Kasomi
JT Founder
Hekaheka za kufunguliwa kwa Kituo Kikubwa cha Biashara na Usafirishaji cha EACLC Ubungo Jijini Dar es salaam zimeendelea kushika kasi ikiwa zimebaki siku chache tu ili Kituo hicho kitakachokuwa kiungo muhimu kwa Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kifunguliwe rasmi.
Wanasema hii sio Shopping Mall bali ni Kituo Kikubwa na cha Kipekee cha Kibiashara na Usafirishaji Afrika Mashariki kilichojengwa na Mwekezaji Raia wa China ambaye alichukua muundo wa ujenzi wa Vituo vingine maarufu vya Nchini China.
Katika hekaheka za kukaribia kufunguliwa kwa Kituo hiki kitakachokuwa na Maduka yasiyopungua elfu mbili huku maegesho ya magari yakiweza kuchukua magari zaidi ya elfu moja kwa wakati mmoja, Uongozi wa EACLC umeiambia AyoTV kuwa hadi leo tayari Mabenki nane yameshajichagulia maeneo yao ndani ya Kituo hiki ili kutoa huduma za kibenki kwa ukaribu zaidi kwa Wateja mbalimbali ambapo Mabenki hayo ni pamoja na NMB, NBC, TCB, EXIM BANK, EQUITY, STANBIC, AZANIA na PBZ.
Vilevile Watanzania mbalimbali ambao walishalipia ‘fremu’ katika eneo hili wameanza kukabidhiwa funguo za Maduka yao lakini pia Uongozi wa Kituo hiki umeendelea kuwakaribisha Wafanyabiashara wengine kuja kujionea muundo wa Kituo hiki pamoja na kukodisha fremu hizi kwa gharama ya kuanzia shilingi milioni moja kwa mwezi