Kasomi
JT Founder
Pamoja na kuwa ofa ya Esperance ya Tunisia kwenda Yanga SC kwa ajili ya kumnasa Clement Mzize kuwa juu kuliko ofa zote zilizotua Yanga SC ikiwemo ofa kutoka Al Masry ya Misri na Umm Salal ya Qatar ila Yanga wametia ngumu.
Yanga wanaonekana hawataki ofa yoyote kuipokea inayotokana na Jasmine Razak ambaye ni msimamizi wa Clement Mzize, hiyo inatokana na kutokuwa na mahusiano mazuri baina yao kitu ambacho kinamuumiza au kumkomoa Clement Mzize.
Esperance wako radhi kuilipa Yanga kiasi cha Dola milioni 1 ambacho wanahitaji Yanga, kumpa USD 100,000 mchezaji kama pesa ya kusaini na kumpa mshahara wa USD 350,000 kwa mwaka wa kwanza kitu ambacho Mzize na Jasmine Razak hawana tatizo ila kipengele kipo Yanga SC.
Ila Yanga mnataka Mzize aende Qatar Umm Salal
NB: Hilo Bango la Yanga linaonesha ramani ya Afrika upande wa Kaskazini iliyopo nchi ya Tunisia kuwa wameikataa ofa yao
OFA ILIYOTUMWA NA ESPERANCE KUHUSU MZIZE.
MSHAHARA
1. Milioni 870 Kwa Mwaka wa kwanza
2. Milioni 73 Kwa Mwezi
3. Milioni 18.25 Kwa Wiki
4. Milioni 2.6 Kwa siku
5. 108,625 Kwa saa.
6. 1800 Kwa dakika
7. 30 Kwa sekunde
8. Milioni 994 Kwa Mwaka wa pili
9. Bilioni 1.12 Kwa Mwaka wa tatu.
10. Milioni 62 endapo akitoa assist 10 au mabao 10 kwa msimu.
11. Milioni 50 akicheza mechi za Ligi Kuu Tunisia kwa asilimia 60.
12. Milioni 250 kama pesa ya kusaini ya Mzize.