Fahamu kwa Nini Israeli ni Taifa Teule

Fahamu kwa Nini Israeli ni Taifa Teule

Moja ya maswali yanayoulizwa na baadhi ya watu ni kujua kwa nini Israeli inaitwa taifa teule.

Kwa ujumla, taifa la Israeli lilijulikana kama taifa teule la Mungu kwa sababu ndilo taifa pekee duniani kote, ambalo lilikuwa linamuabudu Mungu wa kweli Yehova, aliyeumba mbingu na nchi. Mataifa mengine yaliyosalia yalikuwa yanaabudu sanamu, mizimu, miti, mawe, na wanadamu, na ushirikina kwa wingi. Ni taifa la Israeli pekee ndilo lililokuwa linamwabudu Mungu wa kweli. Katika upekee huo, ndiyo maana ni taifa teule.

Kiuhalisia, historia ya Israeli ipo kwenye Biblia. Ukisoma kitabu cha Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Kumbukumbu la Torati, Hesabu, Yoshua, Waamuzi, pamoja na Wafalme, vimeelezea vizuri sana kuhusu taifa la Israeli (wana wa Israeli).


Hakuna mahali popote ambapo pameelezea vizuri historia ya Israeli kama kwenye Biblia, na hakuna mahali pengine historia ya taifa hilo inaweza kupatikana isipokuwa katika Biblia.

Taifa Teule la Israel lilianzaje
Uchambuzi huu unaliangalia taifa hili kwa mtazamo wa Neno la Mungu na ndiyo maana neno “taifa teule” limetangulia, likiashiria kuwa kile kinachozungumzwa kinahusiana na Mungu.

Taifa Teule la Israeli lilianza kwa ahadi
Mtu mmoja aliyeitwa Abramu (baadaye aliitwa Ibrahimu), alimpendeza Mungu. Kwa mujibu wa maandiko, Tera (baba yake Abramu), na nduguze Abramu (Nahori na Harani), walikuwa ni waabudu sanamu, isipokuwa Abramu peke yake (Yoshua 24:2-3). Walikuwa wakiishi katika nchi ya Uru ya Wakaldayo, ambayo ni IRAQ kwa sasa. Mungu hakosei. Abram kumpendeza Mungu, maana yake Abram alimpendeza Mungu miongoni mwa jamii yote ya Iraq na Iran na jirani zao.

Mungu alimtwaa Abramu mpaka nchi ya ahadi ili kusudi afanye naye agano, maana kule kwenye nchi ya baba yake kulikuwa na ibada za miungu mingine. Hivyo Mungu akamwahidi kuwa atakuwa taifa kubwa.

Maelezo kuhusu ahadi yako kwenye Mwanzo 12:
1 “Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; 2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa”.
Ahadi hiyo ilianza kutimia baada ya Ibrahimu kupata mtoto wa kwanza wa kiume, ambaye alimwita Isaka. (Alikuwa na mwingine aliyemwita Ishmaeli, lakini Ishmaeli hakuwa mwana wa ahadi kwa sababu alizaliwa na mwanamke mwingine).
Baadaye, Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo ambaye ni mjukuu wa Ibrahimu, akazaa watoto 12. Hawa watoto 12 wa kiume waliozaliwa na Yakobo, waliitwa wana wa Yakobo, au watoto wa Yakobo. Walikuwa watoto 13 ikiwa ni pamoja na Dina (Mwanzo 30:21), lakini kwa taratibu za Kiyahudi wanawake hawakuhesabiwa.

Ulipofika wakati fulani, Yakobo jina lake lilibadilishwa na kuwa ISRAELI. Tafsiri ya jina Israeli ni “Mshindi”. Hivyo, kama jina la Yakobo lilivyobadilika, kadhalika na watoto wake hawakuitwa tena wana wa Yakobo, bali waliitwa wana wa ISRAELI. Majina ya watoto hao yalikuwa ni Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Zabuloni, Isakari, Dani, Gadi, Asheri, Naftali, Yusufu na Benyamini.
Hawa wana 12, walioa wake na kuzaa watoto wengi, na watoto wao nao pia wakaoa na kuzaa watoto, na wajukuu na vitukuu, na vilembwe, na vilembwekezi. Hatimaye TAIFA likaanza kuwa kubwa na kufikia watu elfu 10, elfu 20, laki hadi milioni na zaidi, taifa la Israeli.

