Kasomi
JT Founder
Watanzania wanatakiwa kufidiwa kwa hasara kubwa walizopata kutokana na kukosekana kwa huduma ya intaneti kwa muda wa siku tano mfululizo (tangu tarehe 29/10/2025) ilhali walikuwa wamelipia bando na data kutoka kwa makampuni ya huduma za mawasiliano ambayo yamekaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea.
Watoa huduma hawa - iwe ni Vodacom, Airtel, Tigo, Halotel, TTCL, au wengine wana leseni kutoka TCRA chini ya sheria ya Electronic and Postal Communications Act, Cap. 306 (EPOCA).
Sheria hii, katika Kifungu cha 18(1), inawataka watoa huduma kuhakikisha huduma zao zinapatikana saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki, kwa ubora uliowekwa na TCRA.
Zaidi ya hapo, Kanuni za Ulinzi wa Wateja wa Mawasiliano za mwaka 2018 (Regulation 3 na 5) zinatamka kwamba:
Endapo huduma haitolewi bila taarifa ya awali (scheduled notice) au bila sababu halali, mteja ana haki ya fidia inayoitwa "Outage Credit."
Kwa maneno mengine:
Kukatika kwa huduma ya intaneti kwa siku tano mfululizo bila maelezo wala taarifa ya awali ni uvunjaji wa sheria na ukiukaji wa haki za watumiaji.
Kwa hiyo, Watanzania wanapaswa kuwadai maelezo na fidia kutoka kwa watoa huduma wote waliohusika.
TCRA pia ina wajibu wa kuwawajibisha watoa huduma hawa kwa kutozingatia masharti ya leseni zao.
Hii siyo tu hoja ya bando - hii ni hoja ya uwajibikaji, haki, na heshima kwa wateja.
Credit: Alan Lucky