Kasomi
JT Founder
Mechi hiyo inatarajiwa kuanza Saa 3:00 usiku na kuonyeshwa moja kwa moja kupitia chaneli ya AzamSports1HD.
Yanga inahitaji ushindi wa ugenini kufuzu Hatua ya makundi baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Haitakuwa mara ya kwanza Yanga kujikuta katika mtego wa kupigania ushindi ugenini – kwani mwaka 2001 katika michuano hii na hatua kama hii, Yanga ilitoa sare ya 2-2 na Highlanders FC ya Zimbabwe Jijini Dar es Salaam.
Lakiki ikafanikiwa kushinda 2-1 Bulawayo katika mchezo wa marudiano mna kusonga mbele, ambako ilitolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 6-5.
Dhidi ya Mamelodi, Yanga ilifungwa 3-2 Johannesburg kabla ya kulazi na sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Chanzo: Binzubeiry sports online