Advertise here

Balthazar Ebang Engonga atupwa jela Miaka 8

Kasomi

JT Founder
1756318123906 (1).jpg

Mahakama moja nchini Guinea ya Ikweta imemhukumu kifungo cha miaka 8 gerezani aliyekuwa afisa mwandamizi wa serikali ya nchi hiyo Baltasar Ebang Engonga kwa makosa ya ubadhirifu wa fedha za umma. Baltasar Ebang Engonga aliutikisa mtandao wa intaneti mwaka jana kwa sifa chafu baada ya kuvuja kwa mamia ya video za ngono zilizopatikana kwenye vifaa vyake vya kielektroniki vilivyokamatwa wakati wa uchunguzi wa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za umma. Baadhi ya waliokuwamo kwenye video hizo walikuwa wake wa maafisa wengine wa serikali. Mbali ya kifungo cha miaka 8, Baltasar ametakiwa pia kulipa faini ya dola 220,000.
 
Back
Top