Advertise here

Krrish 4 Kusogezwa Mbele kwa Sababu ya Bajeti ya Utengenezaji

Kasomi

JT Founder
964

Bollywood : Krrish ni Moja wapo ya Filamu bora za mfululizo kuwahi kutengenezwa Bollywood ambayo imejipatia umaarufu mkubwa nje na ndani ya India. Filamu hiyo iliaza mnamo mwaka 2003 kupitia Koi Mil Gaya na kufata Krrish mnamo mwaka 2006 bila kusahau Krrish 3 ambayo iliachiwa mnamo mwaka 2013.

Ni takriban miaka 13 Sasa mashabiki wa Filamu wamekuwa wakisubiri mwendelezo wa nne wa Krrish ili kutaka kuona nini kinafata kupitia franchise hiyo Walakini bado hakujakuwepo Taarifa rasmi ya ujio mpya wa superhero hiyo ambapo awali imeripotiwa kuwa utengenezaji wa Filamu hiyo utaaza kwenye nusu ya pili ya mwaka huu 2025.

Sasa, Kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka Bollywood Hungama Inaripotiwa kuwa Filamu hiyo imesogezwa mbele tarehe ya kuanza utengenezaji ambapo badala ya kuaza mwezi June inategemewa kuaza mwisho mwaka huu 2025 kutokana na changamoto ya bajeti kubwa ya utayarishaji wa Filamu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chazo cha karibu cha Mtayarishaji wa Filamu hiyo bwana Rakesh Roshan ambae pia ni baba mzazi wa Nyota Hrithik Roshan, Inaelezwa kuwa bajeti ya Krrish 4 inakadiriwa kuwa karibu 700 Crores za India ambazo ni wastani wa Tsh. Billion 213 na Million 938 lakini hadi Sasa hakuna studio iliyo tayari kuwekeza kiasi hicho kikubwa cha pesa na Inaelezwa Director Siddharth Anand kupitia studio yake ya Marflix pamoja na Mtayarishaji wa Filamu Karan Malhotra wamejitenga na mradi huo Kutokana na kushindwa kumudu gharama hizo.

Hivyo, Hrithik Roshan na baba yake Rakesh Roshan walikuwa na kikao cha kujadili hilo na wameamua kujilipua wenyewe na kuongea na studio washirika kutoka India na sasa KRRISH 4 itazalishwa na FilmKraft kama ilivyo kawaida wakati Marflix studio itazingatia miradi mingine nje ya Krrish," chanzo kiliongezea.

Muda wowote kutoka Sasa tutegemee list ya waigizaji watakaoigiza Krrish 4.
 

Attachments

  • 1742383124758.jpg
    1742383124758.jpg
    634.1 KB · Views: 313
Back
Top