Advertise here

9 Wafariki Dunia ajali ya Basi Morogoro

Kasomi

JT Founder
1749719001190.jpg

HABARI Watu tisa wanatajwa kufariki dunia papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Hai kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba shehena ya sukari katika eneo la Lugono Melala, barabara kuu ya Morogoro – Iringa.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Daniel Nkungu, ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Alhamisi Juni 12, 2025 na hospitali imepokea miili ya marehemu tisa, mitano ya wanaume na minne ya wanawake.

Nkungu amebainisha kuwa amepokea majeruhi 44 wengi wao wamepata mivunjiko na wanaendelea kupatiwa matibabu ya haraka chini ya uangalizi wa karibu wa wataalamu wa afya.

Huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema kwamba atatoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari muda si mrefu kuhusu chanzo cha ajali hiyo na hatua zinazochukuliwa.
Chanzo: EastAfricaTV
 
Back
Top