Advertise here

Kocha Fadlu Awaaga Mashabiki wa Simba

Kasomi

JT Founder
1758547301310.jpg

MICHEZO: Kocha Fadlu Davids amewaaga rasmi mashabiki wa klabu ya Soka ya Simba baada ya kuhudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi miwili ndani ya klabu hiyo

Fadlu ambayeni raia wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 44 amesema amepokea upendo mkubwa sana kutoka kwa mashabiki hao tangu awasili Simba na kupata shauku kubwa ya kuipambania klabu hiyo.

“Kwa moyo mzito,nitoe shukrani zangu za dhati kwa mashabiki wa Simba, Rais Mo Dewji, wachezaji, wafanyakazi na wasimamizi wa Simba tulipigana pamoja, tukasherehekea, na tukaimarika kupitia kila ushindi na changamoto, Simba daima itabaki moyoni mwangu, na ninaitakia mafanikio mema na Asanteni Sana, Nguvu Moja” Ameandika kocha Fadlu
 
Back
Top