Advertise here

Moto wateketeza soko la Mashine Tatu Iringa

Kasomi

JT Founder
Screenshot_20250712-111023~2.png

Soko maarufu la Mashine Tatu lililopo katika Manispaa ya Iringa limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, Julai 12, 2025. Moto huo umeharibu vibanda na maduka mengi katika soko hilo linalouza mali mbichi, huku taarifa zikithibitisha kuwa hakuna mali iliyookolewa. Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

Mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na Azam TV wamesema moto ulianza kwa mwendo mdogo majira ya saa sita usiku, lakini uliongezeka kwa kasi kubwa ilipofika saa tisa alfajiri. Wakazi wa maeneo jirani walijitokeza kusaidia kuzima moto huo, lakini juhudi hizo hazikufua dafu kutokana na ukubwa wa moto na ukosefu wa vifaa vya kisasa vya uokoaji.

Kwa sasa, mamlaka husika zikiwemo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na uongozi wa Wilaya ya Iringa zinaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo halisi cha moto huo.

Taarifa zaidi kuhusu madhara kamili na hatua zitakazochukuliwa zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni…endelea kutufuatilia kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii.

Chanzo: Azam TV
 
Back
Top