Advertise here

Mkasa wa Lwanda Magere: Utajiri Wa Nguvu Za Giza Ulivyoharibu Maisha Yangu

Simulizi

Member
UTAJIRI WA NGUVU ZA GIZA ULIVYOHARIBU MAISHA YANGU- Hiki ndicho kisa cha pili cha maisha ya Lwanda Magere, hapo mwanzo nilisema kuna visa viwili, vya Lwanda Magere cha kwanza nimeshakisimulia. Bonyeza hapa kusoma

Hivyo hiki ni kisa cha pili. KARIBUNI MJIFUNZE.

MKASA WA PILI- Sehemu ya 1.

MWAKA 2012.


Baada ya kuwa nimemaliza shule ya sekondari nilirudi nyumbani Mwanza,baada ya mama kuwa ameuza ile nyumba ya Tarime ilibidi ajenge nyumba nyingine Mwanza,japo haikuwa kubwa kama ile ya Tarime lakini kwa kiasi fulani ilikuwa nzuri naya wastani!,nilirudi nyumbani nikawa nafundisha wanafunzi tuisheni ili angalau niweze kupata hela za kununua sabuni na mahitaji madogo madogo,sikuweza tena kumuomba mama pesa maana tayari nishakuwa mtu zima,pia kwa wakati huo hali ya mama haikuwa nzuri kifedha,kuna shuke moja ambayo haikuwa ya serikali huko maeneo ya buhongwa,waliniajiri kama mwalimu wa muda na wakawa wananilipa kutoka na vipindi ambavyo nilikuwa nikihudhuria,hivyo nilikuwa nikitoka hapo shuleni naelekea ilipokuwa kituo cha tuisheni kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi masomo ya ziada,nilikuwa nalipwa na wale wanafunzi Tsh elfu 3000 kila nilipokuwa nikimaliza topic.

Basi kuna siku katika pitapita zangu mtaani wakati natoka huko shuleni,kwa mbali kidogo nikamuona jamaa mmoja tuliyekuwa tumesoma wote shule ya msingi Turwa kule Tarime,kiukweli sikuweza kufahamu kama ndiye au nilimfananisha,jamaa alikuwa pembeni anaongea na simu,hivyo nilijaribu kusogea karibu nione kama ndiye!.Kweli!,baada ya kusogea karibu nikamwita jina lake,jamaa aliitika na aliponiona alinifanyia ishara kwamba nisubiri kwanza amalize kuongea na simu,basi jamaa alipomaliza kuongea na simu alifurahi sana kukutana na mimi,mimi pia nilifurahi sana maana jamaa alikuwa kabadilika sana na kanenepa ile kishenzi,watoto wa mjini wanasema "Shavu dodo",kiukweli jamaa alikuwa kanawili,nilivyomuona tu nilifahamu lazima alikuwa na maisha mazuri.

Jamaa aliniuliza "Aisee za miaka mingi?".

Nikamjibu "Nzuri".

Jamaa akaniambia "Hebu nikumbushe wewe ni nani na nilikuona wapi vile!".

Kimoyo moyo nilijisemea "Ina maana jamaa mara hii kanisahau au ndiyo mambo ya mjini?".

Basi ilibidi nimkumbushie jina langu na tulisoma wote Tarime,jamaa alicheka sana,ndipo tukaanza kukumbushiana matukio,vimbwanga na vitimbi vya shule!,tulipiga michapo sana na nikamueleza mimi niliendelea na shule na nikamwambia Tarime tulihama muda sana.Jamaa alinichukua tukasogea mbele kidogo kumbe alikuwa kapaki gari!.Tulipanda kwenye gari kuelekea maeneo ya Igoma ambako alikuwa kachukua hoteli huko.Wakati tukiwa kwenye gari alikuwa ananiambia kwamba yeye baada ya kumaliza shule ya msingi matokeo yake hayakuwa mazuri,hivyo ilibidi aende kutafuta maisha,akaniambia yupo huko mkoani Geita sehemu moja inaitwa Katoro,kajenga huko na maisha yake yapo huko,ila siku hiyo alikuwa kaja hapo Mwanza kwa ajili ya biashara zake nyingine.Huyu jamaa kipindi tunasoma alikuwa hajiwezi kimasomo(kilaza),kiukweli ningeshangaa sana kusikia aliendelea na Shule!.

Baada ya kufika hapo hotelini alipofikia mimi nilikaa nje yeye akaingia huko ndani,muhudumu alikuja kuniuliza natumia nini lakini nilisita kumwambia maana sikuwa na kitu, mtu ambaye ndiye mwenye pesa alikuwa kaingia ndani,hivyo nisingeweza kuagiza bila ruhusa ya mtoa pesa!,baada ya dakika kadhaa jamaa alikuja kwa mbwembwe huku akiniambia "Mwanangu agiza chochote uletewe ule".


Kabla sijamuita muhudumu jamaa alipaza sauti "Wewe muhudumu njoo umsikilize jamaa hapa".Mrume ndago niliagiza wali samaki pamoja na Soda.

Jamaa aliniuliza "Vipi mwanangu upigi mambo yetu?".

Nikamwambia "Hapana kaka sipigi".

Jamaa akaniambia "inaonekana kijana ushakuwa mlokole,yaani ukorofi na utundu wote ule wa shule ya msingi hupigi huang'unywa?".

Neno "Huang'unywa" alimaanisha pombe,ndizo lugha tulizokuwa tunazitumia kipindi hicho tukiwa wadogo.Basi stori za hapa na pale ziliendelea tukiendelea kukumbushana jamaa na marafiki tuliosoma nao,baada ya kumaliza kula ilibidi nimuulize jamaa alikuwa anapiga ishu gani!,maana alikuwa kanawili sana na ukiangalia mimi wakati huo nilikuwa nimechoka ile kishenzi.Jamaa aliniambia yeye anajihusisha na mambo ya madini ila akasema isingekuwa vyema tuongee pale hilo jambo ila aliniambia nijitahidi nitafute siku niende Geita,ndani ya siku chache ili nika-experience maisha ya kule namna yalivyo.Basi baada ya hapo jamaa akanipa elfu 30 ,mimi nikamuaga ila nilimwambia sina hata simu,aliniambia nisiwaze nijatahidi nitafute siku niende huko Geita kwani angesababisha hayo yote!,Baada ya maongezi nilimuaga jamaa ili kuondoka,alinipakia kwenye gari yake mpaka mabatini kisha nikachukua daladala za kuelekea Nyegezi nyumbani!.

Kiukweli ile elfu 30 niliona kama kanipa milioni,ukizingatia nilikuwa nimepigika na maisha ile sana!,Pia nilikuwa nawaza sana,inawezekanaje mtu niliyemzidi kila kitu kuanzia akili,elimu mpaka maisha enzi hizo leo anizidi maisha?,niliumia sana lakini sikuwa nala kufanya!,sasa pale nyumbani kuna hela nilikuwa nimesevu,hivyo nikachukua na hii jamaa ambayo alinipa nikajumlisha ikawa ya kutosha japo si haba!,kesho yake ilibidi niingie kwenye mitumba kusaka nguo za kushindia hapo mtaani.Nilipata suruali mbili nikanunua na makobazi pamoja na sweta.

Baada ya wiki nilianza kuwaza namna ya kwenda Geita ili nikaonane na jamaa uenda angenipataia kazi yoyote nifanye maana niliona kama nimechelewa sana katika maisha!,jamaa kipindi tupo hotelini kule Igoma, alinipa direction ya kwamba nikifika Katoro kuna jina alilokuwa analitumia huko lilikuwa maarufu sana,hivyo alinitajia hilo jina akasema endapo nitafika hapo nikimuuliza hata watoto wangenipeleka kwake!,lile jina lake la shule ya msingi aliniambia kule hakuna aliyekuwa analifahamu bali lilikuwa limebaki kwenye vyeti vya kuzaliwa tu.

Itaendelea......................
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 2

Inaendelea.............

Ndani ya wiki kadhaa baada ya kupata pesa ilitosha kabisa kufanya nauli ya kuelekea Geita kwa ajili ya kumtafuta jamaa yangu yule;Lengo la mimi kwenda Geita ni kuangalia kama naweza kupata fursa yeyote ile ili na mimi nianze kutengeneza pesa maana nilikuwa naona nimechelewa sana katika maisha.Wakati naondoka nyumbani nilimuaga mama,wakati huo wale dada zangu wote wawili walikuwa wameolewa,yule dada yangu mkubwa alikuwa kaolewa hapo hapo Mwanza,na yule mdogo niliyekuwa nikimfuatia yeye alikuwa kaolewa huko Arusha,hivyo mama alikuwa pale nyumbani na watoto wa shangazi yangu ambao walikuwa mabinti wawili;wao walikuwa wakiishi hapo Mwanza tangu zamani hivyo tulivyohamia Mwanza baada ya dada zangu kuolewa ilibidi waje pale nyumbani kukaa na mama,shuleni walikuwa wakienda ila wakitoka wanarudi pale nyumbani.Nilimwambia mama kwamba rafiki yangu tuliyewahi kusoma naye,maisha yake ni mazuri huko Geita,sasa aliniambia nikaonane naye;mama alinikubalia ila mara zote alikuwa akiniambia “niwe muangalifu” ,hayo ndiyo maneno mara zote alikuwa akiniambia mama yangu.

Niliianza safari ya kuelekea mkoani Geita.Baada ya masaa kadhaa nilifika Geita,sasa kwakuwa jamaa aliniambia yeye anakaa Katoro ilibidi niulizie pale Geita gari zinazoelekea Katoro,nilipofanikiwa kuzipata, nililipa nauli nikajipatia tikiti tayari kwa safari.Nilifika katoro muda umeenda na hapo nilikuwa sijala chochote tangu natoka Mwanza,pale stendi ya Katoro kulikuwa na daladala (Hizi ni zile baiskeli walizokuwa wanazitumia watu wa huko maalumu kwa kubeba abiria),kwa wakati huo zilitumika sana hizi baiskeli maana bodaboda zilikuwa chache na kama zilikuwepo basi mimi sikufanikiwa kuziona hayo maeneo.Nilimfuata jamaa mmoja aliyekuwa na baiskeli ambayo ni daladala kumpatia maelezo ya jina la yule jamaa aliloniambia kwamba nikifika niulize mtu yeyote kwani anafahamika na ningepelekwa mpaka kwake,lakini yule jamaa wa daladala pamoja na maelekezo yote niliyompatia alikuwa hamfahamu yule jamaa.

Jamaa wa daladala aliniambia "Unajua hii Katoro ni kubwa vilevile pia ni ndogo,hapa kuna matajiri wengi,pia kumbuka matajiri wa huku ni nadra sana kupanda daladala maana wengi wana magari yao".

Jamaa akaendelea kuniambia "Unajua hawa matajiri wanapendelea kwenda kwenye mahoteli makubwa na mabaa makubwa kwa ajili ya starehe,sasa unaonaje nikupeleke kwenye mahoteli na mabaa maarufu ninayoyafahamu,uenda ukifika hapo na kuulizia itakuwa rahisi kumpata?”.

Kweli,tulifanikiwa kufika kwenye bar ya kwanza kuuliza,kuna jamaa alikuwa akichoma nyama akatuambia kwamba" jamaa mbona anafahamika sana ila anapoishi ndiyo sipafahamu".

Tulijaribu sana kumuomba yule jamaa mchoma nyama atuulizie pale bar uenda kungekuwa na muhudumu yeyote aliyekuwa akipafahamu kwake atupatie muongozo wa namna ya kufika.Baada ya kuona jamaa akiwa anaendelea na shughuli zake,yule jamaa wa daladala alimfuata jamaa mwingine alikuwa amekaa pembeni,ilioneka yale maeneo yeye ni mwenyeji,jamaa wa daladala alimuuliza na kwa bahati nzuri jamaa alimwambia yule jamaa ninayemtafuta mimi kuna sehemu anakaa,akamuelekeza Yule jamaa wa daladala,kwasababu Yule jamaa wa daladala alikuwa mzoefu wa yale maeneo alionyesha kutingisha kichwa ikiwa ni ishara ya kuelewa.

Basi jamaa aliporudi aliniambia "Kaa kwenye baiskeli twende".

Jamaa aliendelea kuniambia "Wewe twende mpaka yale maeneo jamaa aliyonielekeza maana tukifika hapo tunaweza kuuliza".

Tulipofika yale maeneo jamaa aliyoelekezwa tulisimama,jamaa akaniambia “sasa hebu tutafute mtu atuelekeze".

Yale maeneo yalikuwa na nyumba nzuri na kimuonekano,uenda walikaa watu wenye pesa zao.Kuna mama mmoja alikuwa anapita nilimsimamisha nikamsalimia kisha nikajaribu kumuulizia lile jina aliloniambia jamaa tukiwa Mwanza,Yule mama alionekana kumfahamu sana jamaa maana aliniuliza "wewe ni nani yake mwanangu?” .

Nilimueleza mimi ni rafiki yake;Baada ya mazungumzo ya kueleweshana,yule mama alituelekeza mtaa wa pili toka pale tuliposimama na akatuelekeza namna hata nyumba yake ilivyokuwa,nilimshukuru sana yule mama.Nilipanda kwenye baiskeli na kuelekea huo mtaa wa pili ambao yule mama alituelekeza,ile nyumba mama aliyotuelekeza niliiona na kuitambua vizuri!,kiukweli kwa muonekano tu wa ile nyumba,nilijisemea kimoyomoyo ya kwamba jamaa alikuwa na “pesa na wala si mchezo!”.

Yule jamaa wa daladala ilibidi nimwambie “ndiyo hapa,wewe sasa waweza kurudi”.

Nilimuuliza “ni shilingi ngapi?”.

Jamaa akaniambia "ni 600 tu kaka".

Nilimuuliza jamaa “mbona kama tumezunguka sana halafu bei inakuwa ndogo hivyo?”.

Jamaa alinijibu kwamba "Kwa mzunguko huwa tunabeba abiria kwa shilingi 200, kwakuwa tumefanya mizunguko 3 ndiyo unapaswa kulipia hiyo 600".

Mimi kiukweli niliona kama nimemuibia,ndipo ilibidi nimpe shilingi elfu 1000,jamaa alishukuru sana akawa ameondoka zake.Nililisogelea geti na kuanza kugonga,haukupitia muda kuna binti alifungua geti.

"Shikamoo" alinisalimia.

Nilimuitikia "Marhaba".

Sasa ilibidi nitumie jina la shule la jamaa maana nilijua haiwezekani mpaka nyumbani kwake wasilijue jina lake,niliona lile jina maarufu litakuwa ni huko mtaani tu ila kwake nadhani jina lake halisi lilifahamika.Yule binti alitingisha kichwa kuonesha ishara ya kukataa yaani jamaa hayupo.

Nilimuuliza"Nani yupo?"

Alinijibu "Yupo dada".

Nilimwamba aniitie dada yake ambaye nilifahamu ndiyo anaweza akawa mke wa jamaa;Baada ya kwenda kumuita dada yake inaonekana dada mtu alimwambia niingie ndani.Yule binti alikuja kuniambia “dada kasema karibu ndani".

Baada ya kuingia ndani ya geti yule dada aliniambia "karibu kaka,sijui nikusaidie nini tafadhali”.

Ikabidi nianze kujitambulisha "mimi naitwa Lwanda magere ni rafiki yake na.........”.

Ilibidi nimueleze kila kitu tangu tulipokutana Mwanza na yule jamaa,baada ya kuwa nimejitambulisha alinikaribisha ndani kwani aliniambia jamaa hayupo na huwa anarudi usiku,mida hiyo ilikuwa saa 10 jioni,yule dada alimwambia yule binti aniandalie chakula.Ile nyumba ilikuwa inakidhi vigezo vyote vya mwanadamu mwenye shauku ya kuwa na maisha mazuri,jamaa inaonekana aliyapatia sana maisha.Wakati nikiwa pale sebuleni yule dada ambaye alikuwa mke wake alichukua simu akampigia jamaa akamueleza ujio wangu na ndipo jamaa alimwambia “mpe simu niongee naye!”.

