Advertise here

Taasisi ya JamiiAfrica Yazinduliwa rasmi

Kasomi

JT Founder
DAR ES SALAAM — Taasisi ya JamiiAfrica imezinduliwa rasmi Jana April 24, 2025, ikichukua nafasi ya iliyokuwa JamiiForums, sambamba na uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka sita unaoelekeza mwelekeo mpya wa taasisi hiyo ndani na nje ya Tanzania.

Mpango huo unalenga kupanua wigo wa utendaji, kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kwa maamuzi sahihi, kuongeza ushirikishwaji wa wananchi katika masuala ya maendeleo, na kuhakikisha mamlaka zinawajibika ipasavyo kwa umma.

JamiiAfrica inasimamia majukwaa mbalimbali yakiwemo @JamiiForums, JamiiCheck, Stories of Change, Fichua Uovu na JamiiData, huku ikidhamiria kukuza demokrasia, utawala bora na uwajibikaji kwa kutumia majukwaa ya kidijitali na ya moja kwa moja kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.
1745672714470.jpg
 
Back
Top