Mambo 12 Unayo Weza Kufanya katika Chakula chako Kama mapishi Yako yameenda Sivyo au Mengine ya Kinyumbani fanya Hivi

Kasomi

JT Founder
MAMBO 12 UNAYO WEZA KUFANYA KATIKA CHAKULA CHAKO KAMA MAPISHI YAKO YAMEENDA SIVYO AU MENGINE YA KINYUMBANI FANYA HIVI

1) chumvi Ikizidi Kwenye Mchuzi Menya Kiazi Mbatata Weka Ganda Lake Acha Uchemke Chumvi Itapungua Sana

2) Ukiunguza Wali Kata Kitunguu Maji Nusu Weka Kwenye Wali Funika Kwa Dakika 5 Kinasaidia Kutoa Harufu Ya Moshi

3) Tui Lisipokolea Kwenye Maharage Weka Unga Wa Sembe Tikisa Acha Itokote Hata Kama Nazi Ni Nusu Itakuwa Kama Umeweka Nazi 3

4) Maharage, Nyama, Mahindi, Muhogo Ukiwa cherema, ndizi zikiwa ngumu, ukitaka Yaive Upesi Weka Baking Powder

5) Mchuzi Wowote Ukitaka Uwe Rosti Nzito Na Hauna Nyanya Za Kuosha Weka Kijiko kimoja Cha Chakula Unga Wa Ngano Ukoroge Na Maji Kidogo Kisha Weka Acha Uchemke Dk 5 Au Parua Kiazi Mbatata Ndani Yake

6) Nyama Pia Ikiwa Ngumu Parua Papai Bichi Weka Humo

7) Wali Ukishika Chini Na Kuungua Kabla ya Kufunikia Weka Margarine Au Blueband Unaondosha Harufu Ya Kuungua

8) Carrot Kama Umeitoa Katika Friji Imesinyaa Weka Kwenye Maji Ya Baridi Nusu Saa Itakuwa Kama Imetoka Shambani

9) unga, mchele, maharage ukitaka Kuepusha Wadudu Weka Kiasi Cha Pcs 10 Za Karafuu ndani yake

10) ukitaka nguo zako zinukie vizuri Wakati Unapiga Pasi Puliza Parfume Au Maji Ya mawaridi nguo zako zitakuwa na harufu Nzuri

11)Ukitaka Kuondoa Harufu Ya Chakula nyumbani mara ukimaliza kupika kabla ya kuweka udi au ubani kwanza fukizia sukari au Kahawa Kidogo Kisha Weka Udi Au Ubani

12) Mwisho Ukimaliza Kazi Za
jikoni fua mataulo ya jikoni kwanza kwa Kuyachemsha Pia Sponge Za Vyombo Ili kuepusha wadudu na maradhi

Credit: Edward C Lukindo
 
Back
Top