Yule dada alinipa simu nikaanza kuongea na jamaa,jamaa alionesha kufurahi sana,aliniambia nisiwe na wasiwasi kwani hapo ni kama kwangu tu!,alisema angerudi muda si mrefu maana yupo Geita kazini kwake.Basi baada ya kuwa nimemaliza kuongea na jamaa niliendelea kuwa mtulivu nikimsubiria.Chakula kilipokuwa tayari kilitengwa kwenye chumba maalumu cha kulia chakula(dinning room)ndipo nilisogea kuelekea kula,yule dada yeye muda wote alikuwa chumbani kwake,huku yule binti alikuwa akiendelea na shughuli zake, hivyo nilibaki mwenyewe pale sebuleni nikijiachia kama kwangu.Baada ya kumaliza kula nilielekea sebuleni kukaa kuangalia luninga.

Itaendelea...........................
 
MKASA WA PILI - Sehemu 3.

Inaendelea.............

Ilipofika mida ya saa 1 usiku nilisikia honi ya gari ikipiga kwa nje ya nyumba hivyo nilifahamu atakuwa ni jamaa karudi.Kweli!,alikuwa ni jamaa ndiye kafika,alionekana kunichangamkia sana na bila kupoteza muda alinitambulisha kwamba yule mwanamke niliyemkuta hapo kwake ndiye mke wake na yule binti alikuwa ni mdogo wa huyo mkewe.Aliniambia pia anao watoto wawili mabinti na kwa wakati ule mimi sikuwaona pale sebuleni kumbe baada ya kutoka shule walikuwa wamelala.Basi mazungumzo ya hapa na pale yaliendelea na jamaa akawa ananielezea namna yeye baada ya maisha kule Tarime kuwa magumu aliamua kutokomea huko Geita ambako aliitwa na rafiki yake,Kwahiyo baada ya mapambano ndiyo kama ninavyomuona alivyo.Mkewe baada ya kumwambia mimi ni msukuma aliniambia "Kumbe wewe niwa kwetu kabisa" .Jamaa yeye alikuwa mkurya wa Tarime.

Baada ya kupiga msosi wa usiku niliona kama ile nyumba imechangamka tofauti na mwanzo maana jamaa kama kawaida yake akaanza kupiga huang'unywa na mimi kama kawa nikakamata soda!,basi yule mke wake akawa ananishangaa mimi kunywa soda wakati wao wakipombeka!,nilimwambia sikuwahi kunywa pombe katika maisha yangu yote, alikuwa akinishangaa sana!,baada ya kuburudika sana usiku ule na stori za hapa na pale jamaa alimwambia mkewe aende akaniandalie chumba cha kulala,ndipo mkewe alimuita yule mdogo wake akamwambia "nenda kaandae chumba cha mgeni"

Yule dogo alisema "Kipo tayari dada"


Baada ya muda nilimwambia jamaa inabidi nikapumzike,ndipo jamaa aliniambia kesho asubuhi tutaondoka wote kuelekea geita akanionyeshe kazi zake zinavyofanyika,nilimkubalia ukizingatia nilienda kule ili kama ingepatikana kazi yeyote nianze kuifanya ili kujipatia kipato maana maisha ya jamaa tayari yalishanichanganya akili!.Basi niliingia chumba cha wageni ambacho kilikuwa kilikuwa na kila kitu ndani,kabla ya kulala nikaona kwanza nikaoge ili kuuweka mwili katika hali ya usafi.Asubuhi baada ya kupata kifungua kinywa jamaa alinichukua na safari ya Geita ikaanza,jamaa alikuwa akimiliki enzi hizo gari aina ya Harrier old model na hiyo ilikuwa miaka ya 2012,Kiukweli jamaa niliona kama kayapatia sana maisha!,tukiwa ndani ya gari mastori ya hapa na pale yaliendelea,alikuwa akinisimulia namna alivyompata huyo mkewe mpaka wakaoana!.

Tulivyofika pale Geita jamaa alipaki gari mahala fulani hivi akaniambia "nisubiri kidogo nakuja"

Aliingia kwenye duka moja la vifaa vya ujenzi na ilimchukua kama dakika 10 akawa amerejea,jamaa akawa ananiambia lile duka la vifaa vya ujenzi nilakwake na mara nyingi huwa anashinda hapo kama akiwahi kutoka huko kazini kwake tulipokuwa tukielekea.Tulikuwa tukielekea nje ya mji wa Geita,ilikuwa kama tunarudi Mwanza,baada ya kusonga kwa umbali mrefu hatimaye tuliikamata barabara ya vumbi kuelekea kwa ndani ndani huko!,Baada ya muda wa dakika 45 tulifika hapo kazini kwake.Kiukweli lile eneo lilikuwa kubwa na kulikuwa na watu wengi wakifanya kazi,palikuwa pamechangamka sana,jamaa aliniambia lile ndilo lilikuwa eneo analo miliki kunapofanyika kazi zake za kila siku,akaanza kunitembeza na kunionyesha namna watu walivyokuwa wakifanya kazi.Kumbe lile eneo lilikuwa linahusika na mambo ya uchenjuaji wa udongo wa dhahabu,wao kule walikuwa wanaita "Marudio",haya marudio ni ule udongo ambao migodi mbalimbali huwa wameshauondoa dhahabu,sasa yeye kumbe alikuwa akiununua anafanya kazi ya kuuozesha kwenye mashimo kisha anaufanyia process unatoa dhahabu,na pale tulipofika kumbe ndiyo ilikuwa kambi ya huo udongo maana ulikuwa umerundikwa mwingi sana,ulikuwa umetengeneza kama mlima!,Kiukweli niliamini jamaa alikuwa vizuri maana hapo kambini alikuwa kajenga nyumba fulani hivi za mabati ambazo hao wafanyakazi wake walikuwa wakiishi hapo.

Basi baada ya jamaa kuwa amenizungusha hapo nilimwambia aniajiri nami nianze kupiga kazi maana niliona kama nimechelewa sana katika maisha,jamaa aliniambia kama naweza kweli kufanya kazi,turudi kwanza nyumbani kwake tukapumzike kwa siku hiyo halafu kesho yake tungerudi wote hapo kazini.Tulirudi Geita nakumbuka tuliingia kwenye moja walilokuwa wakiuza nguo na viatu,jamaa akaninunulia jinsi mbili,mashati mawili,akaninunulia na viatu aina ya wanchoma(four angle),Kiukweli nilijiona kama mtu niliyeyapatia maisha kwa wakati huo kumbe nilikuwa msindikizaji tu!.

Tuliingia duka jingine walikuwa wakiuza simu fulani hivi zilikuwa za promosheni ya zain (Airtel),na mbele ya kioo kwa juu vilikuwa vimendikwa Zain,basi jamaa alininunulia nikasajili na laini ya Zain maana ile simu ilikuwa inatumia laini ya Zain tu!,kiukweli nilimshukuru sana Jamaa.Kweli kesho yake ilibidi nimuage yule mke wake nikamwambia ngoja nikapambane na siku si nyingi tungeonana.Tulielekea huko porini kama kawaida na baada ya kufika jamaa aliniambia kwa kuwa sina uzoefu ataniweka niwe kama kibarua ili niendelee kujifunza,ndani ya hiyo kambi kulikuwa na watu walioajiriwa rasmi na kulikuwa na vibarua,walioajiliwa wao walikuwa wakifanya shughuli zilizohitaji uzoefu lakini vibarua wengine ikiwemo mimi kazi yetu ilikuwa ni kupiga chepe kwenye udongo na kupangiwa shifti ya kuzungukia kwenye maduara ya kuozeshea udongo ili kuhakikisha mambo yanaenda sawa!,Wale jamaa walioajiliwa walikuwa wakilipwa mishahara rasmi na sisi vibarua ilitegemea kama dhahabu ingepatikana ndipo tulikuwa tunalipwa posho tu!.

Basi baada ya jamaa kuwa ameondoka alinikabidhi kwa jamaa mmoja tulikuwa tukimuita bonge ambaye alikuwa mmoja wa wale jamaa walioajiliwa,ilipofika mida ya saa 10 jioni,yule bonge aliniambia twende tukale maana ugali wa pale ni kama wa gerezani,ukiukosa muda huo wa jioni ndiyo ilikuwa inatoka,labda mpaka kesho yake tena ndiyo kulikwa na mlo mwingine.Japo nilienda kutafuta maisha lakini kiukweli hali ya pale ilianza kunitisha!,maana ugali wenyewe uliyokuwa umepikwa ulikuwa na sura mbaya sana,siunajua tena ugali wa masela unavyoga kuwa!,walikuwa wamepika na dagaa bila kuungwa nyanya,mchuzi ndiyo ulikuwa mwingi kuliko hata dagaa wenyewe!,Yaani kiukweli nilikula tu ili isije ikaonekana niilikuwa nina dharau!.Ilibidi nizoee ile hali maana sikuwa na namna,nakumbuka kila baada ya siku 7 walikuwa wanafanya kazi ya uchenjuaji kwa baadhi ya mashimo na dhahabu ilikuwa inapatikana,kwa wakati huo aliyekuwa akitulipa ni yule bonge,Pesa yangu ya kwanza kupata kwa kipindi kile ilikuwa laki moja na themanini(180000),nilifurahi sana maana ndiyo ilikuwa hela kubwa kuanza kuikamata hiyo miaka ya 2012,baada ya siku kupita nilikuwa mzoefu wa ile kazi na kuanza kupata marafiki.

Siku moja nakumbuka kuna jamaa miongoni mwa wale vibarua tuliokuwa pale alikuwa rafiki yangu sana,tulikuwa tushazoena alikuwa akipiga stori na mimi akawa anaieleza kwamba yule jamaa yangu aliyenipeleka pale ile kambi si ya kwake bali kuna mtu alikuwa akimuangalizia tu!,ilibidi nimuulize tena jamaa mara mbilimbili!,yule rafiki yangu hapo kambini akawa anasisitiza kwamba yule jamaa ile kambi si yake,yeye pale alikuwa anazuga tu.Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na kumuelewesha ya kwamba mimi sikuwa ndugu yake bali nilikuwa rafiki yake ambaye nilikuwa nimesoma naye tu,huyo rafiki yangu wa hapo kazini aliniambia yule jamaa hakuwa mmiliki wa lile eneo,bali alikuwa ni Jambazi mkubwa sana!.Kiukweli mimi mara ya Kwanza nilikataa sana na sikukubali ila huyo rafiki yangu akanisihi nisimwambie mtu maana watu wengi hapo kazini walikuwa hawafahamu ila aliyekuwa akifahamu ni yule Bonge,wengine wote walikuwa hawafahamu chochote!,rafiki yangu huyo akawa ananiambia kwamba,mwenye lile eneo alikuwa akiishi Mwanza na huwa anakuja mara moja moja kuangalia namna kazi ilivyokuwa inaendelea,huyo rafiki yangu aliendelea kuniambia kwamba,huyo mmiliki wa hilo eneo,anamiliki sehemu kama hizo za kutosha hapo Geita!.Nilirejesha mawazo nyuma maana kuna maswali kadhaa niliwahi kumuuliza jamaa akawa anaishia tu nisiwe na wasiwasi!.

Basi kweli kwakuwa nilikuwa nimezoeana na yule bonge siku moja tukiwa maeneo ya jirani mimi nikipata soda na bonge akipiga Pombe,baada ya Pombe kumkolea ndipo nilimuuliza kuhusiana na yule jamaa yangu aliyenipeleka huko kazini,bonge ndiyo aliponieleza ukweli kwamba "Yule jamaa ni Jambazi na mara nyingi ishu zake yeye na wenzie wanaenda kupigia huko Mutukula kwenye mpaka wa Uganda na Tanzania, kwa kuwa yeye aliniambia toka mwanzo kwamba wewe ni ndugu yake nikajua utakuwa unaelewa!"

Bonge akaendelea kuniambia "watu wote hapo kazini wanafahamu wewe ni ndugu yake!"


Kiukweli baada kusikia vile niliishiwa nguvu maana sasa nikaona linaweza kutokea suala lolote lile nikajumlisha na mimi wakati ndiyo hata sikuelewa chochote!.Siku hiyo ilibidi niweke vocha kwenye kile ki simu changu alichoninunulia jamaa nikawapigia nyumbani,kuna nyumba ya jirani nilikuwa nawapigia halafu wanaenda kumuita mama naongea naye!,basi walipomuita mama niliongea naye nikamueleza kazi namna zilivyokuwa ngumu,akaniambia kuna mtoto wa mama mdogo kutoka Bunda alikuwa amekuja kuniulizia pale nyumbani,alitaka kuna kazi tukaifanye huko Bunda,hivyo alipokuta sipo akawa ameondoka.
Ile taarifa ya mama ni kama ilinichanganya akili yangu,nikamwambia ngoja niweke mambo sawa kesho yake ningeanza safari ya kurudi Mwanza.

Kesho yake asubuhi nilichukua mkoba wangu nikaweka nguo zangu ambazo nyingine zilikuwa chafu,nilimuaga bonge na yule aliyekuwa rafiki yangu nikaondoka zangu kupanda gari nielekee Mwanza,japo bonge alinisihi sana nibaki ili niendelee kukomaa na ile kazi kwakuwa ilikuwa na hela lakini mimi niligoma kabisa;siku zote nilizokuwa hapo kazini,yulee jamaa yangu niliyeambiwa ni Jambazi sikuwahi kumuona tena toka aliponipeleka hapo kambini,alikuwaga akinipigia simu tu na kunijulia hali.

Itaendelea..................
 
MKASA WA PILI -Sehemu ya 4

Inaendelea.............

Safari ya kutoka Geita mjini kuelekea Mwanza ilianza,nilifika Mwanza mida ya saa 9 alasiri,kiukweli nilimshukuru sana Mungu maana niliona ilikuwa ni bahati mimi kupata taarifa zile za kazi haramu aliyokuwa akiifanya jamaa!.Baada ya kuwa nimefika hapo nyumbani kuna kiasi kidogo cha pesa nilimpatia mama,sikutaka kupoteza muda nilimuomba mama anieleze yule mtoto wa mama alikuwa kamueleza nini kuhusiana na hiyo kazi?mama aliniambia kuna namba ya simu alimwachia na akasema nitakapo rudi nihakikishe namtafuta!,Kumbe siku ambayo mimi nilimpigia simu mama,huyo mtoto wa mama mdogo alikuwa kamaliza kama siku mbili toka kaondoka kurudi Kwao Bunda.Iilibidi nimtafute dogo akaniambia kama ninaweza kwenda Bunda siku hiyo au kesho niende,kwani kuongelea ishu kama ile kwenye simu nisingeweza kuielewa vizuri,basi kulipo kucha mrume ndago nilimueleza mama kwamba inabidi nielekee Bunda kwa mama mdogo nikaonane na dogo ili nikaone kama hiyo kazi inalipa tukaifanye ili niweze kupata kipato.

Kauli ya mama yangu mara zote ilikuwa ni "Kuwa makini".

Basi nilielekea stendi ya buzuruga kwa ajili kukata tikiti kwa ajili ya safari ya kuelekea wilaya ya Bunda,mida ya saa 7 mchana nilikuwa tayari nishafika mji wa Bunda,ni mji uliyokuwa umechangamka,kulikuwa na pilikapilika za hapa na pale zilizochochewa na watafutaji,baada ya muda dogo alifika kunichukua tukaanza kuelekea nyumbani kwao,tulikuwa tukipiga stori za hapa na pale hasa ukizingatia mimi na huyo dogo tulikuwa hatukuonana muda mrefu,dogo alikuwa akinikubali sana na ndiyo maana anasema ilibidi aje Mwanza kunitafuta maana alisikia tayari nishamaliza shule,hivyo nilikuwa tu nyumbani bila kazi, hakujua kwa wakati ule kama nilikuwa nimeenda Geita.Basi baada ya kuwa tulifika hapo nyumbani kwa mama mdogo,niliwakuta ndugu zangu upande wa mama mdogo,tulisalimiana nao na kisha nilimsalimia na mama mdogo,stori za hapa na pale ziliendelea hasa ukizingatia ulikuwa umepita muda mrefu bila kuonana na hao ndugu zangu,baada ya kupita muda kidogo,yule dogo tukaelekea mitaa flani ya shule ya msingi Miembeni,japo pia mama mdogo mitaa aliyokuwa akikaa ni huko huko Miembeni lakini haikuwa jirani na shule,Kuna nyumba moja tuliingia tukamkuta jamaa mmoja alikuwa akiongea kiswahili chenye rafudhi ya Kikenya,ilitosha kuonyesha kabisa yule jamaa hakuwa mtanzania bali alikuwa Mkenya!.Mazungumzo yakaanza pale na yule dogo alinitambulisha kwa jamaa kuwa mimi ni mtoto wa mama yake mkubwa.Jamaa pia alijitambulisha kuwa anaitwa Gachui n hapo Bunda alikuwa kaja kwa kazi moja tu,akaniuliza "bila shaka dogo atakuwa amekwambia".

