john achila mukumwa
Member
Mtu anayetungisha mimba wenye chupa maabara ana hatia mbele ya Mungu au la
Kwanza ni muhimu kufahamu nini maana ya watoto wa kwenye chupa.
Ikitokea mama anakuwa ana mayai lakini anapata shida kushika mimba, huwa kuna uwezekano wa kuyatoa mayai yake kutoka kwenye uzazi na kuyaweka kwenye kifaa maalum kinachoitwa test tube au kwa kiswahili chupa. Wakishaliweka hilo yai la mwanamke mle, huwa wanachukua mbegu za mwanamume na kuziweka mle kitaalam, ili kurahisisha lile yai kurutubishwa kirahisi. Baada ya lile yai kurutubishwa ndani ya ile chupa, wanalichukua lile yai na kulirudisha kwenye tumbo la yule mama, na kuendelea na hatua nyingine za ukuaji wa mtoto kwenye tumbo la mama yake. Hiyo ndiyo maana ya mtoto wa kwenye chupa.
Siyo kwamba yule mtoto anawekwa kwenye chupa maisha yake yote, hapana. Ni yai tu ndilo linalorutubishiwa kule na kurudishwa mahali husika.
Kwa hiyo hakuna mazingira yo yote nje na tumbo la mama, mtoto anaweza kukua. Wanadamu hawajafikia huo uwezo.
Tumbo la mama ndiyo sehemu pekee ambapo mtoto anaweza kukua hadi kufikia hatua ya kuzaliwa.
Tukirudi kwenye swali. je, ni dhambi yai kurutubishiwa kwenye chombo hicho maalum nje na tumbo la mama?
Jambo la msingi ni kwamba, uumbaji wa Mungu, ikiwa ni pamoja na utungaji wa mimva, unafanyika ndani ya mwili, na siyo nje yake.
Aidha, binadamu hawezi kumchagulia Mungu njia mbadala ya uumbaji.
Ni jukumu la binadamu anayehitaji mtoto kumuomba Mungu kwa bidii, kama Eliya (Yakobo 5:17-18) na Danieli (Danieli 10:2-12), walivyoomba kwa bidii, ili naye mtu huyo, Mungu ampe mtoto.
Binadamu hawezi kutumia njia mbadala kwa niaba ya njia rasmi ya Mungu.
Pamoja na nia ya mtu kufanya vile ni kutafuta mtoto, kwani wengi wanaofanya hivyo unakuta wana matatizo ya kutoshika mimba, ambapo njia rahisi wanayoshauriwa na madaktari ni kutumia hiyo njia. Hata hivyo, matatizo ya kidunia, (yakiwemo ya nguvu za giza ya kuzuia mtu kupata mtoto), hayawezi kubatilisha utaratibu wa Mungu wa kupata mtoto.
Hata kama hatua hiyo ya kurutubisha yai kwenye chupa ni hatua ya awali kabisa hata mtoto hajaanza kutengenezwa, bado mbele ya Mungu, ni hatua batili.
Ni vizuri kumtegemea Mungu kuliko madaktari, yaani kumwamini Mungu kuliko kutafuta njia mbadala.
Watu wana imani zisizofanana. Wako wenye imani kuwa Mungu atawapa watoto pasipo njia hizo, na wapo wasio na imani hiyo. Lakini mtu akitumia njia hiyo, ajue kabisa kuwa ana hatia mbele ya Mungu, hata kama atakuwa na nia njema ya kupata mtoto. Nia njema haiwezi kubatilisha utaratibu wa Mungu.
Kitabu cha Warumi 14:5, kinasema: ...Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe".
Hivyo, mwenye kuhitaji kupata mtoto, amwombe Mungu kwa bidii, yeye peke yake, au hata kupitia kwa mtumishi sahihi wa Mungu.