Advertise here

Yanga Wana roho mbaya sana wakala wa mzize atoa lawama

Kasomi

JT Founder
Screenshot_20250811-102030~2.png

Wakala wa mshambuliaji wa Yanga SC, Clement Mzize, Bi. Jasmine Razaq, ameikosoa vikali klabu hiyo kwa kile alichokiita kuwa ni “roho mbaya” baada ya kuzuiwa kwa mteja wake kujiunga na klabu ya Al Masry ya Misri, licha ya ofa nono iliyotumwa mezani.

Kwa mujibu wa Jasmine, Al Masry imetuma ofa ya dola 700,000 (sawa na takribani Shilingi Bilioni 1.8) kwa ajili ya kumnunua Mzize, lakini Yanga SC wameshikilia msimamo wa kutaka kiasi kisichopungua dola milioni 1 (sawa na Bilioni 2.6) ndipo wawe tayari kumruhusu kuondoka.

"Yanga wanaroho mbaya. Miaka miwili iliyopita walikuwa wanamlipa Clement milioni 2 kwa mwezi, sasa analipwa milioni 15. Lakini bado hawataki kumwachia wakati huu ambapo ana nafasi ya kubadili maisha yake na ya familia yake," amesema Jasmine kwa hisia kali.

Ameeleza kuwa Mzize ni mchezaji chipukizi anayehitaji nafasi ya kukuza kipaji chake kimataifa na kupata maisha bora. Ameongeza kuwa familia ya Mzize inamtegemea kwa kiasi kikubwa, na fursa kama hii haipaswi kuzuiwa kwa misingi ya masharti magumu ya uhamisho.

Sakata hili limezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa soka Tanzania, wengi wakitaka klabu hiyo kuangalia maslahi ya mchezaji na kuonyesha huruma kwa mustakabali wake wa maisha na taaluma.
Mpaka sasa uongozi wa Yanga SC haujatoa kauli rasmi juu ya madai haya, huku ikisubiriwa kuona iwapo watalegeza msimamo wao au kusimama kidete kwenye dau la dola milioni moja.
 
Back
Top