Mimi nikasema "hapana kaka sijaambiwa kitu chochote".

Alimgeukia dogo na kumuuliza "Mbona hujamwambia jamaa yako".

Dogo alimjibu "Mimi sikutaka kumuelezea kitu bro niliona nije kwako maana ndiye unaelewa namna mchongo ulivyo na bila shaka ataelewa zaidi kuliko ningemueleza mimi".

Yule Mkenya akamwambia "Nyie watanzania mko na maneno mingi sana!".

Yule jamaa aliongea rafudhi ya Kiswahili cha Kikenya ambacho kilimfanya maneno mengi kutoyatamka kwa ufasaha.Basi jamaa akaanza kutuelezea tena ule mchongo namna ulivyo,kwamba kuna kampuni huko Kenya ambayo walikuwa wanahusika zaidi na pesa za zamani,zikiwemo pesa za sarafu na noti!,sasa akawa anasema kwamba,amekuja Tanzania kama wakala wa hiyo kampuni na lengo la yeye kuwa pale ni kuitafuta sarafu ya shilingi 100 ya mwaka 1993,jamaa alikuwa anasema hiyo sarafu ilikuwa inahitajika kama vile Almasi!.Jamaa akatuambia hiyo sarafu ingepatikana,basi tulikuwa tunapewa Tsh milioni 100.Kiukweli niliona kama maigizo lakini ndiyo maelezo jamaa aliyotupatia,nilimuuliza maswali kadhaa ya kujiridhisha ili kwamba atuhakikishie kama kweli tukipata hiyo sarafu tungelipwa na hiyo kampuni hizo hela au ilikuwa janja janja tu za matapeli wa mjini?.

Jamaa alituambia endapo tungepata hiyo sarafu,kabla ya mambo yote zingewekwa hizo pesa kwenye akaunti na tukishajiridhisha ndiyo nasi tungeitoa hiyo sarafu.Maelezo yake kidogo kama yaliniingia akilini na jamaa akasema yeye si tapeli maana alikuwa katoka Kenya kuja Tanzania kufanya hiyo kazi tu,baada ya kuondoka pale kwa huyo mkenya nilihitaji kufahamu siri ya ile sarafu ya 100 ya mwaka 1993 ilikuwa ni nini?.
Tulipofika nyumbani nilijaribu kumshirikisha mama mdogo naye akaniambia "Tayari mwenzio alishaniambia mwanangu".

Ndipo nilimuuliza siri ya ile sarafu ya ilikuwa ni nini?,mama mdogo aliniambia siri ya hiyo hela kiukweli haijui ila anachofahamu hiyo sarafu ya 100 ya mwaka 1993 kipindi fulani waliitumia kama dawa!.

Mama mdogo alisema "miaka fulani ulikuwa ukiumwa na nyoka au ng'e au kitu chochote chenye sumu ulikuwa ukichanja na wembe yale maeneo ulipong'atwa na ukiiweka ile shilingi 100 basi ilikuwa ikinata kama sumaku na kunyonya sumu yote,na endapo sumu ingeisha mwilini basi ile sarafu ilianguka chini yenyewe ikiashiria kwamba sumu imeisha!".

Akaendelea kusema "miaka ya karibuni hizo sarafu zimeadimika sana,pia zilikuwaga nzito sana tofauti na hizi za sasa,ulikuwa ukiichukua sarafu ile ukilinganisha na sarafu ya sasa hazilingani kabisa kwa uzito".

Basi baada ya maelezo yale ya mama mdogo kiukweli nilianza kupata mwanga,Mama mdogo alituambia hizo hela za zamani kuna mzee anamfahamu aliwahi kupata shilingi 10 za zamani zilikuwa zinatafutwa na yeye alikuwa nazo 2,hivyo yule mzee alilipwa milioni 10,Hivyo mama mdogo alituelekeza kwa huyo mzee twende tukamuulize labda angetusaidia kupata angalau mwanga kidogo!.Basi mimi na yule dogo tulielekea maeneo fulani panaitwa Balili,kiongozi wangu alikuwa yule dogo maana mimi mitaa nilikuwa siifahamu,Kweli baada ya kuwa tumefika ile mitaa ambayo mama mdogo alimpatia yule dogo maelekezo,tulimuulizia yule mzee kwenye hayo maeneo na tukaelekezwa mpaka kwake,tulipofika hapo kwenye huo mji wake tulimkuta mzee mmoja wa makamo tukamsalimia,dogo akajitambulisha na akamueleza sisi ni watoto wa mama.......,Yule mzee alikuwa akimfahamu vizuri mama mdogo,hivyo haikuwa taabu sana kujieleza,ilibidi nianze kufunguka,Yule mzee akatuambia hiyo nyumba anayokaa yeye na familia yake waliijenga baada ya kupewa pesa kiasi cha shilingi milioni 10 miaka kadhaa nyuma iliyopita kwani walitokea watu fulani kipindi hicho wakawa wanatafuta shilingi 10 zamani na kwa bahati nzuri yule mzee anaseman alikuwa nazo 2 ndiyo kupewa hiyo milioni 10!.

Yule mzee alitupatia maelekezo kama ya Mama mdogo aliyotupatia kuhusu hiyo sarafu ya 100 na akasema "si nyinyi peke yenu mnaoitafuta bali kuna watu kadhaa nimekutana nao wakitafuta hiyo shilingi 100".

Basi nikajisemea "kumbe hii ishu iko very serious!".

Yule Mzee alitushauri ya kwamba kwa hapo mjini tutapoteza muda hatutaambulia chochote,mzee akasema "nendeni vijijini na ikiwezekana kwa waganga wa kienyeji maana wale huwa wanakuwaga na kila pesa ya miaka ya zamani".

Hilo wazo la mzee lilituingia akilini,Yule mzee akatuambia twende wilaya ya Musoma vijijini sehemu moja inaitwa Bukima,akatuelekeza kwa Mganga mmoja ambaye alikuwa ndugu yake,kwamba tukifika hapo Bukima center tuulizie hilo jina alilokuwa ametutajia,tutakapofika kwa huyo mganga akituuliza tumtaje huyo mzee kwamba ndiye aliyetuagiza hapo kwake na tumueleze shida yetu!.Basi tulirudi nyumbani kujipanga kwa ajili ya safari ya kuelekea Bukima.

Itaendelea................
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 5

Inaendelea.............

Kulipokucha ilitubidi tuamke mapem maana tuliambiwa kupata magari ya huko Bukima ilikuwa inatupasa tupitie Musoma mjini ambako ndiko tungepata usafiri,ilibidi tukae barabarani kusubiri Hiace zilizokuwa zinaelekea Musoma,kiukweli mpaka wakati huo mfukoni nilikuwa nina Tsh elfu 48 tu,nauli ya kutoka Bunda kwenda Musoma kwa wakati huo ilikuwa elfu 3 hivyo nilivyolipia naulia ya watu wawili nilibakiwa na elfu 42,basi safari ikaanza na ilituchukua kama saa 1 hadi kufika Musoma.Tulipofika pale stendi ya Musoma hatukutaka kupoteza muda maana tuliambiwa huwa kuna gari moja la kuelekea huko Bukima,endapo tungelikosa hilo gari ingetubidi tulale!,kuna basi moja tulilikuta stendi likiwa limechoka sana!,ilikuwa ni aina fulani ya magari ya zamani,ilibidi sasa nikaulizie nauli ya kuelekea huko Bukima ilikuwa ni kiasi gani,tulimkuta mtu mmoja ambaye alijinasibu kwamba ndiye Konda wa lile gari,akatuambia nauli ya kutoka Musoma mpaka huko tulipo kuwa tunaenda ni elfu 5,ila huyo konda akatuambia hilo gari litaishia njiani,akasema kuna kijiji kinaitwa Mrangi ndiyo wao wangeishia hapo,ilibidi nimuulize kutoka hapo Mrangi mpaka Bukima kulikuwa na umbali gani?.

Jamaa alisema hakukuwa mbali sana,alituambia tungefika Mrangi angefanya namna ili sisi tuendelee na safari,jamaa alisisitiza sana kwamba kwa wakati huo pale stendi hakukuwa na gari lingine la kuelekea huko Bukima,hivyo tupande lile gari kisha tungefika Mrangi angetutafutia usafiri wa kuelekea Bukima.Basi nilitoa elfu 10 nikampa yule konda,baada ya kumpa akasema" Gari itaanza safari saa 5 asubuhi hivyo kama mnzunguka nyie zungukeni ila msiende mbali sana!".

Kwakuwa tulitoka Bunda bila kupata chochote kitu nilimwambia dogo twende tukatafute sehemu wanauza chai tunywe.Kwa bahati nzuri tulipozunguka nyuma ya stendi kulikuwa na mama akichoma vitumbua,hivyo tulikaa hapo tukaagiza na chai tukaanza kunywa!,wakati huo mfukoni nilibaki na elfu 30.Hapo kwenye chai tulitumia elfu 2,baada ya kupata chai na vitumbua nikamwambia dogo tusikae sana mbali maana hatukuwa wenyeji hapo Musoma,Masaa yaliposogea ilibidi na sisi tusogee kwenye gari na baada ya muda ule aliyotuambia konda kufika gari lilianza kuondoka,watu walikuwa wengi kwenye gari na wengine walisimama,yawezekana uenda gari lilikuwa lile tu maana yangekuwepo mengi watu wasingesimama na kubanana kiasi kile.Ilikuwa ni safari ya muda mrefu sana,Kuna jamaa alikuwa amesimama kando yangu nilimuuliza hiyo safari huwa inachukua muda gani hadi kufika,jamaa aliniambia kwamba,kwasababu lile gari lilikuwa likisimama simama sana njiani,ingetuchukua takribani saa 2 : 30 hadi kufika hapo Murangi.Baada ya saa 3 njiani,hatimaye lile gari lilifika hapo Murangi,tuliteremka nikamfuata dereva nikamueleza kwamba sisi tulikuwa tunaenda Bukima na yule jamaa aliyekuwa anakata tikiti alituambia tukifika hapo angetufanyia namna ya kufika huko Bukima.

Yule dereva alisikitika sana akawa anasema"Yule jamaa ni mpumbavu,kwanini akuwaambia kwamba kulikuwa na Hiace ya Bukima?".

Jamaa akaendelea kusema "Maana kutoka hapa mpaka Bukima bado kuna umbali,lakini subirini kuna watu hapa niongee nao huwa wanakodisha baiskeli kama vipi wawapeleke,japo itachukua muda kwasababu ni mbali".

Jamaa alituitia vijana wawili akaanza kuongea nao kwa lugha ya kwao,wale jamaa wakamwambia yule dereva kwa kilugha kwamba tuwalipe elfu 5 wote wawili!,hatukuwa na namna ilibidi niwape ile hela wakatuchukua mimi na dogo kila mmoja kwenye baiskeli yake na safari ikaanza,hiyo ilikuwa yapata saa 9 alasiri,safari ilikuwa ndefu kidogo na tuliingia hapo Bukima mnamo saa 10 kasoro.Tulivyofika hapo Bukima hatukupoteza muda,ilibidi sasa tuanze kumuulizia yule mganga tuliyeelekezwa na yule mzee wa Bunda,Kwa bahati nzuri huyo mganga hakuwa mgeni sana hapo Bukima,tulianza safari ya kuelekea kwake tukiongozwa na dogo mmoja tuliyemkuta pale center ya Bukima,Kwa kuwa tulikuwa wageni watu walikuwa wakitushangaa sana,nadhani kwakuwa ilikuwa mji mdogo hivyo watu au wenyeji wengi walikuwa wakifahamiana,hivyo kwa wageni ilikuwa ni rahisi sana kufahamika!.Tulifanikiwa kufika kwa huyo mganga,alikuwa akiishi nje ya mji na ilikuwa karibu na ziwa Victoria,ulikuwa ukikaa nje ya nyumba ya huyo mzee,ziwa lilionekana umbali wa mita 300 hivi!,tulimsalimia mzee na tukajitambulisha kwake,tulimueleza ya kwamba tuliagizwa kwake na mzee yule wa Bunda,kiukweli alionyesha kumfahamu yule mzee na alikuwa akituuliza hali ya maisha yake na familia yake.
Baada ya mazungumzo kadhaa ilibidi tumueleze kilichokuwa kimetupeleka hapo kwake.Baada ya kutusikiliza kwa muda mrefu alituambia ya kwamba kuna watu fulani waliwahi kwenda hapo kwake miaka 2 iliyopita na wao walikuwa wakitafuta zile pesa zilizokuwa na tundu katikati,kwakuwa kwa wakati huo alikuwa nazo ilibidi awape na walimpa pesa,alituuliza endapo hiyo sarafu ya 100 ya mwaka 1993 ingepatikana tungempa kiasi gani?,kiukweli moyo ulipiga Paaah!,kichwani mwangu nilikuwa naamini ya kwamba sasa naenda kuuaga umasikini na utajiri ulikuwa ushafika mlangoni,kazi iliyokuwepo ni kufungua tu mlango uingie ndani!.
Nilimwambia mzee endapo tungeipata ile sarafu,basi tungempa laki 2,Yeye alituuliza "Nyinyi mkiipata mnaenda kupata bei gani?".

Ilibidi nimdanganye Yule mzee kwamba "Sisi tumeambiwa tukiipeleka hiyo sarafu tunalipwa milioni 1, hivyo endapo tukikup wewe hiyo laki 2,sisi tungebaki na laki 8 ambayo tutagawana na mwenzangu maana kuna gharama pia zimetumika mpaka kufika hapa kwako".

Basi yule mzee alisema funguo za Sanduku ambamo zimo hela mbalimbali za miaka ya nyuma anazo mke wake ambaye kwa wakati ule hakuwepo,alituambia tumsubiri mpaka atakareje na akatusihi ya kwamba kwakuwa jioni ilishaingia hatuna budi tulale pale,basi mimi na dogo ilibidi twende ziwani tukashangae huku tukibadilisha mawazo,ilipofika saa 12 jioni tulirudi hapo nyumbani kwa huyo mzee,siku hiyo yule mzee alichinja Bata kwa ajili ya kitoweo!.Yule mzee kiukweli sikuona uganga wowote aliyokuwa nao maana hata pale kwake hatukukuta watu bali walikuwa watu wa familia yake!,nadhani kama alikuwa mganga basi ni wale wasiyokuwa na mbwembwe nyingi.Jioni ile mkewe alirudi akiwa na baiskeli kafunga mzigo nyuma,alipokewa na kijana wake mmoja tuliyemkuta pale,Kwakuwa sasa usiku ulishaingia mzee alituambia zoezi lingefanyika kesho yake asubuhi.
Usiku ule tulikula ugali wa muhogo na nyama ya Bata,kiukweli chakula kile kilikuwa kitamu sana!,baada ya chakula ilibidi kile chumba alichokuwa analala yule kijana wa yule mzee tulale sisi na yeye nadhani alienda kulala kwa jirani au marafiki zake,Kama mjuavyo tena mambo ya vijijini,suala la wapi pa kulala huwaga halisumbui,Siyo kama mjini.

Itaendelea...................
 
MKASA WA PILI -sehemu ya 6

Inaendelea.............

Asubuhi tuliamka tukaanza kusalimia wenyeji,Mzee alipoamka kumbe alidamka asubuhi na mapema kwenda ziwani kwenye samaki,Kumbe licha ya kuwa mganga kama tulivyoambiwa lakini biashara au kazi nyingine aliyokuwa akiifanya yule mzee ni kulangua samaki na kuwauza kwa wateja mbalimbali!.Kwahiyo ilibidi tumsubiri mpaka atakaporejea kutoka ziwani,asubuhi hiyo tulipoamka tulielekea ziwani kuoga kisha tulirudi hapo nyumbani kwa mzee,kuna binti mmoja wa yule mzee alikuja kutukaribisha twende tukale,mimi nilijua uenda ingekuwa uji maana nilijua watu wa vijijini wao na chai ilikuwa ni mbalimbali!.Baada ya kuingia mle ndani tukakutana na bonge la ugali,Samaki na vipande vya bata kwenye bakuli,yule bata alikuwa ni yule tuliyemla usiku akabaki sasa tulipakuliwa ili tummalizie kabisa!.

Kwanza nilibaki nimeshangaa maana sikuwahi kula Ugali asububi,katika maisha yangu yote nilishazoea kunywa chai au uji,ilibidi nimuulize yule dogo kama alishawahi kula Ugali asubuhi.

