Advertise here

Watanzania Watoa Milioni 100 kwa Kila Goli la Stars AFCON

Kasomi

JT Founder
WATANZANIA WATOA MILIONI 100 KWA KILA GOLI LA STARS AFCON
1766770641051 (1).jpg

Kuelekea mechi kati ya Timu ya ya Taifa ya wanaume (Taifa Stars), Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Paul Makonda amesema amepigiwa simu na Watanzania mbalimbali ambao wameahidi kutoa Sh100 kwa kila goli watakalofunga dhidi ya Uganda Desemba 27 na ile ya Tunisia Desemba 30 katika mashindano ya Afcon yanayoendelea nchini Moroco.

Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wachezaji na benchi la ufundi la Stars kuelekea mchezo wao dhidi ya Uganda utakaochezwa Desemba 27, 2025.

“Kuwathibitisha kuwa Watanzania wako pamoja na nyinyi, juzi na jana nimepokea simu za Watanzania ninaowaamini na kuwaheshimu wameniambia nenda kawaambia vijana wa Taifa Stars tupo nao na kuanzia mechi ya Uganda na Tunisia Watanzania wananunua goli moja Sh100 milioni,” amesema Makonda.

Taifa Stars inakutana na Uganda na Tunisia, baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Nigeria kwa bao 2-1 mchezo uliocheza Desemba 23, 2025.
 
Back
Top