Fani ya Akiba; Ususi Tegemeo La Vijana na Mabinti

pius pius

New member
Fani ya Ususi imekuwa tegemezi na kimbilio la watu wengi; vijana na mabinti ambao hawakubahatika kuendelea na elimu ya sekondari, na wale ambao walibahatika kuendelea na sekondari, wamemaliza kidato cha nne na kushindwa kuendelea na masomo na kwa wale ambao wanaipenda bila kujali hali zao za kielimu. Vyuo mashuhuri kama VETA, FARIDA BEAUTY ACADEMY na vinginevyo vimekuwa vikijizolea umaarufu na kujipatia kipato kutoka kwa wanafunzi ambao Ususi na fani nyingin
1000326302.jpg
e za urembo ndio ndoto za maisha yao.
Kuwa msusi mashuhuri na mwenye kufanya kazi nzuri si lazima uwe na cheti kutoka sehemu yeyote. Ususi ni fani ya kiutendaji, cheti huwa na maana pale tu kazi ya msusi ikingaa na kuangaza macho ya wateja na wazazi ambao wanatamani vijana wao na mabinti zao kufanya kazi kama hizo. Binafsi, nimekutana na wasusi wengi nje na jamii ya watu wa kimaasai ambao ni mashuhuri kwa kusuka nywele yao ya kitamaduni iitwayo Kimasai. Wasusi hao hawakuwa na cheti kutoka chuo chochote kinachotambulika na serikali, yaani, walijifunza mtaani, wengi wao walifundishwa na wazazi, ndugu au majirani. Kazi zao zilikuwa nadhifu, bei rafiki na zakiushindani.

MASOKO.
Kama zilivyo fani nyingine, fani ya Ususi inaweza kupoteza masoko yake. Fani ya Ualimu kwa mfano, kila mwaka vyuo mbalimbali hutoa wahitimu walio tayari katika masoko yasiyo tayari kuwapokea kwa wingi huo. Mahitaji ya Soko hubadilika kama kinyonga, miaka michache iliyopita fani ya Ususi haikuwa na umuhimu iliyonayo sasa, bila shaka, itachukua miaka michache kwa fani hii kuwa na soko gumu lenye ushindani mkubwa.
Urahisi wa soko na ugumu wa soko unategemea na unadhifu wa kazi yako na wala si cheti au tuzo zinazotolewa vyuoni. Mteja wako ndio bango la matangazo. Kuna watakao vutiwa na kazi yako uliyoifanya. Wengine watakutafuta ili wapate huduma hiyo au inayoendana na hiyo. Na bango hilo halitangazi kazi zako tu, bali, hutangaza mazungumzo yako, tabia zako ambazo mteja imeziona mda mfupi mlio pamoja n.k. Ni muhimu kuzingatia kila neno utakalosema kulikanga na aina ya mteja.
Wepesi wa mkono wako kukamilisha kazi kwa muda mfupi iwezekanavyo. Soko lako litakuwa gumu na utazidi kupoteza wateja kama mkono wako utakuwa mzito. Wateja wengi hawapendi kukaa foleni. Huduma ambayo inachukua masaa mawili, isikuchukue masaa sita. Hakikisha unachangamsha mkono wako kwa kufanya mazoezi ya kutosha ili kuhakikisha unaendana na soko. Wakati unamaliza siku nzima kuhudumia wateja wawili, wenzako wanatumia masaa kumi kuhudumia wateja zaidi ya watano. Kumbuka una Kodi ambazo inabidi ulipe, bili za maji, umeme, nauli na chakula binafsi pamoja na TRA wanakutazama.

MTAJI
Ukweli ni kwamba, kwa wale ambao wanataka kufanya kazi kwenye saluni za watu, hauhitaji msingi wala mtaji wowote. Ujuzi wako ndio utakao kupeleka pale, na kazi zako ndio zitakazokupa sauti na mapato.
Kwa wale ndugu zangu wa uswahilini, sio lazima kuwa na fremu au kibanda kuanza kazi, unaweza kuanza na mkeka na kiti hapo nyumbani kwako au kwa wazazi wako. Ndugu zako na jirani zako, ndio wateja wako wa kwanza. Sio wote watakao kuwa na imani na wewe, na sio lazima wawe na imani na wew siku za mwanzoni. Unahitaji uvumilivu wa hali ya juu, kuona watu wakienda kupata huduma sehemu nyingine, wakati wewe upo na unatoa huduma hiyo kwa gharama nafuu zaidi.
Gharama za kufungua saluni zinatofautiana kulingana na maeneo. Bei za fremu ni kubwa kulingana na eneo, hivyo, mtaji wa mtu atakayefungua saluni Manzese ni tofauti na atakayefungua Tandika. Vifaa vya saluni vinapatikana kwa bei inayopimwa kwa ubora na usasa wa kifaa hicho. Ni muhimu kufanya uchunguzi wa eneo unalotaka kufungua na vifaa utakavyo nunua.
MASLAHI.
Hakuna maneno ya kuelezea fahari ya msusi anayekubarika katika Soko, watu hutoka huku na huko kufata huduma ambayo wapo tayari kulipia kwa bei yoyote, na wengine wapo tayari kusubiri kwenye foleni siku nzima bila malalamiko.
Malipo ni mazuri na maradufu. Huitaji kulipia matangazo, unaweza kutumia simu yako na ucheshi kwa wateja zako.
 
Back
Top