Dogo akaniambia "Mbona bro haya mambo ya kawaida sana".

Basi sikuwa na namna ilibidi tulianzishe,kiukweli ule Ugali ulikuwa mtamu sana,japo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kula ugali asubuhi,nilitamani niendelee kubaki huko ili niwe napikiwa kila asubuhi,kiukweli nilipenda sana maisha ya wale watu.Baada ya kuwa tumemaliza kula tukiwa hapo nje tunapunga upepo,yule mzee alirejea kutoka huko ziwani kwenye biashara zake za samaki,na yeye kama kawaida alitengewa chakula akaanza kula,alipo maliza kula alileta lile sanduku lililokuwa na zile fedha za zamani pale,akalifungua na kuanza kusaka ile sarafu ya 100 ya mwaka 1993,mzee aliendelea kutafuta kwa makini sana,Kuna shilingi ishirini ya zamani ambayo sikuwahi kuiona kabla lakini siku hiyo niliiona hapo kwa huyo mzee,mzee aliendelea kutafuta lakini hakukuwa na mafanikio yeyote,sarafu zilikuwemo nyingi lakini ya 1993 haikuwemo.

Baada ya kutafuta sana na kwa umakini mkubwa Mzee akatuambia hiyo hela tuliyokuwa tunaitafuta haikuwepo!,kiukweli moyo wangu uliuma sana lakini nikajipa moyo maana ilikuwa bado ni mapema sana kukata tamaa,ndio kwanza hata wiki ilikuwa haijaisha.Basi yule Mzee akatuambia ili tusiendele kupoteza muda kuna mtu alikuwa anafahamiana naye,naye alikuwa anafanya kazi za kuagua kama yeye,akatutaka twende kwa huyo mtu,lakini kabla ya kutupatia maelekezo ya huyo mtu na anakopatikana aliniomba simu yangu akaingiza namba za huyo mtu akaanza Kumpigia,alipompata walikuwa wanaongea kwa kilugha,Baada ya maongezi mzee akatuambia yule mzee mwenzie amesema twende na yeye pia anazo hela za zamani tukaangalie uenda anaweza akawa nayo!.Mzee alituambia huyo mzee mwenzie anapatikana kijiji kimoja kinaitwa Saragana,alituambia tukifika hapo kijijini tutampigia simu,kwakuwa namba yake alikuwa keshamaliza kuongea naye muda si mrefu akanitaka niisevu ili iwe rahisi kumtafuta.

Nikamuuliza yule mzee "tutafikaje huko kijiji cha Saragana?".

Mzee alisema "kuna baiskeli hapa kijijini za kukodi,ngoja niwaite vijana 2 ili muelewane nao wawapeleke".

Yule Mzee alituitia kijana mmoja tukaongea naye akasema "ngoja nikamuite mwenzangu ili tuelewane kwa pamoja tuwapeleke!"

Wale jamaa wakasema kutupeleka kijiji cha Saragana kwa kuwa ni mbali tuwape elfu 10 kwa wote wawili,basi kwakuwa mpaka muda huo nilikuwa nina elfu 25,ilibidi niwape hiyo elfu 10 nikabaki na elfu 15,ilibidi tuanze safari ikiwa mida ya saa 5 asubuhi,Kiukweli ile safari ya kuelekea kijijini Saragana ilinichosha sana maana palikuwa mbali sana!,Kuna muda niliona kama wale vijana kuwapa ile elfu 10 ni kama nilikuwa nimewadhurumu!,sikuwa na namna maana sikuwa na hela nyingine zaidi ya ile elfu 15.Tulipokuwa tukifika kwenye milima ilitubidi tushuke tusukume baiskeli mpaka sehemu tambarare ndiyo tuendelee na safari.Ile safari ilituchukua kama masaa 6,Kuna njia jamaa walikuwa wanatupitisha za porini ambazo walidai wao ndiyo njia za karibu,walikuwa wanasema tungefuata barabara moja kwa moja ingetuwia vigumu kufika mapema.

Tuliingia hapo Kijiji cha Saragana mida ya saa 11 jioni,tulikuta kulikuwa na mnada na kuna baadhi ya wafanyabiashara walikuwa wameanza kufungasha mizigo maana sasa jioni ishaanza kuingia,tulivyofika hayo maeneo ilibidi nimpigie yule mzee na bahati nzuri alipokea simu,baada ya kupokea simu nilianza kusikia sauti ya kilevi,ilionyesha yule mzee alikuwa amekunywa pombe!,baada ya kumulekeza tulipokuwa tumesimama alikuja akatuchukua kuelekea kwenye vibanda vya hapo mnadani!,Mzee akaanza kuongea mambo mengi nikajua tu tayari atakuwa amelewa pombe!,inavyoonekana alikuwa hapo mnadani muda mrefu akilewa pombe,basi nikamwambia dogo "hapa hakuna kitu maana huyu mzee mwenyewe kalewa hatotuelewa!".

Yule Mzee akaanza kututambulisha kwa wazee wenzie waliyokuwa hapo kwamba sisi ni wanaye!,Kumbe mzee wakati sisi tukiwa pale tunashangaa alikuwa kaagiza pombe fulani hivi walikuwa wanawekewa kwenye makopo makubwa,kibaya zaidi akaagizia na wenzie waliyokuwa watatu halafu akamwambia mama muuzaji kwamba "Yule kijana wangu aliyesimama pale atakupa hela".

Kiukweli nilighafirika sana hasa ukizingatia kilichotupeleka hapo ni kitu kingine halafu yeye analeta habari za pombe tena!,basi baadae yule mama muuza pombe alinifata akasema nimpe hela yake maana wao wanataka kufunga,sikuwa na namna ilibidi nilipe,nilimpa elfu 5 akiniletea chenji ya elfu 2,kwa maana hiyo yule mzee na wenzie walikunywa pombe ya elfu 3,ile elfu 2 ilibidi nimpe dogo nikamwambia akanunue miwa alete tutafune wakati huo tunaangalia cha kufanya!,basi haukupita muda dogo akaja na miwa miwili iliyogharimu elfu 1,ile elfu 1 nyingine iliyobaki ikabidi niirudishe mfukoni.Baadae wazo likanijia ya kwamba nimpigie simu Yule mzee wa Bukima nimweleze hali halisi ya mzee mwenzie,nilipomueleza mzee alisikitika sana akasema kwamba nimpe simu aongee naye,inavyoonekana yule mzee wa Bukima alimgombeza sana yule mzee mlevi,maana alikuwa amekaa kimya hata kujibu hajibu!.Baada ya mazungumzo yale nilimwambia mzee wa Bukima kwamba inabidi turudi Bunda maana mzee ambaye ilibidi atusaidie ndiye huyo kalewa chakari,wazo lilikuja kwamba hayo magari ya minadani ndiyo ambayo tutarudi nayo,nilimwambia dogo tuanze kuzungukia yale magari tuulize yalikuwa yakienda wapi ili kama tukipata la Bunda tuongee nao tuwalipe tujiandae kwa safari!.

Kiukweli tulizungukia yale magari na yote baada ya huo mnada wa hapo kijijini Saragana yalikuwa yakielekea sehemu moja inaitwa Kiabakari maana siku iliyofuata kulikuwa na mnada huko,nikamuuliza dogo hapo Kiabakari na Bunda kulikuwa na umbali gani?,dogo akasema ilikuwa ni mbali sana ila akasema kuna unafuu maana ni njiani hivyo kupata Hiace ilikuwa simpo!,ikabidi nimfate tena dereva wa lori moja lililokuwa hapo jirani nikamuuliza kutoka hapo Kijiji cha Saragana mpaka Bunda kulikuwa na umbali gani?,jamaa akasema si chini ya km 30!,Kiukweli nilichoka sana maana nilitaka endapo ingekuwa karibu tutembee kwa miguu!,ikabidi nimuulize dogo tunafanyaje?.Dogo kuna wazo alitoa nikaona kama lilikuwa na mantiki.

Dogo alisema "Tupande gari zinazoenda kiabakari tukifika huko kwakuwa pia ni vijijini tutaendelea kuitafuta ile shilingi sarafu uenda tungefanikiwa kuipata".

Nimuulize dogo "Usiku huu tulala wapi?".

Dogo akasema "haya magari moja wapo tutakalo panda tutalala humohumo kwenye mizigo".

Ilibidi iwe hivyo kama dogo alivyoshauri!,Kuna muda nilikuwa ninachoka lakini najipa moyo nikiamini siku si nyingi naenda kuwa tajiri!,kuna gari tuliipata na dereva akasema tutampa elfu 6 kwa wote wawili mpaka huko Kiabakari,mfukoni nilibaki na balansi ya elfu5 ,baada ya kuwa wamemaliza kukusanya mizigo tulifanikiwa kuondoka hapo mida ya saa 1 usiku kuelekea Kiabakari!.

Itaendelea.....................
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 7.

Inaendelea.............

Safari ilianza hiyo mida ya 1 Usiku kama kawaida na sisi tulikaa nyuma ya lile lori kwenye mizigo,lile lori lilikuwa halijabeba watu wengi maana jamaa walisema askari wa barabarani walikuwa wakiwasumbua sana endapo wakibeba mizigo na abiria kwa pamoja,hivyo magari ya abiria yalikuwa yametangulia halafu hayo ya mizigo yalikuwa ya mwisho,hivyo yule dereva alituambia tuhakikishe tunapata upenyo wa kukaa ambako si rahisi kuonekana kirahisi.Mimi na dogo tuliendelea kutafuna miwa yetu tuliyoinunua hapo mnadani maana tulifahamu kwa usiku huo tusingekula na hiyo miwa ndiyo ingekuwa chakula chetu!.Safari ilisonga kwa muda sana na tuliingia pale Kiabakari yapata saa 6 usiku,kwakuwa hatukuwa napa kwenda ilibidi tulale mle kwenye lori,mimi kichwani niliwaza ya kwamba pakipambazuka tu,ni kutafuta usafiri na kurudi Bunda maana hata hela ilikuwa imetuishia,mfukoni nilikuwa nimebaki na elfu 5 tu.

Asubuhi kulipokucha mida ya saa 12 asubuhi ilibidi tushuke kwenye lori maana jamaa walisema muda si mrefu wao walikuwa wakielekea mnadani.Nilimwambia dogo tukae hapo barabarani tusubirie garu zilizokuwa zinatoka Musoma tupande twende Bunda.

Dogo alianza kuniambia "Inamaana bro umekata tamaa?".

Nilimgeukia dogo nikamwambia "Hapana".

Dogo aliniuliza "Sasa kama hujakata tamaa tunarudi Bunda kufanya nini?,jana tulikubaliana kwamba tukifika hapa Kiabakari tuanze kuitafuta ile hela maana huku ni vijijini uenda tukaipata".

Kiukweli ilibidi nimwambie dogo pesa niliyokuwa nayo imeisha na hata nguo hatukuwa naza kubalisha,Yule dogo ilionekana anatamani sana kuipata ile sarafu maana alisema "Nguo kitu gani bro,mbona tutanunua nyingi tu endapo tukifanikiwa kuipata hiyo hela!".

Kuna muda nilikuwa nakata tamaa lakini dogo alikuwa akinipa morali na hali ya kuendelea kuisaka ile sarafu ya 100 ya mwaka 1993,basi nilimwambia dogo "Hapa mfukoni nina elfu 5 tu,twende tutafute sehemu tunywe chai na nyingine niweke vocha nimpigie mama Mwanza maana nina muda sijaongea naye!".

Yale maeneo ya hapo Kiabakari kulikuwa kuna wafanyabiashara wa mazao mbalimbali na hasa ndizi na nyanya.Dogo aliniambia "Bro tununue ndizi mbivu tule maana hapa ni nyingi sana na bei ni chee,kisha tukishushia na maji ya kunywa naamini itatusaidia maana chai inawahi kuisha tumboni".

Kuna mama mmoja alikuwa akiuza ndizi hayo maeneo tulimuita aje atuuzie,tulimsalimia kisha nikamuuliza "ndizi unauza bei gani?".

Yule mama alisema "Hiki kibeseni chote nipeni elfu 2500 wanangu".

Kiukweli zile ndizi zilikuwa ni nyingi sana halafu zilikuwa kubwa!,ilibidi nimuulize vizuri ni kweli ni 2500 au kakosea kutamka?,Yule mama alisisitiza hiyo ndiyo bei,nilichomoa ile elfu 5 mfukoni nikampa yule mama kisha akaturudishia chenji,ilibidi nimwambie dogo akanunue mfuko wa rambo wa 500 ili tuweke zile ndizi kwa maana zilikuwa nyingi,nikamwambia aniletee na vocha ya Zain (Airtel) ya 500.Wakati dogo akiwa kaenda dukani nilimuita yule mama aliyetuuzia ndizi nikawa namuuliza yale maeneo kama tungeweza kumpata mganga.

Yule mama aliniuliza "Kwani mlikuwa na shida gani wanangu?".

Kwa wakati ule sikutaka kumficha kitu yule mama ilibidi nimueleze kila kitu kuhusu ile sarafu,Mama aliniambia kwamba kwa waganga wa hapo Kiabakari hakuona kama tungeweza kuipata hiyo sarafu,Yule mama aliniambia kuna mganga ambaye yeye huwa anamsaidia kwenye mambo yake ikiwemo biashara zake na hakuwa hapo bali alikuwa anapatikana maeneo ya Ikizu,mama akasema uenda anaweza akawa nazo!,nilimuuliza yule mama kutoka hapo Kiabakari mpaka huko Ikizu kulikuwa na umbali gani?.

Yule mama aliniuliza "Kwani haya maeneo wewe ni mgeni mwanangu?".

Nilimjibu "Ndiyo".

Wakati tunaongea na yule mama bahati nzuri dogo naye akawa kafika,akachukua zile ndizi akaziweka kwenye mfuko,nilimsimulia yule dogo jinsi yule mama alivyokuwa ameniambiania.Dogo akasema "Huko Ikizu mpaka turudi tena Bunda ndiyo tunapanda gari za kuelekea huko".

Yule mama alisema "Huko Bunda ni mbali sana,ukiwa hapa kwenda Ikizu mbona ni jirani tu wanangu?".

Alituambia kuna njia moja ambayo tungeipita kisha tungetokezea kijiji cha Butiama halafu tungeikuta njia kubwa ambayo inaelekea Ikizu.Basi yule mama alitoa simu yake aliyokuwa ameiweka kwenye matiti akawa anaitafuta namba ya yule mganga aliyesema yupo huko Ikizu,alipoipata alinitajia namba akaniambia kama nina salio nimpigie yeye aongee naye,niliichukua ile vocha aliyonunua dogo nikajiunga dakika za kutosha kisha nikaanza kumpigia yule mganga,Simu ilipokuwa ikiita nilimpa yule mama nikamwambia "Inaita,Ongea naye".

Yule mama alianza kuongea naye kwa kilugha na alimueleza kila kitu kuhusu sisi.Yule mganga alimwambia yule mama anipatie simu niongee naye,mganga aliniambia endapo kama hiyo sarafu ingepatikana hapo kwake tungempatia shilingi ngapi?,ilibidi nimwambie dau kama nililomwambia yule mzee wa Bukima lakini yule mganga akasema hilo dau ni dogo sana tuongeze dau,baada ya kusikia ile kauli ya mganga nilijipa moyo sana,nilijua uenda yule mganga angekuwa na ile sarafu maana kama asingekuwa nayo asingeniambia kwamba lile dau lilikuwa dogo.Nilimuuliza yule mganga aseme yeye alikuwa anataka shilingi ngapi?,yule mganga alitamka kwamba tumpatie laki tatu.Nilicheka kimoyomoyo nikajisemea "laki tatu kitu gani wakati sisi tunapata milioni 100!".

Basi tulikubaliana na nikamwambia tunaanza safari ya kuelekea huko kwake na muda wote apatikane hewani,baada ya kuwa tumekubaliana tukamshukuru sana yule mama,alitueleza ya kwamba tulikuwa waungwana ndiyo maana na yeye alionyesha ushirikiano kwetu,alituambia ngoja kwanza akachukue ndizi nyingine ili aje atuonyeshe njia fupi ambayo isingekuwa rahisi kupotea.Wakati huo dogo alishauri tuanze kula zile ndizi ili tutakapoianza safari iwe rahisi kutembea,tulikula zile ndizi na kwa namna zilivyokuwa nyingi nyingine zilibaki nikamwambia dogo tutakula mbele ya safari!,tulipomaliza kula ndizi kuna kibanda kilikuwa maeneo ya hapo jirani walikuwa wanauza chai tuliingia kuomba maji ya kunywa tukapewa kwenye jagi.Kiukweli nilishiba sana kwa wakati ule maana zile ndizi hazikuwa za mchezo hata kidogo.

