Dina Alivyojiunga na Anasa za Dunia Akaishia Kuharibikiwa

Dina Alivyojiunga na Anasa za Dunia Akaishia Kuharibikiwa

Dina ni nani
Katika biblia, Yakobo, Myahudi, alikuwa na wake wawili: Lea alikuwa mkubwa na Raheli alikuwa mdogo. Baba yao alikuwa ni mmoja. Dina alikuwa binti wa Lea. Dina pia alikuwa bikira (Mwanzo 34:1-31).


Moja kati ya jambo baya katika jamii yo yote ni tendo la kumdhalilisha mwanamke. Hakuna jamii inayoweza kuvumilia udhalilishaji/unyanyasaji wa kijinsia. Hata zamani unyanyasaji wa kijinsia ulipigwa vita vikali pamoja na kwamba kulikuwa na watu ambao waliendesha mfumo dume.

Maadili ya zamani yalikuwa ni rafiki kwa mabinti. Kwa sababu hiyo, unyanyasaji wa kijinsia ulikuwepo kwa kiwango kidogo sana ukilinganisha na siku hizi.

Hebu tuone kilichomtokea Dina
“Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona binti za nchi.
Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona, akamtwaa, akalala naye, akambikiri.
Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri (Mwanzo 34:1-3).

Biblia inasema “akatoka kuwaona binti za nchi”, maana yake alijichanganya na kwenda kujiunganisha/kuwasabahi mabinti wa kimataifa, mabinti wa Kanaani, mabinti wa mitaani.

Kujichanganya huko ndiko kulisababisha kubakwa kwake. Hii inaonesha kuwa hawa binti za nchi/mataifa (Wakaanani) hawakufanana kitabia na Dina. Kwa hiyo, kuna roho/mambo aliyaona au kuyapata, ambayo hakuwa nayo hapo mwanzo.

Kutoka na kwenda nje ya hema, kulifungua lango kwa adui Shekemu hata kumwona na kupanga mipango mibaya ya kubaka.

Hili ni fundisho. Ukitoka na kujichanganya na mabinti wa nchi (mabinti machachari wa mitaani), ujue utanaswa na adui. Hii ni kwa sababu umeingia kwenye eneo la adui alilo na uzoefu nalo (unaweza kusema katika hatua 18 zake).

Shekemu alikuwa hajamwona Dina kwa ukaribu na kuona uzuri wa binti wa Kiyahudi, binti mrembo. Hivyo, Dina alipojichanganya tu kwa kutoka kwenye hema lao (nyumbani kwao), Shekemu akaona fursa, naye akatimiliza lengo lake baya.

Hebu fikiria, kama Dina angeendelea kubaki hemani (nyumbani). Hivi Shekemu angembaka? Biblia inasema, "Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi" (Yakobo 4:7-8).

Maana yake ni kuwa tusimpe ibilisi nafasi. Ibilisi ni adui. Ukimpa nafasi adui, basi ujue atakukimbilia akudake kabla hujafika, na atakumaliza hapo hapo kabla hujapoa.

Siku hizi kuna visa vingi vya mabinti kubakwa kule walipoenda. Yaani wanapojichanganya tu, basi akina Shekemu hawafanyi uzembe, wanabaka bila kuchelewa. Akina Shekemu wapo wengi wa kutosha.

Hebu tujiulize. Je, unajua kuwa binti habakwi hemani (akiwa nyumbani)? Bali atabakwa akiwa nje ya hema (akiwa nje ya nyumbani kwao). Akijichanganya kwenda kwa binti za nchi, basi ujue hawezi kurudi salama.

Kisa hiki kinatuonesha kwamba mwenye makosa ni Dina binti Yakobo. Hii ni kwa sababu, bila shaka alikuwa anajua imani ya baba yake na taifa zima, kwamba ni watu wa Mungu waliotengwa na waovu. Hivyo, alitakiwa aendelee kutulia hemani (nyumbani).

Aidha, bila shaka alifundishwa maadili ya kutunza usichana wake, na ndiyo maana aliweza kuwa bikira kwa muda wote huo.
Kwa hiyo, mwenye jukumu hasa la kuzuia kubakwa ni mwanamke mwenyewe. Kwa upande wa Dina, alikosea. Yakobo baba yake, yeye alimfundisha mambo yote muhimu. Alitekeleza jukunu lake. Dina ndiye alijichanganya mwenyewe.

Shekemu adui wa Dina, baada ya kutimiza lengo lake, biblia inasema “moyo wake ukaambatana na Dina, akampenda”

Kumbuka, kumbe hata adui anayekutafuta akikupata, naye anachanganyikiwa.
Tunajifunza kitu kikubwa hapo, kwamba ikitokea binti amebakwa, au ametembea na kijana, basi ni rahisi moyo wa kijana kuambatana na binti. Katika kuambatana huku, kuna roho ambayo binti lazima apokee kutoka kwa kijana.

Ndiyo maana unaweza kuona hata leo mabinti ambao walianza vizuri na bwana. Lakini walipompa nafasi adui na kujikuta wameangukia kubakwa, au kulala na kijana, basi wanakuwa na mapepo hatari.

Biblia inasema huyu mbakaji “akawa anasema naye Dina kwa maneno mazuri” Hii ni kuonesha kwamba mbakaji tendo alilolifanya, yeye alichukulia kuwa ni la kawaida. Ni sawa na kusema alikuwa akimpooza Dina achukulie kawaida tendo la kubakwa.

Adui ibilisi naye hufanya hivyo hivyo kwa maneno, kama kwamba ni mazuri. Lakini mwisho wa maneno hayo mazuri ni mauti.

Tujifunze kutoka kwa Dina. Alikuwa ni bikira. Akafanya kosa la kutotulia hemani, yaani nyumbani kwao. Akatoka kwenda kwa rafiki zake mitaani, waliokuwa kwenye anasa za mataifa, kwenye mambo ya dunia. Akajichanganya nao. Matokeo yake, akabakwa. Akaharibikiwa.

Hata kama ni kijana wa kiume, angalia nawe usijichanagnye, usije ukabakwa, au ukabaka.

Simama na Mungu. Usihangaike na anasa za dunia. Tulia nyumbani, au tulia na mambo yako.
 
Back
Top