BADALA YA SHERIA NA KATIBA TULIA KATUMIA NGUVU KUWABAKIZA AKINA MDEE BUNGENI
Ibara ya 71(1) (f) inatamka kwamba " Mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge LITOKEAPO lolote kati ya mambo yafuatayo-
(f): Iwapo mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge.
Swali la msingi ni mwanachama anakomaje kuwa mwanachama wa chama cha siasa? Jibu ni pale ambapo anakosa sifa za uanachama kulingana na katiba na miongozo ya chama chao na si vinginevyo!
Hakuna sehemu ambapo katiba inasema kwamba uanachama wa mtu kwenye chama cha siasa utahesabiwa kuwa umekoma pale ambapo mwanachama atakuwa amevuliwa uanachama na Mahakama. Mahakama tunakwenda kulalamika baada yakutendewa tofauti na tunavyotaka.
Cha ajabu Tulia hajasema ni kifungu gani cha katiba kinachomzuia yeye kuwaondoa akina Mdee Mahakamani mpaka pale mahakama itakapokuwa imesikiliza kesi yao. Kifungu hicho hakipo. Yeye kaamua tu kutumia nguvu.
Nilisema kwamba mahakama haiwezi kutoa injunction kwa sababu mchakato ulishakamilika na principles za injunction kinachozuiwa huwa ni mchakato na sio matokeo. Matokeo yanapingwa tu mahakamani. Lakini wakati matokeo yakipingwa mahakamani wahusika lazima wabanwe na kile kilichokwishatokea.
Mbunge anapopoteza sifa ya kuwa mbunge, whether kwa kufukuzwa uanachama au kwa sababu nyingine yoyote, hastahili kuendelea kuwa mbunge kwa siku moja zaidi.
Na hali hiyo inaendelea hadi hapo Mahakama Kuu, au Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, itakapoamua vinginevyo.
Mheshimiwa Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu. Alitolewa nje ya Bunge kwa kukosa sifa kutokana na kuvuliwa ubunge. Alikata rufaa Mahakama ya Rufaa, lakini aliendelea kuwa nje ya Bunge hadi Mahakama ya Rufaa ilioamua kwamba alikuwa mbunge halali.
Wabunge tisa wa chama cha CUF walifukuzwa uanachama wa kilichokuwa chama chao. Walitolewa Bungeni kwa kukosa sifa ya kuendelea kuwa wabunge.
Wabunge hao walifungua kesi Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa kuwafukuza uanachama. Kufungua kesi peke yake hakukuwarudisha Bungeni.
Mifano ya aina hii ni mingi sana katika historia yetu ya kisiasa na kibunge.
Spika Tulia Ackson anasemekana kuwa na PhD ya sheria. Alikuwa mwalimu wa sheria Chuo Kikuu na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Anajua sheria za nchi yetu na misingi yake. Uamuzi wake ni wa kisiasa; kwa sababu za kisiasa. Kwa mtanzamo wangu naona amekosea
Kama watu wamekosa sifa kwenye chama Chao kwanini waendelee kuwa bungeni??