Namshukuru sana Mungu maana hii safari ya kutafuta maisha ilinifanya nikayafahamu maeneo mengi ya nchi hii ya Tanzania pamoja na nchi jirani,basi baada ya yule mama kurejea,alituchukua mpaka kwenye njia ya vumbi akatuambia "Fuateni hili barabara hamtapotea na huko mbele mtakuwa mnauliza watu njia ya kuelekea Butiama watawaonyesheni".

Yule mama aliendelea kusisitiza ya kwamba hatutoweza kupotea,alituambia kwamba tukifika hapo Butiama tutauliza njia ya kwenda Ikizu tutaelekezwa na wenyeji wa hapo.Safari ikaanza kama kawaida,muda huu kwa kuwa hatukuwa na hela ilibidi tuanze kupiga kwato taratibu!.

Itaendelea............
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 8.

Inaendelea.............

Tulitembea kwa muda wa saa 1:30 tukawa tumefika hayo maeneo ya Butiama,tulitoka Kiabakari saa 4,hivyo ukijumlisha hayo masaa tuliyotumia mpaka hapo Butiama ni kama masa 5 :30,kipindi tupo Kiabakari yule mama muuza ndizi alituambia kwamba tukifika hayo maeneo ya hapo Butiama tuulize mtu yeyote atuelekeze njia ya kwenda Ikizu.Basi kuna jamaa tulikutana naye tulimuomba atuelekeze njia ya kwenda Ikizu,Yule jamaa kuna njia alituonyesha ambayo ilikuwa inapitia porini,ingawa hakukuwa na mapori makubwa sana ila ilikuwa ni vichaka tu vidogo vidogo na mashamba ya watu,nilimuuliza kutoka hapo Butiama mpaka Ikizu kuna umbali gani?,jamaa alituambia haikuwa mbali sana maana wao walishazoea kwenda kwa kutumia baiskeli,kwakutembea ingetuchukua kama saa 3 au 4,yule jamaa kuna njia alituonyesha akatuambia "nyie ifuateni hii njia mkifika huko mbele mtakuwa mnauliza watu watawaelekeza".

Kabla ya kuanza safari ya kutoka hapo Butiama nilimpigia yule mganga nikamwambia ndiyo tulikuwa tumefika Butiama, akasema hatukuwa mbali sana,alituambia tujitahidi taratibu tungefika mapema.Nilimpgia pia na mama tukasalimiana nikamweleza namna ilivyokuwa,nikamwambia na mahala tulipokuwa,Kauli ya mama yangu mara zote ilikuwa ni kunisisitiza niendelee kuwa makini!.Zile ndizi ambazo dogo alikuwa kazibeba kwenye mfuko ilibidi sasa nimsaidie maana niliona alikuwa ameanza kuchoka.Wakati tukiwa tunatembea yule jamaa Mkenya aliyetupatia hiyo dili alinipigia simu akawa anataka kujua ni nini kilikuwa kinaendelea,nilimwambia bado tunaendelea kutafuta ile sarafu na endapo ingepatikana,basi tungemjulisha haraka iwezekanvyo!.Jamaa aliniambia kwa wakati huo naongea naye alikuwa Mwanza,kuna bosi wake alikuwa ameenda kumpokea maana kuna dili nyingine pia walikuwa wanafuatilia!,nilimwambia asiwe na shaka.

Safari ilisonga sana tukipita milimani na mashambani ambako tulikuwa tukielekezwa na kila tuliyekutana naye,Kuna mahali tulifika kulikuwa kuna mti wa Mkwaju ikabidi dogo aniambie tupumzike kidogo,basi tulipumzika pale tukaanza tena kula zile ndizi mpaka zikaisha!,Kiukweli zile ndizi zilikuwa kubwa na tamu,hivyo tulishiba sana,ishu sasa ilikuwa ni kupata maji ya kunywa,maana tulikuwa na kiu ya kufa mtu.Nilimwambia dogo "tumepumzika vya kutosha hivyo hatuna budi kusonga mbele!".

Tulifika maeneo fulani kulikuwa kumechangamka sana,ulikuwa unapigwa muziki fulani hivi wa kilugha!,Kumbe maeneo hayo kulikuwa na harusi!,bila shaka harusi za vijijini wengi wetu tunafahamu zinavyokuwaga na mbwembwe,kulikuwa kumefungwa spika zile za vipaza sauti juu ya miti,huku wakiwa wamefunga Kanga na mashuka yakipepea juu ya miringoti.Basi dogo akaniambia tutafute mji au nyumba yeyote hapo tuombe maji ya kunywa,tulitafuta nyumba zilizokuwa hapo jirani ulipokuwa ukipigwa mziki hatimaye tulifanikiwa kupata nyumba moja ambayo tulimkuta mama mmoja aliyetupokea kwa ukarimu,tulimsalimia kisha tukamwomba maji ya kunywa.

Yule mama alituuliza "Nyinyi ni wageni haya maeneo?".

Nilimjibu "Ndiyo mama".

Yule mama akasema ametuuliza kwasababu ameona sura zetu hazikuwa za hapo kijijini,Yule mama alituletea maji na baada ya kunywa nilimuuliza Kutoka hapo kijijini mpaka Ikizu kulikuwa na umbali gani?,yule mama alituambia kwamba hakukuwa mbali sana kwani bado kidogo tungefika,alituambia tuifuate ileile njia tuliyokuwa tumekuja nayo.Baada ya masaa 4 tulifanikiwa kufika hapo Ikizu,ulikuwa ni mji au kijiji kilicho changamka,dogo aliamua kukaa chini maana alikuwa kachoka sana,ndipo nilimpigia simu yule mganga nikamueleza tulipokuwa tumefikia akasema tulikuwa bado hatujafika Ikizu,alituambia lile eneo tulilokuwa tumefika palikuwa maeneo ya Nyamuswa,alituambia tutembee tena kidogo kama nusu saa hivi tukifuata barabara tutafika Ikizu,kumbe sisi tulidhani tulikuwa tumefika kumbe ilikuwa bado,ilitubidi tuamke mahali tulipokuwa tumekaa tuianze tena safari.Baada ya dakika 45 tukafika hapo Ikizu,tulipofika nilimpigia tena simu huyo mganga akatuelekeza kuna maeneo tusimame akaja hapo kutuchukua.

Tulifika hapo Ikizu ilikuwa mida ya saa 11 jioni,kiukweli yule dogo alikuwa kachoka sana,yule mzee alituchukua kuelekea kwake ambako nako kulikuwa nje kidogo ya mji wa Ikizu.Tulipofika hapo kwake kulikuwa na watu wengi ambao ilionyesha wale watu walienda kufata tiba,baada ya muda mzee alituambia alishindwa kutuambia wakati tukiwa njiani maana alisema ingetukatisha tamaa!,Mzee alituambia ile sarafu tuliyokuwa tukiitafuta alikuwa nayo ila kuna kipindi alikuja mdogo wake ambaye aliondoka na hela za zamani,aliendelea kutuambia kwamba alikuwa na muda mrefu hajakagua kwenye masanduku yaliyokuwa na hizo hela maana hakuwa na kazi nayo kwa wakati huo.Baada ya hayo maelezo yake ambayo tayari yalishanikatisha tamaa,ilibidi nimuulize huyo mdogo wake alikuwa anapatikana wapi?,alituambia mdogo wake huyo kwa wakati huo alikuwa akiishi Ukerewe ila akasema kwakuwa simu yake haikuwa na salio nikamnunulie vocha ampigie,Kwakuwa simu yangu ilikuwa na dakika za kutosha ilibidi nimpe ampigie huyo mdogo wake,kweli Mungu saidia huyo mdogo mtu akapatikana na wakaanza kuzungumza,walizungumza kwa muda meefu,baada ya mazungumzo mzee alirudi tulipokuwa tumekaa.

Mzee alituambia yule mdogo wake alikuwa anasema hiyo sarafu tuliyokuwa tunaitafuta ilikuwepo ila yeye katoka yupo Ukerewe ila inabidi twende Bunda jirani na Chuo cha Ualimu kuna mke wake alikuwa nyumbani tutamkuta na angempatia maelekezo yote,tukifika hapo akishatuonyesha hiyo sarafu ingepaswa tuache hiyo hela tuliyokuwa tumekubaliana na huyo mzee,kiasi cha shilingi laki 3 ndipo tuchukue hiyo sarafu.Kiukweli baada ya hayo maelezo nilifurahi sana na nikapata nguvu mpya japo hatukujua kutoka hapo kwenda Bunda tungefikaje maana tulikuwa tumechoka sana na giza tayari lilishaanza kuingia.Nilimuuliza dogo usiku ule tungelala wapi na kula wapi? maana tukiangalia pale kwa mganga kulikuwa hakuna uelekeo wa kulala na kula maana kulikuwa hakueleweki!,dogo alinishauri tuondoke hapo kwa mganga ili tukajadiliane mbele.
Tulimuaga yule mganga na kuondoka na wala hakuonyesha mashaka ya sisi kuondoka pale usiku!,tulivyofika maeneo ya center ya hapo Ikizu nilimwambia dogo kwakuwa nilikuwa nina elfu 1 mfukoni,tutafute maeneo walipokuwa wanauza uji ili tunywe halafu tungejua la kufanya.

Itaendelea.................
 
MKASA WA PILI -sehemu ya 9

Inaendelea.............

Tulitafuta maeneo ya pale jirani walipokuwa wakiuza uji,Kuna dada tulimkuta pale na alitukaribisha.

Nilimuuliza "Uji unauzaje?".

Alituambia "Nauza shilingi 100 kwa kikombe".

Niliendelea kumuuliza "hizo karanga hapo unauzaje?".

Alijibu "karanga nazo nauza shilingi 100".

Basi nikamwambia dogo "Kwenye hili buku kila mtu atatumia 500".

Nilimwambia yule dada atuweke uji,maeneo hayo wakati sisi tunakwenda kupata uji hakukuwa na mtu yeyote,ila kadri muda ulivyozidi kwenda ndiyo vijana nao wakawa wanaongezeka kupata uji!,haikuwa ngumu mimi kutambua kwamba yule dada hakuwa mgeni hayo maeneo,kwasababu vijana wengi walionekana kumchangamkia na kuanza kutaniana.Nilitamani sana nianzishe mazoea na yule dada kwa wakati ule lakini kwakuwa vijana walikuwa wengi ilibidi nisubiri kwanza wapungue!.Kadri muda ulivyosonga vijana nao wakawa wakipungua maeneo yale,na sisi tulichokifanya ni kunywa ule uji kwa madaha,hatukuwa na haraka maana hatukuwa na mahali pakwenda usiku huo!.

Nilijikuta nimemsemesha yule dada ghafla "Unaitwa nani?".

Alijibu "Naitwa Mkami".

Nilimwambia "Dada mkami inaelekea wewe ni mcheshi sana,maana naona vijana wengi wanakutania sana".

Yule dada alianza kucheka akaniambia "Hawa tumeshazoeana nao ndiyo maana wanapenda kunitania".

Baada ya mazungumzo ya hapa na pale ilibidi nimwambie ya kwamba maeneo yale sisi tulikuwa wageni na hatukuwa na mwenyeji.

Nilimwambia "ningeomba uwe mwenyeji wetu dada Mkami".

Aliniuliza "Kwani nyinyi mnatoka wapi?".

Ilibidi nimdanganye kwamba tulikuwa tumetokea Musoma na tulikuja hapo kumfata jamaa mmoja ambaye tulikuwa tunamdai pesa,tulipofika kumtafuta kwenye simu akawa kazima simu hakupatikana na hatukuwa na pesa yeyote ya kuturudisha Musoma.Dada Mkami alionekana kushangaa sana.
Aliniuliza "Kwahiyo haya maeneo nyinyi ni wageni?".

Nikamjibu "Ndiyo".

Nilijaribu kuongea na kuonyesha huzuni ili angalau huruma imwingie aone namna ya kutusaidia,nilijikaza kisabuni nikamuomba atusaidie tu sehemu ya kulala kwa usiku huo ili asubuhi tungejua la kufanya.Mkami alituambia kwamba yeye anakaa na mama yake na nyumba wanayokaa kuna chumba kimoja na sebule hivyo ingekuwa ngumu sisi kupata nafasi kwa usiku huo pale kwao!.

Alituambia "Ngoja kuna kijana mmoja huwa anakuja kunywa uji hapa tunafahamiana naye,akija nitajaribu kumueleza najua atawasaidia".

Baadae kidogo mida ya saa 3 usiku alikuja jamaa mmoja wakaanza kuongea,jamaa alimuuliza "Mtoto anaendeleaje?".

Kwa yale mazungumzo yao kwa haraka haraka nikajua yule jamaa atakuwa mpenzi wake na Mkami japo ilionesha hawakai wote,kapo Mkami yeye hakutuambia lakini kwakuwa mimi nilikuwa mtu mzima tayari nikaelewa!.Basi baadae tukasalimiana na yule jamaa pale na ukimya ukatawala kidogo!,tulikaa pale mpaka mida ya saa 4 usiku ndipo yule jamaa akataka kuondoka,Mkami alimuita akamueleza hali halisi kuhusu sisi,jamaa kiukweli nilimpenda sana maana hakuwa na maneno mengi.

Alituambia "Twendeni nyumbani".

Alituuliza "Vipi,mmekula?".

Nilimjibu "Tushakula bro".

Nilimshukuru sana Mkami kwa wakati ule maana sikutegemea sana,Yule jamaa ilionekana alikuwa mnyenyekevu sana maana hata wakati tukiwa njiani tulikuwa tukipiga stori na ilionekana na yeye kuna mambo mengi tu ya maisha alikuwa kapitia hivyo alikuwa akitutia moyo!.Tulifika hapo geto kwake na jamaa alituelekeza tukachote maji kwenye kisima kilichokuwa nje ya hiyo nyumba kwa ajili ya kuoga kuondoa uchovu!,kiukweli mimi nguo zangu zilishaanza kutoa harufu kwa ajili ya jasho.

Jamaa wakati tukiwa njiani tunaelekea kwake alituambia yeye jina lake ni Mashauri na sisi pia tulimtajia majina yetu.Usiku ule mimi nilimwambia Mashauri atusaidie sabauni kama anayo ili tuweze kufua nguo zetu,jamaa alituletea kipande cha Sabuni tukaanza kufua huku mastori yakiendelea kama kawaida.Mashauri alituambia ya kwamba yule dada Mkami alikuwa mpenzi wake na walifanikiwa kupata mtoto mmoja ambapo kwa wakati ule wa kuuza uji mtoto huwa anamwacha nyumbani na bibi yake.Katika maongezi nilimwambia jamaa kwamba tulikuwa na safari ya kwenda Bunda,kwakuwa Mkami alikuwa keshamueleza kuhusu sisi,nilimwambia baada ya kumkosa mtu tuliyemfuata hapo Ikizu ilibidi tuondoke kuelekea Bunda halafu ndiyo tungerudi Musoma,sikutaka sana kupindisha uongo ambao nilikuwa tayari nilikuwa nishamdanganya Makami.Mashauri alituambia kama tunaenda Bunda,asubuhi tujitahidi kuamka mapema ili twende naye mpaka kile kijiji cha Nyamuswa tungepata gari.

Mashauri alituambia yeye ni dalali wa Mbuzi,hivyo huwa anaenda huko vijijini anawakusanya kisha anawapeleka hapo Nyamuswa kuna eneo maalumu wanawekwa halafu yeye hupewa chake.Hivyo akatuambia kwakuwa kesho kuna magari yangekuja kuchukua mbuzi angetuombea tupate lift mpaka Bunda,Kiukweli nilimuona Mashauri ni muungwana sana.

