Kasomi
JT Founder
Askofu Gwajima amesema Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuwa entertained
Gwajima anasema huwa haongei kwa kubahatisha, mpaka anakuja kuongea mbele za watu ni kwasababu ana data, na data hizo amekuzikusanya kutoka matukio yaliokuwa yanafanyika miaka kadahaa na kupata orodha ya watu takribani 83 waliopitia matukio haya ya utekaji, amewataja Mzee Soka, Mdude Nyangali, wanaharakati wa Kenya na Uganda na wengine wengi akijenga hoja kuwa kuendelea kunyamaza Katika Hali hii hauwezi kujua atayefuata kutekwa ni nani, hivyo Bora kusema na kushauri Ili mambo yatatuliwe.
"Utekaji si utamaduni wetu wa kitanzania na ni jambo ambalo halitakiwi kuvumiliwa na mtu yeyote, nitoe mfano mimi natokea jimbo la Kawe kuna huyu bwana anaitwa Ali Kibao alikuja akashushwa kwenye gari watu wanaona, abiria wote wanaona halafu kesho yake akapatikana amekufa"
"Nataka nimuulize mtu yeyote kama baba yako akishushwa mbele yako wewe mwenyewe halafu kesho yake akapatikana amekufa utajisikiaje? lakini siyo huyo tu, tumeona juzi juzi kule Mbeya mtu anaitwa Mdude"
"Watu wamekuja nyumbani kwake wamevunja mlango wamemchukua akiwa hai mbele ya familia yake wameondoka nae na mpaka leo hatujui yuko wapi na hatujui nani sasa anaefuata unaweza ukanyamaza kumbe unafuata wewe"
"Juzi juzi hapa tena mwanaharakati wa Uganda anaitwa Agather Atuhaire amekuja hapa amehudhuria mahakamani huyo mtu amechukuliwa na watu waliojitambulisha kama watu wa vyombo nimeona anaongea kwenye Youtube"
"Kwa uchungu kabisa kwamba wakaenda mahali akavuliwa nguo akafanyiwa udhalilishaji na akaenda kutupwa mpakani, sasa hebu tujaribu kuwaza kama angekuwa ni mama yako mzazi anachukuliwa anavuliwa nguo anadhalilishwa anatupwa mahali ungejisikiaje au kama angekuwa ni dada yako kabisa wa tumbo moja"