Kasomi
JT Founder
Samuel Eto'o Ashinda Kesi Yake CAS, CAF Yatakiwa Kumrudisha Kwenye Orodha Ya Wagombea Urais
Samuel Eto'o ameshinda kesi yake katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) iitwayo CAS dhidi ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Samuel Eto'o ameshinda kesi hiyo baada ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kutoa uamuzi uliomuunga mkono na kumfanya kuwa mgombea tena katika uchaguzi ujao wa Kamati ya Utendaji ya CAF.
Baada ya uamuzi huo wa CAS, sasa CAF itatakiwa kumlipa Etoo Faranga 8000 za Uswizi ambayo ni sawa na Milioni 24.2 za Tanzania na kutakiwa kurejeshwa katika orodha ya wagombea wa urais CAF zikiwa zimebaki siku 5 pekee tu kuelekea uchaguzi.
Hukumu hiyo, imeyotolewa leo Machi 7, 2025, huko Lausanne nchini Uswisi, na kusafisha njia kwa Eto'o na Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT), ambalo lilipinga kutengwa kwake kwenye kinyang'anyiro hicho.
Mgogoro huo ulizuka wakati Kamati Utendaji ya CAF, katika uamuzi uliotolewa Januari 25, 2025, kuondoa jina la Eto'o katika orodha ya wagombea walio na sifa za kuchaguliwa katika Mkutano Mkuu wa Machi 12, 2025 jiji Cairo nchini Misri.
Chanzo: Msasa online