Kila kizazi kilichokuwa kinatokea kilirekodiwa asili ya baba yake wa kwanza, kama ni Rubeni, au Lawi, au Gadi au mwingine ye yote akijulikana asili yake. Hivyo, kama ilivyo huku kwetu, walivyozidi kuwa wengi, majina ya baba zao yakageuzwa na kuwa MAKABILA YAO. Hivyo kila mtu alikuwa na kabila lake, miongoni mwa yale makabila 12. Hivyo ndivyo taifa la Israel lilivyoanzishwa.

Waisraeli walihamia Misri kisha wakaenda nchi ya ahadi
Kuna wakati njaa ilikuwa kali pale walipoishi taifa la Israeli. Ikabidi wahamie Misri ambako kulikuwa na chakula. Waliingia kwa amani, lakini walitoka kwa ushindani mkali dhidi ya Farao wa Misri, ambaye hakutaka waondoke kutokana na uhodari wao katika utendaji wa mambo mbalimbali. Farao alitaka waendelee kuwa watumwa wao. Baada ya kutolewa Misri kwa mkono wa Mungu mwenyewe, walianza safari ya kuelekea nchi ya ahadi, ijulikanayo kama KAANANI. Iliwachukua miaka 40 kukamilisha safari yao hadi kufikia nchi ya ahadi.

Kaanani ni jina la zamani la eneo la Mashariki ya Kati, ambalo siku hizi limegawanyika katika nchi za Israeli, Palestina, Lebanoni na sehemu za Magharibi za Jordan na Syria.

Yesu alizaliwa katika Taifa Teule la Israeli

Ilipofika wakati wa ahadi ya Mungu kuuokoa ulimwengu, alimtuma mwanawe mpendwa ambaye alizaliwa katika taifa hilo la Israeli, katika uzao wa kabila la YUDA. Yesu alizaliwa Maskini lakini alikuwa Mfalme. Alikufa kifo cha aibu, lakini alipofufuka alipata heshima. Yesu alifanyika kuwa wokovu kwa Waisraeli wenyewe, pamoja na watu wa mataifa. Watu wa mataifa ni watu wa mataifa mengine yote, tofauti na taifa la Israeli.

Jina lingine la Waisraeli
Waisraeli kwa jina lingine wanaitwa WAYAHUDI. Wayahudi ndio hao hao Waisraeli. Hivyo, ukiona mahali popote wanataja Wayahudi, fahamu kuwa ni hao hao Waisraeli.

Kwa ujumla, TAIFA LA ISRAELI LILIJULIKANA KAMA TAIFA TEULE LA MUNGU, KWA SABABU NDILO TAIFA PEKEE DUNIANI KOTE, AMBALO LILIKUWA LINAMUABUDU MUNGU WA KWELI YEHOVA, ALIYEUMBA MBINGU NA NCHI.
Mataifa mengine yaliyosalia yalikuwa yanaabudu sanamu, mizimu, miti na wanadamu.
Ni Israeli pekee ndilo lililokuwa linamwabudu Mungu wa kweli. Mahsusi, lilikuwa likifuata mambo ya Mungu. Ndiyo maana likaitwa Taifa Teule.


Kijeografia, taifa hili lipo katika bara la Asia, eneo linalojulikana kama mashariki ya kati. Nchi ya Israeli ni ndogo tu, kama mkoa wa Njombe nchini Tanzania, lakini ina utajiri mwingi, japokuwa asilimia kubwa ni jangwa. Watu wake wamejaliwa kuwa na uwezo wa ubunifu na uvumbuzi.