Nilipomaliza kufua nilihakikisha zile nguo zangu nazikung'uta kisawasawa,hiii yote nilitaka kwa usiku ule ziwahi kukauka kwa upepo maana hakukuwa na jua.Baada ya shughuli za kufua na kuoga zilipokamilika tuliingia geto kwa Mashauri ambako kulikuwa kumenakishiwa vizuri kwa magazeti ukutani!,japo ile nyumba ilikuwa niya nyasi lakini kijana mwenzetu alikuwa kajitahidi sana kupendezesha geto lake,kwakuwa alikuwa na kitanda kidogo nilimwambia yeye alale na dogo na mimi kuna jamvi lilikuwa pale nje aliniletea nikatandika chini akanipa na shuka mrume ndago nikauchapa usingizi!.Usingizi japo ulikuwa wa mang'amu ng'amu lakini nilimshukuru sana Mungu maana kupata sehemu ya kulala kwa usiku ule halikuwa jambo jepesi,tena kwa mtu ambaye tulikuwa hatufahamiani.

Usiku huo jamaa alifungulia redio yake iliyokuwa ikitumia betri akaweka stesheni fulani hivi tukaanza kusikiliza miziki,nilipitiwa na usingizi nikajikuta nashituka kushakucha.Mashauri yeye aliwahi kuamka,mimi na dogo tuliamka mida ya saa 1 asubuhi ndipo Mashauri alisema tujiandae twende kwao Mkami akatupikie uji tunywe kisha tuelekee Nyamuswa.Basi tulijiandaa pale japo nguo zangu hasa suruali ilikuwa haijakauka vizuri nilivaa hivyo hivyo,dogo naye mambo yalikuwa yale yale!.Tuliondoka na Mashauri mpaka kwao Mkami asubuhi hiyo na tulipofika tulimkuta Mkami na mama yake na yule mtoto wa Mashauri,kilikuwa kibinti cha miaka 3 hivi!.
Basi Mashauri akaanza kuongea na Mkami kilugha,baadae mkami aliondoka na jembe pale nyumbani ambapo hakupita muda alikuja na mihogo mibichi!,Kumbe kwa wakati ule inaonekana jamaa alimwambia akachimbe mihogo aje atupikie ili tule tuondoke.

Baada ya kuwa tumemaliza kupata uji na mihogo ya kuchemsha tulianza sasa kutembea kuelekea Nyamuswa,wakati tunaenda nilimshukuru sana Mashauri,jamaa alikuwa ni mtu mmoja muungwana sana,ile roho aliyokuwa nayo Mashauri sijui kama vijana wa leo wangekuwa nayo!.Tulitembea kwa muda kidogo na hatimaye tukafika hapo Nyamuswa,tulifika mpaka mahala wanapowahifadhi wale mbuzi,jamaa akatuambia tusubilie gari la kubebea mbuzi maana halikuwa mbali.Gari lilipofika mbuzi walianza kupakiwa kwa kuhesabiwa na sisi ilibidi tuanze kumsaidia Mashauri kupakia wale mbuzi kwenye ile fuso,tulipomaliza ile kazi Mashauri aliongea na yule dereva kwamba sisi ni ndugu zake na akifika Bunda atuache.Kabla ya kuingia kwenye lori nilimuomba Mashauri namba yake ya simu nikamwambia tungekuwa tunawasiliana.

Nyuma ya lile lori kulikuwa na jamaa wengine wawili ukiacha sisi,jumla tulikuwa 4,Kuna jamaa nilimuuliza kwa wakati ule walikuwa wakielekea wapi baada ya hapo?,jamaa alisema wanaelekea Tabora ila katikati ya safari kabla ya kufika Bunda kuna vituo viwili wangesimama kuchukua mbuzi wengine.


Itaendelea.................
Aneel munawar
JF-Expert Member
Dec 20, 2020
#613
sontable said:
Stori ishaanza kukosa Radha Haina hata uzuri wowte yaani ,kisa huko chini itaendelea nachokushauri usilete huo mwendelezo badala ya kusema itaendelea andika hata siku mbili au tano kabisa ikisha kamilika ndo uilete hapo hakuna hata Cha kukielewa ,smart people always doing smart thing
"Always doing"😂😂😂 my shit.. !
T11
T11
JF-Expert Member
Dec 20, 2020
#614
LwandaMagere said:
MKASA WA PILI -sehemu ya 9

Inaendelea.............


Tulitafuta maeneo ya pale jirani mahala walipokuwa wakiuza uji,Kuna dada tulimkuta pale na alitukaribisha!,Nilimuuliza uji anauzaje,Alisema "Nauza shilingi 100 kwa kikombe",Na hizo karanga hapo unauzaje?,niliendelea kumuuliza!,Pia alituambia karanga anauza 100!

Basi nikamwambia dogo "Kwenye hili buku kila mtu atatumia 500",Nilimwambia yule dada atuweke uji!
Maeneo hayo kiukweli wakati sisi tunakwenda hapo kupata uji hakukuwa na mtu yeyote ila kadri muda ulivyozidi kwenda ndo vijana nao wakawa wanaongezeka kupata uji!,Haikuwa ngumu mimi kutambua kwamba yule dada hakuwa mgeni pale maana vijana wengi walionekana kumchangamkia na kuanza kutaniana!
Nilitamani sana nianzishe mazoea nae kwa wakati ule lakini kwakuwa vijana walikuwa wengi ilibidi nisubiri kwanza wapungue!

Kadri muda ulivyosonga vijana nao wakawa wakipungua maeneo yale,na sisi tulichokifanya ni kunywa ule uji kwa madaha,hatukuwa na haraka maana hatukuwa na pa kwenda!

Nilijikuta nimemsemesha yule dada ghafla "Unaitwa nani"?,Naitwa "Mkami" yule dada alijibu!

"Dada mkami inaelekea wewe ni mcheshi sana,maana naona vijana wengi wanakutania sana",Yule dada alianza kucheka akanambia "Hawa tumeshazoeana nao ndo maana wanapenda kunitania"

Baada ya mazungumzo ya hapa na pale ilibidi ni mwambie ya kwamba maeneo yale sisi ni wageni na hatuna mwenyeji na ningeomba yeye awe mwenyeji wetu!
Aliniuliza "Kwani nyinyi mnatoka wapi",Ilibidi nimdanganye kwamba Tunatoka Musoma na tulikuja hapo kumfata jamaa mmoja ambaye tulikuwa tunamdai na tulipofika na kumtafuta kwenye simu akawa kazima simu hakupatikana na hapo hatukuwa na pesa yeyote ya kuturudisha Musoma,Dada Mkami alionekana kushangaa kidogo,Aliniuliza "Kwahiyo haya maeneo nyinyi ni wageni"?,Nakamwambia "Ndiyo"

Nilijaribu kuongea na kuonyesha uzuni ili angalau huruma imwingie ili aone namna ya kutusaidia!,Nilijikaza kisabuni nikamuomba atusaidie tu sehemu ya kulala kwa wakati huo ili asubuhi tutajua la kufanya!

Mkami alituambia kwamba yeye anakaa na mama yake na nyumba wanayokaa kuna chumba kimoja na sebule hivyo ingekuwa ngumu sisi kupata nafasi kwa usiku huo pale kwao!,Ila alituambia "Ngoja kuna kijana mmoja huwa anakuja kunywa uji hapa tunafahamiana naye,akija ntajaribu kumueleza najua atawasaidia".

Baadae kidogo kama mida ya saa 3 usiku alikuja pale jamaa na wakaanza kuongea na jamaa ilionekana anamuuliza "Mtoto anaendeleaje"?,Kwa yale mazungumzo yao kwa haraka haraka nikajua yule jamaa atakuwa Mpenzi wake na Mkami japo ilionesha hawakai wote,Japo Mkami yeye hakutuambia lakini kwa mimi ni mtu mzima tayari nshaelewa!

Basi baadae tukasalimiana na yule jamaa pale na ukimya ukatawala kidogo!,Tulikaa pale mpaka mida ya saa 4 usiku ndipo yule jamaa akataka kuondoka,Mkami alimwita akamwambia situation iliyotukuta na jamaa kiukweli nilimpenda sana maana hakuwa na maneno mengi,Alituambia "Twendeni Nyumbani",Alituuliza pale "Vp mmekula"?,Nilimwambia "Tushakula bro"

Nilimshukuru sana Mkami kwa wakati ule maana sikutegemea sana,Yule jamaa inaonekana alikuwa mtu wa watu maana hata wakati tukiwa njiani tulikuwa tukipiga stori na ilionekana na yeye kuna mambo mengi tu ya maisha alikuwa kapitia hivyo alikuwa akitutia moyo!
Tulifika hapo geto kwake na jamaa alituelekeza tukachote maji kwenye kisima kilichokuwa nje ya hiyo nyumba kwa ajili ya kuoga kuondoa uchovu!,kiukweli mimi nguo zangu zilishaanza kutoa hatufu kwa ajili ya jasho na dogo nae vile vile!

Jamaa wakati tukiwa njiani àlituambia anaitwa Mashauri na sisi pia tulimtajia majina yetu!

Usiku ule mimi nilimwambia Jamaa atusaidie sabauni kama anayo ili tuweze kufua nguo zetu,jamaa alituletea kipande cha Sabuni tukaanza kufua pale huku mastori yakiendelea kama kawaida!
Mashauri alituambia ya kwamba yule Dada Mkami alikuwa demu wake na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja ambapo kwa wakati ule wa kuuza uji Mkami mtoto huwa anamwacha nyumbani na Bibi yake!,Basi tuliendelea sana kupiga stori na jamaa alikuwa mtu wa watu sana!

Katika maongezi nilimwambia Jamaa kwamba kesho sisi tunasafari ya kwenda Bunda na kiukweli sikutaka kabisa kumweleza chochote kuhusu kilichotupeleka kule!,Jamaa alituambia kama tunaenda Bunda Asubuhi twende nae mpaka kijiji kimoja kinaitwa Nyamuswa kwani yeye anafanya biashara ya mbuzi na kuzipeleka hapo baadae kuna magari yanakuja kufata kupeleka Mwanza na sehemu nyingine!,Mashauri alivyotuambia kwamba yeye ni kama dalali wa Mbuzi,hivyo huwa anaenda huko vijijini anawakusanya kisha anawapeleka hapo Nyamuswa huwa kuna eneo maalumu wanawekwa halafu yeye hupewa chake!
Hivyo akatuambia kwakuwa kesho kuna magari yangekuja kuchua mbuzi pale angetuombea tupate lift mpaka Bunda,Kiukweli nilimuona Mashauri ni muungwana sana!

Nilipomaliza kufua nilihakikisha zile nguo zangu nazikung'uta kisawasawa,Hii yote nilitaka kwa usiku ule ziwahi kukauka kwa upepo!

Baada ya shughuli na kufua na kuoga zilipokamilika tuliingia geto kwa Mashauri na kulikuaa kumenakshiwa vizuri kwa magazeti ukutani!,Japo ile nyumba ilikuwa niya nyasi lakini kijana mwenzetu alikuwa kajitahidi sana kupendezesha chumba chake!,kwakuwa alikuwa na kitanda kidogo nilimwambia yeye alale pale na dogo na mimi kuna jamvi lilikuwa pale nje aliniletea nkatandika chini akanipa na shuka Mrume ndago nkauchapa usingizi!
Usingizi japo ulikuwa wa mang'amu ng'amu lakini nilimshukuru sana Mungu maana kupata sehemu ya kulala kwa usiku ule ilikuwa ni ishu!

Usiku huo jamaa alifungulia redio yake mmoja hivi iliyokuwa ikitumia betri na akaweka stesheni fulani hivi tukaanza kusikiliza!,Nilipitiwa na usingizi na nimejikuta nashituka kushakucha!

Mashauri yeye aliwahi kuamka,Mimi na dogo tuliamka mida kama ya saa 1 asubuhi ndipo Mashauri alisema tujiandae twende kwao Mkami akatupikie uji ili tuelekee Nyamuswa!

Basi tulijiandaa pale japo nguo zangu hasa suruali ilikuwa haijakauka vizuri nilivaa hivyo hivyo,dogo nae mambo yalikuwa yale yale!
Tuliondoka na Mashauri mpaka kwao Mkami asubuhi hiyo na tulipofika tulimkuta Mkami na Mama yake na yule mtoto wa Mashauri,kilikuwa kibinti kama cha miaka 3 hivi!
Basi Mashauri akaanza kuongea na mkami pale kilugha baadae mkami aliondoka na jembe pale nyumbani,Baadae kidogo alikuja na mihogo mibichi!,Kumbe kwa wakati ule inaonekan jamaa alimwambia akachimbe mihogo aje atupikie ili tule tuondoke!

Hivyo ndivyo ilivyokuwa ndugu zangu!


Baada ya kuwa tumemaliza kupata uji na mihogo ya kuchemsha tuliagana pale na kuanza sasa kutembea kuelekea Nyamuswa!,wakati tunaenda nilimshukuru sana Mashauri!,Jamaa alionekana ni mtu wa watu kweli!,Hii roho sijui kama vijana wa leo wangekuwa nayo!

Tulitembea kwa muda kidogo na hatimaye tukafika hapo Nyamuswa!,tulifika mpaka mahala wanapowahifadhi wale mbuzi na jamaa akasema ngoja tusubilie gari la kubebea mbuzi maana halikuwa mbali sana na pale!

Gari lilipofika mbuzi walianza kupakiwa kwa kuhesabiwa na sisi ilibidi tuanze kumsaidia Mashauri kupakia wale mbuzi kwenye ile fuso!
Tulipomaliza ile kazi Mashauri aliongea na yule dereva pale kwamba sisi ni ndugu zake na akifika Bunda atuache!,Basi kabla ya kuingia kwenye lori nilimuomba Mashauri namba za simu na akanipa nkamwambia tutawasiliana!,Nyuma ya lile lori kulikuwa na jamaa wengine wawili ukiacha sisi,Jumla tulikuwa 4!,Kuna jamaa nilimuuliza kwa wakati ule walikuwa wakienda wapi?,Jamaa alisema wanaelekea Tabora ila humo katikati kabla ya kufika Bunda kuna vituo kama viwili watasimama kuchukua mbuzi!

Itaendelea.................
 
MKASA WA PILI -sehemu ya 10.

Inaendelea.............

Wakati tukiwa kwenye lile lori nilikuwa nikipiga stori na dogo nilimuuliza endapo tungefanikiwa kupata hela yeye angefanyia nini,ndipo nikagundua dogo anapenda sana maisha ya starehe,maana alikuwa akiniambia angeipata hiyo hela kitu cha kwanza ni kununua gari la kifahari na kutafuta mwanamke mzuri wa kuishi naye.Kiukweli mimi nilikuwa nawaza namna ya kumkwamua mama yangu kutoka kwenye umasikini hasa ukizingatia baada tu ya kutoka Tarime na kuhamia Mwanza maisha yalibadilika na kuwa ya Hovyo sana.
Baada ya muda kupita aliniambia "Hawa jamaa inabidi tuwashitue watuache shule ya sekondari ya Bunda".

Baada ya kufika Bunda tuliwashitua wale jamaa wakatuacha karibu na Bunda Sekondari,dogo akaniambia kutoka hayo maeneo tulipoachwa mpaka kilipo chuo cha ualimu si mbali hivyo tutembee taratibu tutafika.Kiukweli wakati huo nilikuwa nanuka harufu ya mbuzi kwasababu ya kukaa nyuma ya lile lori lakini sikujali sana,tulianza kutembea taratibu kuelekea hayo maeneo ya chuo ambayo jamaa alituambia kwamba ndipo kuna ile sarafu ya 100 ya mwaka 1993.
Nilimtafuta yule jamaa wa Ukerewe akatuelekeza hayo maeneo,sasa kwakuwa dogo yeye alikuwa mwenyeji wa Bunda alikuwa akielewa maeneo mengi ya huko chuoni,lakini jamaa akasisitiza ya kwamba tuhakikishe kweli kama tunataka kuichukua hiyo sarafu,inapaswa tumuachie huyo mke wake tutakaye mkuta hapo nyumbani kwake shilingi laki 3 kama tulivyokuwa tumekubaliana.

Tulipofika hapo nyumbani kwa jamaa tulifanikiwa kumkuta huyo mwanamke na kwakuwa jamaa alikuwa amempa maelekezo haikuwa ngumu sana kujieleza,aliingia ndani akatoka na sarafu za shilingi 100 kama tatu hivi,akaanza kuangalia ya mwaka 1993 na ndipo akaipata.Alituonyesha ile sarafu ili kujihakikishia kama ndiyo yenyewe,baada ya kuishika ile sarafu na kujihakikishia ya kwamba ni yenyewe,nilianza kuingiwa na kitete kisichokuwa cha kawaida.Nilikuwa nina furaha isiyokuwa na kifani,yule mwanamke alisema amepewa maelekezo na mumewe ya kwamba inapaswa tulipe ile laki tatu ndiyo tutaruhusiwa kuondoka na hiyo sarafu.Kwakuwa hatukuwa na laki tatu wakati huo,niliamua kumpigia simu yule Mkenya nikamueleza kwamba tushaipata ile sarafu,ikiwezekana atume hiyo laki tatu halafu wao wangetukata kwenye ile milioni 100 ambayo aliahidi tungelipwa,sasa nilipokuwa naongea naye ilionekana yeye pia kapagawa.

