Nimezungumzia utekaji, Kanisa likafungwa Gwajima afunguka

Kasomi

JT Founder
1752688497750.jpg

Askofu wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Josephat Gwajima ambaye kanisa lake limefungwa na serikali ya Tanzania amesema bado haelewi uhusiano uliopo kati ya hotuba yake ya kupinga vitendo vya utekaji na kanisa lake kufungwa.

Amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari leo Julai 16, akifafanua masuala kadha wa kadha.

"Kama mnakumbuka vizuri tarehe 24.05 nilongea na nyinyi kuhusu kutekwa kwa watu katika nchi yetu na ushauri wangu kwa taifa. Na hiyo hotuba yangu ikasababisha kanisa letu la Glory of Christ Tanzania likafungwa na makanisa mengine zaidi ya 2,000 yakafungwa, kwa hiyo kuna wachungaji zaidi ya 2,000 na maaskofu wetu zaidi ya 32 hawana kazi kwa sababu makanisa yamefungwa.

Amesema anadhani watu hawakumuelewa kufuatia hatua hiyo ya kufungwa kanisa baada tu ya kutoa hotuba hiyo na kuongeza kuwa haelewi kuna uhusiano upi.

Aidha kiongozi huyo wa kanisa amesema ataendelea kusalia kwenye chama hicho tawala bila ya kujali kile kinachoendelea. "Lakini nataka nisisitize kwamba mimi bado ni mwanachama wa CCM na nitaendelea kuwepo. Mara nyingi watu wengi wasiopenda mema ukizungumza tu jambo lolote la kujaribu kusahihisha au kuweka sawa, wanasema anataka kuhama CCM!" alisema Askofu Gwajima.

Akasisitiza "Mimi sihami CCM nipo sana, tunabanana humuhumu ndani mpaka paeleweke, pakae vizuri. CCM ni chama cha kidemokrasia kama yalivyo madhumuni ya katiba yake. Kwa hiyo tunabanana humuhumu."
 
Back
Top