Idadi ya waisraeli waliopo Israeli sasa hivi inakadiriwa kukaribia milioni 10. Ndiyo nchi pekee duniani yenye idadi kubwa ya maadui kuliko nchi nyingine zote, kwani imezungukwa na nchi za kiarabu pande zote, ambazo zinalipinga vikali taifa hilo.

Pamoja na maadui wote hao wanaoizunguka, lakini bado Mungu anawashindania. Ni kwa sababu ni Taifa Teule. Pia, ana kusudi nao katika siku za mwisho. Baada ya unyakuo wa kanisa kupita, Mungu atalirudia tena taifa hilo kwa nguvu na kuwapa watu wake moyo wa toba. Wayahudi wote watatubu kwa machozi na maombolezo kwa uchafu wote wanaoufanya, na kwa sababu walimsulubisha Masihi wao, na Bwana atawasamehe na kuanza kuwashindania tena kama nyakati za kale. Mataifa yote yatapanga vita dhidi ya taifa hilo, lakini Mungu atalishindia dhidi ya mataifa mengine yote.

Ukitaka kujua ni kwa jinsi gani Waisraeli watarudiwa na Mungu katika siku za mwisho, ni muhimu kusoma maandiko katika: Warumi 11:26-29, Isaya 59:20-21 na Yeremia 31:33-34.
 
"Mimi mweusi mweusi lakini ni mzuri"King solomon kwenye wimbo uliobora anaandika!!

"Ngozi yangu ni nyeusi nayo yanitoka"Ayubu analalamika kila siku! Kitabu Cha ayubu!

Nakuuliza waisrael weusi weusi wako wapi siku hizi!!?mbona wote weupe tu!!?
 
Umesomeka vizuri sana mkuu,nilikuwa naitafuta sana hii story kwa muda mrefu,ta last nimeipata.Nilikuwa nawaza tu,hivi nikiomba uraia wa Israel nikawa muisrael naweza nikaingia kwenye huo msamaha au ni wale wa damu tu ndui watahusika...?
 
Kwani wapi umeliona andiko hilo!!?au hapo aliposema nduguze walimuweka malangoni akapigwa na jua akawa mweusi!!?
Wimbo Ulio Bora 1:6
[6]Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi,
Kwa sababu jua limeniunguza.
Wana wa mamangu walinikasirikia,
Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu;
Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.
 
Fahamu kwa Nini Israeli ni Taifa Teule

Moja ya maswali yanayoulizwa na baadhi ya watu ni kujua kwa nini Israeli inaitwa taifa teule.

Kwa ujumla, taifa la Israeli lilijulikana kama taifa teule la Mungu kwa sababu ndilo taifa pekee duniani kote, ambalo lilikuwa linamuabudu Mungu wa kweli Yehova, aliyeumba mbingu na nchi. Mataifa mengine yaliyosalia yalikuwa yanaabudu sanamu, mizimu, miti, mawe, na wanadamu, na ushirikina kwa wingi. Ni taifa la Israeli pekee ndilo lililokuwa linamwabudu Mungu wa kweli. Katika upekee huo, ndiyo maana ni taifa teule.

Kiuhalisia, historia ya Israeli ipo kwenye Biblia. Ukisoma kitabu cha Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Kumbukumbu la Torati, Hesabu, Yoshua, Waamuzi, pamoja na Wafalme, vimeelezea vizuri sana kuhusu taifa la Israeli (wana wa Israeli).


Hakuna mahali popote ambapo pameelezea vizuri historia ya Israeli kama kwenye Biblia, na hakuna mahali pengine historia ya taifa hilo inaweza kupatikana isipokuwa katika Biblia.

Taifa Teule la Israel lilianzaje
Uchambuzi huu unaliangalia taifa hili kwa mtazamo wa Neno la Mungu na ndiyo maana neno “taifa teule” limetangulia, likiashiria kuwa kile kinachozungumzwa kinahusiana na Mungu.