Aliniambia"Subiri kidogo nakupigia".

Baada ya dakika 5 alinipigia simu akaniuliza kwa wakati huo tupo maeneo gani?,nilimwambia tupo maeneo fulani hapo Bunda.

Jamaa akaendelea kuniambia"Subirini hapo hapo kuna watu wanakuja na hiyo laki 3 ya kumpa huyo mama!”.

Nilianza kuingiwa na wasiwasi,ilibidi nimuulize kuhusu hela yetu inakuwaje?,jamaa akasema kwamba wakishachukua hiyo sarafu tutaongozana nao kuelekea Mwanza maana hata tajiri aliyekuwa katoka
Kenya bado alikuwa hapo Mwanza na tungefika tulikuwa tunalipwa hiyo pesa bila wasiwasi wowote.Nilimkumbushia kwamba,mwanzo kabla hatujaanza kazi alisema hiyo pesa wangetuwekea kwenye akaunti, sasa inakuwaje wakatupe mkononi?.

Jamaa alisema"Nitumie namba ya akaunti yako ya benki”.

Kwa kipindi hicho sikuwa na akaunti ya benki,hivyo nilimwambia jamaa anitumie vocha nimwambie mama yangu anitumie namba ya akaunti ya kwake ili hiyo hela itumwe huko.Ndani ya dakika kadhaa jamaa aliponitumia vocha,nilimpigia simu mama na kumueleza kila kitu,ndipo akanitumia namba ya akaunti nikamtumia jamaa yule mkenya.

Jamaa baada ya kuipata ile akaunti alisema "sawa tutaingiza hiyo pesa muda si mrefu lakini kuna vijana wanakuja hapo kuichukua hiyo 100 wapeni".

Baada ya mazungumzo kwenye simu nilimuita yule dogo tukaanza kujadiliana,Yule dogo alikuwa na akili sana,alianza kuniambia kwamba hao jamaa tusipokuwa makini wanataka kututapeli,endapo tungewaelekeza maeneo tuliyokuwepo wangefika na kuichukua hiyo sarafu tusingepata kitu.Maelezo ya yule dogo ni kama sasa yalianza kunifungua akili,kwa ujasiri nilimpigia simu yule mkenya kumueleza ya kwamba pasipo hiyo hela kutumwa kwenye akaunti niliyomtumia nisingemuelekeza tulipo na nisingempa ushirikiano wa aina yeyote,jamaa aliendelea kusisitiza kwamba pesa ingewekwa muda si mrefu kwenye akaunti.Baadae nilimpigia mama simu nikamwambia aende benki akaangalie kama ile hela ishawekwa;Baada ya muda mama yangu akasema “hakuna hela yoyote iliyoingia mwanangu”.

Nilimwambia dogo tuelekee nyumbani maana hatukuwa na shaka yeyote kwakuwa hiyo sarafu tayari tushaipata.Kabla hata hatujafika nyumbani kwa mama mdogo jamaa akawa amepiga simu akaanza kusema kwamba hao jamaa wapo maeneo ya hapo stendi Bunda tuwaelekeze maeneo tulipo ili waje,nilimwambia yule jamaa siwezi kuwaelekeza wale jamaa bila hela kuingizwa kwenye akaunti.

Nilimwambia "kwanini usinitumie hiyo laki tatu nikatoe nimlipe yule mama?".

Yule jamaa mkenya inaonekana alianza kuchukia akaanza kuongea kwa ukali sana.Alikata simu kwa muda kidogo,aliponipigia tena aliniambia "Wewe mjinga si unajifanya mjanja?,sasa itakula kwako,mtake msitake tutawatafuta popote mlipo na kuhakikisha hiyo sarafu tunaipata,vinginevyo lazima mfe".

Jamaa akakata simu,nilimueleza dogo namna jamaa alivyoniambia,dogo akasema "Mimi nilijua tu maana ishu za pesa kama hizi mara nyingi huwa si salama sana".

Nilipatwa na uoga ambao sikuwahi kukutana nao kwa kipindi chote ambacho tuko huko,ilibidi nimpigie simu mama nikamueleza kila kitu,aliniambia nihakikishe kesho narudi Mwanza haraka iwezekanavyo hao jamaa wasije nifanyia kitu kibaya.Yule jamaa alikuwa akinipigia simu sana lakini sikuweza kupokea,jamaa alianza kutuma sms za vitisho na matusi makali,alisema lazima watupate tu hata kama tungeenda wapi maana wao wanakikosi kazi ambacho kisingeshindwa kazi ya kutusaka.Tulipofika nyumbani ilibidi tumsimulie mama mdogo namna hali ilivyokuwa tangu siku tunaondoka mpaka kupatikana kwa hiyo hela,niliendelea kumwambia mama mdogo kuhusu huyo mkenya na sms zake alizokuwa akituma,mama mdogo alituambia hao jamaa wangetudhulumu na isingekuwa ajabu kutuua ili wapate wanachokitaka.
Baadae kidogo nikiwa nyumbani kuna simu ilipigwa nikaipokea,jamaa alijitambulisha kama askari akasema kwa usalama wetu tujisalimishe pale kituo cha polisi cha wilaya ya Bunda maana hatutaweza kukimbia mahali popote bila kukamatwa,nilibaki najiuliza maswali mengi sana kichwani,wanataka watukamate kwa kosa gani tulilokuwa tumefanya?,nilijua kabisa kutakuwa na askari ambao hawakuwa waaminifu walikuwa wakishirikiana na lile genge la waharifu,sasa walidhani kupitia vitisho vyao tungeogopa,niliamua kuitoa ile line kwenye simu na kuitupa.

Itaendelea.......................
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 11

Inaendelea................

Baada ya kuitupa ile line ya simu nilikaa kwa kutulia nikiwaza na kuwazua," Ina maana kuhangaika kote siku kadhaa za kuitafuta hiyo hela leo hawa majinga wanataka kututoa uhai kisa sarafu ya 100?",kiukweli niliwaza bila kupata majibu.

Nilimwambia dogo ahakikishe anakaa kwa kutulia mpaka hali itakapokuwa shwari maana nilijua wale jamaa wangeendelea kumtafuta pale Bunda hasa ukizingatia mji wenyewe haukuwa mkubwa sana.Kesho yake nilimuomba mama mdogo nauli ili niondoke kurudi Mwanza maana niliona kila kitu kilikuwa kimeshaharibika!,Niliona ni heri nikaishi masikini kuliko kuendelea kukaa hapo kwa wasiwasi huku maisha yangu yakiwa rehani!.Niliondoka Bunda na sikutaka dogo anisindikize maana nilijua anaweza kukamatwa na wale mafia hatimaye mambo yakaharibika.Niliingia Mwanza mida ya saa 8 mchana na nilimweleza mama kila tukio lililo kuwa limetokea kwa siku hizo.

Basi kwakuwa sikuwa na kazi ya kufanya kwa wakati huo niliamua niende nikaendelee na ile kazi yangu ya ualimu wa temporary niliyokuwa nikiufanya baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari,Kwahiyo nilikuwa nikitoka kwenye vipindi mchana jioni nilikuwa naenda kuwafundisha wanafunzi niliyokuwa nao kwa wakati ule kabla sijaenda Geita na walikuwa wakinilipa elfu 3 kwa kila topic tuliyokuwa tunamaliza.Baada ya kukaa pale nyumbani kwa muda mrefu,nilimwambia mama ya kwamba,ulifika wakati sasa na mimi niende kupanga chumba changu ili nijitegemee!,mama yangu alikaataa kabisa akasema nyumba bado ni kubwa na mimi sipaswi kuondoka hapo nyumbani,niliona kama kanibana maana kuna mambo yangu niliona kama hayataenda,niliendelea kumsihi mama aniruhusu nikapange lakini ningekuwa narejea nyumbani kuwasalimia,baada ya kumsihi sana mama alikubali na akanitaka endapo maisha yakinishinda nirudi nyumbani!.

Nilikuwa namuhurumia sana mama yangu kiukweli na nilimpenda sana japo sikuwa na kitu!.Kwakuwa kuna vihela vyangu nilikuwa nimevikusanya kwa wakati huo nilienda kutafuta chumba nikalipia miezi 3 na nikanunua godoro na vyombo kadhaa vya kupikia,nilinunua pia na vitu kadhaa vya ndani na kadri siku zilivyoenda nilipokuwa nikilipwa nilikuwa nikinunua vitu taratibu!.

Maisha yalisonga na muda nao ukazidi kuyoyoma,siku moja wakati nikiwa geto kwangu,mama alinipigia simu akataka niende kule nyumbani maana kulikuwa kuna maongezi ya kifamilia.Basi nikajianda nikaondoka zangu mpaka nyumbani,nilipofika nilimkuta dada yangu mkubwa,mama,shangazi,pamoja na wale mabinti waliokuwa wakikaa hapo nyumbani ambao walikuwa watoto wa Shangazi.Mama alisema ametuita hapo kwasababu kuna jambo kalisikia ambalo halikuwa zuri.

Nilimuuliza mama "ni jambo gani hilo?"

Ndipo binti mmoja wa Shangazi aliyekuwa mkubwa akawa nasema alikutana na Shemeji yangu mmoja ambaye kwa upande wa dada zangu alikuwa ni wifi yao,kuna maneno aliyaongea ambayo hayakuwa mazuri!,Yule mtoto wa shangazi akawa anasema alikutana na shemeji kanisani akawa anamwambia kwamba sisi hapo nyumbani ni Masikini na alikuwa anajuta kaka yao kuoa hapo nyumbani kwenye ukoo masikini!,Yule shemeji aliendelea kusema kwamba anaogopaga hata kuwapeleka rafiki zake ukweni kwasababu tulikuwa tunanuka umasikini!.Yule binti akawa anasema yule shemeji alikuwa anasema kwamba hizo taarifa zimfikie mama yangu maana hatukuwa nala kumfanya kwasababu sisi ni masikini wa kutupa,alikuwa akilaani sana kwanini kaka yake asingeenda kuoa kwenye familia ya kitajiri akaenda kuoa kwetu kwenye familia masikini.

Hayo ndiyo yalikuwa maelezo ya yule binti mtoto wa shangazi.

Sasa huyo shemeji tuliyekuwa tukimjadili hapo kwenye kikao labda nimuelezee kidogo.Huyo shemeji kaka yake ndiye alikuwa amemuoa dada yangu niliyekuwa nikimfuatia katika uzao ambaye kwa wakati huo walikuwa wakiishi mkoani Arusha,huyu shemeji alikuwa anafanya kazi kwenye benki fulani hapo mjini na alikuwa amekaa sana Afrika kusini,Kwahiyo dharau na nyodo zote alikuwa anazifanya kwakuwa alikuwa na ajira benki na kukaa tu hapo Afrika Kusini!.

Baada ya hayo maelezo nilikuwa najiuliza maswali mengi kichwani yasiyokuwa na majibu.
Nilijikuta namwambia mama "kwani umasikini ni nini?,maana sisi kama ni kula mbona tunakula vizuri?,kama ni nyumba mbona tuna nyumba?,huyo malaya anataka maisha gani?,au kwakuwa yeye ana gari na kufanya kazi benki ndiyo anadharau watu?".

Toka wakati huo nilimwambia mama "sitokaa niimtambue yule mume wa dada kama shemeji maana dada yake anatudharirisha na kutuahibisha".

Tulipomaliza yale mazungumzo niliondoka zangu pale nyumbani kuelekea Geto kwangu kulala,siku hiyo nilikosa raha sana na nilikuwa nimechukia sana,nilijiona bado nilikuwa nina safari ndefu sana ya kuwa tajiri.Pale nyumbani nilipokuwa nimepanga kuna jamaa mmoja tulikuwa tumepakana vyumba na alikuwa rafiki yangu sana maana hata alipokuwa akielekea kwenye shughuli zake ambazo zilimchukua hata mwezi alikuwa akiniachia funguo!.Sasa baada ya kuona sikuwa na raha,jamaa aliniuliza "Mwanangu mbona leo huna raha?,una shida gani?".

Nilimwambia nilikuwa sijisikii vizuri tu!,huyu jamaa alikuwa akifanya kazi kampuni ya ujenzi ya Nyanza,usiku ule nilimfuata jamaa nikamwambia kwa ujasiri mkubwa "Nataka kuwa tajiri".

Jamaa alioneshaa kushituka sana na kuniuliza "Mwanangu leo umepatwa na nini?,tafadhali nieleze ukweli".

Basi nilimsimulia yaliyonisibu na kiukweli alihuzunika sana,akaniambia nisijali niende nikapumzike halafu kesho tungeongea.Siku iliyofuata baada ya kutoka kwenye shughuli zangu za kushika chaki ilibidi nimueleze jamaa adhma yangu ya kuutafuta utajiri.

Nilimwambia jamaa "Mimi ninachotaka ni utajiri,haijalishi ni utajiri wa namna gani"

Dhumuni la mimi kutaka kuwa tajiri ni kumuonyeshea uwezo yule shemeji yangu na watu wengine waliyokuwa wanatuona sisi masikini!,Kiukweli kwa wakati huo nilikuwa nipo tayari kufanya jambo lolote ili niweze kuwa tajiri.

Jamaa aliniambia "tafuta nauli twende zetu kigoma maana kuna kipindi tulienda kufanya kazi ya ujenzi wa barabara kule,kuna bibi tuliwahi kwenda kwake alikuwa ni balaa!,kipindi hicho mimi nilienda kwake kufata dawa ya kinga dhidi ya watu wabaya pale kazini hivyo sikufata utajiri,lakini safari hii nataka na mimi nikatafute dawa ya kupanda cheo na kupata pesa!".

Basi hayo mazungumzo ya jamaa yalinipa faraja kidogo na yakaniondolea upweke wa nafsi.Niliendelea kutafuta pesa za nauli maana jamaa aliniambia nikipata kama laki 2 nimshitue ili tuondoke maana yeye alikuwa yuko tayari muda wote.Mwezi uliofuatia ulikuwa mwezi wa 6 mwaka 2012 ambao tulipanga tuondoke,sikutaka kumwambia mtu yeyote,hata mama pia sikutaka kumuaga,mtu aliyekuwa akifahamu ni huyo jamaa tuliyekuwa tukikaa naye hapo nyumbani vyumba jiarani.

Basi tulipanga safari ya kwenda kigoma na tuliondoka Mwanza siku iliyofuata!




Itaendelea..............
Behaviourist
Behaviourist
JF-Expert Member
Dec 20, 2020
#635
Kwa kweli mleta uzi ana kipaji cha kusimulia story!
Dickson mwaipopo
Dickson mwaipopo
JF-Expert Member
Dec 20, 2020
#636
LwandaMagere said:
MKASA WA PILI -sehemu ya 11

Inaendelea................


Baada ya kuitupa ile line ya simu nilikaa kwa kutulia nikiwaza na kuwazua!," Ina maana kuhangaika kote siku kadhaa za kuitafuta hiyo hela leo hawa majinga wanataka kututoa uhai kisa shilingi 100"?,Nilijisemea!

Basi nilimwambia dogo ahakikishe Anakaa kwa kutulia mpaka hali itakapokuwa shwari maana nilijua wale jamaa wangeendelea kumtafuta pale Bunda hasa ukizingatia mji wenyewe haukuwa mkubwa hivyo!

Kesho yake ilibidi mimi niondoke Pale kwa Mama mdogo kurudi Mwanza maana niliona kila kitu kilikuwa kimeshaharibika!,Nikajisemea ni heri nkaishi masikini kuliko kuendelea kukaa hapo kwa wasiwasi huku maisha yangu yakiwa rehani!
Niliondoka hapo nyumbani Bunda na sikutaka dogo anisindikize maana nilijua anaweza kukamatwa na wale mafia hatimaye mambo yakaharibika!

Niliingia Mwanza mnamo mida ya saa 8 mchana na nilimweleza Bi mkubwa kila tukio lililo kuwa limetokea kwa siku hizo!

