Kasomi
JT Founder
Baada ya aliyekuwa DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya wenzake na wenzake wawili Silvester Nyegu na Daniel Mbura kuachiwa huru kwenye kesi ya unyang'anyi wa kutumi silaha leo, wamerudishwa Mahabusu kwenye Gereza Kuu la Kisongo kutokana na kuwa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi ambayo ilikuwa haina dhamana, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imepanga May 31, 2022 kutoa hukumu ya kesi hiyo ya uhujumu uchumi inayomkabili Sabaya na wenzake sita.
Katika kesi hiyo washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.
Tarehe hiyo imetajwa leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo ambapo amesema kwakuwa Watuhumiwa hao wapo Mahabusu kesi hiyo itatolewa hukumu May 31,2022.
Pia soma Sabaya ashinda rufaa na kuachiwa huru na mahakama kuu ya Arusha