!!?? " kisha nikacheka.
.
Peter akacheka, akaniambia "Sijui nilikua nawaza nini wakati naweza adhabu hiyo".
.
Nikamshika bega na kumuambia "Hakuna atakaye vaa dera. Sababu kipindi mimi nimempata ninayempenda, wewe umempata unayestahili kuwa nae."
.
Akauliza "Umemuona??? "
Nikamjibu "Huyo nyuma yako".
.
Alipogeuka alikuta mchumba wake aliyechaguliwa na wazazi wake, amesimama nyuma yake.
Sote kwa pamoja tukasogereana na kutambulishwa kwa mchumba wake anayeitwa Emilie, na wote tukafurahi kwa story mbili tatu.
.
Abdulrahman: Mnaonaje wote tukienda kula bata siku tatu Zanzibar, tutembelee Changuu Island, na Sandbank.
.
Wote tukakubaliana na wazo la Abdulrahman

Ivan: Chris umesahau unatakiwa uende Arusha?? .
.
"Umenikumbusha chalii yangu"- Nikachukua simu na kumpigia mama na kumwambia nitakuja wiki ijayo.
.
Peter akaniambia subiri, akaenda kwenye gari lake na kuleta kimfuko.
Tulipotazama ndani yake tukakuta kuna Wigi, make up, na dera.
.
"Kumbe ulikua serious na mechi "- nikamuuliza Peter.
Abdulrahman akajibu "We acha tu, alikua nayo serious ila baadae aliachana nayo kabisa... alitaka akuache na maumivu tu, dera akasamehe".
.
"Ila leo tumejifunza, tulikua na akili za kitoto "- Peter alijibu na kumkabidhi Careen kama ukumbusho wa mechi ya kumpata yeye.
.
Akaipokea na mwisho tukaagana, na Abdulrahman, Peter na Emilie wakaondoka.
Na sisi wengine tukaenda tukaenda panda daladala turudi Gongo La Mboto.
.
lakini ghafla wakati tunasubiria abiria kadhaa washuke ili nasi tupande.
Nikastuka kumuona Careen akitoa mshangao kumuona kijana mmoja sharobaro akishuka kwenye daladala.
Nikazidi kuwatazama wanavyoshangaana.
.
Nikaona wanasalimiana, ikabidi nipande ndani ya daladala ili niwatazame vizuri.
Kina Ivan na Nasra nao waliokuwa seat ya nyuma yangu, wakanistua kwa mkono "Chris vipi huibiwi!? "
.
Mwisho wa kusalimiana kwao niliona Careen akimkabidhi yule mwanaume kile kifuko chenye dera, wigi na makeup ndani yani.
Na Careen kupanda ndani ya gari.
.
Kwa wivu nilionao, nikauliza "Yule nani na mbona umempa kile kifuko!?? "
Akaniambia "Yule anaitwa Andrew, ndiye yule boyfriend wangu aliyekuwa ananisaliti na kunitesa kihisia."
.
Nikakumbuka pindi Careen analalamika kuhusu boyfriend wake anavyomtesa na hata kumuacha kwasababu ya kijinga.
.
Careen akaendelea kueleza "Pale alikuwa ananilalamikia kuwa alinitania tuachane, bado ananipenda.
Nikamshangaa, mimi siwezi rudia takataka.
Na kuhusu kile kifuko nilichompa, hajajua ndani kuna nini, amedhani nimempa zawadi tu, na akienda kukifungua nadhani atalia mpaka basi.
Wewe na Peter ni wanaume wa shoka, yule ni limbukeni wa kupendwa, kwangu namuona kama ana tabia za kidada, sasa acha akavae hilo dera na wigi ili atongozwe vizuri mxieeeew".
.
Tukacheka sana huku tukigonga mikono.
Nikampa kombatio la nguvu.
Na akakilaza kichwa chake kifuani mwangu.
Nikaanza kukumbuka yote niliyopitia na kusema nimejifunza mengi sana kupitia Careen.
Nikaanza kukumbuka moja baada ya jingine.
.
Pindi nipo kwenye mawazo, simu ya Careen iliita namba ngeni.
Kupokea ni Andrew amepiga kwenye namba nyingine.
Careen alivyomsikia tu, akachomeka earphone na kunipa sikio moja nisikilize.
.
Alilalamika sana huku akilia, lakini nilijifunza kitu kimoja kupitia Andrew kuwa kumbe kuna watu ukiwaonyesha upendo huwa wanakua malimbukeni, wanaanza kukufanyia visa na vituko, na hata kukutishia kukuacha.
Anadhani akikuacha utateseka, hutaweza ishi bila yeye, anakufanya atakavyo.
.
Ila unapoamua kuachana nae na ukawa huna muda nae tena, ukazidi kuwa bora zaidi yake.
Ndipo huwa anakumbuka kuwa sio wewe ambae huwezi ishi bila yeye, bali ni YEYE ambaye hawezi ISHI bila WEWE.
.
Nilipoona bado Andrew anaendelea kulia lia, nikakaza sauti na kumkaripia kwa nguvu "NANI HUYU AMBAYE ANAZUNGUMZA NA MPENZI WANGU".
.
Hapo hapo akakata simu, gari zima walicheka.
Nikambusu na kumuambia "Umenipa tulizo la maumivu yangu yasiyo kwisha".
Akaniambia "Nimekupa tulizo darling, maumivu tumemuachia Andrew".
.
******MWISHO******
 
Back
Top