Otis
New member
SEHEMU 01
Yalikuwa majira ya asubuhi, Jua lilianza kuchomoza, miale ya rangi ya chungwa ilianza kugusa nyumba kadhaa, sauti ya jogoo waliokuwa wakiwika zilisikika.
"Vuu Vuu" huu ulikuwa muungurumo wa simu ya Eric, baada ya dakika kupita aliichukua simu yake na kujiegemeza kwenye kitanda, kwa haraka akafungua upande wa sms, huko alikutana na meseji ya Grace iliyoandikwa: Mbona umenisusa?
Eric aliguna na kuamka kutoka kitandani, chumba chake kisafi kilikuwa kimya kwa muda huu, kwa asubuhi huwa hasikilizi muziki wala redio, huwa anaiacha siku iende hivyo hivyo.
Baada ya kuoga na kurejea kwenye chumba chake kwa taratibu akaanza kuandaa kifungua kinywa. Muda ulipita kama dakika arobaini na tano hivi hatimaye kifungua kinywa kikawa tayari. Eric aliomba na kuisogelea meza yake ndogo na hapo aliwasha TV na kuendelea kuangalia series aliyokuwa akiiangalia kwa siku iliyopita.
"Vuu Vuu" simu iliunguruma tena, kwa haraka Eric alisimamisha series yake na kuiangalia simu, hapo alikutana na mpigaji ambaye alikuwa Grace, kwa jazba alipokea na kuweka simu sikioni.
"Eric mambo my love!"
"Poa, vipi mzima?"
"Mi' mzima, mbona unanijibu kwa haraka hivyo? Kwani unafanya nini?"
"Kwaheri"
"Aah aah, hapana, nisamehe babe wa.." hapo hapo Eric alikata simu na kuendelea kula, simu ilipigwa tena, Eric aliweka kindege (flight mode), na baada ya kumaliza kula alirejea nje na huko aliosha vyombo na kurejea ndani na hapo usingizi ukampitia.
Eric alilala kwa saa 3 mfululizo, alipoamka alimuona Grace akiwa amelala kitandani.
"Hey!"
"Umekuja saa ngapi?"
"Babe ulikuwa umelala sikutaka kukuamsha, kwani nimekosea?" sauti hii ilitoka kwa unyonge.
"Grace umeanza kunipanda kichwani, sio?"
"Hapana babe, mekumiss sana" aliongea Grace kwa kunong'ona muda huu sauti yake ya kubembeleza ilikuwa ikitoka kwa mhemo na msisimko uliomshtua sana Eric.