Advertise here

Naomie Pilula akataa kufuta Picha zake Mtandaoni kisa Muonekano wake

Kasomi

JT Founder
1756838278564.jpg

Naomie Pilula, mwanasheria kutoka Zambia, alichapisha selfie mwezi Juni ambayo ilisambaa sana mtandaoni na kupata zaidi ya maoni 530,000 Instagram, mengi kati yake yakiwa ya kejeli na maneno mabaya kuhusu muonekano wake, wengine wakithubutu kuuliza kama ni picha ambayo imetengenezwa kutumia AI.

Licha ya shinikizo la watu, Naomie alikataa kufuta picha hiyo.

Mwanamke huyu alikulia Zambia na amekuwa akipokea maoni mbalimbali juu ya mwili na sura yake, hasa kuhusu pua yake ambayo yeye mwenyewe huihusisha na urithi kutoka kwa baba yake.

Alipohamia Australia na New Zealand kusomea masomo yake, mara nyingi alikuwa mtu pekee mweusi darasani, jambo lililomsaidia kutafakari upya dhana ya uzuri.

Miongoni mwa maoni aliyoyapata, kuna lililomshauri afanye upasuaji wa kubadilisha pua (rhinoplasty).
Awali alikasirika na alitaka kujibu kwa hasira, lakini dada yake akamuuliza swali: “Kwa nini hii inakukera sana?” Swali hilo lilimfanya kutambua kuwa bado alihitaji kuendelea kuponya baadhi ya majeraha ya ndani.

Nguvu yake kuu aliipata kupitia imani ya Kikristo, akitafakari mistari ya Biblia kama Zaburi 139 na simulizi la Yosefu. Badala ya kurudi nyuma, aliamua kubaki na picha hiyo kama ishara ya uthubutu.

Kile ambacho watu walitaka kitumike kumvunja moyo, kiliishia kuwa nafasi ya ukuaji na kuunganishwa na wengine.

Baada ya tukio hilo, wafuasi wake Instagram walipanda kutoka karibu 1,000 hadi zaidi ya 20,000, na sasa anaendelea kutumia jukwaa lake kuhamasisha wengine wajikubali na kujipenda kwa dhati, bila kuongozwa na vigezo vya jamii vya “uzuri".
1756838583080.jpg
 
Back
Top