Kasomi
JT Founder
KENYA: Benki ya Dunia imeitaja Kenya kuwa ya kumi kati ya nchi maskini zaidi duniani ambapo taarifa hiyo imetolewa wakati taifa hilo likijiandaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, huku hali ya kisiasa ikielezwa kuwa na mvutano unaozidi kuongezeka katika kipindi cha maandalizi ya uchaguzi huo.
Migogoro kati ya vyama vya siasa na viongozi wakuu wa kitaifa inaendelea kuathiri mwenendo wa uchumi wa Kenya na kusababisha kushuka kwa imani ya wawekezaji wa ndani na wa kimataifa.
Benki ya Dunia inaeleza kuwa mazingira ya kisiasa yasiyo na utulivu huathiri uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni, husababisha kukimbia kwa mitaji na kudhoofisha masoko ya fedha na fursa za ajir utekelezaji wa sera za fedha na miradi ya maendeleo.
Benki Kuu ya Kenya inaweza kukabiliwa na changamoto ya kudhibiti mfumuko wa bei, hali inayoweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya riba na kupunguza shughuli za biashara, utalii na uwekezaji wa miundombinu nchini humo.
Aidha Benki ya Dunia imeonya kuwa endapo hali ya kisiasa itaendelea kuwa tete, Kenya inaweza kushindwa kufanikisha mipango yake ya maendeleo ya muda mrefu.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa ucheleweshaji wa sera za kiuchumi na kupungua kwa uwekezaji vinaweza kuongeza kiwango cha umaskini na ukosefu wa ajira nchini humo.