Taifa Teule la Israeli lilianza kwa ahadi
Mtu mmoja aliyeitwa Abramu (baadaye aliitwa Ibrahimu), alimpendeza Mungu. Kwa mujibu wa maandiko, Tera (baba yake Abramu), na nduguze Abramu (Nahori na Harani), walikuwa ni waabudu sanamu, isipokuwa Abramu peke yake (Yoshua 24:2-3). Walikuwa wakiishi katika nchi ya Uru ya Wakaldayo, ambayo ni IRAQ kwa sasa. Mungu hakosei. Abram kumpendeza Mungu, maana yake Abram alimpendeza Mungu miongoni mwa jamii yote ya Iraq na Iran na jirani zao.

Mungu alimtwaa Abramu mpaka nchi ya ahadi ili kusudi afanye naye agano, maana kule kwenye nchi ya baba yake kulikuwa na ibada za miungu mingine. Hivyo Mungu akamwahidi kuwa atakuwa taifa kubwa.

Maelezo kuhusu ahadi yako kwenye Mwanzo 12:
1 “Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; 2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa”.
Ahadi hiyo ilianza kutimia baada ya Ibrahimu kupata mtoto wa kwanza wa kiume, ambaye alimwita Isaka. (Alikuwa na mwingine aliyemwita Ishmaeli, lakini Ishmaeli hakuwa mwana wa ahadi kwa sababu alizaliwa na mwanamke mwingine).
Baadaye, Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo ambaye ni mjukuu wa Ibrahimu, akazaa watoto 12. Hawa watoto 12 wa kiume waliozaliwa na Yakobo, waliitwa wana wa Yakobo, au watoto wa Yakobo. Walikuwa watoto 13 ikiwa ni pamoja na Dina (Mwanzo 30:21), lakini kwa taratibu za Kiyahudi wanawake hawakuhesabiwa.

Ulipofika wakati fulani, Yakobo jina lake lilibadilishwa na kuwa ISRAELI. Tafsiri ya jina Israeli ni “Mshindi”. Hivyo, kama jina la Yakobo lilivyobadilika, kadhalika na watoto wake hawakuitwa tena wana wa Yakobo, bali waliitwa wana wa ISRAELI. Majina ya watoto hao yalikuwa ni Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Zabuloni, Isakari, Dani, Gadi, Asheri, Naftali, Yusufu na Benyamini.
Hawa wana 12, walioa wake na kuzaa watoto wengi, na watoto wao nao pia wakaoa na kuzaa watoto, na wajukuu na vitukuu, na vilembwe, na vilembwekezi. Hatimaye TAIFA likaanza kuwa kubwa na kufikia watu elfu 10, elfu 20, laki hadi milioni na zaidi, taifa la Israeli.

Kila kizazi kilichokuwa kinatokea kilirekodiwa asili ya baba yake wa kwanza, kama ni Rubeni, au Lawi, au Gadi au mwingine ye yote akijulikana asili yake. Hivyo, kama ilivyo huku kwetu, walivyozidi kuwa wengi, majina ya baba zao yakageuzwa na kuwa MAKABILA YAO. Hivyo kila mtu alikuwa na kabila lake, miongoni mwa yale makabila 12. Hivyo ndivyo taifa la Israel lilivyoanzishwa.

Waisraeli walihamia Misri kisha wakaenda nchi ya ahadi
Kuna wakati njaa ilikuwa kali pale walipoishi taifa la Israeli. Ikabidi wahamie Misri ambako kulikuwa na chakula. Waliingia kwa amani, lakini walitoka kwa ushindani mkali dhidi ya Farao wa Misri, ambaye hakutaka waondoke kutokana na uhodari wao katika utendaji wa mambo mbalimbali. Farao alitaka waendelee kuwa watumwa wao. Baada ya kutolewa Misri kwa mkono wa Mungu mwenyewe, walianza safari ya kuelekea nchi ya ahadi, ijulikanayo kama KAANANI. Iliwachukua miaka 40 kukamilisha safari yao hadi kufikia nchi ya ahadi.