Basi kwakuwa siku na kazi ya kufanya kwa wakati huo nilitafuta shule kadhaa pale mjini wa kufundisha tuition,kwa bahati nzuri kuna shule fulani niliipata pale Mjini ambayo nilipewa ajira temporary ya kuwa mwalimu wa History na Geography na nilikuwa nalipwa kila Mwezi 150000/=Nilimshukuru Mungu sana hasa ukizingatia sikuwa na chochote!,Kwahiyo nilikuwa nikitoka kwenye vipindi mchana jioni nilikuwa naenda kuwafundisha wanafunzi niliokuwa nao kwa wakati ule kabla sijaenda Geita na walikuwa wakinilipa 3000 kwa kila topic tunayomaliza!

Baada ya kukaa pale nyumbani kwa muda nilimwambia Bi mkubwa ni wakati sasa na mimi niende kupanga chumba changu ili nijitegemee!,Bi mkubwa alikaataa na akasema nyumba bado ni kubwa na mimi sipaswi kuondoka hapo nyumbani!,Niliona kama Bi mkubwa kanibana maana kuna mitikasi yangu niliona kama haitaenda!,Niliendelea kumsihi Bi mkubwa kwamba ntaenda kupanga ila ntakuwa sikauki pale nyumbani,Baada ya kumsihi sana Bi mkubwa alikubali na akanitaka endapo maisha yakinishinda basi nirudi nyumbani!

Nilikuwa namuhurumia sana Mama yangu kiukweli na nilimpenda sana japo sikuwa na kitu!
Kwakuwa kuna vihela vyangu nilikuwa nimevikusanya kwa wakati huo nilienda kutafuta chumba nkalipia miezi 3 na nkanunua godoro na vyombo kadhaa vya kupikia,nilinunua pia na vitu kadhaa vya ndani na kadri siku zilivyoenda nilipokuwa nikilipwa nilikuwa nikinunua vitu taratibu!

Maisha yalisonga na muda ukayoyoma!,Hatimaye Mungu akasaidia nikauona Mwaka 2011.

Sasa siku moja wakati nikiwa homu Bi mkubwa alinipigia simu akataka niende kule nyumbani maana kuna maongezi!
Basi nkajianda nkasepa zangu mpaka nyumbani,Nilipofika nilimkuta Yule sista mkubwa kaja,Bi mkubwa pia alikuwepo pamoja na wale mabinti waliokuwa wakikaa hapo kwa Bi mkubwa watoto wa Shangazi!
Bi mkubwa alisema ametuita hapo kwasababu kuna jambo kalisikia si zuri!,Nilimuuliza bi mkubwa ni jambo gani hilo?

Ndipo binti mmoja wa Shangazi aliyekuwa mkubwa kuliko yule Mwenzake akawa nasema alikutana na Shemeji yangu mmoja hivi ambaye kwa upande wa Ma sista alikuwa ni wifi yao,kuna maneno aliongea ambayo hayakuwa mazuri!,Yule binti akawa anasema alikutana na Yule shemeji kanisani akawa anamwambia kwamba sisi hapo nyumbani ni Masikini na anajuta hata kaka yao kuuoa hapo nyumbani kwenye ukoo masikini!,Yule shemeji aliendelea kusema kwamba anaogopaga hata kuwapeleka rafiki zake ukweni kwasababu tunanuka umasikini!

Yule Binti akawa anasema tena yule Shemeji alikuwa anasema kwamba hizo taarifa zimfikie mama maana hatuna la kumfanya kwasababu sisi ni masikini wa kutupa,Alikuwa akilaani sana kwanini kaka yake asingeenda kuoa kwenye familia ya kitajiri akaenda kuoa kwetu kwenye familia masikini!

Hayo ndiyo yalikuwa maelezo ya yule Binti mtoto wa Shangazi!

Labda tu niseme hapa kitu ndugu zanguni

Huyu shemeji kaka yake ndo kamuoa dada yetu yule mdogo ambae wanaishi Arusha,Huyu shemeji alikuwa kaajiriwa Benki fulani hapo Mjini na amekaa sana Africa kusini,Kwahiyo hizi mbwembwe zote Alikuwa anazifanya kwakuwa alikuwa na Ajira benki na kukaa tu hapo afrika kusini!.

Baada ya hayo maelezo nilikuwa najiuliza maswali mengi sana,nilikuwa namuuliza mama kwani umasikini ni nini?,Maana sisi kama ni kula mbona tunakula?,kama ni nyumba mbona tuna nyumba?,Huyo malaya anataka maisha gani ?,au kwakuwa yeye ana gari na kufanya kazi benki ndo anadharau watu?
Toka wakati huo nilimwambia Bi mkubwa kwamba sitokaa niimtambue yule Mume wa sista kama shemeji maana dada yake alikuwa akituahibisha na kutusimanga!

Tulipomaliza yale mazungumzo niliondoka zangu pale nyumbani kuelekea Geto kwangu kulala!,Siku hiyo nzima nilikosa raha sana na kutafakari haya maisha,Nilijiona bado nina safari ndefu sana ya kuwa tajiri!

Pale nyumbani kuna jamaa mmoja tulikuwa tumepakana vyumba na alikuwa Rafiki yangu sana maana hata alipokuwa akielekea kwenye shughuli zake ambazo zilimchukua hata mwezi alikuwa akiniachia funguo!
"Mwanangu mbona leo huna raha?,una shida gani"?,Jamaa aliniuliza.

Nilimwambia nilikuwa sijisikii vizuri tu!,Huyu jamaa alikuwa akifanya kazi kampuni ya ujenzi ya Nyanza,Usiku ule nilimfuata jamaa nikamwambia kwa ujasiri mkubwa "NATAKA KUWA TAJIRI",Jamaa alioneshaa kushituka kidogo na kuniuliza "Mwanangu leo umepatwa na nini?,tafadhali nieleze ukweli"
Basi nilimsimulia yaliyonisibu na kiukweli alihuzunika sana na akanambia nisijali niende nikapumzike halafu kesho tutaongea!

Siku iliyofuata baada ya kutoka kwenye shughuli zangu za kushika chaki ilibidi nimueleze jamaa adhma yangu ya kuutafuta utajiri!
Nilimwambia jamaa "Mimi ninachotaka ni utajiri,haijalishi ni utajiri wa namna gani"

Dhumuni la mimi kutaka kuwa tajiri ni kumuonyeshea uwezo yule shemeji yangu na watu wengine waliokuwa wanatuona sisi masikini!,Kiukweli kwa wakati huo nilikuwa tayari kufanya jambo lolote!

Jamaa aliniambia tafuta nauli twende zetu kigoma maana kuna kipindi tulienda kufanya kazi ya ujenzi wa Barabara kule na kuna Bibi tuliwahi kwenda kwake alikuwa ni balaa!,Jamaa akawa anasema kipindi hicho mimi nilienda kwake kufata dawa ya kinga dhidi ya watu wabaya pale kazini hivyo sikufata utajiri,lakini safari hii nataka na mimi nikatafute dawa ya kupanda cheo na kupata pesa!,

Basi hayo mazungumzo ya jamaa yalinipa faraja kidogo nkajiona siko mpweke!

Niliendelea kutafuta pesa za nauli maana jamaa alinambia nikipata kama laki 200000/= nimshitue ili tuondoke maana yeye alikuwa tayari muda wote!
Mwezi uliofata nakumbuka ulikuwa mwezi wa 4 mwaka 2011 sikutaka kumwambia mtu yeyote na sikutaka kumuaga hata Bi mkubwa naelekea wapi!,Mtu aliyekuwa akifahamu ni huyo jamaa tuliyekuwa tukikaa nae hapo nyumbani vyumba jiarani!

Basi tulipanga safari ya kwenda kigoma na tuliondoka Mwanza siku iliyofuata!

Itaendelea..............
 
MKASA WA PILI - sehemu ya 12.

Inaendelea.............

Tuliondoka Mwanza majira ya saa 12 asubuhi,ile njia kuipita mwisho wangu ulikuwa Katoro Geita,lakini kuelekea huko mbele sikuwahi kufika na hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza,nilibeba kibegi kidogo nikaweka nguo za kubadilisha,jamaa yangu yeye alienda akiwa amevaa nguo alizokuwa nazo tu,nikasema uenda safari kama zile yeye alikuwa ni mzoefu!.Ile safari ilikuwa ndefu sana,jamaa aliniambia tukifika Kasulu tungeshuka maana baada ya kufika hapo Kasulu ingetubidi tuelekee kijiji kimoja kinaitwa Munyegera.Ilituchukua masaa 9 mpaka kufika Kasulu mjini,kwakuwa bado ilikuwa mapema jamaa aliniambia tutafute kwanza sehemu wanayouza chakula tule.

Baada ya kumaliza kupata chakula jamaa aliniambia tutafute usafiri wa kuelekea huko kijijini Munyegera,Kwa kuwa mimi ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika hapo kasulu nilikuwa nikishangaa yale mazingira ya mji wa Kasulu yalivyokuwa.Nchi ya Tanzania ni kubwa sana,sikuwahi kudhani kama ipo siku ningefika Kasulu,jamaa akaniambia inabidi tuchukue bodaboda mpaka huko kijiji cha Munyegera,Kwakuwa jamaa alikuwa mwenyeji mimi sikuwa na shaka yeyote.
Tulimuita muendesha boda mmoja akawa amekuja kutusikiliza,jamaa alioongea naye akakubali kutupeleka Munyegera kwa elfu 15 kwa wote wawili.Tulianza safari ya kuelekea huko Munyegera na ilituchukua saa 1:30 mpaka kufika,baada ya kufika tulimpa hela yake jamaa akaondoka zake na sisi kuianza safari ya kutembea kwa miguu kuelekea maporini!.Ilikuwa tayari ishaingia giza lakini hatukujali tuliendelea kuchanja mbuga!,mfukoni wakati huo mimi nilikuwa nina laki tatu,jumla ya pesa niliyobeba ilikuwa laki tatu na sabini(370000/=),hivyo ukijumlisha nauli pamoja na mambo mengine humo njiani nilibaki na laki tatu,sikutaka kupata shida kama niliyoipata hapo nyuma wakati tunaitafuta ile sarafu,japo wakati tuko Mwanza jamaa aliniambia nitafute laki mbili lakini mimi niliamua kujiongeza.

Basi baada ya kutembea kwa muda mrefu hatimaye tulifika hapo nyumbani kwa huyo mama mganga na tulipokelewa na mabinti wawili waliyokuwa hapo,Kuna watu tuliwakuta pale ilibidi nimuulize jamaa mwenyeji wangu akaniambia hao pia walikuwa pale wamefata tiba!,akili yangu mara zote nilipokuwa ugenini,ilikuwa ni mawazo ya namna ya kupata mahali pa kulala tu!.Kwakuwa ilikuwa ishafika usiku tulikuta umekokwa moto,kuna raia wengine walikuwa wakiota moto pale huku wakiendelea kupiga stori za hapa na pale kwa kiswahili chenye lafudhi ya Kiha!.

Jamaa aliniambia "ngoja niende kumuona mama mganga kama yupo halafu narudi".

Baada ya dakika kadhaa alirudi na kuniambia msaidizi wa yule mama kamwambia yule mama hayupo ila angerudi asubuhi,hata hao watu tuliowakuta walikuwa wakimsubiri yeye!,Kwakuwa baridi ishaanza kuwa kali ilibidi mimi na jamaa tusogee kwenye moto,tulikaa hapo chini ya mkeka mpaka mimi usingizi ukanipitia,nilishituka nikakuta bado jamaa wako macho wakiendelea kupiga stori,niliendelea na hiyo hali ya kulala na kushituka mpaka kulipo pambazuka!,Kuna jamaa tulimkuta pale kazi yake ilikuwa ni kuongeza magogo tu kwenye ule moto kila ulipoonyesha hali ya kufifia!.

Asubuhi kila mtu alikuwa na ishu zake,niliona kila mtu alikuwa amekaa na mtu ambaye walikuwa wakifahamiana naye!,Yule mama mganga tuliambiwa alikuwa amerudi,nilijiuliza alirudi vipi wakati usiku huo wote hakukuwa na mtu mwingine aliyeingia hapo? nikakosa majibu!.Watu tuliowakuta hapo ndiyo walioanza kuingia ndani kwenye nyumba ya mganga na kuelezwa walichoelezwa,kuna wengine walikuwa wakitoka wanaondoka jumla na kuna wengine walikuwa wakitoka wanarudi tena nje kukaa nadhani waliambiwa wasubiri!.Tulikaa kwa muda mrefu ndipo zamu yetu ilipofika tuliitwa na msaidizi wa yule mama,tuliambiwa tunaingia mmoja mmoja ndani,ndipo mimi nikamwambia yule jamaa yangu aanze yeye!.Jamaa alikaa humo ndani kama nusu saa halafu akatoka akaniambia na mimi niende ndani.Nilipofika ndani nilimsalimia Yule mama ambaye hakuwa mzee sana kama nilivyofikiria,kabla sijaanza kuongea naye aliniambia ninyamaze maana maisha yangu yote toka tukiwa Tarime mpaka nimefika hapo kwake alikuwa anayafahamu hivyo akaniambia nimwambie kilichokuwa kimenipeleka kwake!,kiukweli aliponiambia anayafahamu maisha yangu Tangu nikiwa Tarime nilishangaa sana!.Hivyo ilibidi nimueleze kwamba ninataka kuwa tajiri,aliniangalia akawa anatikisa kichwa tu,kisha akaniambia "Mbona mwanangu umeharibiwa sana"!,huwezi kuwa tajiri mpaka usafishwe kisawa sawa!".

Akaendelea kuniambia kwamba "nyota ya marehemu baba yako unayo wewe,ila kuna kitu kimekuzuia usiipate,kitu hicho ndicho kinafanya nyota ya baba yako ising'ae kwako ili uwe tajiri".

Akaniambia yeye atanisafisha na kunipa dawa ya kinga ili chochote kibaya kitakachonisogelea basi kiende na maji!,akaniambia baada ya kunisafisha itanipaswa niende mpaka Kigoma halafu nivuke ng'ambo ya pili upande niingie upande wa Kongo sehemu moja inaitwa Kalemii,huko kuna mtu ambaye angeniondolea hilo tatizo hatimaye nyota ya baba yangu niipate mimi ili niwe tajiri.Kiukweli nilivuta pumzi sana maana nilifahamu nilikuwa nimemaliza kazi kumbe ndiyo kwanza kazi ilikuwa haijaanza!,aliniambia itanibidi nikae pale kwake siku tatu ili akimaliza kuwashughulikia wale wagonjwa wengine niliyowakuta ndipo nianze dozi!.Nilipomaliza kuongea na yule mama ilibidi nitoke nje kuongea na yule jamaa aliyenipeleka,baada ya kumsimulia kila kitu jamaa kashangaa sana!.

Jamaa akaniambia "Mwanangu jipe moyo,kwakuwa umeamua pasipo kulazimishwa inakupasa uwe na uvumilivu".

Yule mama alitoka nje na kuanza kuongea na wateja wake,alipofika kwetu alimwambia yule jamaa yangu kwamba "huyu mwenzio bado nina kazi naye!,Wewe kama utamsubiri endelea kumsubiri,lakini akimaliza hapa bado anasafari nyingine!".

Jamaa tuliongea naye na hakuwa na namna ilibidi aondoke akawahi kazi zake lakini akaniambia mimi ni mwanaume nijipe moyo!.Nilimwambia jamaa endapo nisingerudi nyumbani kwa chochote ambacho kingenipata basi anichukulie vile vyombo vyangu anipelekee nyumbani kwetu Nyegezi,jamaa alikubali!,jamaa aliniaga na akaniongezea laki moja tena ila nilimwambia ningerudi ningemrudishia hiyo hela.Wakati jamaa anaondoka nilijikuta nalia kama mtoto maana sasa nilijiona bado nilikuwa nina safari ndefu ukizingatia nilikuwa mgeni hayo maeneo.Nilijipa moyo sana maana niliona ningekata tamaa hakuna ambacho ningefanikisha!.

Itaendelea..............
 
Simulizi hii imewezeshwa na JamiiTalk hivyo itaendelea kama kawaidi lakini kama ungependa kuisupport JamiiTalk unaweza ichangia kupitia lipa namba ya Vodacom

67326343 - Jina JamiiTalk

Lipa hii ni lipa ya Vodacom lakini inapokea kutoka Mitandao yote kama ungependa kuchangia kwa njia nyingne unaweza uliza hapa au unaweza wasiliana na @JamiiTalk kwa PM au Email: support@jamiitalk.com au contact@jamiitalk.com
 
Back
Top