Kasomi
JT Founder
Dunia inajiandaa kushuhudia tukio adimu la anga la Kupatwa kwa Jua la karne, litakalotokea mwaka 2027, Dunia kukumbwa na giza dakika 6 ifikapo Agosti 2, 2027 likitajwa kama The Great North African Eclipse. Tukio hili linatarajiwa kuwa kupatwa kwa jua kwa muda mrefu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 100, likidumu kwa dakika sita na sekunde 22.
Kwa mujibu wa wataalamu wa anga, kupatwa huku hakujashuhudiwa juu ya ardhi kwa ukubwa huu tangu mwaka 1991, na baada ya 2027, hakutatarajiwa kutokea tena hadi mwaka 2114 hali inayofanya tukio hili kuwa la kipekee na la mara moja maishani.
Luxor, Misri, imeainishwa kuwa eneo bora zaidi duniani kwa kutazama kupatwa huku kikamilifu. Wasafiri kutoka pande zote za dunia tayari wameanza kupanga safari kuelekea mji huo wa kihistoria, ambapo watapata fursa ya kushuhudia tukio hili la anga.
Katika siku hiyo, Mwezi utaufunika kabisa Jua kwa watazamaji waliopo Afrika Kaskazini, huku kupatwa kwa kiwango cha sehemu au kamili kikitarajiwa kuonekana pia katika nchi kadhaa zikiwemo Hispania, Morocco, Algeria, Tunisia, Libya, Misri, Saudi Arabia na Yemen.