Kaanani ni jina la zamani la eneo la Mashariki ya Kati, ambalo siku hizi limegawanyika katika nchi za Israeli, Palestina, Lebanoni na sehemu za Magharibi za Jordan na Syria.

Yesu alizaliwa katika Taifa Teule la Israeli

Ilipofika wakati wa ahadi ya Mungu kuuokoa ulimwengu, alimtuma mwanawe mpendwa ambaye alizaliwa katika taifa hilo la Israeli, katika uzao wa kabila la YUDA. Yesu alizaliwa Maskini lakini alikuwa Mfalme. Alikufa kifo cha aibu, lakini alipofufuka alipata heshima. Yesu alifanyika kuwa wokovu kwa Waisraeli wenyewe, pamoja na watu wa mataifa. Watu wa mataifa ni watu wa mataifa mengine yote, tofauti na taifa la Israeli.

Jina lingine la Waisraeli
Waisraeli kwa jina lingine wanaitwa WAYAHUDI. Wayahudi ndio hao hao Waisraeli. Hivyo, ukiona mahali popote wanataja Wayahudi, fahamu kuwa ni hao hao Waisraeli.

Kwa ujumla, TAIFA LA ISRAELI LILIJULIKANA KAMA TAIFA TEULE LA MUNGU, KWA SABABU NDILO TAIFA PEKEE DUNIANI KOTE, AMBALO LILIKUWA LINAMUABUDU MUNGU WA KWELI YEHOVA, ALIYEUMBA MBINGU NA NCHI.
Mataifa mengine yaliyosalia yalikuwa yanaabudu sanamu, mizimu, miti na wanadamu.
Ni Israeli pekee ndilo lililokuwa linamwabudu Mungu wa kweli. Mahsusi, lilikuwa likifuata mambo ya Mungu. Ndiyo maana likaitwa Taifa Teule.


Kijeografia, taifa hili lipo katika bara la Asia, eneo linalojulikana kama mashariki ya kati. Nchi ya Israeli ni ndogo tu, kama mkoa wa Njombe nchini Tanzania, lakini ina utajiri mwingi, japokuwa asilimia kubwa ni jangwa. Watu wake wamejaliwa kuwa na uwezo wa ubunifu na uvumbuzi.

Idadi ya waisraeli waliopo Israeli sasa hivi inakadiriwa kukaribia milioni 10. Ndiyo nchi pekee duniani yenye idadi kubwa ya maadui kuliko nchi nyingine zote, kwani imezungukwa na nchi za kiarabu pande zote, ambazo zinalipinga vikali taifa hilo.

Pamoja na maadui wote hao wanaoizunguka, lakini bado Mungu anawashindania. Ni kwa sababu ni Taifa Teule. Pia, ana kusudi nao katika siku za mwisho. Baada ya unyakuo wa kanisa kupita, Mungu atalirudia tena taifa hilo kwa nguvu na kuwapa watu wake moyo wa toba. Wayahudi wote watatubu kwa machozi na maombolezo kwa uchafu wote wanaoufanya, na kwa sababu walimsulubisha Masihi wao, na Bwana atawasamehe na kuanza kuwashindania tena kama nyakati za kale. Mataifa yote yatapanga vita dhidi ya taifa hilo, lakini Mungu atalishindia dhidi ya mataifa mengine yote.

Ukitaka kujua ni kwa jinsi gani Waisraeli watarudiwa na Mungu katika siku za mwisho, ni muhimu kusoma maandiko katika: Warumi 11:26-29, Isaya 59:20-21 na Yeremia 31:33-34.
Nimekutana na chapisho hili kwenye page ya JamiiTalk watu wamepinga hakuna taifa teule kwamba hii ni ukoloni mamboleo na utumwa wa kihistoria na kidini
 
Back
Top